Na Mwandishi Wetu Kibaha Pwani
TIMU ya Taifa ya mchezo wa Masumbwi ya ridhaa inayojiandaa na mashindano ya kufuzu kucheza Olimpiki inatarajia kucheza michuano ya kujipima nguvu na timu ya Combaini ya Ngome.
Michuano hiyo imepangwa kufanyika April 5 mwaka huu katika ukumbi wa Jeshi uliopo Mwenge jijiji, Dar es Salaam.
Akizungumza katika Shule ya Sekondari ya Filbert Bayi ilipokuwa Kambi hiyo, kocha wa timu hiyo David Yombayomba alisema mchezo huo ndio utakaoangalia viwango vya mabondia hao vilipofikia.
"Kambi ya ngumi kwa ujumla inaendelea vizuri na wachezaji wote wapo katika kiwango cha kuridhisha na tunategemea mashindano hayo ya April 5 yatatoa mwanga kwa timu hii kwa kile tulichokifundisha kama kimezingatiwa,"alisema Yombayomba.
Alisema Combaini hiyo ya Ngome itakuwa na wachezaji wazuri mmoja mmoja ambao uwezo wao ni mkubwa na utaweza kuleta changamoto kubwa kwa mabondia hao.
Yombayomba pia ameliomba Shirikisho la Ngumi za Ridhaa nchini kuwatafuia mapambano mengine kama itawezekana kabla ya kwenda Kasablanka nchini Moroko kwa ajili ya kusaka viwango hivyo vya kucheza Olimpiki.
Mashindano hayo ya kufuzu kucheza Olimpiki kwa upande wa ngumi yataanza April 27 mwaka huu ambapo mashindanmo hayo ndiyo yatakayotoa idadiya mabondia wa Tanzania watakaokwenda London Uingereza kwenye mashindano ya Olimpiki yatakayofanyika Julai mwaka huu.
Mbali na hivyo alikumbusha kuwa wadau mbali mbali kujitokeza kuwapa sapoti kwa kutoa udhamini wa aina yoyote ikiwemo vifaa vya mchezo pamoja na vya mazoezi kwa ajili ya mabondia hawo waliopo Kasmbini.
Makampuni yamekuwa wakichagua mchezo flani kwa ajili ya kutoa sapoti yao basi watukumbuke na sisi japo kidogo kwani mchezo wa ngumi ndio pekee mpaka sasa iliyoleta sifa nchini kwa kiwango cha juu na kutambulika Duniani kote
No comments :
Post a Comment