Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Thursday, November 24, 2011

KOMBAINI YA SIMBA NA YANGA KUCHEZA NA ASANTE KOTOKO MIAKA 50 YA UHURU

Anayezungumza ni mwenyekiti mtendaji wa kampuni ya future century limited, Helen Masanja, kushoto kwake ni mwenyekiti wa Yanga Loyd Nchunga na Amini Bakhresa mwenyekiti wa chama cha soka mkoa wa Dar es Salaam, DRFA.

TIMU ya soka ya Kumasi Asante kotoko ya Ghana inatarajiwa kuwasili nchini Desemba 9 tayari kucheza mchezo mmoja wa kirafiki dhidi ya kombaini ya timu za Yanga na Simba siku ya Desemba 11 kwenye uwanja wa Taifa.

Mchezo huo ni sehemu ya kukamilisha maadhimisho ya sherehe za miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania na maandalizi yake yamekwisha kamilika kwa mujibu wa mwenyekiti mtendaji wa kampuni ya Future Century Limited, Helen Masanja.

Masanja alisema kuwa timu hiyo itafikia Zanzibar na baadaye kuja jijini Dar es Salaam kwenye hotel ya Lamada tayari kwa mchezo huo ambao umedhaminiwa na PPF, Kenya Airways, Vanedrick Tanzania Limited, Lamada Hotel na Vanne Fashion Tabata.

Alisema kuwa wanatarajia kuwa na burudani ya aina yake kwani tayari kombaini ya timu ya Yanga na Simba itaundwa na wachezaji nyota wanaocheza Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu huu.

Aliongeza kuwa makocha wawili, mkongwe, Abdallah “King Mputa” Kibaden na Fred “ Minziro” Felix ndiyo watakuwa wakuu wa benchi la ufundi la timu hiyo ambayo itaundwa na wachezaji 20 watakaotangazwa hapo baadaye.

Wengine katika benchi la ufundi na meneja, Boniface Pawasa na daktari wa timu, Juma Sufiani.Alifafanua kuwa uteuzi wa timu hiyo hautajali uraia wa wachezaji hivyo kama wachezaji kutoka nchi za nje ambao wanachezea timu hizo watateuliwa, basi watacheza mchezo huo.

Masanja alisema kuwa Yanga na Simba zimekubaliana na kuweka historia kwa mara ya kwanza tangu timu hizo zitengane mwaka 1935.

Alisema kuwa historia inaonyesha kuwa timu hizo zilikuwa pamoja kuanzia mwa 1922.Mwenyekiti wa Yanga Lyod Nchunga alisema kuwa mechi hiyo itaondoa tofauti iliyopo baina ya mashabiki wa Simba na wale wa Yanga hasa zinapotokea timu hizo zinacheza mechi za kimataifa ambapo imekuwa ni kawaida mashabiki wa timu hizo kushangilia timu pinzania.

Wakati Nchunga akisema hayo, Katibu Mkuu wa Simba, Evodius Mtawala alisema kuwa muungano huo utaleta tija kwa timu hizo ambapo mashabiki wa Simba na Yanga siku hiyo watakuwa kitu kimoja kwa ajili ya kuishangilia timu yao tofauti na ilivyokuwa miaka ya nyuma.Alisema kuwa huu ndiyo mwanzo wa kuanza kushirikiana katika mechi za kimataifa na kuwataka mashabiki kufika kwa wingi na kutoa sapoti kubwa kwao.

Wednesday, November 23, 2011

Diamond Trust Bank yazindua tawi Mbeya

Diamond Trust Bank yazindua tawi Mbeya

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro katikati akikata utepe kuashilia uzinduzi wa Diamond Trust Bank Mbeya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Habbas Kandoro katikati akiwa na Maofisa wa Bank hiyo baada ya uzinduzi

WANAHABARI WAHUDHURIA KILINIKI YA TUSKER CECAFA CHALLENGE CUP 2011 DICC



Mkurugenzi wa Mashindano katika Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) Bw. Saad Kawemba akizungumza wakati wa kliniki ya mashindano ya Shirikisho la Vyama Vya Michezo Afrika Mashariki CECAFA yanayojulikana kama (TUSKER CACAFA CHALLENGE CUP 2011) inayofanyika kuanzia asubuhi hii kwenye ukumbi wa mikutano wa DICC PPF Tower jijini Dar es salaam, ambapo waandishi wa habari watakaoandika habari za mashindano hayo kutoka nchi mbalimbali ukanda wa Afrika Mashariki wanahudhuria na kupata maelezo mbalimbali .
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama Vya Michezo Afrika Mashariki CECAFA Bw. Nicholas Musonye akitoa mada katika Kliniki hiyo, mbele ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari kutoka ukanda wa Afrika Mashariki.
Kulia ni Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama Vya Michezo Afrika Mashariki CECAFA Bw. Nicholas Musonye na Meneja wa bia ya Tusker inayozalishwa na kampuni ya Serengeti Breweriers Ritah Mchaki wakifuatilia jambo, wakati Mkurugenzi wa Mashindano wa TFF Saad Kawemba alipokuwa akitoa mada yake na kukaribisha waandishi mbalimbali waliokuja nchini kwa ajili ya kuandika habari za mashindano ya TUSKER CACAFA CHALLENGE CUP 2011.
Washiriki wa Kliniki hiyo wakiandika mambo muhimu yaliyokuwa yakitolewa na watoa mada katika kliniki hiyo.
Wanahabari wakifuatilia kwa umakini mkubwa mambo mbalimbali yaliyojiri katika kiliniki hiyo.
Wanahabari wakifuatilia kwa umakini mkubwa mambo mbalimbali yaliyojiri katika kiliniki hiyo.
zaidi tembelea http://fullshangwe.blogspot.com/

PROF. TIBAIJUKA AWACHACHAMALIA WALIOVAMIA MAENEO YA WAZI SINZA



Waziri wa Ardhi Nyumba na Makazi Prof. Anna Tibaijuka wa pili kutoka kulia akiangalia ramani halisi inayoonyesha maeneo ya wazi wakati alipokagua maeneo ya wazi yaliyovamiwa na wananchi maeneo ya Sinza E wilaya ya Kinondoni, ambapo pia alikuwa akikagua mabango yaliyowekwa kwa ajili ya kuataarifu wananchi na kuwaelimisha maeneo ambayo ramani inaonyesha yako wazi kwa ajili ya mipango ya maendeleo ya Serikali.
Diwani wa Sinza Bw. Renatus Pamba akimuonyesha Waziri wa Ardhi Nyumba na Makazi Prof. Anna Tibaijuka maeneo ya wazi yaliyovamiwa na wananchi katika maeneo ya Sinza E wengine ni waandishi wa habari walioongozana na Waziri Tibaijuka.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Makazi Prof. Anna Tibaijuka akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukagua maeneo ya wazi yaliyovamiwa na wananchi katika maeneo ya Sinza E leo mchana.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Makazi Prof. Anna Tibaijuka akiongea na mkazi wa Sinza Ndahani Yohana ambaye amenunua eneo la wazi kwa utapeli kwa shilingi milioni 500 wiki mbili zilizopita, ambapo ramani halisi inaonyesha eneo hilo ni la wazi.

BENKI YA POSTA YAZINDUA HUDUMA YA "TPB POPOTE"



Waziri wa Fedha, Mustafa Mkulo (katikati) akibonyeza simu ya mkononi ikiwa ni ishara ya kuzindua huduma ya TPB POPOTE, ambayo inamwezesha mteja kupata taarifa mbalimbali, kununua muda wa maongezi, luku na kutuma na kuweka fedha. Kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania, Sabasaba Moshingi, ambaye anaangalia Projector ili kuangalia taarifa za Waziri Mkulo na kulia ni mfanyakazi wa benki hiyo. Uzindunzi huo ulifanyika kwenye hoteli ya Kilimanjaro Hyatt Regency jijini Dares Salaam leo. PICHA NA MAGRETH KINABO - MAELEZO
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania, Sabasaba Moshingi, akizungumzia kuhusu uzindunzi wa huduma ya TPB POPOTE ulifanyika kwenye hoteli ya Kilimanjaro Hyatt Regency jijini Dares Salaam leo
Kikundi cha burudani cha Simba Theatre akitoa burudani wakati wa uzinduzi wa baada ya uzindunzi wa huduma ya TPB POPOTE ulifanyika kwenye hoteli ya Kilimanjaro Hyatt Regency jijini Dares Salaam leo.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania, Sabasaba Moshingi, ( kushoto) akimsikiliza kwa makini Posta Master Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania, John Mndeme(kulia ) anayesisitiza jambo mara baada ya uzindunzi wa huduma ya TPB POPOTE ulifanyika kwenye hoteli ya Kilimanjaro Hyatt Regency jijini Dares Salaam leo.
Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya Posta Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa watendaji mara baada ya uzindunzi wa huduma ya TPB POPOTE ulifanyika leo kwenye hoteli ya Kilimanjaro Hyatt Regency jijini Dares Salaam.

Monday, November 21, 2011

Ngumi kupigwa Desemba 18,MZALENDO PUB




Na MWANDISHI WETU

WASANII mbali mbali hapa nchini wanatarajiwa kutoa burudani katika pambano la mchezo wa ngumi lisilo na ubingwa litakalowakutanisha bondia, Mada Maugo na mpinzani wake Suleimani Saidi 'Toll' Desemba 18 mwaka huu katika Ukumbi wa Mzalendo Pub Kijitonyama JIjini Dar es Salaam.

Akizungumza na kona hii ya burudani Raisi wa shirikisho la ngumi za kulipwa hapa nchini (PST) Emanuel Mlundwa alisema, maandalizi kwa ajili ya pambano hilo yamekamilika.


Aliwataja wasanii watakaotoa burudani siku hiyo kuwa ni Kundi la mapacha watatu Khalid Chokoraa (Halidi Chuma)pamoja na msanii wa mziki wa bongo fleva Mwana FA (Hamisi Mwinjuma).

Alisema licha ya kuwepo kwa burudani hizo vile vile atakuwepo kocha wa mchezo wa ngumi Rajabu Mhamila Super D kwa ajili ya kutoa mafunzo kupitia Dvd pamoja na kuzisambaza.

Aliwataka mashabiki wao wajitokeze kwa wingi kushuhudia burudani hiyo, licha ya kuwa mchezo huo haupewi kipaombele watahakikisha wanasonga mbele katika kuazimisha miaka 50 ya uhuru.

aidha katika mapambano ya ngumi ya utangulizi mabondia Yohana Miyayusho na Shadrack Juma, Doto Kipacha atazidunda na Saidi Muhidini na kwa upande wa mchezo wa Kick Boxing ambao utatuwakilisha kimataifa Tanzania Muaythai Academy of Combat watawaletea mpambano kwa mara ya kwanza nchini kati ya bondia Emanuel Shija kutoka Tanzania na Munyeshyaka Vincent kutoka Rwanda Mpambano huo utakuwa wa kimataifa kutokana na ushiriki wake wa nchi hizo mbili nchini zitakuwa zikipeperusha bendera zao.

Bendi ya Twanga Pepeta kufanya shoo London kwa mara nyingine





Mwandishi wetu
BENDI ya muziki wa dansi ya African Stars “Twanga Pepeta International” itafanya onyesho kwa mara ya pili nchini Uingereza Jumamosi hii.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa kampuni ya Afrikan Stars Enterteinment (ASET), Asha Baraka alisema kuwa jumla ya wasanii 13 wanatarajiwa kwenda huko kwa ajili ya kusherehekea miaka 50 ya Uhuru na Watanzania wahishio huko.
Baraka alisema, wanamuziki wao wanatarajiwa kuondoka Ijumaa na shoo itafanyika Jumamosi kwenye ukumbi wa Silver Spoon, Wembley bendi hiyo ikiwa huko itaendelea kufanya shoo zake kama kawaida nchini.
Mara ya kwanza kwa bendi hiyo kufanya shoo ilikuwa mwaka 2007 ambapo ilifanya shoo kwa wiki tatu katika miji mbali mbali mikubwa duniani.
Alisema, mgeni rasmi katika shoo hiyo anatarajiwa kuwa Balozi wa Tanzania wa Uingereza ambaye ni Peter Kallaghe na maandalizi yanaendelea vizuri ya safari hiyo.
“Kama unavyofahamika kuwa Tanzania tulitawaliwa na Waingereza na huko wapo Watanzania wanaohishi huko tumeona ni vyema tukaenda kuungana nao wenzetu kwa ajili ya kusherehekea miaka 50 ya Uhuru, alisema Baraka.
“Wasanii wanaoenda huko ni 13 na wengine watabaki kuendelea na shoo kama kawaida kwenye kumbi mbalimbali kwenye viwanja vya Leaders tutaungana na Msondo Ngom,” alisema Baraka.

VODACOM YAKABIDHI WASHINDI WA MEGA PROMOSHENI ZAWADI ZAO



Baadhi ya washindi wa promosheni ya Mega inayoendeshwa na Vodacom Tanzania nchi nzima wakiwa na Televisheni aina ya Samsung LCD walizojishindia na kukabidhiwa jana katika hafla iliyoambatana na tamasha la wazi la burudani katika ufukwe wa bahari ya Coco - Oysterbay jijini Dar es salaam.
Meneja Mauzo wa Vodacom Tanzania Kanda ya Pwani Henry Tzamburakis kulia, akimkabidhi hundi yenye thamani ya shilingi milioni 11 mshindi wa Promosheni ya Mega Bw.Said Mbegu inayoendeshwa na Vodacom Tanzania nchini,Jumla ya washindi 16 kila mmoja walikabidhiwa hundi zao hapo jana,anaeshuhudia katikati ni Mkuu wa Vodacom Kanda ya Pwani Atilio Lupala.Hafla ya kmakabidhiniano ilifanyika jana katika ufukwe wa bahari ya Hindi jijini Dar es salaam.
Mmoja wa wasanii Spider Man(Yombo Chaka) akisherehesha kwa kutembea juu ya kamba wakati wa tamasha la burudani la wazi lililoandaliwa na kampuni ya Vodacom Tanzania jana katika ufukwe wa bahari ya Coco jijini Da res salaam kwa lengo la kutoa zawadi za fedha na televisheni kwa washindi wa promosheni ya Mega inayoendeshwa na kampuni hiyo nchini. Jumla ya washindi kumi na sita kila mmoja alikabidhiwa shilingi milioni 11.
Mkuu wa Vodacom Tanzania Kanda ya Pwani Atilio Lupala mwenye suti nyeusi akimpa hongera Bw.Alex Barush ambae ni mmoja wa washindi wa promoheni ya Mega aliyejishindia Televisheni aina ya Samsung LCD wakati wa hafla ya utoaji wa zawadi kwa washindi mbalimbali iliyofanyika jana kwenye ufukwe wa bahari ya Coco jijini Dar es salaam
Meneja Mauzo wa Vodacom Tanzania Kanda ya Pwani Henry Tzamburakis (kulia) akimkabidhi mshindi wa promosheni ya mega Televisheni aina ya Samsung LCD Bw.Alex Barush aliyejishindia kwenye promosheni hiyo ya Vodacom inayoendelea nchini kote. Zawadi kwa washindi mbalimbali wanaotokeoa mikoa ya Pwani zilikabidhiwa jana katika hafla iliyoambatana na tamasha la lawazi la burudani katika eneo la Ufukwe wa Coco jijini Dar
Mmoja wa wasanii Spider Man(Yombo Chaka) akisherehesha kwa kutembea juu ya kamba wakati wa tamasha la burudani la wazi lililoandaliwa na kampuni ya Vodacom Tanzania jana katika ufukwe wa bahari ya Coco jijini Da res salaam kwa lengo la kutoa zawadi za fedha na televisheni kwa washindi wa promosheni ya Mega inayoendeshwa na kampuni hiyo nchini. Jumla ya washindi kumi na sita kila mmoja alikabidhiwa shilingi milioni 11.

MBUNGE WA MBEYA MJINI JOSEPH MBILINYI AKA MR. SUGU Azungumza NA WANAHABARI



Waziri kivuli wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo (kulia) Joseph Mbilinyi a.k.a Mr, SUGU akionyesha kitabu ambacho ameelezea maisha yake kitakachopatikana wakati wa Shoo ijulikanayo Anti Virus katika Tamasha la Burudani kwa washabiki2011 litaakalofanyika Nov. 26,2011 jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali pamoja na wadau wa michezo, (kushoto) ni Msanii Fred Malaki a.k.a. MKOLONI. ( _Picha na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO,)
Waziri kivuli wa Wizara ya Habari,Vijana ,Utamaduni na Michezo Joseph Mbilinyi (a.k.a. MR. SUGU -alievalia kadeti) leo akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam 21-nov-2011 kuhusu shoo ijulikanyo Anti Virus wakati wa Tamasha la Burudani kwa washabiki 2011-i litalaofanyika jijini DSM hapo Nov. 26 na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali pamoja na wananchi,(kushoto) ni Msanii Fred Malaki (a,k,a- MKOLONI) n a Mwanadada Zainab Lipangile a.k.a ZAY –B, Katika tamasha hilo Wasanii mbalimbali watatumbuiza, -Picha zote na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO,
Msanii Suma g akiimba mbele ya wana habari katika mkutano uliofanyika kwenye ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo jijini Dar es salaam leo.
Mheshimiwa Nchimbi mgeni rasmi uzinduzi wa Albamu ya Anti Virus 2
Gradice Sigera
Maelezo
Dar es Salaam
Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Dkt.Emanuel Nchimbi anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa albamu ya wanamuziki wa kizazi kipya inayoitwa Anti Virus 2.
Akizungumza na wanahabari Jijini Dar es Salaam mratibu wa uzinduzi huo ambaye pia ni Mbunge wa Mbeya mjini, Joseph Mbilinyi alisema uzinduzi wa albamu hiyo unalengo la kuwakomboa vijana waweze kunufaika na kazi zao.
Mheshimiwa Mbilinyi amesema kwa muda mrefu wasanii wa muziki wa kizazi kipya wamekuwa wakizulumiwa na wajanja wachache kitu ambacho kimewaacha wasanii hao kuendelea kuwa maskini.
"Kuna wajanja wachache ambao kwa muda wa miaka mingi wamekuwa wakinufaika na jasho la wasanii sasa tumeamua kufanya mapinduzi kwa kuwaungunisha wasanii ili waweze kutetea haki zao".Alisema Mheshimiwa Mbilinyi.
Uzinduzi huo unatarajiwa kufanyika katika viwanja vya Chuo cha Ustawi wa Jamii tarehe 26 Novemba kuanzia saa 12-6 usiku ambapo jumla ya wasanii zaidi ya 20 watashiriki ikiwa ni pamoja na waheshimiwa wabunge na mawaziri ambapo kiingilio kitakuwa ni shilingi 5000.
Katika tamasha hilo Mheshimiwa Mbilinyi atauza kitabu kinachoelezea historia ya maisha yake ambacho kitauzwa kwa shilingi 5000.

UZINDUZI WA MIAKA 10 YA KUZALIWA KWA CHUO KIKUU CHA TAIFA ZANZIBAR (SUZA)



Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) Prof.Idris Ahmada Rai akifafanua jambo mbele ya waandishi wa Habari ambao hawapo pichani katika uzinduzi wa Sherehe za kutimiza Miaka 10 ya Chuo hicho, kushotoni kwake ni Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma Dk. Abdallah Ismail Kanduru
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) Prof.Idris Ahmada Rai akizindua CD ya Utafiti wa Mabadiliko ya Tabia ya Nchi katika Visiwa vya Zanzibar kwa Waandishi wa Habari katika hafla iliyofanyika Chuoni hapo Vuga Mjini Zanzibar.
Mmoja kati ya Waandishi wa Habari akiuliza Swali kwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) Prof.Idris Ahmada Rai ambaye hayupo pichani katika uzinduzi wa Sherehe za kutimiza Miaka 10 ya Chuo hicho kwenye hafla iliyofanyika katika Ukumbi wa Chuo hicho Vuga Mjini Zanzibar.
PICHA ZOTE NA Yussuf Simai-Maelezo Zanzibar

SHOO KALI YA BURUDANI KUPIGWA Novenba 26



Mwimbaji wa Mziki wa KIzazi Kimpya ambaye ni Mbunge wa Mbeya Mjiji, Josephe MBilinyi (Sugu) katikati akizungumza na waandishi wa habari Dar es salaam leo kuusu tamasha la burudani kwa mashabiki litakalofanyika, Novenba 26 katika viwanja vya ustawi wa jamii Kijitonyama (kushoto) ni msanii Fred Malik (Mkoloni) na Zainabu Lipagile (Zay B)

BENDI YA TWANGA PEPEPA KUKAMATA WAUZA CD FEKI NCHINI


Mkurugenzi wa bendi ya Afrikan Stars 'Twanga Pepeta' Asha Baraka (kushoto) akiwaonesha waandishi wa habari (hawapo pichani) CD feki aliyouziwa, Dar es salaam leo ambapo amesema kwa kushirikia na na Kampuni ya Msama watahakikisha wanawasaka na kuwakamata watu wote wanaodurufu kimakosa kazi za wasanii na kuwafikisha mahakamani kwa wizi kulia ni Meneja wa Utawala wa bendi hiyo, Hassani Rehani

Ngumi kupigwa Desemba 9, DDC Keko Dar es Salaam



BONDIA wa ngumi za kulipwa nchini, Ramadhan Nassib, anatarajia kupanda ulingoni kuzichapa na mpinzani wake Antony Kariuki wa Kenya, katika pambano la maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru litakalopigwa kwenye Ukumbi wa DDC Keko Dar es Salaam, Desemba 9 mwaka huu. Akizungumza Mratibu wa pambano hilo, Pius Aghaton, alisema kuwa pambano hilo linatarajiwa kuwa na upinzani mkali kutokana na rekodi zilizopo kwa mabondia wote. Alisema kuwa pambano hilo litakuwa la uzito wa Fly ambalo litapigwa katika raundi 10. “Tumeandaa pambano la aina yake kwa ajili ya kusherekea miaka 50 ya Uhuru na pia kuweza kuwajengea mabondia wetu uwezo wa kucheza mapambano ya kimataifa” alisema. Mratibu huyo alisema kuwa katika pambano hilo, kutakuwa na mapambano ya utangulizi ambapo bondia Juma Fundi atazichapa na Juma Seleman katika pambano la uzito wa Fly la raundi sita, Fred Sayuni atazipiga na Bakari Dunda katika pambano la uzito wa Feather la rfaundi sita. Pambano jingine litawakutanisha mabondia Rashid Ally pamoja na Daud Mhunzi katika pambano la uzito wa Feather la raundi sita na Faraji Sayuni atazichapa na Alpha George katika pambano la uzito wa Fly la raundi nne. Katika Mchezo huo kutakua na DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi pamoja na kutambua sheria zake mbalimbali zitakazokua zikisambazwa na kocha wa mchezo huo Rajabu Mhamila 'Super D Boxing Coach' kwa ajili ya kuwapa mambondia mbalimbali mbinu za mchezo na mashabiki kujua sheria za masumbwi. Super D alisema katika DVD hizo kutakuwa na mapambano mengi ambayo yanaweza kutumika kama mafunzo muhimu kwa mabondia ,makocha marefa pamoja na mashabiki wa mchezo kujua sheria mbalimbali. '' Kuna mapambano kama ya akina Amir Khan, Manny Paquaio, Floyd Maywhether, David Haye, Mohamedi Ali pamoja na mtanzania Roja mtagwa anaefanya shughuli zake Marekani, DVD hizo ni nzuri na hata walio tayari katika mchezo huo wanatakiwa kujua sheria na mafunzo ya ngumi mana zinafundisha mambo mengi '' alisema Super D DVD hizo za mafunzo zinapatikana makutano ya barabara ya Uhuru na Msimbazi au katika kambi ya ngumi ILala na klabu ya AShanti nayo ya Ilala.

WATANZANIA WANAOISHI UJERUMANI ! WAANZA KWA KASI! KUSHEREKEA MIAKA 50 YA UHURU WA TANGANYIKA



Watanzania wanaoishi nchini Ujerumani wanaanza kusherekea sherehe za miaka 50 ya uhuru wa Tanzania bara,
kwa vishindo na vilivyochanganyika na shangwe zisizo mfano, kuwa siku ya Jumamosi 3 -12-2011 Uzinduzi wa.
sherehe hizo utaanzia mjini München,katika mtaa wa Siebold Str,11,majira ya saa 10 alhasiri, na usiku bendi maarufu ya
muziki wa dansi Ngoma Africa Band wanatarajiwa kutumbuiza katika sherehe hizo za kihistoria.
Huko Mjini Berlin ,ambako ndio makao makuu ya ujerumani,kuanzia siku ya 9.Dec.2011 mji huo utatingishika na
sherehe hizo siku ya JUMAMOSI 10 Dec 2011 ndio siku ambayo watanzania na marafiki wa watanzania,wakiwemo
wahisani ,watajimwaga uwanjani kusherekea miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania bara, bendi ya muziki kikosi kazi cha
NGOMA AFRICA BAND aka FFU ambacho kinatazamiwa kumwaga burudani ya muziki kitakuwepo uwanjani,
katika usiku usiokucha, Ngoma Africa band pia wanatamba na CD mpya ya "Shangwe 50 Uhuru Anniversary",
ambayo imeshaanza kutingisha katika vituo mbali mbali vya Redio ndani na nje ya Tanzania,unaweza kusikiliza pia hapa
WATANZANIA WANAOMBWA KUJITOKEZA KWA WINGI ! Kama wahenga wanavyosema
CHEREKO ! CHEREKO ! NA MWENYE MWANA !

SHEREHEKEA MIAKA 50 YA UHURU NA FILAMU YA C.P.U MLIMANI CITY 25/11/2011



WAKATI tukielekea katika kusherekea miaka 50 ya Uhuru wetu, ni wakati wako wa kuburudika na kufurahia filamu bora kabisa ya CPU kuanzia tarehe 25 novemba 2011, filamu hiyo iliyotengenezwa na kampuni ya Haak Neel Production kwa kushirikiana na Wegos Works zote za Jijini Dar es Salaam ni filamu ya kipekee, na ni filamu ya kwanza kushirikisha wanataaluma wengi katika tasnia ya filam

VODACOM FOUNDATION YAJENGA MADARASA MAWILI IRINGA



.Haya ndiyo madarasa mawili yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 29 yaliyojengwa na Vodacom Tanzania kwa kupitia mfuko wake wa kusaidia jamii”Vodacom Foundation” kwa ajili ya shule ya sekondari ya Lipuri ya mkoani Iringa.
Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania Kanda ya Kusini Jackson Kiswaga akiongea na wazazi na wanafunzi wa kata ya Kalenga Mkoani Iringa wakati wa hafla ya kuwakabidhi msaada wa madarasa mawili yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 29 kwa shule ya sekondari ya Lipuri ya mkoani humo ,yaliyojengwa na Vodacom Tanzania kupitia mfuko wa kusaidia jamii”Vodacom Foundation”Kulia ni Afisa Elimu wa Sekondari za Wilaya ya Iringa William Mkangwa na Mkuu wa Vodacom Foundation Yessaya Mwakifulefule.

Wazee wa kabila la Kihehe, kata ya Kalenga mkoani Iringa wakimpa heshima ya kichifu Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania Kanda ya Kusini Jackson Kiswaga kwa kumkabidhi mkuki baada ya kumvisha vazi la mgorole ikiwa ni heshima kubwa kwa mkoa huo wakati walipofika kukabidhi madarasa mawili yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 29 katika shule ya sekondari ya Lipuri mkoani humo.

Afisa Elimu wa Sekondari za Wilaya ya Iringa William Mkangwa akikata utepe kuashiria kupokea msaada wa madarasa mawili yenye thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 29 yaliyojengwa na Vodacom Tanzania kwa kupitia mfuko wake wa kusaidia jamii”Vodacom Foundation”kwa ajili ya shule ya sekondari ya Lipuri, iliyopo kata ya Kalenga mkoani Iringa, wakishuhudia kutoka kushoto ni Mkuu wa Vodacom Foundation Yessaya Mwakifulefule,Mkurugenzi wa Vodacom Kanda ya kusini Jackson Kiswaga,Diwani wa kata ya Kalenga Ameria Galinoma na diwani viti maalum Shakila Kiwanga.
Mkuu wa mfuko wa kusaidia Jamii wa Vodacom Tanzania Yessaya Mwakifulefule akiteta jambo na mmoja wa wanafunzi wa shule ya sekondari ya Lipuri iliyopo kata ya Kalenga mkoani Iringa Agness John,mara baada ya kukabidhi msaada wa madarasa mawili yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 29 yaliyojengwa na Vodacom Tanzania kupitia mfuko huo.Akishuhudia watatu kutoka kulia ni Mkuu wa shule hiyo Alex Mwakiyanga akiwa na walimu wa shule hiyo.

Sunday, November 20, 2011

Mashindano ya ngumi ya Kova Cup yamalizika


Bondia Mussa Mohamedi (kulia) akimfulumusha makonde mfululizo, Fadhili Hassani wakati wa mpambano wa mashindano ya Kova Cup yaliyomalizika, Dar es salaam jana Mussa alishinda kwa K,O ya raundi ya tatu.(Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com)
Mabondia wa kike Mariamu Edwer (kushoto) na Matha George wakipambana wakati wa mashindano ya Kova Cup yaliyomalizika, Dar es salaam, jana Matha alishinda kwa ponti.(Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com)

SAFARI YA TIMU YA TAIFA KWENDA MALAWI YAOTA MBAWA YAGEUKA ZIARA YA MIKOA TANZANIA BAADA YA KUCHAPWA NA TIMU YA MBEYA



Wachezaji wa timu ya Taifa ya Pool, ilipokuwa ikiwasili Mkoani Iringa wakati ikiwa safarini kuelekea Malawi, ambapo safari hiyo imeota mbawa na kuwa ni ziara ya mikiani.
KAMPUNI ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager imetangaza rasmi kufutwa kwa mashindano ya 'ALL AFRICA CUP 2011-BLANTYRE- MALAWI' yaliyotarajiwa kuanza Novemba 22, hadi 26, 2011.

Akitangaza mabadiliko ya safari hiyo, Meneja wa bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo, alisema kuwa Pamoja na mashindano hayo kufutwa Bia ya Safari, imeandaa ziara ya timu ya Taifa ya Pool katika mikoa ifuatayo ya Dodoma, Manyara, Arusha, Kilimanjaro na Tanga baada ya kushauriana na chama cha mchezo huo ili kuwafanya wachezaji wa timu ya taifa kuwa katika hali ya mchezo na kufanya mazoezi baada ya kuahirishwa kwa mashindano hayo yaliyokuwa yafanyike Malawi.

Aidha imeelezwa kuwa kuahirishwa kwa mashindano hayo kufanyika Malawi kumefuatia kutokea kwa machafuko ya Kisiasa na hii itatoa nafasi kwa mikoa iliyotajwa kuiona timu yao ya Taifa na baadhi ya wachezaji wakali wa mikoa hiyo kupata nafasi ya kucheza na wachezaji wa timu yhiyo ya Taifa.

Akizungumzia na mtandao huu kuhusu mashindano hayo, Katibu wa chama cha Pool Taifa. Amos Kafwinga alisema, ”Katika mashindano ya mwaka huu ya 'ALL AFRICA CUP –MALAWI' yamefutwa kutokana sababu zilizo nje ya uwezo wa chama cha pool Africa lakini tumefarijika sana kuona kwamba Bia ya Safari Lager bado iko na sisi bega kwa bega na kuipa nafasi timu yetu kufanya ziara ya michezo ya kirafiki na timu za mikoa’’ alisema katibu.

Akitoa salam za shukrani kwa Safari Lager kwa niaba ya Chama cha Mchezo wa Pool Tanzania (TAPA), Mwenyekiti wa chama hicho, Isaac Togocho alisema “ Tulipokea taarifa za kufutwa mashindano kwa masikitiko makubwa sana kwani tulikuwa tumejiandaa vilivyo kwa ajili ya mashindano hayo, lakini nilifarijika sana kusikia kuwa wadhamini wetu SAFARI LAGER wametupa nafasi ya kujiandaa zaidi kwa kutupa michezo ya kirafiki katika mikoa

THE SHELL COVER



Cover la mzigo mpya wa THE SHELL kwa mbele linavyoonekana

Kwa nyuma
Kwa ndani ya cd

THE SHELL YATINGIA MTAANI KWA KISHINDO


Ule mzigo uliokuwa ukisubiriwa kwa hamu na wadau wengi wa tasnia hii hatimaye sasa yaingia mtaani kwa kishindo pata nakala yako original na sio feki

Karibuni wadau alafu sio vibaya kama mtanipatia maoni baada ya kuucheki mzigo huo wa THE SHELL