Gari la Cheka likiwa Kituoa cha Polisi Magomeni baada ya kupata ajali jana usiku.
***************************
*Furaha ya ushindi wa Cheka kumchapa maugo
yaishia kituo cha Polisi
*Alala Oysterbay Polisi adhaminiwa leo
Ikiwa ni siku moja tu baada ya kuvishwa
taji la ubingwa huo na kukabidhiwa mchuma wake, Cheka alikamatwa na Polisi
masaa machache tu baada ya kukabidhiwa gari na kuanza safari ya kuelekea
nyumbani kwake ambayo iliishia mitaa ya Manzese baada ya kupata ajali kwa
kugonga Pikipiki na kuwajeruhi dereva wa pikipiki hiyo na abiria wake ambao
walikimbizwa Hospitali ya Mwananyamala kwa matibabu.
Pikipiki iliyogongana na gari la Cheka |
Leo asubuhi baada ya kupata taarifa ya
tukio hilo mtandao huu wa
ulifanya jitihada za kupata dondoo za tukio hilo na kufika Kituo cha Polisi Oysterbay
ambako alikuwa ameshikiliwa Bondia huyo na kupata taarifa kuwa muda mchache tu
uliopita kabla ya kuwasili mahala hapo aliondoka akiwa ameongozana na nduguze
baada ya kupata dhamana.
Baada ya kupishana na bondia huyo mtandao
ulitinga Kituo cha Polisi Magomeni na kufanikiwa kuliona gari hilo likiwa limeharibika na kuvunjika kioo
huku Pikipiki hiyo iliyogongwa yenye namba za usajiri T507 BYR, ikiwa mahala
hapo.
Akizungumza na Mtandao huu kwa njia ya simu
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela, alithibitisha kutokea kwa
ajali hiyo iliyotokea jana usiku majira ya saa nane maeneo ya Manzese na
kuwajeruhi dereva na abiria wake waliokuwa katika pikipiki hiyo.
Aidha Kenyela, alisema kuwa baada ya ajali
hiyo Dereva wa gari hilo lenye namba za usajiri T 321 AAU, aliyefahamika kwa
jina la Francis Cheka, alifikishwa kituo cha Polisi Oysterbay na kushikiliwa
hadi asubuhi ya leo walipofika ndugu zake na kumuwekea dhamana.
Akielezea tukio hilo
Kenyela, alisema kuwa Gari la Cheka lilikuwa likitokea maeneo ya Manzese
kuelekea Ubungo na Pikipiki ikitokea Ubungo kuelekea Manzese na walipofika
maeneo ya Tip Top Manzese, dereva wa pikipiki aliutan na kuhamia barabara ya
pili ili kuelekea Ubungo na kugongana na gari hilo .
Aidha alisema kuwa dereva huyo wa pikipiki
bado amelazwa katika Hospitali ya Mwananyamala akiendelea na matibabu huku
abiria wake akitibiwa usiku wa jana na kuruhusiwa.
No comments :
Post a Comment