Abiria
waliokwama na treni Dodoma wakisubiri mabasi kwa ajili ya usafiri wa
kuelekea kwenye mikoa ya Morogoro na Dar es saalam ambapo shirika la
Reli limewakodia mabasi kutokana na kushindwa kuendelea na safari
kutokana na Mafuriko Gulwe na Godegode wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma.
Abiria
hao wakiwa hawajui la kufanya kutokana na kukosa chakula katika
stesheni ya reli mkoani Dodoma walipotangaziwa kuanza kusafirishwa kwa
mabasi lakini mpaka kufikia leo jioni zaidi ya abiria 900 kati ya 1600
walikuwa bado hawajapatiwa usafiri huo.
Mfanyakazi wa shirika Reli kituo cha Dodoma akibandika tangazo katika ubao wa matangazo lililowataka abiria waliokuwa wanaelekea mikoa ya kanda ya ziwa kurudishiwa nauli zao kutokana na usafiri wa treni kusitishwa kwa muda usiojulikana.
Askari
wa kuzuia Ghasia (FFU) wakiangalia usalama kwa abiria wa treni
waliokwama kutokana na treni kushindwa kuendelea na safari tangu juzi
mara baada ya kufika kituo cha reli mkoani Dodoma kutokana na mvua
iliofunika reli wilayani Mpwapwa.
No comments :
Post a Comment