Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Sunday, April 22, 2012

MWAKALEBELA ATOA SOMO KWA WAJUMBE WA MKUTANO MKUU WA TFF


Fredrick Mwakalebela pichani (kulia)
Na Mwandishi wetu
WAKATI mkutano mkuu wa Shirikisho la Kandanda nchini (TFF) unafanyika leo, Katibu Mkuu wa zamani wa shirikisho hilo, Fredrick Mwakalebela amewashauri wajumbe kujadili masuala ya kulipatia uwezo shirikisho hilo na kuepuka kuwa tegemezi.
Akizungumza na mwandishi wa mtandao huu jijini jana, Mwakalebela alisema kuwa TFF inaweza kuepukana na hali ya kuomba fedha kwa wadau ili kusafirisha timu ya Taifa ya wanawake na baadala yake kutengeneza sera itakayowafanya wadhamini washindani kudhamini timu na shughuli mbali mbali bila kuingilia shughuli za mwengine.
Alifafanua kuwa udhamini wa kampuni ya simu ya Vodacom unawazuia kampuni nyingine za simu kama Tigo, Zantel na Airtel kudhamini timu shughuli nyingine za shirikisho hilo na kunyimwa fursa ya kuendeleza michezo nchini.
Mwakalebela alisema kuwa TFF inatakiwa kuandaa sera ambazo zitawaruhusu wadhamini kama hao kudhamini hata timu za taifa za vijana na wanawake ili watanzania waweze kufaidi matunda ya uwekezaji wao.
Katibu Mkuu huyo pia alitoa ushauri kwa wajumbe hao kujadili suala la matumizi ya uwanja wa kumbukumbu ya Karume kutumika kibiashara zaidi kutokana na ukweli kuwa upo katika eneo zuri (Prime Area) kwa ajili ya shughuli hiyo na kuwaingizia kipato.
Alisema kuwa eneo hilo linaweza kutumika kwa ujenzi wa maduka, hotel na vitega uchumi mbai mbali ambavyo vitaiondolea shirikisho hilo uhaba wa kupata fedha kwa ajili ya shughuli zake mbali mbali mbali.
Kuhusiana na kushuka kwa soka la Tanzania, Mwakalebela aliwaomba wajumbe kujadili na kuweka mikakati mikubwa ya kuanzisha soka la vijana wadogo kwa kushirikiana na Cecafa, CAF na Fifa ili kufikia lengo.
Alisema kuwa kwa kuandaa vijana hao, wataweza kushindana katika mashindano ya vijana na baadaye kufanya vyema kwa upande wa soka la wakubwa.
“Kwa sasa soka la vijana lipo jijini Dar es Salaam, Zanzibar na pengine Arusha, mikoa mingine ni sawa na hakuna na hii inatokana na changamoto za maeneo ya kuchezea, hivyo mipango thabiti inatakiwa kuwekwa ili kufanikisha hilo,” alisema.
Vile vile Mwakalebela aliwataka wajumbe hao kujadili maenedeleo ya soka la wanawake kwa kupanua wigo na kuiwezesha mikoa mengine nao kuwa na timu za wanawake na syo kutegemea Dar es Salaam tu na hasa Kinondoni.
Alisema kuwa soka la wanawake limeonyesha kuwa ndilo linaweza kuitoa Tanzania kimasomaso kimataifa

No comments :

Post a Comment