Taarifa kwa vyombo vya habari
Tigo Ngorongoro
Marathon ya karibia
10 April, 2012, Dar es Salaam. Jumamosi tarehe
14,2012, kwa mara ya tano Mbio za Ngorongoro zitashuhudia wakimbiaji wa kms 21
wakitokaka katika geti la Ngorongoro Crater kupitia milima na mabonde hadi
kwenye utepe wa kukamilisha hizi mbio mjini Karatu kwenye ‘ Mbio dhidi ya
Malaria.’
“Moja ya vipaumbele vyetu katika programu zetu za kuisaidia jamii
Afrika ni kwenye Afya na hali njema” alisema bi Ester Palsgraaf,ambaye ni Meneja
Mahusiano na jamii …………………….. “Katika program ya mwaka 2012 tunashirikiana na
Zara Charity ili kuwaelimisha watu kuhusu ugonjwa wa malaria,lengo likiwa ni
kusaidia kupunguza maambukizi,” alisema.
Mwaka huu Zara Charity wamechukua
uongozi wa mbio za Ngorongoro kutoka kwa Minnesota International Health
Volunteers (MIHV). Zara Charity inafanya kazi na kamati ya Olimpiki Tanzania
(TOC) kuhakikisha ushiriki wa wanariadha duniani,mpaka sasa wakimbiaji wenye
sifa za kimataifa 200 wameshajiandikisha.
Zara charity pia inashirikiana na
wizara ya afya na ustawi wa jami kuelimisha watu kuhusu malaria kabla ya siku ya
malaria duniani tarehe 25 mwezi wa nne 2012. Mbio hizi zinaonekana kama nafasi
ya kueneza uelewa kuhusu malaria na juhudi za moja kwa moja za kupambana na
ugonjwa huu unaozuilika
“Tumefurahishwa sana na ushirikiano ambao
tumeupata kutoka mashirika tunayofanya nayo kazi” alisema bwana Silevery Tesha
mratibu wa Zara Charity. “Tunajua jinsi gani malaria ilivyo na athari Tanzania
na ndiyo maana tumejitoa kuupiga vita. Mbio hizi zitatumia njia ya kufurahisha
kuleta uelewa wa tatizo hili na tunafuraha mwaka huu kwa timu ya olimpiki ya
Tanzania kushiriki katika mbio hizi kama moja ya maandalizi ya olimpiki za
London Julai hii” alisema.
Waandaaji wa mbio hizi wamepanga kuwa na zaidi
ya timu za makampuni 50, ikiwa ni pamoja na kuandaa mbio za kawaida kwa watoto
wa umri wa wanafunzi wa shule za msingi kushiriki katika mbio za kilometa 2.5.
Mbio zote zitaanza saa 2:30 asubuhi
Malaria ni ugonjwa hatari ambao unaua
watu milioni moja hadi tatu kwa mwaka na kusababisha vifo 3000 vya watoto kila
siku, inaendelea kuwa moja ya magonjwa yanayoongoza kwa kuua duniani. Waathirika
wakubwa wakiwa ni watoto chini ya miaka mitano na kina mama
wajawazito.
Kuhusu Tigo
Tigo, the first cellular network in
Tanzania, started operations in 1994 and is Tanzania’s most affordable and
innovative mobile phone operator covering 26 regions in mainland Tanzania and
Zanzibar.
Tigo is part of Millicom International Cellular S.A (MIC) which
provides affordable, widely accessible and readily available cellular telephony
services to more than 43 million customers in 13 emerging markets in Africa and
Latin America.
For further information visit: www.tigo.co.tz
No comments :
Post a Comment