Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Tuesday, June 3, 2014

BOMOABOMOA KITUO CHA DALDALA MWENGE





 Hivi ndivyo kituo cha Daladala cha Mwenge kilivyo bomolewa asubuhi ya leo
 Hiki kilikuwa Choo cha kulipia kilichokuwa Mwenge nacho kikiwa kimebomolewa
 Ulinzi ukiwa umeimarishwa
 Kazi ya Kubomoa na kuondoa vibanda ikiwa inaendelea Mwenge

 Hili lilikuwa eneo la kupumzikia zamani la Abiria kungoja usafiri nacho kikiwa kimebomolewa

Monday, June 2, 2014

COSMAS CHEKA AMSHINDA KWA K,O RAUNDI 10 SUMA NINJA MOROGORO



Bondia Cosmas Cheka akiwa na mkanda wake baada ya kumtwanga bondia Suma Ninja kwa k,o ya raundi ya kumi jana picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Jems Bondi kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Richard Lucas wakati wa mpambano wao uliofanyika katika ukumbi wa vijana socil hall morogoro Lucas alishinda kwa point picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Bondia Suma Ninja kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Cosmas Cheka katika ukumbi wa vijana socil hall morogoro Cheka alishinda kwa k,o ya raundi ya kumi mpambano huo picha na
Baadhi ya mashabiki wakifatilia mchezo huo
Bondia Cosmas Cheka kushoto akioneshana umwamba na Suma Ninja wakati wa mpambano wao uliofanyika jana morogoro cheka alishinda kwa k,o ya raundi ya kumi picha na

Mwili wa Mama Yake Mbunge wa Kigoma Zitto Kabwe Wasafirishwa Kwenda Kigoma


Zitto kabwe akiwa na Prof  Ibrahimu Lipumba wakati wa kuuaga Mwili wa mama yake kipenzi Bi Shida Salumu aliyefariki leo kabla ya kusafirishwa kwenda Kigoma kwa mazishi
Ndege Ikiandaliwa Ili kuweza Kuingiza Mwili wa Marehemu Mama yake Zitto Kabwe
Waheshimiwa Wabunge na Baadhi ya Viongozi wakibeba Jeneza lililobeba Mwili wa Marehemu Mama Yake Zitto Kabwe Bi Shida Salum  kuingiza kwenye ndege Tayari kwa safari ya kwenda Kigoma Kwenye mazishi

Prof Ibrahimu Lipumba akijadili jambo na Mwenzie baada ya kupakia mwili wa marehemu kwenye ndege kuelekea kigoma Kwenye maziko

Kili music tour yavunja rekodi Mwanza



 Vanessa Mdee na Fid Q wakishirikiana kutoa burudani wakati wa show ya Kilimanjaro Music Tour iliyofanyika katika Uwanja wa Kirumba na kuwavutia maelfu ya mashabiki. Ziara hii inadhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager.
Wakazi wa Mwanza wakiwa wamefurika kwa maelfu huku wakishangilia wakati kundi la Weusi likitumbuiza  katika show ya Kilimanjaro Music Tour iliyofanyika katika Uwanja wa Kirumba na kuwavutia maelfu ya mashabiki. Ziara hii inadhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager.
 Msanii wa Bongo flava, Ben Pol akitumbuiza maelfu ya wakazi wa Mwanza wakati wa show ya Kilimanjaro Music Tour iliyofanyika katika Uwanja wa Kirumba na kuwavutia maelfu ya mashabiki. Ziara hii inadhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager.
 Msani wa muziki wa dance, Christian Bella akikonga nyoyo za wakazi wa Mwanza katika show ya Kilimanjaro Music Tour iliyofanyika katika Uwanja wa Kirumba na kuwavutia maelfu ya mashabiki. Ziara hii inadhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager.
 Msanii wa bongo flava, Fid Q akizungumza na wakazi wa Mwanza wakati akitumbuiza katika show ya Kilimanjaro Music Tour iliyofanyika katika Uwanja wa Kirumba na kuwavutia maelfu ya mashabiki. Ziara hii inadhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager.
Vanessa Mdee na Ommy Dimpoz wakimakinika katika show ya Kilimanjaro Music Tour iliyofanyika katika Uwanja wa Kirumba na kuwavutia maelfu ya mashabiki. Ziara hii inadhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager.

DIAMOND APAGAWISHA NA KUWEKA HISTORIA NEW JERSEY



 All Star Club Elizabeth New Jersey Diamond akikamua licha ya show kuchelewa kuanza na wapenzi wa Diamond kushikwa na jazba wakitaka aendelee lakini ikashindika kutokana na muda wa kufunga club kufika. 
 AJ nae akifanya yake baada ya kupewa nafasi ya ufunguzi katika show hiyo iliyofanyika New Jersey.
AJ Ubao na Dirty Hary wakishambulia jukwaa kwenye show ya kufungua pazia iliyoanyika New Jersey na baadae Prezidaa wa Wasafi, Diamond Plutnumz kuwapagawisha mashabiki wake wa ukanda wa pwani ya mashariki.

TAIFA STARS YASONGA MBELE KWA JUMLA YA MABAO 3-2 DHIDI YA ZIMBABWE, SASA KUKUTANA NA MSUMBIJI



 Pichani (kulia) ni Winga wa timu ya Taifa, Taifa Stars, Simon Msuva, akimtoka beki wa Zimbabwe, wakati wa mchezo huo uliopigwa jana, jijini Harare.
**************************************
TIMU ya Taifa Taifa Stars, jana imefanikiwa kusonga mbele katika michuano ya kuwania kufuzu Kombe la Mataifa Afrika (Afcon 2015) baada ya kulazimisha sare ya mabao 2-2 dhidi ya Zimbabwe.

Kwa matokeo hayo sasa Stars imesonga mbele kwa jumla ya mabao 3-2 kutokana na ushindi wa bao 1-0 katika mchezo wa awali uliopigwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Baada ya kutinga katika hatua ya pili sasa Stars inatarajia kukutana na Msumbiji wiki mbili zijazo ambapo ikifanikiwa kupita hatua hiyo itaingia katika hatua ya makundi.

Mabao yaliyoiwezesha Stars kusonga mbele katika mchezo wa jana yalifungwa na Nahodha wa timu hiyo Nadir Haroub 'Canavaro' katika dakika ya 26, na Thomas Ulimwengu katika dakika ya 46, huku mabao ya wenyeji yakifungwa na Danny Phiri katika dakika ya 13 na Willad Katsande katika dakika ya 55.

Baada ya kumalizika dakika 90 za mchezo huo, Mwamuzi aliongeza dakika saba, lakini bado hali ilionekana kuzidi kuwa ngumu kwa wenyeji waliokuwa wakitafuta bao la kuongoza ili angalau kujaribu kujitetea kwa matuta.

Katika mchezo ujao unaoikabiri Stars, iwapo Msumbiji wakitolewa Stars itatinga moja kwa moja katika kundi F lenye timu za Zambia, Cape Verde na Nigeria.
 Wachezaji wa Taifa Stars wakijipa morali ya ushindi kabla ya kuanza kwa mtanange huo dhidi ya Zimbabwe jana. 
 Sehemu ya mashabiki wa Taifa Stars walioambatana na timu na baadhi ya Watanzania waishio Harare, wakishangilia kuisapoti Taifa Stars jana.
 Kiungo wa Taifa Stars, Frank Domayo akimtoka beki wa Zimbabwe.

Sunday, June 1, 2014

TANGAZO BUJINGA TRADERS




Machinga complex (Karume stadium)
3rd floor, E4
P.O. Box 43063, Dar es Salaam
Tel: +255 754 623320 / +255 784 623320

Deals with: Promotional Materials as Large format printing (flex & rigid), embroidery, screen printing, heat press, graphics & design, corporate giveaways, vehicle branding, offset printing & sign boards

PICHA ZA GARI ALILOKUWEMO MAREHEMU TYSON WAKATI WAKITOKA MKOANI DODOMA NA KUPATA NALO AJALI



IMG_4162
Marehemu Geogre Tyson pichani hapa alikuwa yupo kijiji cha Chilonwa Chamwino kwenye utoaji wa madawati katika shule ya msingi Chaula iliyopo Dodoma. Baada ya kumaliza shughuli hii huku akiwa kama producer wa The Mboni Show mauti yalimkuta majira ya saa 12 jioni masaa 4 tu toka tuanze safari ya kurudi Dar es Salaam maeneo fulani hivi kama unataka kukaribia GAIRO mjini.
Katika gari hilo walikuwa watu 8 ila yeye pekee ndio aliyepoteza maisha na wengine kupata majiraha mwilini pamoja na dereva wa gari hilo. Kwa sasa mwili wa marehemu umehifadhiwa Morogoro katika  hospital ya mkoa Morogoro, baadae asubuhi mwili utaanza safari ya kuelekea Dar es Salaam.
IMG_4166 IMG_4213IMG_4214IMG_4215
Kweli ajuae mwisho wetu ni Mungu pekee. Tunaishi kama vile tunajua maisha yetu yataisha lini kumbe tunajidanganya. Haya matukio yote ni kwa ajili yetu kuamka na kujifunza kitu. Tumrudieni Mungu, tuungame dhambi zetu maana hakuna ajuae siku wala saa yake itakuwa lini. R.I.P Tyson na wote mliotutangulia.
Picha zote kutoka DJ Choka Music.

USAILI WA SHINDANO LA TANZANIA MOVIE TALENTS KWA KANDA YA PWANI WASITISHWA HADI HAPO TUTAKAPOWATANGAZIA



 Baadhi ya wadau wa Tanzania Movie Talents wakijadiliana Jambo Kwa ajili ya Kusitisha Usaili wa Dar Kutokana na Msiba uliotokea wa Muongozaji Mahiri wa Vipindi na Filamu Tanzania, Marehemu George Tyson.
 Majaji wa Shindano la Tanzania Movie Talents, Single Mtambalike na Roy Sarungi wakijadiliana jambo kutokana na Kufiwa na Mmoja wa Jaji katika Shindano hilo Vyonne Cherry
Washiriki waliofika wakipewa maelekezo kuhusiana na kusitishwa kwa usaili wa Shindano la Tanzania Movie Talents kwa Kanda ya Pwani

SERIKALI YATOA ZAIDI YA SHILINGI 6.7 BILIONI KUJENGA HOSPITALI YA RUFAA SINGIDA.



DSC_0473
Katibu Mkuu wa CCM Taifa Abdulrahamani Kinana akiongozwa na Mkuu wa Moa wa Singida Dk, Parseko Kone, Katibu Tawala Lianna Hassan na viongozi wengine wa Mkoa wa Singida  kukagua hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida, wakati Kinana alipokuwa Mkoani Singida kwa ziara ya kikazi ya siku saba.(Picha na Zainul Mzige wa modewjiblog).
Na Nathaniel Limu, Singida
MKUU wa Mkoa wa Singida,Dk.Parseko Vicent Kone amesema serikali imetoa zaidi ya shilingi 6.7 bilioni kwa ajili ya kugharamia ujenzi wa hospitali ya rufaa ya mkoani hapa iliyoko kijiji cha Madewa nje kidogo ya Singida mjini.
Dk.Kone amesema hospitali hiyo itakapokamilika,itahudumia wagonjwa kutoka mikoa yote ya kanda ya kati.
Mkuu huyo alitoa rai hiyo wakati akitoa akitoa taarifa yake kwa katibu mkuu CCM taifa,Abrahamani Kinana aliyetembelea hospitali hiyo hivi karibuni.
Amesema mkoa umetegewa eneo la ekari 283 kwa ajili ya uendelezaji wa mradi wa hospitali hiyo, ambayo itakuwa ya mfano hapa nchini.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk Dorothy Gwajima amesema lengo la mradi huo ni kuimarisha huduma za afya mkoani pamoja na mikoa jirani.
DSC_0429
 Katibu Mkuu wa CCM akiweka saini kwenye kitabu cha hospitali ya Rufaa huku Naibu Katibu Mkuu wake Mwigulu Nchemba na mkuu wa Mkoa wa Singida Kone wakishuhudia.
Dk.Gwajima amesema mradi huo utakapomalizika,utakuwa na majengo 29 yatakayotumika kutoa huduma mbali mbali.
Mganga huyo mkuu,amesema changamoto inayowakabili ni pamoja na uhaba wa watumishi,nyumba za kuishi watumishi na ufinyu mdogo wa bajeti ya dawa kutoka bohari kuu ya madawa (MSD).
Kwa upande wake Kinana,alitumia fursa hiyo kumpongeza Dk.Kone kwa utendaji kazi wake ambao umesaidia kujengwa kwa hospitali hiyo.
DSC_0446
 Mganga mkuu wa hospitali ya Mkoa wa Singida (RMO) Bi. Doroth Bwajima akisoma taarifa ya ujenzi wa hospitali hiyo.
Amesema baada ya mradi huo kukamilika mkoa wa Singida utaondokana na matatizo ya huduma za afya.
"Ili kumuunga mkono Dk.Kone kwa hili jambo nzuri la ujenzi wa hospitali ya rufaa ambayo itasaidia Watanzania wengi kupata huduma ya afya kwa kiwango kizuri,nitahakikisha nina muunganisha na baadhi ya marafiki zangu wa ndani na nje ya nchi ili waweze kusaidia kumalizika kwa ujenzi wa hospaitali hii inayovutia",amesema Kinana.
DSC_0453
 Mganga mfwawidhi wa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida, Dkt Joseph Malunda, akiwaonesha michoro ya hospitali hiyo viongozi walioambatana na Kinana.
DSC_0463
Viongozi mbalimbali wa mkoa huo wakimsikiliza Dkt Malunda.
DSC_0481
 Muuguzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida Pendael Maasai akisisitiza jambo kwa Kinana.
DSC_0499
Muuguzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida Pendael Maasai akimwonyesha Katibu Mkuu kinana vifaa mbalimbali vilivyopo kwenye hospitali hiyo ya rufaa.
DSC_0506
Mbunge MO akiangalia mojawapo ya vifaa vya hospitali ya rufaa ya singida.
DSC_0496
Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini Mohammed Dewji akisalimiana na Daktari bingwa wa magonjwa ya kina mama wa mkoa wa Singida Dkt, Seleman Mutani wakati wa ukaguzi wa hospitali hiyo.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AZINDUA MFUKO WA ELIMU WA HALMASHAURI YA MJI WA KIBAHA



 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mfuko wa Elimu wa Halmashauri ya Mji wa Kibaha Mkoa wa Pwani, iliyofanyika kwenye Uwanja wa Kibaha Mailimoja leo, Mei 31, 2014.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akivishwa Skafu na vijana wa Scout wa mji wa Kibaha, wakati alipowasili kwenye uwanja wa Mailimoja Kobaha, kwa ajili kuzindua Mfuko wa Elimu wa Halmashauri ya Mji wa Kibaha Mkoa wa Pwani, leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na baadhi ya viongozi wakati akiwasili uwanjani hapo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisimama na viongozi waliokuwa meza kuu kwa ajili ya kupokea maandamano ya wanafunzi wakati wakiingia kwenye uwanja huo leo wakati wa uzinduzi wa Mfuko wa Elimu wa Halmashauri ya Mji wa Kibaha mkoa wa Pwani, uliofanyika kwenye Uwanja wa Mailimoja Kibaha.

NITATUMIA MSHAHARA WANGU WA BUNGE KUSOMESHA YATIMA KISARAWE-JAFO



Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akimnadi Seleman Said Jafo wakati wa kampeni za uchaguzi.

KWA wabunge wengi wanaomaliza muda wao wa miaka mitano ya kuwatumikia wananchi wao baada ya kuchaguliwa katika uchaguzi mkuu uliopita, wakati muda ukizidi kuyoyoma, matumbo yao yako moto kwa hofu ya kutojua majaaliwa yao, kama watarejea tena mjengoni au la.
Mbunge wa Kisarawe mkoani Pwani, Seleman Said Jafo.
Lakini hata hivyo, wapo baadhi yao ambao baada ya kufanikiwa kwa kiwango kikubwa kukidhi matakwa ya wapigakura wao, hivi sasa hawana wasiwasi wa kutetea tena nafasi zao, kwani wamefanikiwa kwa kiwango kikubwa kuondoa kero, sambamba na kutimiza ahadi mbalimbali walizoahidi.
Miongoni mwa wabunge hao ni Seleman Said Jafo wa Kisarawe mkoani Pwani, ambaye pamoja na kuwa hii ni mara yake ya kwanza kuingia bungeni, lakini ametatua kero nyingi ambazo wananchi wa jimbo lake walikuwa nazo kwa kipindi kirefu kilichopita.
“Ninaweza kusema nimejitahidi kiasi cha asilimia 90 ya ahadi nilizoahidi kwa wapiga kura wangu nimetekeleza, wananchi wa Kisarawe ni mashahidi wa suala hili, nadhani nimetimiza wajibu wangu kama Mbunge,” alisema Jafo katika mahojiano maalum hivi karibuni.
Akizungumzia kuhusu sekta ya afya, mbunge huyo alisema wakati akiingia madarakani, aliikuta hospitali ya wilaya hiyo, iliyojengwa mwaka 1975, ikiwa chakavu kiasi kwamba hata chumba maalum cha kuhifadhia maiti kilishindwa kufanya kazi na kuwalazimu wananchi wake kupeleka maiti kuhifadhiwa katika Hospitali za Temeke na Amana.
Lakini kwa sasa hali imekuwa tofauti kwani imefanyiwa ukarabati mkubwa na sehemu zote muhimu, ikiwemo mochwari zimetengenezwa.
Alisema wakati akipata ubunge, wilaya yake ilikuwa na zahanati 14, lakini katika kipindi chake, amewaongoza wananchi wake kuongeza zingine nane.
Katika moja ya vituo hivyo vipya vya afya vilivyojengwa, kile kilichopo Kijiji cha Chole kiliivutia hata kamati mojawapo ya Bunge wakati ilipokitembelea na kusema kilikuwa ni kizuri na mfano wa kuigwa kwani ndani yake kina wodi maalum ya wazazi, kikiwa kimegharimu kiasi cha shilingi milioni 37.
Alilipongeza Shirika  la Plan International kwa kuwa karibu na wananchi katika sekta ya afya kwani lilinunua vitu vyote muhimu katika wodi ya wazazi.
Alisema shirika  hilo limesaidia Kituo cha Afya Masaki, Zahanati  ya Kijiji cha Kisanga, gari  la  kubebea wagonjwa Wilaya ya  Kisarawe, vitu vyote hivyo vikiwa na thamani ya shilingi 1.2 bilioni, achilia mbali mafunzo maalum ya kiafya kwa  watumishi wa vituo  hivyo.
Akielezea mafanikio zaidi katika sekta hiyo, alisema uhusiano wake mzuri na Kairuki Foundation, alipata msaada wa gari la wagonjwa katika Kituo cha Afya Masaki kilichopo Kijiji cha Masangu.
Kuhusu maji, mbunge huyo mwenye umri wa miaka 41, alisema kero hiyo ilikuwa kubwa na iliwapa shida mno wananchi wa Kisarawe, lakini  kwa  jitihada zake amefanikisha  mradi mkubwa wa maji  wenye  thamani ya sh.mil. 540 ambao pia umefadhiliwa na Plan International  kwa  kushirikina  na serikali.
Aidha, kwa ushirikiano mzuri  na benki ya dunia, amefanikisha ujenzi wa visima katika vijiji tisa huku serikali ya China ikiwa katika ujenzi wa visima 30.
Plan International pia wamehusika katika mradi  mkubwa wa usambazaji maji mitaani katika Kijiji cha Gwata kwa kutumia chanzo cha mto Ruvu na wameweza kukamilisha  mradi mkubwa wa maji wenye  thamani ya shilingi milioni 375 uitwao Kuruyumatayo.
Katika miundombinu ya barabara, mbunge huyo alisema mkakati uliopo ni kuhakikisha kila mtaa unapitika na hivi sasa ujenzi unaendelea kuanzia Kisarawe mjini kwenda Maneramango na vijiji vya jirani.
“Udongo wa Kisarawe ni  mbaya sana hasa wakati wa mvua na ndiyo maana pia nguvu  nyingine nimeihamishia ili kupata  barabara yenye kiwango safi,” alisema na kusisitiza kuwa lengo ni kuwa na barabara za lami jimbo zima.
Kuhusu ulinzi na usalama, mbunge huyo alisema hiyo ni changamoto kubwa kwake, kwani kituo kikuu cha polisi jimboni kwake hakina ubora unaotakiwa.
“Rais Jakaya Kikwete alipofika hapa Oktoba mwaka jana, moja ya kilio nilichompa ni kituo cha polisi cha kisasa na nyumba za askari wake, alilichukua na linafanyiwa kazi,” alisema.
Juu ya upatikaji wa nishati ya umeme, mbunge huyo alisema wakati akiingia madarakani, ni vijiji vinne tu ndivyo vilivyokuwa na huduma hiyo muhimu, lakini katika kipindi chake, amepanua upatikanaji wa umeme hadi kufikia vijiji 26 kati ya 79 wilayani hapo.
Hadi kufikia 2015 anaamini vijiji vingi zaidi vitapata umeme.
Akilizungumzia Bunge Maalum la Katiba, alikerwa na kejeli, matusi na vijembe vinavyoendelea, kwani hilo siyo jambo walilotumwa na wananchi.

Alitaka sheria zitumike kuwabana wabunge wa namna  hiyo, ili mijadala ipate nafasi kubwa ya kufanyiwa kazi, huku akisisitiza kuwa muundo wa muungano wa serikali mbili ndiyo unaofaa na kuhitajiwa na watu wengi.
Amewaasa wajumbe wa bunge hilo kuzingatia kanuni ili kufikia matarajio ya utungwaji wa katiba mpya ambayo itawaongoza Watanzania kwa miaka mingi ijayo.
Alitumia nafasi hiyo kuwaomba wananchi wa Kisarawe kumpa tena nafasi hiyo katika uchaguzi ujao ili aendelee kufanya mambo makubwa.