Vyama
vya ngumi za kulipwa nchini vimekubali kuungana na wenzao TPBO
kushiriki mkutano wa mapromota wa ngumi na mabondia wote wa Tanzania.
Mkutano huo unaotarajiwa kufanyika katika ukumbi wa vijana Kinondoni,
siku ya jumamosi tarehe 1/2/2014 kuanzia saa nne asubuhi. Mkutano huo
ulioitishwa na TPBO chini ya udhamini wa KITWE GENERAL TRADERS ukiwa na
lengo la kuweka mikakati ya sasa na ya baadae kwa ajili ya kuinua ngumi
za hapa nchini,sanjali na kutambulikana kwa mapromota na mabondia
wenyewe kwa kutengenezewa vyeti maalum na vitambulisho, vitakavyowafanya
watambulike katika jamii ya wanamasumbwi wa hapa Tanzania na hata nje
ya mipaka ya nchi yetu,hizo ni sehemu ya mada zitakazozungumzwa.
Ibrahim
kamwe akizungumza na vyombo vya habari ,alisema ‘Mkutano huo ambao
utawahusisha mapromota wote ,pamoja na viongozi wa vyama vya ngumi za
kulipwa,makocha na mabondia wote wa ngumi za kulipwa, haijalishi wewe ni
nani ili mradi ni mwalimu wa ngumi, mratibu wa ngumi au bondia ni vema
ukafika katika mkutano huo ambao ni mara ya kwanza kufanyika katika
historia ya ngumi za kulipwa kuwakutanisha kwa pamoja waratibu, viongozi
na mabondia wa nchi nzima kwa pamoja, pia mkutano huo utaendana na
mapromota kupewa vyeti na kurekebisha usajili wa mabondia ambao usajili
wao haujakaa sawa.
No comments :
Post a Comment