Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Monday, January 6, 2014

Dr Wiliam Mgimwa. azikwa


Mjane  wa Dr Mgimwa akiaga  mwili  huo kabla ya mazishi kijiji   cha Magunga  Iringa  leo 
Mwili  wa Dr Mgimwa ukishushwa kaburini  leo 
Wabunge  Deo  Sanga  wa jimbo la Njombe Kaskazin  kushoto na Deo Filikunjombe wa Ludewa  
rais  Kikwete na mkewe  wakiweka  shada la maua 

MAELFU   ya  wakazi  wa mkoa  wa Iringa na  baadhi  ya  viongozi  wa  vyama  vya  siasa na  Serikali  wakiongozwa na  Rais Dr  Jakaya  Kikwete  wameshiriki  katika mazishi ya  aliyekuwa  mbunge wa   jimbo la Kalenga na  waziri wa fedha  Dr  Wiliam Mgimwa.

Huku   waziri  mkuu Mizengo  pinda katika  salam  zake za serikali akielezea  jinsi ambavyo  Taifa  lilivyopata  pigo kubwa  kufuatia  kifo  cha Dr Mgimwa kutokana na mchango  wake  katika baraza la mawaziri.

Katika  mazishi  hayo   yaliyofanyika  leo kijiji  kwake Magunga  jimbo la Kalenga   wananchi   mbali  mbali   walionyesha  kujipanga  barabarani  kutoka Manispaa ya  Iringa  hadi  kijijini kwake  huku  wakiupungia mkono msafara  wa    rais Kikwete na baadhi yao  wakilazimika  kutumia  usafiri wa baiskeli na pikipiki  kwenda katika mazishi  hayo.

Akitoa   shukrani za  familia kwa niaba ya  familia  mtoto wa marehemu Dr Mgimwa Godfrey  Mgimwa  aliishukuru   serikali kwa  jinsi ambavyo ilivyohangaika  kumuuguza baba  yake  na  kutoa wosia  mzito wa marehemu  Dr Mgimwa ambao  alimtaka kuufikisha kwa Rais  Kikwete..

Alisema  katika  uhai  wake kabla  ya kifo  chake  ikiwa ni siku tano kabla  Dr  Mgimwa alimwita na  kumtaka  kufikisha  shukrani zake kwa Rais  Kikwete kwa  kumtembelea mara mbili Hospital  alipokuwa amelazwa  pamoja na  spika wa bunge Anne makinda .

Pia  alisema  kuwa alieleza dhamira  yake ya  kuwatumikia  wana Kalenga na  kusema  zawadi kubwa ni msaada wa bati  zaidi ya  2000 kwa wananchi hao  ili kuendeleza ujenzi wa shule na  vituo  vya afya  jimboni.

"Baba  kabla ya  kufa  aliniachia  wosia  huo juu ya wana Kalenga kwa kuwashukuru kwa  ushirikiano  wao na  kutoa  bati ila alipenda  kuona  Kalenga  inakuwa na maendeleo zaidi"

Kwa  upande  wake  waziri Mkuu Pinda  alisema  kuwa  serikali imepata pigo kubwa  juu ya kifo hicho na kuwa  bado serikali  itaendelea  kuwa karibu na familia ya Dr Mgimwa  na pale  penye tatizo  isisite  kuwasiliana .

Hata  hivyo  Rais  Kikwete  hakupata  kuzungumza  chochote  katika msiba  huo  zaidi ya  kuweka mchanga na shada la maua pamoja na kuwapa mkono  ndugu wa Dr Mgimwa .


Spika  wa bunge Anne Makinda  alisema kuwa  bunge  limempoteza kiongozi na mbunge aliyependa kutumia  nafasi yake kwa ajili ya Taifa  na kuwa kamwe mchango  wake  hawataacha kuukumbuka.PICHA NA HABARI KWA HISANI YA FRANSIS GODWIN IRINGA

Babi ajitabiria makubwa UiTM



Babi (kati)nakiwa na wachezaji wenzake wa UiTM
KIUNGO wa kimataifa wa Tanzania, Abdi Kassim 'Babi' amesema ameyazoea kwa haraka mazingira ya nchi ya Malaysia alikoenda kucheza soka la kulipwa katika klabu ya UiTM na kudai ana imani atafanya vyema Ligi Kuu ya nchi hiyo ikianza.
Nyota huyo wa zamani wa klabu ya Mlandege, Mtibwa Sugar, Yanga, Azam na KMKM, aliliambia gazeti hili kwamba anashukuru kwa kipindi kifupi tangu atue katika nchi iliyopo Mashariki ya Mbali, ameweza kuzoea mazingira na kuzoeana na wachezaji wenzake wanaojiandaa na msimu mpya wa ligi.
Babi anayefahamika pia kama 'Ballack wa Unguja' alituma picha yake ikimuonyesha akiwa na wachezaji wenzake wa klabu hiyo wakiwa wamepozi baada ya kutokana kufanya mazoezi na kusema tofauti na fikira zake Malaysia kunaonekana kutakuwa kwepesi kwake kuliko ilivyokuwa Vietnam alipocheza soka la kulipwa.
Mchezaji huyo aliwahi kuichezea DT Long ya Vietnam kwa muda wa miezi nane baada ya kujiunga nayo mwaka 2010 akitokea klabu ya Yanga na kurejea nyumbani kujiunga na Azam kwa mkataba wa miaka miwili.
"Kwa hali hii nadhani nitafanya vyema kwa sababu nimeyazoea mazingira kwa kipindi kifupi mno tofauti na nilivyodhani. Bahati nzuri asilimia kubwa ya watu wa hapa ni waislam hivyo hata chakula ni kile nilichozea kula. Kwa sasa tunajifua kwa ajili ya msimu mpya wa ligi utakaoanza Januari 18," alisema Babi.
Babi alijiunga na klabu hiyo kwa mkataba wa mwaka mmoja akitokea KMKM waliomsajili baada ya kuachana na Azam aliyoichezea msimu uliopita kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara.

Simba yaifuata Azam Robo fainali Mapinduzi, Kiemba aaah




BAO pekee la mapema la Amri Kiemba liliisaidia Simba kufuzu robo fainali ya michuano ya Kombe la Mapinduzi kuungana na Azam ambayo leo itakamilisha ratiba kwa kuvaana na Ashanti United katika mechi za kundi C.
Kiemba alifunga bao hilo akimalizia kwa kichwa pasi ya Ally Badru na kuwa bao lake la pili katika michuano hiyo na mawili kwa Simba ambayo imemaliza mechi za makundi usiku wa jana kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mabingwa wa visiwani, KMKM ikifikisha pointi 7.
Azam ambao ni mabingwa watetezi wa michuano hiyo wenyewe walikuwa wa kwanza kufuzu hatua hiyo baada ya kuongoza kwenye kundi lake la kupata ushindi mara mbili mfululizo na leo itaumana na Ashanti walioingizwa dakika za jioni baada ya Yanga kuchomoa kushiriki mashindano hayo.
Ashanti yenyewe ina pointi moja kutokana na mechi mbili.
Nyingine zilizofuzu hatua hiyo ni KCC ya Uganda, iliyoongoza kundi B lenye timu ya Simba, KMKM na AFC Leopards ya Kenya iliyoaga mashindano.

Saturday, January 4, 2014

DVD MPYA ZA MASUMBWI HIZI HAPA ZA KITANZANIA


DVD MPYA YA BONDIA FRANSIC MIYEYUSHO IKIWA IMESHEHENI MAPAMBANO MBALIMBALI YA NGUMI
MAPAMBANO MAKALI YA NGUMI ZOTE KALI LIPO KWENYE DVD MOJA SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 
Rajabu Mhamila 'Super D'

Email.superdboxingcoach@gmail.com
mhamila1@gmail.com
www.superdboxingcoach.blogspot.com
Mob;+255787 406938
+255774406938, +255713406938
Po.Box. 15493
Dar es Salaam Tanzania

DVD YA FRANSIC MIYEYUSHO 'CHICHI MAWE' VS MBWANA MATUMLA 'GOLDEN BOY'
DVD YA FRANSIC MIYEYUSHO 'CHICHI MAWE' VS MBWANA MATUMLA 'GOLDEN BOY'
DVD MPYA YA BONDIA FRANSIC MIYEYUSHO IKIWA IMESHEHENI MAPAMBANO MBALIMBALI YA NGUMI

RAIS WA ZANZIBAR DKT SHEIN AFUNGUA KITUO CHA AFYA CHA BUMBWINI KIONGWE


  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akifungua pazia kukifungua Kituo cha Afya Bumbwini Kiongwe,Jimbo la Bumbwini Wilaya ya Kaskazini B,Mkoa wa Kaskazini Unguja jana,katika shamra shamra za miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar,(kulia) Waziri wa Afya Juma Duni Haji.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akikata utepe kufungua Kituo cha Afya Bumbwini Kiongwe,Jimbo la Bumbwini Wilaya ya Kaskazini B,Mkoa wa Kaskazini Unguja jana,katika shamra shamra za miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akipata maelezo kutoka kwa Daktari dhamana Abdulwahab  Mohamed,baada ya kukifungua Kituo cha Afya Bumbwini Kiongwe,Jimbo la Bumbwini Wilaya ya Kaskazini B,Mkoa wa Kaskazini Unguja jana,katika shamra shamra za miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akimuuliza suala Daktari wa huduma za Mama na  Mtoto,Halima Abdalla Saidi,wakati alipotembelea sehemu mbali mbali zinazotoa huduma katika kituo cha Afya Bumbwini Kiongwe,Jimbo la Bumbwini Wilaya ya Kaskazini B,Mkoa wa Kaskazini Unguja,baada ya kukifungua jana,katika shamra shamra za miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL ASAINI KITABU CHA MAOMBOLEZO YA KIFO CHA ALIYEKUWA WAZIRI WA FEDHA DKT. WILLIAM MGIMWA


  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisani Kitabu cha maombolezo ya kifo cha aliyekuwa Waziri wa Fedha, Dkt. William Mgimwa, aliyefariki dunia Januari 01, 2014 huko nchini Afrika ya Kusini alikokuwa amelazwa kwa matibabu. Dkt. Bilal alifika kuhani msiba huo nyumbani kwa marehemu Mikocheni B, jijini Dar es Salaam, leo jioni. 
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete, akisani Kitabu cha maombolezo ya kifo cha aliyekuwa Waziri wa Fedha, Dkt. William Mgimwa, aliyefariki dunia Januari 01, 2014 huko nchini Afrika ya Kusini alikokuwa amelazwa kwa matibabu. Dkt. Bilal alifika kuhani msiba huo nyumbani kwa marehemu Mikocheni B, jijini Dar es Salaam, leo jioni.
 Pia wageni wengine walipata fursa ya kusaini kitabu cha maombolezo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwafariji wanafamilia wa marehemu Dkt. Mgimwa, wakati alipofika kuhani msiba huo nyumbani kwa marehemu Mikocheni B, jijini Dar es Salaam, leo jioni.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimfariji mke wa marehemu Dkt. Mgimwa, Jane Mgimwa, wakati alipofika kuhani msiba huo nyumbani kwa marehemu Mikocheni B, jijini Dar es Salaam, leo jioni.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwafariji wanafamilia wa marehemu Dkt. Mgimwa, wakati alipofika kuhani msiba huo nyumbani kwa marehemu Mikocheni B, jijini Dar es Salaam, leo jioni.
Baadhi ya Mawaziri na wabunge waliofika kuhani msiba huo nyumbani kwa marehemu Mikocheni B,

CHARLES BONIFACE MKWASA NA JUMA PONDAMALI WAANZA KUKIFUA KIKOSI CHA WANAJANGWANI


 Kocha mpya wa makipa wa timu ya Yanga, Juma Pondamali (kushoto) akimfanyisha mazoezi kipa wa timu hiyo, Juma Kaseja wakati wa mazoezi yanayofanyika kwenye Uwanja wa Bora Kijitonyama jijini Dar es Salaam. Pondamali na Boniface Mkwasa, wameteuliwa kukinoa kikosi hiho baada ya kutimuliwa aliyekuwa kocha mkuu kutimuliwa mwishoni mwa mwezi uliopita.
Kocha mpya wa Yanga, Charles Mkwasa (kulia) akiwafua wachezaji wakati wa mazoezi yao yanayoendelea kwenye Uwanja wa Bora Kijitonyama, Dar es Salaam. Kocha huyo ameteuliwa kuchukua mikoba ya kocha mkuu aliyetilimuliwa mwishoni mwa mwezi ulipoita.

TEMEKE QUEENS YATWAA KOMBE LA TAIFA CUP BAADA YA KUIFUNGA MOROGORO QUEENS








TIMU ya mchezo wa pete ya mkoa wa Temeke imefanikiwa kutetea ubingwa wake wa mashindano ya Taifa Cup, baada ya kuifungaMorogoro mabao 52-38 kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Temeke walianza kuliandama lango la Morogoro  tangu robo ya kwanza ya mchezo kwani walikwenda mapumziko wakiwa mbele kwa mabao 15 na Morogoro  wakiwa na mabao 7 pia Temeke walizidi kung’aa kwenye robo ya pili baada ya kuifunga Morogoro  mabao 12 kwa 8.

Kwenye robo ya tatu Morogoro  walizidi kupotea  na kujikuta wakifungwa mabao 14 kwa 10 na robo ya nne ya kukamilisha mchezo Morogoro walizinduka na kuifunga Temeke mabao 17  kwa 14. 

Morogoro hawatamsahau GS wa Temeke Mwanaidi Hassan kwani ndiye alikuwa mwiba mchungu kwa kutumbukiza mabao mengi  katika mchezo wao.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu alisema kuwa Temeke wanafanya vizuri na watatetea ubingwa wake kutokana na maandalizi mazuri walioyafanya 

Naye Mwenyekiti  wa Chama cha Netbali (CHANETA) Anna Kibira alimpongeza na wafadhili waliojitoa kukisaidia Chama chake na kuomba wadau wengine kujitokeza kuisaidia timu ya Taifa “Kilimanjaro Queens” inayokwenda kwenye mashindano ya Mapainduzi.

Wednesday, January 1, 2014

SAIDI MBELWA ALIPIZA KISASI KWA K,O RAUNDI YA 5 ALIYOPIGWA KWA POINT NA AMBOKILE CHUSA 2010





Bondia Said Mbelwa  kushoto akimchachavya Amokile Chusa wakati wa mpambano wao wa kufungua mwaka Mbelwa alishinda kwa K,O ya raundi ya tano mwaka 2010 mbelwa alipigwa kwa pointi na Chusa hivyo kulipiza kisasa kwa K,O ya raundi ya tano Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Mabondia Ambokile Chusa kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Saidi Mbelwa wakati wa mpambano wao wa kushelekea mwaka mpya uliofanyika katika ukumbi wa Zulu Paredaise pugu kirumba mbelwa alishinda kwa K,O ya raundi ya tano hii ni mara ya pili kukutana ambapo mara ya kwanza mwaka 2010 mbelwa alipigwa kwa pointi na chusa picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Twaribu Mchanjo kushoto akioneshana umwamba wakutupiana makonde na Shabani Mtengela wakati wa mpambano wao wa kuukaribisha mwaka 2014 uliofanyika katika ukumbi wa zulu paraies pugu kirumba Mchanjo alishinda kwa pointi picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Twaribu Mchanjo kushoto akimshambulia kwa makonde Shabani Mtengela wakati wa mpambano wao wa kuukaribisha mwaka 2014 uliofanyika katika ukumbi wa zulu paraies pugu kirumba Mchanjo alishinda kwa pointi picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Shabani Mtengela akiwa chini oi baada ya kupewa konde zito na TWARIBU MCHANJO WAKATI WA MPAMBANO WAO PICHA NA www.superdboxingcoach.blogspot.com

cheka na pambano la urusi.



Awali ya yote napenda kuwapongeza na kuwatakia heri na fanaka ya mwaka mpya wa 2014.

pia ninamuomba mwenyezi mungu awape afya na nguvu mpya katika majukumu yanayow
akabili katika mwaka huu mpya.

Ndg waandishi organaizesheni ya ngumi za kulipwa nchini tanzania TPBO-LTD,inawashukuru waandishi wote ambao wamehusika katika kuripoti taarifa za shughuri za tpbo katika mwaka uliopita,wapo ambao waliripoti kwa ufasaha na wapo ambao walilenga kutuingiza katika changamoto sizizo na uhakika kwa maslahi ya vyombo vyao kibiashara lakini yote hayo tpbo ilizichukulia kama ni promotion za kuikuza TPBO,ninawashukuru wote.


Sasa napenda kutowa ufafanuzi kuhusu kichwa cha habari hapo juu ili wale wanaoandika bila kutafuta ukweli wa mambo katika mwaka huu mpya wasirudie makosa yao ya kuandika habari za uzushi.


TPBO-LTD imekuwa ikishutumiwa na baadhi ya watu wasiojuwa hata taratibu za ngumu za kulipwa kuhusu safari ya bondia francis cheka kwenda kupigana nchini urusi hapo dec 21.


ukweli ni huu ambao mimi nauweka hadharani kwenu japo wengi wenu hamkuniomba nifanye hivyo.


Bondia francis cheka alituarifu mimi na rais wa PST ndg emanuel mlundwa kwamba anakabiliwa na matatizo makubwa sana ambayo yameathiri kwa kiasi kikubwa biashara zake za ujasiria mali na anadaiwa na Benki ya posta TPB ,Pia NMB, na kwamba nyumba yake nzuri ambayo ndiyo aliifanya dhamana katika mikopo hiyo ingeuzwa muda mfupi ujao ili kulipia deni hilo.


hivyo alitaka msaada wetu kama viongozi wake.


tulilichukuwa wazo na matatizo yake kwa uzito mkubwa sana ,hasa tukifikiria kwamba tutafanyeje ili kuokowa familia
yake.na matatzo ya kukosa makazi.

Kwa bahati nzuri haikuchukuwa muda mrefu wakala wa masumbwi raia wa kenya FRNKLYN IMBENZI alibahatika kupata pambano nchini russia lililomtaka bondia francis cheka akapambane huko pambano lisilo la ubingwa.

Kwa kweli hakukuwa na makubaliano kati ya francis cheka na wakala huyo IMBENZI kuhusu malipo,kwani imbenzi alimwambia cheka angelipwa usd 8000 tu.

Baada ya imbenzi kushindwana maelewano na cheka ilibidi ampatie namba yangu promota wa russia mr maxx ,


max alinipigia simu kuhusu azma yake ya kumpatia cheka pambano,na nikamwambia pesa ambazo anataka kumlipa cheka ni kidogo mno, promota aliongeza dola 2000 zaidi na kuwa dola 10000m za kimarekani.


Baada ya makubaliano hayo nilimuaru atume mkataba ,na alituma mkataba kweli kupitian e-mail yangu hii ninayoitumia.


kwa kuwa sikuwa na pesa za kulipia visa ya urussi kwa wakati ule,nilimpigia simu rais wa PST ndg emanuel mlundwa kumueleza kama anazo pesa za kumsaidia cheka apate visa na bima ya safari na amsaidie cheka.


mambo yote hayo wakati yanafanyika bondia mwenyewe francis cheka alitowa ushirikiano wa hali ya juu ikiwa ni pamoja na kuongozana na rais wa PST mpaka ubalozi wa urusi kwa ajili ya kulipia visa na bima ya safari.


Kwa kuwa kiutaratibu mashirikisho mawili hayawezi kumuandikia kibali bondia kupigana nje ya nchi kwa pambano linalomhusu promota mmoja ,TPBO iliachia kazi ya kumpatia kibali cheka ifanywe na PST,Pia kwa ridhaa ya bondia mwenyewe cheka.


PST ilimpatia bondia cheka kibali na akaenda kupigana hali akijuwa wazi kwamba yeye ni bingwa na akijuwa matokeo mabaya hasa ya kupigwa KO yatagharimu ubingwa wake kupotea,


aliahidi angejitahidi kupigana kufa na kupona lakini bahati haikuwa upande wake kama siku zote amepoteza pambano na ubngwa,lakini ameweza kuyatatuwa matatizo makubwa yaliyomkabili na anaendelea kufanya kazi kama zamani kama mjasiria mali ,bondia mwenye kiwanda.


Naomba muelewe yote yaliyofanyika kuhusu bondia francis cheka tulikuwa tunayajadili kwa pamoja ,PST,TPBO,NA CHEKA MWENYEWE.


Ninashangazwa sana na kauli za watu wanaojifanya wana uchungu na bondia cheka kupoteza ubingwa wake ,nawauliza katika matatizo yaliyomkabili cheka ingekuwa wao ndiyo viongozi je wangeachia mali za bondia zipigwe mnada wa mabenki ili abaki na ubingwa hali wakijuwa wazi kwamba mtaji wa masikini ni nguvu zake mwenyewe? au walitaka bondia aadhirike na wamcheke?


TPBO-LTD inaamini kabisa kwamba katika ngumi za kulipwa kokote duniani bondia anajiwakilisha mwenyewe kama mfanyabiashara na haiwakilishi nchi kama watu wasioelewa wanavyotaka kuliingiza suala hili liwe la kisiasa wakati siyo pahala pake.


NGUMI ZA RIDHAA NDIZO HUWAKILISHA NCHI NA NDIYO MAANA ZINASAIDIWA NA SERILKALI KWA KIASI KIKUBWA SANA KOTE DUNIANI.


SIONI  KAMA KUNA  MTU AMBAYE ALIPASWA KULALAMIKA KWA CHEKA KUPOTEZA UBINGWA WAKE KAMA BABA YAKE MZAZI CHEKA, LAKINI ALITUSHUKURU SANA KWA KUMSAIDIA MTOTO WAKE KUPATA PESA ZA KULIPIA MIKOPO BENKI,NA AENDELEE NA BIASHARA ZAKE.


NA HATA CHEKA MWENYEWE ALISIKIKA KUPITIA REDIO CLOUDS AKITAMKA WAZIWAZI KWAMBA KAMA KUNA WATU WANADHANI MIKANDA YA UBINGWA INAPIKWA NA KUWA CHAKULA ,WAENDE AKAWAPATIE WAIFANYE CHAKULA,YEYE ANACHOHITAJI NI PESA KUTOKANA NA KAZI YAKE YA ULINGONI ,


TENA LA KUSHANGAZA ZAIDI NI KATIKA WANAOLALAMIKIA HILI WAMO MAPROMOTA MATAPELI WA KIMATAIFA AMBAO VYOMBO VYENU VIMEWARIPOTI KWA KUWADHULUMU MABONDIA WA KIGENI NA MPAKA KUKAMATWA NA POLISI.


KWA BAHATI MBAYA LEO HII BAADHI YA WAANDISHI WANAANDIKA HABARI ZAO ZA UPOTOSHAJI BILA HATA KUWAHIMIZA WALIPE MADENI YA MMAREKANI,NA WATANZANIA WANAOWADAI ,NAJIULIZA JE NI SABABU YA KITU KIDOGO?


NAWAKUMBUSHA NDG WAANDISHI KWAMBA UMAARUFU WA TPBO-LTD MMEUTENGENEZA NYINYI KUTOKANA NA KUSAIDIANA VYEMA KATIKA UPASHANAJI WA HABARI ,LAKINI ISIWE SABABU YA KILA LIFANYIKALO KWENYE NGUMI ZA KULIPWA NI TPBO-LTD


VIKO VYOMBO VINGINE VINAFANYA KAZI IFANYAZO TPBO-LTD.


TPBO-LTD INAAMINI KUWA;-


BONDIA FRNCIS CHEKA NA UMRI ZAIDI YA MIAKA 18


[1]BONDIA FRANCIS CHEKA ALISAINI MKATABA WA KUPIGANA RUSSIA BILA KULAZIMISHWA


[2] ALIKABIDHI PASSPORT KWA BALOZI WA URUSSI ILI AGONGEWE VISA BILA KULAZIMISHWA

 [3] BONDIA FRNCIS CHEKA ALICHUKUWA TAX TAREHE 17 DEC AKIELEKEA UWANJA WA NDEGE WA JULUS NYERERE HALI AKIWA NA AKILI TIMAMU NA HAKULAZIMIWHWA NA YEYOTE  [4]BONDIA FRANCIS CHEKA ALIINGIA NDANI YA NDEGE YA KLM BILA KULAZIMISHWA ,AKIJUWA WAZI ANAPITIA AMSTERDAM ,NA ATABADILISHA NDEGE PALE NA KUELEKEA URUSI KWA HIYARI YAKE MWENYEWE.

[5]BONDIA FRANCIS CHEKA ALIPANDA ULINGONI NCHINI RUSSIA KWA HIYARI YAKE MWENYEWE BILA KULOAZIMISHWA.



NINAWAOMBA WOTE WANAOJARIBU KUUPOTOSHA UMMA KATIKA HILI WAWACHE KWANI UWONGO WAO HAUTAIBOMOWA TPBO-LTD.

BALI WANAIZIDISHIA UMAARUFU SANA.

WANAPOTEZA MUDA WAO BURE BILA MAFANIKIO


NA TPBO-LTD TUNAAMINI KABISA KWAMBA KUANDIKWA VIZURI AU KUSEMWA VIBAYA KUPITIA VYOMBO VYA HABARI YOTE HAYO NI PROMOTIONS KWETU ,TUTAHESHIMU YOTE KATI YA HAYO DAIMA MILELE.

                          AHSANTENI SANA
                         IMELETWA KWENU NAMI;
                   YASSIN ABDALLAH MWAIPAYA-USTAADH

MBUNGE WA CHADEMA IRINGA MJINI AMFAGILIA RAIS KIKWETE KATIKA KUHAKIKISHA KATIBA MPYA INAPATIKANA.




Mbunge  wa jimbo la  Iringa Mjini,Mh.Peter Msingwa amefanya mkutano hapo jana katika  viwanja vya Mwembetogwa,  mkoani humo.
Mkutano huo ambao ulikuwa wa kufungia mwaka 2013 ,Msigwa pia aliutumia mkutano huo kwa kuwapongeza baadhi  ya  mawaziri ambao utendaji kazi wao unaonekana kuwa mzuri,akiwemo   Waziri wa Wizara ya Maji na  Naibu Wake ,Waziri wa Ujenzi na  Waziri wa Mazingira  ambao wameonesha  msimamo wa kweli katika  kuwatumikia  wananchi .

katika hatua nyingine  mbunge Msigwa  amemshukia aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chadema,Zitto  Kabwe na kusema kuwa anatafuta umaarufu binafsi  kuliko  kukijenga chama  chake na  kuwa  hana nia njema  na CHADEMA,hivyo amewataka Wanachadema wa jimbo la Iringa mjini kutomsikiliza huku akibainisha kuwa Mwanachama na Kiongozi mzuri ni  yule ambae  anafanya kazi ya  kukijenga chama chake na  si kujijenga  yeye binafsi.


Amesema  kuwa iwapo  Zitto hatotaka kumsikiliza mwasisi wa Chama  hicho, Mzee Mtei  wala  kuwasikiliza viongozi wa juu wa chama  hicho akiwemo  mwenyekiti wa katibu mkuu, ni  wazi hakitakii mema CHADEMA,na wana Chadema hawana budi kumpuuza kiongozi na mwanachama yeyote mwenye lengo la kuua chama.


Kuhusu rasimu ya Katiba,   Mbunge  Msigwa amempongeza Rais Kikwete  kuwa ameonyesha ushujaa wa hali ya juu  katika kupigania  upatikanaji wa katiba mpya, na  kuwa  iwapo  wabunge wa CCM watapinga  wao kama Chadema  watarudi kwa wananchi   kuhamasisha  kupiga kura ya kuikataa  katiba  itakayopendekezwa na wabunge wa CCM.

Aidha Msigwa ameongeza kusema kuwa atakuwa mstari wa mbele kuikosoa serikali kama itaonekana kuwa na viongozi dhaifu huku akiwataka watanzania kutathimini yale yote waliyofanya mwaka 2013 na kuwatakia kheri ya mwaka mpya.

TASWA FC YAANZA MWAKA MPYA KWA KUICHAPA TWANGA PEPETA 1-0



 Beki wa timu ya Taswa Fc Sufianimafoto (kulia) akiwania mpira na mshambuliaji wa Twanga Fc, wakati wa mchezo wa kirafiki wa Bonanza la kufunga mwaka na kuukaribisha mwaka mpya wa 2014, lililofanyika kwenye Viwanja vya Leaders Club Kinondoni, leo jioni. Katika mchezo huo Taswa ilianza mwaka mpya kwa ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na Juma Pinto katika kipindi cha pili.
 Mshambuliaji wa Taswa Fc, Juma Pinto (katikati) akiwatoka mabeki wa Twanga Pepeta Fc, wakati wa mchezo huo.
 Beki wa Taswa Fc, Athuman (kulia) akiwatoka wachezaji wa Twanga Pepeta.
 Winga wa Taswa Fc, Zahro Milanzi (kulia) akimiliki mpira......
 Kocha wa Twanga Pepeta Fc, ambaye pia ni Mkurugenzi wa bendi hiyo Asha Baraka, akitoa mawaidha kwa wachezaji wake wakati wa muda wa mapumziko.
 Wachezaji wa Taswa Fc, wakimsikiliza Kocha mchezaji Ally Mkongwe, wakati wa mapumziko.
 Benchi la Twanga likiwa haliamini kilichotokea uwanjani...
 Hapa utaenda wewe mpira utabaki.........tulia kama ulivyooooo.....
 Hapiti mtu hapa........
 Mwamuzi wa mchezo huo akichezesha huku akiwa na chupa ya soda ya Novida iliyo na kinywaji cha Konyagi ndani yake......