Wachezaji wawili Watanzania wameombewa Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) kwa ajili ya kucheza mpira wa miguu katika nchini za Denmark na Jamhuri ya Czech.
Chama cha Mpira wa Miguu cha Denmark (DBU) kimemuombea hati hiyo William Benard Okum kama mchezaji wa ridhaa ili ajiunge na timu ya Brabrand IF. Klabu ya zamani ya Okum ni Viko Pham FC ya Zanzibar.
Naye
Samwel Jonathan Mbezi ameombewa hati hiyo na Chama cha Mpira wa Miguu
cha Jamhuri ya Czech (FACR) ili aweze kuchezea timu ya Sokol Dolany
akiwa mchezaji wa ridhaa. Katika maombi hayo, FACR imeonesha kuwa Mbezi
kwa sasa hana timu anayochezea hapa nchini.
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linafanya mawasiliano na pande husika
kabla ya kutoa hati hizo kwa wachezaji hao kama walivyoomba DBU na FACR.
MECHI KUCHANGIA TWIGA STARS MEI 4
Mechi
maalumu ya hisani kwa ajili ya kuchangia timu ya Taifa ya wanawake
(Twiga Stars), kati ya timu hiyo na wasanii wa filamu maarufu kama Bongo
Movie itachezwa Mei 4 mwaka huu.
Kwa
mujibu wa kampuni ya Edge Entertainment iliyoandaa mechi hiyo
itafanyika kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10 jioni
kwa kiingilio cha sh. 2,000, sh. 5,000 na sh. 10,000.
Twiga
Stars kwa sasa hivi haina mdhamini na iko kambini katika kambi ya Jeshi
la Kujenga Taifa (JKT) ya Ruvu mkoani Pwani inashiriki michuano ya
Afrika kwa Wanawake (AWC) ambapo Mei 26 mwaka huu itacheza na Ethiopia
jijini Addis Ababa. Fainali za AWC zitafanyika Novemba mwaka huu nchini
Equatorial Guinea.
MECHI ZA LIGI KUU WIKIENDI HII
Ligi
Kuu ya Vodacom inaendelea katika raundi ya 25 kesho (Aprili 28 mwaka
huu) ambapo Coastal Union itakuwa mwenyeji wa Kagera Sugar kwenye Uwanja
wa Mkwakwani jijini Tanga huku Mtibwa Sugar ikiwa mgeni wa African Lyon
kwenye Uwanja wa Chamazi.
Aprili
30 mwaka huu Azam na Toto African zitacheza Chamazi wakati Mei 1 mwaka
huu Villa Squad itaumana na Oljoro JKT kwenye Uwanja wa Chamazi.
Ligi
hiyo itafunga msimu wa 2011/2012, Mei 5 mwaka huu ambapo timu zote 14
zitakuwa uwanjani. Simba vs Yanga (Uwanja wa Taifa), Oljoro JKT vs
Polisi Dodoma (Sheikh Kaluta Amri Abeid, Arusha) na Ruvu Shooting vs
Villa Squad (Mabatini, Mlandizi).
Mechi
nyingine zitakuwa kati ya Coastal Union vs Toto African (Mkwakwani,
Tanga), African Lyon vs JKT Ruvu (Manungu, Morogoro), Azam vs Kagera
Sugar (Chamazi, Dar es Salaam) na Moro United vs Mtibwa Sugar (Jamhuri,
Morogoro).
MKUTANO MAKOCHA SIMBA, AL AHLY SHANDY
Makocha
wa timu za Simba na Al Ahly Shandy ya Sudan kesho (Aprili 28 mwaka huu)
watakuwa na mkutano na Waandishi wa Habari kuzungumzia walivyoandaa
vikosi vyao kwa ajili ya mechi ya Jumapili.
Mkutano
huo utafanyika saa 4 kamili asubuhi kwenye ofisi za Shirikisho la Mpira
wa Miguu Tanzania (TFF). Mechi hiyo ya Kombe la Shirikisho itachezwa
Uwanja wa Taifa kuanzia saa 10 kamili jioni.
No comments :
Post a Comment