BAO pekee la mapema la Amri Kiemba liliisaidia Simba kufuzu robo fainali
ya michuano ya Kombe la Mapinduzi kuungana na Azam ambayo leo
itakamilisha ratiba kwa kuvaana na Ashanti United katika mechi za kundi
C.
Kiemba alifunga bao hilo akimalizia kwa kichwa pasi ya Ally Badru na kuwa bao lake la pili katika michuano hiyo na mawili kwa Simba ambayo imemaliza mechi za makundi usiku wa jana kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mabingwa wa visiwani, KMKM ikifikisha pointi 7.
Azam ambao ni mabingwa watetezi wa michuano hiyo wenyewe walikuwa wa kwanza kufuzu hatua hiyo baada ya kuongoza kwenye kundi lake la kupata ushindi mara mbili mfululizo na leo itaumana na Ashanti walioingizwa dakika za jioni baada ya Yanga kuchomoa kushiriki mashindano hayo.
Ashanti yenyewe ina pointi moja kutokana na mechi mbili.
Nyingine zilizofuzu hatua hiyo ni KCC ya Uganda, iliyoongoza kundi B lenye timu ya Simba, KMKM na AFC Leopards ya Kenya iliyoaga mashindano.

No comments :
Post a Comment