Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Monday, July 30, 2012

WASANII KUNDI LA MIZENGWE WATEMBEZA DVD ZAO MITAANI KUOGOPA KUCHAKACHULIWAW

Wananii wa kikundi cha Mizengwe ambao wajasiliamali wakiuza DVD zao walizozitoa kwa ajili ya kuwapa wapenzi wao burudani wakiwa nyumbani kushoto ni Mkwere na

Wasiooana wapigwa mawe hadi kufa Mali




Mji wa Timbuktu kaskazini mwa Mali
Wapenzi ambao walifanya mapenzi nje ya ndoa wamepigwa mawe hadi kufa mwishoni mwa wiki na wapiganaji wa kiislam katika mji wa Aguelhok kaskazini mwa Mali, maafisa wamesema.
Mwanamume na mwanamke huyo walizikwa mpaka kwenye shingo na kupigwa mawe hadi kufa.
Kaskazini mwa Mali nusu yake inaendeshwa na waasi wa Tuareg na wapiganaji wa Kiislam baada ya mapinduzi katika mji mkuu wa Mali.
Aguelhok katika eneo la Kidal alikuwa ni wa kwanza kukamatwa na waasi wa Tuareg .
Waislamu katika eneo la Aguelhok waliwapiga mawe mpaka kufa watu hao mbele ya watu 200 maafisa wamesema.
"Nilikuwepo. Wapiganaji hao wa Kiislamuwaliwachukua watu hao katikati ya Aguelhok. Watu hao waliwekwa kwenye mashimo mawili na wakapigwa mawe mpaka wakafa." Afisa wa serikali eneo hilo alisema.
"Mwanamke alizimia mara baada tu ya mapigo," alisema, akiongeza kuwa mwanaume alipiga kelele mara moja tu na baadaye akanyamaza.
Uasi wa Tuareg kaskazini ulichangia mapinduzi ya kijeshi mwezi Machi na kusababisha vurugu za makunbdi ya wapiganaji wa kiislam na kasha kuchukua udhibiti wa miji kadhaa ya kaskazini.
Bw Traore alisema ataongoza mazungumzo kuunda serikali ya umoja wa kitaifa nchini Mali na kuongoza juhudi za kuanzisha mazungumzo na Waislamu.
"Wananchi wa Mali hawana budi kuungana dhidi ya wavamizi,” alisema, akimaanisha wapiganaji wa kigeni wa jihadi ambao wanatuhumiwa kudhibiti eneo la kaskazini.
"Kutokana na ugumu wa mgogoro huu na ukubwa wa mateso ya watu wa Kaskazini, kwa pamoja, nasema pamoja, tunaweza kusafisha njia mbele yetu kuiweka huru nchi yetu kutoka kwa wavamizi hawa, ambao wanaacha uharibifu na huzuni, na kuwasababishia watu wetu maumivu, " alisema Bw Traore.
Kumekuwa na shutuma kutoka jumuiya ya kimataifa kwa wapiganaji wa kiislam katika mji wa zamani wa Timbuktu wakilaumiwa kwa kuharibu kumbukumbu za karne nyingi za viongozi muhimu wa dini ya Kiislam ambao wanaheshimika kwa Waislam wa madhehebu ya Sufi.

BIASHARA ITATOKA TUU ATA NIKIWA NIMELALA


Maisha popote pale iwe usiku iwe mchana mtu unaweza kujitafutia ridhiki yako ni mmoja ya wafanya biashara makutano ya Barabara ya Uhuru na Msimbazi akiwa ameuchapa usingizi huku akiwa katika biashara zake usiku wa leo wafanya biashara wengi wa machinga wamekuwa wakiwakwepa mngambo wakati wa mchana kutokana na kukamatwa na kupelekwa mahakamani kwa makosa ya kufanya bihashara hizo

BENKI YA CBA KUIPIGA JEKI SMZ KUNUNUA MELI YA KISASA



 
Afisa Mtendaji Mkuu wa benki ya CBA, Bw Yohane Kaduma  akimkabithi mfano wa hundi yenye thamani ya Tsh Millioni 5 kwa makamu wa pili wa Raisi wa Zanzibar Balozi Seif Idd, Afisa Mtendaji Mkuu wa CBA Bw Kaduma amesema benki yake iko tayari kuikopesha serikali ili iweze kununua meli mpya ili kuhakikisha inaboresha huduma za usafiri majini.Nae balozi Seif Idd ameshukuru msaada huo kutoka CBA na ametoa wito kwa wadau mbalimbali na serikali kuitembelea benki hiyo ili kuona ni jinsi gani taifa linaweza kufaidika hasa kwenye kuisaidi serikali kuboresha usafiri majini

Na Mohammed Mhina, Zanzibar

Wakati Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ikiwa kwenye mchakato wa kutafuta fedha za kununua meli mpya, Benki ya Biashara ya Afrika (CBA), imesema iko tayari kuikopesha SMZ fedha za kununulia Meli hiyo.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo Bw. Yohane  Kaduma, amesema benki yake iko tayari kuipitia SMZ mkopo wa kununulia Meli hiyo endapo watakubaliana na kushirikishwa kwenye mchakato huo.

Bw. Kaduma alikuwa akizungumza na Waandishi wa Habari mjini Zannzibar mara baada ya kukabidhi msaada wa shilingi milioni 5, kwa Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibat Balozi Seif Ali Iddi ili kusaiidia ghala za matibabu kwa majeruhi na ubani kwa wafiwa wa ajali ya Meli ya Skagit.

Bw. Kaduma amesema kuwa endapo Benk yake itaombwa kutoa mkopo huo inaweza kufanya hivyo ili mradi tu kukaa meza moja na Serikali na kukubaliana aina ya mkopo pamoja na mambo mengine.

Awali akipokea msaada huo, Makam wa pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi, amesema kuwa pamoja na kusimamishwa kwa baadhi ya meli za watu binafsi kuchukua abiria, SMZ pia imeagiza meli zake kufanyiwa uchunguzi kama zinafaa kuchukua abiria.

Balozi Seif amesema kuwa ameziagiza Mamlaka ya usafiri majini Zanzibar na Sumatra, kuzifanyia uchunguzi meli hizo za SMZ ikiwemo MV Maendeleo ambayo imerejea siku za karibuni ikitokea Mombasa nchini Kenya ambako ilikuwa katika matengenezo makubwa.

Amesema Serikali haiwezi kukaa kimya huku ikiona kuwa wananchi wake wanapatwa na majanga ya mara kwa mara kutokana na kusafiri kwa meli zisizo na uhakika.

Katika hatua nyingine idadi ya maiti za MV Skagit, imeongezaka hadi kufikia 128 baada ya maiti nyinine mbili kupatikana leo karibu na Kisiwa cha Chumbe nje kidogo ya mji wa Zanzibar na nyingine sita zikipatikana mkoani Tanga.

Tofauti na taarifa za awali kuwa maiti tano zilipatikana Bagamoyo mkoani Pwani, ifahamike kuwa maiti hizo zilipatikana katika fukwe za bahari wilayani Pangani na nyingine mjini Tanga.

Kwa mujibu wa Taarifa ya Kamanda wa Polisi mkoani Tanga ACP Costantine Masawe, maiti nne ikiwemo ya mwanamke mmoja zilipatikana huko Pangani na nyingine mbili ikiwemo ya mwanamke mmoja zikapatikana kwenye fukwe za bahari mjini Tanga.

Kamanda Masawe amesema kuwa maiti zote zilichukuliwa vipimo kwa ajili ya uchunguzi wa Vinasaba (DNA) pamoja na kupigwa picha kabla ya kuzikwa.

Hata hivyo Kamanda huyo wa Polisi amesema kuwa maiti moja kati ya hizo, ilitambuliwa kuwa ni ya Mohammed Saidi Salum  mkazi wa Ziwani Chakechake mkoa wa Kusini Pemba ambaye alitambuliwa baada ya simu aliyopatikana nayo kufanyiwa uchunguzi.

Hadi sasa maiti ambazo hazijapatikana ni 16 kutokana na kupatikana kwa watu 146 wakiwa hai ikilinganishwa na idadi ya watu 290 waliokuwemo ndani ya meli hiyo ya Skagit siku ya tukio

Walimu wagoma, wengine waukataa, waendelea na kazi


 Mwalimu wa Shule ya Msingi Mnazi Mmoja, Salma Mtili akisahihisha daftari la mwanafunzi wa darasa la nne wa shule hiyo, licha ya Rais wa Chama cha Walimu Tanzaniza (CWT), kutangaza mgomo wa walimu nchi nzima. (Picha zote na Mseto Blog)

Mwalimu wa Shule ya Msingi Mnazi Mmoja, Salma Mtili akiangalia kazi kwenye daftari la mwanafunzi wa darasa la nne wa shule hiyo, licha ya Rais awa Chama cha Walimu Tanzaniza (CWT), kutangaza mgomo wa walimu wote nchi nzima.

MAMA MWANAMWEMA SHEIN ATEMBELEA MAKAZI YA WAZEE LIMBANI LEO



 Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akimkabidhi futari Mzee wa Nyumba ya Wazee Limbani Hamadi Ali, wakati alipofika katika makazi yao kuwatembelea na kutoa  Futari kwa ajili ya mwezi mtukufu wa Ramadhani,(katikati) ni Waziri wa Ustawi wa Jamii Maendeleo ya Wanawanke na Watoto Bi Zainab Omar. Picha zote na Othman
Maulid,Pemba
 Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akizungumza na Wazee wa Nyumba ya Wazee Limbani Wete Pemba alipofika kuwatembelea na kutoa futari kwa Wazee hao leo.
 Baadhi ya Wazee wanaoishi katika  Nyumba ya Wazee Limbani Wilaya ya Wete Pemba, wakimsikiliza Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, alipofika kuwatembelea na kutoa futari kwa ajili ya Mwezi  mtukufu wa
Ramadhani leo.
MKE wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein, akiagana na Viongozi wa Wizara ya Ustawi wa Jamii,  Pemba, baada ya kuwatembelea Wazee wa Limbani Wete na kutoa Futari kwa Wazee hao leo.

GAZETI LA Mwana Halisi LAFUNGIWA



SERIKALI ya Jamhuri ya Tanzania, imelifungia gazeti la Mwanahalisi kwa muda usiojulikana kwakile kilichoelezwa kuwa na mwenendo wa kuandika habari na makala za uchozezi.
Sababu nyingine ya kufungiwa kwa gazeti hilo ni pamoja na kujenga uhasama na uzushi likiwa na nia ya kusababisha wananchi kukosa imani na vyombo vya dola hali inayoweza kuhatarisha amani na mshikamano wa nchi. 
Akisoma tamko la Serikali leo jijini Dar es salaam, Kaimu Mkurugenzi Wizara ya Habari (MAELEZO), Phabian Lugaikamu, alisema kuwa katika toleo la gazeti hilo namba 302, 303 na 304 ya mwaka 2012 na mengine yaliyotangulia yalichapisha habari na makala zenye kueneza na kujenga hofu kwa jamii.
“Mhariri wa gazeti la Mwanahalisi ameitwa na kuonywa mara nyingi lakini hataki kukiri kuwa maudhui ya makala zake hazina tija kwa jamii,pia hazifuati weledi na maadili ya taaluma ya uandishi wa habari”alisema
Aidha alisema kuwa mhariri huyo mara zote katika utetezi wake amekuwa akinukuu kifungu cha 18 cha katiba ya nchi kinachotoa uhuru wa kutoa maoni na kwa makusudi kutokunukuu kifungu ca 30 cha katiba hiyo kinachoweka ukomo wa uhuru.
“Serikali imeamua kulifungia gazeti hilo kutochapishwa kwa muda usiojulika kwa mujibu wa sheria ya magazeti ya mwaka 1976, kifungu namba 25(i),adhabu hiyo itaanza tarehe 30 julai,2012 kwa mujibu wa tangazo la serikali namba 258 lililochapishwa katika gazeti la Serikali na kutolewa jijini Dra es salaam julai 27,2012”alisema

TASWA YATOA TAMKO JUU YA WAANDISHI NA WAPIGA PICHA KUNYANYASWA WAKATI WA MECHI YA MWISHO YA FAINALI KOMBE LA KAGAME UWANJA WA TAIFA




TAMKO LA TASWA KUHUSU CECAFA

CHAMA Cha Waandishi wa Habari za Michezo (TASWA), kimesikitishwa na hatua ya Baraza la Michezo la Vyama vya michezo la Afrika Mashariki (CECAFA),  kuwanyanyasa na kuwadhalilisha waandishi wa habari na wapiga picha katika mchezo wa fainali Jumamosi iliyopita kwenye uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.

Kufuatia kudhalilishwa huko kwa waandishi katika fainali hiyo ya michuano ya kombe la Kagame kati ya Yanga na Azam, TASWA imelaani kitendo hicho na kuwaondolea utu, udhalilishaji na unyanyasaji kulikosababishwa na baadhi yao kutandikwa makofi na askari polisi mithiri ya vibaka.

Waandishi wa habari za michezo wa Tanzania wamekuwa wasikivu, waadilifu na watu wanaofuata taratibu,  lakini katika fainali hiyo mara baada ya mchezo walifanyiwa vitendo ambavyo havikulingana na tabia yao.

Lengo la waandishi si kuleta vurugu bali kuhakikisha wananchi wanapata habari kwa kila tukio lilikuwa linatokea uwanja, badala yake walionekana hawana thamani mbele ya jamii inayowawakilisha.

TASWA inalaani kitendo cha Katibu Mkuu wa CECAFA, Nicolas Musonye kwa kutoa agizo kwa polisi kuwazuia waandishi kuingia uwanjani kumalizia kazi zao za kuhoji makocha na wachezaji, hali iliyosababisha vurugu.

CECAFA walijenga urafiki wa karibu na waandishi kipindi chote cha mashindano hayo na Kagame kwa lengo la kuyatangaza , lakini mwisho wa yote walionekana kama taulo la deki limekuwa na thamini pale ambapo linahitajika kwa deki, lakini baada ya hapo halina thamani tena.

Lakini TASWA inafanya uchunguzi juu ya tukio hilo, kufuatia baadhi ya waandishi kuonesha utovu wa nidhamu kama baadhi ya viongozi wa TFF na CECAFA walivyodai kuwa walionesha vitendo vya utovu wa nidhamu kwa kutoa maneno ya kashfa na kutaka kumpiga Musonye

Kufuatia hatua hiyo TASWA imechukua maamuzi yafuatayo
1.Kutoandika jambo lolote linahusu Shirikisho la vyama vya michezo Afrika Mashariki (CECAFA).
2.Kutoandika jambo lolote linahusu mashindano yoyote yaliyo chini ya  CECAFA.

Ili kuweza kufanya kazi pamoja na CECAFA,TASWA inataka kuombwa radhi na CECAFA kutokana na kitendo hicho na kuwalipa fidia waandishi ambao wamepoteza vifaa vya vya kazi na wengine kuhalibiwa vifaa vyao.

TASWA inatoa onyo kali kwa baadhi ya vyama,viongozi na makampuni wenye tabia ya kutotoa ushirikiano na dharau kwa waandishi wanapokuwa kwenye kazi zao.

Juma Abbas Pinto
CHAIRMAN
Julai 30, 2012
Committee Members:  A. Lucas, S. Jaba, G. Hoka, E.Kambili, O.Kapinga,  Z. Chande
You might also like:

MATUKIO YA MGOMO WA WALIMU LEO WANAFUNZI WAANDAMANA KUWAPINGA



 Baadhi ya wanafunzi wa shule za Msingi za jijini Dar es Salaam, Morogoro na Singida, wakiandamana leo asubuhi kupinga hatua ya walimu kugoma kuingia madarasani kufundisha jambo ambalo wanafunzi hao wamelielezea kuwa ni kunyimwa haki zaoza msingi kuwakosesha masomo, ambapo nao wamepanga kutinga Mahakamani kuwafungulia kesi walimu wao kutokana na kwamba madai wanayoidai Serikali wao hayawahusu na hawahusiki kwa mamna yeyote ile, alisikika mmoja wa viongozi wa wanafunzi hao aliyejitambulisha kwa jina la Shaban Mudunda.
 DAR:- Wananfunzi wa Shule ya Msingi Mbezi ya Jijini Dar es Salaam, nao hawakuwa nyuma katika kudai haki yao ambapo nao walifikisha ujumbe kwa njia hii ya Bango, wakiwa pembezoni mwa barabara Morogoro leo asubuhi.
 Nako Mkoani Singida wanafunzi walijitokeza kwa wingi katika mitaa ya mji huo huku wakiimba na wakiwa na baadhi ya Mabango yenye ujumbe kuhusu tukio hilo la kugoma kwa walimu.
 Hawa ni Wanafunzi wa shule za msingi za Ipembe, Nyerere, Unyankindi na Singidani ktk Manispaa Singida, wakiwa nje ya Ofisi za Mkuu wa mkoa huo leo asubuhi, ili kumfikishia ujumbe baada ya walimu wao kugoma.
Wakati walimu wakigoma kuingia madarasani leo asubuhi na wanafunzi wengine kushika mabango na kuandama ili kufikisha ujumbe wa kudai hazi zao, ilikuwa ni tofauti kwa wanafunzi hawa wa Shule ya Msingi Yeta, ambao wao waliamua kuwaonyesha walimu wao kuwa hata wao wanaweza ambao wanafunzi wa Darasa la Saba waliamua kujitolea na kutinga madarasa ya chini na kushusha Nondoz kwa wadogo zao. 

Na katika Shule ya Msingi Lugalo, leo baada ya walimu kugoma wanafunzi wa shule hiyo, walifundishwa na Ma MP pamoja na wanafunzi wa Darasa la saba walifanya kama ambavyo wamefanya wanafunzi wa Yeta amapo wao pia wamejitolea kuwafundisha wadogo zao wa madarasa ya chini.
********************************************

Na: Elisante John Singida.
MGOMO Uliondaliwa Chama cha walimu CWT nchini, umeleta madhara katika Manispaa Singida, baada ya wanafunzi wa shule za msingi kuandamana hadi ofisi za Mkuu wa Mkoa leo asubuhi.

Kwenye maandamano hayo, watoto wa shule za msingi Nyerere, Singidani, Ipembe na Unyankindi, waliamua kutembea umbali wa kilomita tatu hadi ofisi za Mkuu wa Mkoa, wakiwa na mabango yenye ujumbe mbalimbali huku barabarani wakiimba '‘tunataka haki zetu, walimu wamegoma, tunataka haki zetu'’.

Baada ya askari polisi kubaini usalama wa watoto hao upo hatarini, waliingilia kati na kuongoza maandamano hayo hadi ofisi za Mkuu wa Mkoa kwa amani.

WAKAZI WA NANGOO LINDI WANAHANGAIKA KUSAKA MAJI SAFI

.


Wakazi wa Kijiji cha Nangoo Mkoani Lindi wakichota maji kwenye daraja la Nangoo kama walivyokutwa na Mdau leo asubuhi. Wanakijiji hao wamekua wakipata shida ya maji kwa muda mrefu sasa hali inayosababisha kutumia maji taka. Picha na Ahmed Abdullaziz Lindi.

RAIS KIKWETE AFUTURISHA VIONGOZI WA DINI.


Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na viongozi na wawakilishi wa madhehebu mbalimbali ya dini walioshiriki katika futari aliyoiandaa kwa viongozi wa dini ikulu jijini Dar es. Salaam leo jioni
(picha na Freddy Maro)
Ahsanteni tutaonana tena Inshaallah.
Karibuni tena.

WALIMU IRINGA WAKACHA MGOMO, WAIGEUZIA KIBAO CWT, WATAKA TAARIFA ZA MAPATO NA MATUMIZI YA MICHANGO YAO



BAADHI ya walimu wa shule za msingi mjini Iringa wamekigeuzia kibao Chama cha Walimu Tanzania (CWT) wakipinga mgomo wake wa walimu ulioanza nchini kote leo na badala yake wametaka waelezwe kwanza mapato na matumizi ya michango yao ya kila mwezi kwa chama hicho.
“Tunasikia kuna majengo ya walimu yanajengwa nchi nzima, makatibu wa cwt wananuliwa magari, sasa kuna mpango wa kuanzisha benki, lakini hatupewi taarifa ya mapato na matumizi, na hata magari waliyopewa makatibu hayana msaada kwa walimu ambao ndio wenye mali hata kama wakiumwa,” alisema Mwalimu Mkuu wa Shule ya msingi Mtwivilla,. Sidified Mapunda.

Alisema mgomo huo unawapa umaarufu viongozi wa chama hicho na hauna maana yoyote kwa walimu wa kawaida kwasababu taratibu za kuongeza mishahara ya walimu hazina tofauti na za watumishi wengine wa umma.
Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa Shule ya msingi y a Wilolesi ambayo pia walimu wake wote walisusia mgomo hu, George Kameka alisema kabla ya kumgomea mwajiri wao, wanataka kufahamu tangu kutoka kwa chama chao hicho cha wafanyakazi tangu walimu nchini kote waanze kukatwa asilimia mbili kwa ajili ya kukichangia, mapato na matumizi yake yakoje.

Alisema kuna taarifa zisizo rasmi kwamba CWT iko katika mstari wa mbele kudai maslai ya walimu ili mishahara yao ikipandishwa na wao wapandishe michango yao.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Chemichemi  ambayo ni moja kati ya shule zake chache ambazo walimu wake wamegoma, Demetrius Mgohamwende alisema walimu wote 20 wa shule hiyo wamegoma.

WALIMU IRINGA WAKACHA MGOMO, WAIGEUZIA KIBAO CWT, WATAKA TAARIFA ZA MAPATO NA MATUMIZI YA MICHANGO YAO



BAADHI ya walimu wa shule za msingi mjini Iringa wamekigeuzia kibao Chama cha Walimu Tanzania (CWT) wakipinga mgomo wake wa walimu ulioanza nchini kote leo na badala yake wametaka waelezwe kwanza mapato na matumizi ya michango yao ya kila mwezi kwa chama hicho.
“Tunasikia kuna majengo ya walimu yanajengwa nchi nzima, makatibu wa cwt wananuliwa magari, sasa kuna mpango wa kuanzisha benki, lakini hatupewi taarifa ya mapato na matumizi, na hata magari waliyopewa makatibu hayana msaada kwa walimu ambao ndio wenye mali hata kama wakiumwa,” alisema Mwalimu Mkuu wa Shule ya msingi Mtwivilla,. Sidified Mapunda.

Alisema mgomo huo unawapa umaarufu viongozi wa chama hicho na hauna maana yoyote kwa walimu wa kawaida kwasababu taratibu za kuongeza mishahara ya walimu hazina tofauti na za watumishi wengine wa umma.
Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa Shule ya msingi y a Wilolesi ambayo pia walimu wake wote walisusia mgomo hu, George Kameka alisema kabla ya kumgomea mwajiri wao, wanataka kufahamu tangu kutoka kwa chama chao hicho cha wafanyakazi tangu walimu nchini kote waanze kukatwa asilimia mbili kwa ajili ya kukichangia, mapato na matumizi yake yakoje.

Alisema kuna taarifa zisizo rasmi kwamba CWT iko katika mstari wa mbele kudai maslai ya walimu ili mishahara yao ikipandishwa na wao wapandishe michango yao.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Chemichemi  ambayo ni moja kati ya shule zake chache ambazo walimu wake wamegoma, Demetrius Mgohamwende alisema walimu wote 20 wa shule hiyo wamegoma.

MATUKIO MBALIMBALI YA PICHA BUNGENI JULAI 30,2012 DODOMA



Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi ya  Mbwanga mkoani  Dodoma wakisubiri kuingia katika ukumbi  wa Bunge, 30, Julai 2012. (Picha na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO)
Baadhi ya  wadau  wa masuala ya Ayfa wakielekea  ndani ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma Julai 30.2012 kusikiliza  Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa mwaka wa fedha 2012-2013 iliyowakilishwa na Waziri waa Ustawi wa Jamii Dkt,  Hussein Mwinyi, ((Picha na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO).

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt Hussein Mwinyi (kushoto) pamoja na Naibu wake Dkt, Seif Rashid(kulia) wakipitia  hotuba yao ya Makadirio  ya Mapato na Matumiz i ya Wizara yao kwa mwaka 2012-2013 iliyowasilishwa leo  Bungeni Dodoma . Picha na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO.
Mwenyekiti  wa  Kamati ya Hesabu za Serikali  za Mitaa Dkt, Augustine Mrema (kushoto)   pamoja na  Mkurugenzi  Mtendaji  wa Taasisi  ya  Utawala Bora(SEGODETA) Thomas Ngawaiya wakiwa katika viwanja vya Bunge Dodoma  Jualai 30,2012. (Picha na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO

Rais wa Zanzibar awasili Pemba leo



 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Viongozi mbali
mbali,wa Chama na Serikali, alipowasili katika uwanja wa Ndege wa
Karume Pemba leo akiwa katika  ziara maalum ya Mikoa ya Kusini na
Kaskazini.[Picha na Ramadhan Othman,ORZ.]
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,na Mkewe Mama Mwanamwema
Shein,wakisalimiana na Viongozi mbali mbali,wa Chama na Serikali,
alipowasili katika uwanja wa Ndege wa Karume Pemba leo akiwa katika
ziara maalum ya Mikoa ya Kusini na Kaskazini.[Picha na Ramadhan
Othman,ORZ.]
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Viongozi  wakuu wa
Vikosi vya Ulinzi Pemba, alipowasili katika uwanja wa Ndege wa Karume
Pemba leo akiwa katika  ziara maalum ya mikoa ya Kusini na
Kaskazini.[Picha na Ramadhan Othman,ORZ.]

MGOMO WA WALIMU WAANZA!!



 Wanafunzi wa shule ya msingi Makuburi manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam,  wakiwa wameuchapa usingizi baada ya kuchoka kuwasubiri walimu kuja kufundisha bila mafanikio, wiki iliyopita Chama cha Walimu CWT kilitangaza kuwa leo jumatatu walimu wa shule za Sekondari na Msingi wangeanza mgomo nchi nzima kutokana na kutofikia muafaka kwa madai yao dhidi ya Serikali.
(PICHA NA PHILEMON SOLOMON WA FULLSHANGWE) 

 Wanafunzi wa Shule ya Msingi Mabibo iliyopo wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam wakiwa wamelala baada ya kuchoka kuwasubiri walimu kuja kuwafundisha madarasani

ALEX MSAMA ALIPOTEMBELEA BUNGENI LEO



Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda akizungumza na Mkurugenzi wa Msama Promotion Bw. Alex Msama wakati alipotembelea bungeni leo mjini Dodoma na kuongea na  Mawaziri wabunge na viongozi mbalimbali wanaohudhuria vikao vya Bunge mjini Dodoma.
Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mh. Amos Makala akizungumza na Mkurugenzi wa Msama Promotion Alex Msama mjini Dodoma leo.
Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mh. Amos Makala akifurahia jambo na Mkurugenzi wa Msama Promotion Alex Msama mjini Dodoma leo.
Mbunge wa jimbo la Tabora mjini Mh. Aden Rage akizungumza na Mtangazaji wa TBC Shaban Kisu katikati ni Mkurugenzi wa Msama Promotion Alex Msama.
Waziri wa Nishati na Madini Prof. Muhongo akizungumza na Mtangazaji wa TBC Shaban Kisu kulia  ni Mkurugenzi wa Msama Promotion Alex Msama.

Mama Pinda azindua mradi wa maji wa Hospitali ya Mawenzi mjini Moshi leo



Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda akizindua mradi wa maji katika Hospitali ya Mawenzi pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti anaemaliza Muda wake wa, Richard Wells. Hadi kukamilika kwa mradi huo wa maji safi, Kampuni ya bia ya Serengeti Breweries Limited imetumia zaidi ya milioni 55 za kitanzania kujenga tanki kubwa la kuhifadhi maji kwa ajili ya matumizi ya hospitali ya Mawenzi mkoani Kilimanjaro.
 Mkurugenzi wa Mahusiano na Mawasiliano wa Kampuni ya bia ya Serengeti Bi. Teddy Mapunda, akifafanua juu ya gharama halisi za mradi huo. 
 
“Sisi kampuni ya bia ya Serengeti tunatambua sana changamoto zinazowakabili watanzania, taasisi na mashirika mbalimbali hususani hospitali juu ya upatikanaji wa maji safi na salama, na kwasababu hiyo kampuni ya bia ya Serengeti imeona hilo na kuamua kusadia kutatua tatizo hilo katika maeneo mbalimbali ikianza katika maeneo yanayohitaji huduma ya maji kwa haraka zaidi” alisema Mapunda na kuongeza kuwa kujitolea kusaidia jamii ni moja yab sera za kampuni hiyo kama njia mojawapo ya kurudisha shukrani zake kwa wateja wake na watanzania kwa ujumla.

Mgeni rasmi akifungua maji yanayotoka katika bomba lililounganishwa katika matanki hayo.
Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda akisalimiana na Meneja Miradi Endelevu na Uwajibikaji wa SBL, Nandi Mwiyombela 
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Dkt. Mtumwa Mwako
 Mkurugenzi wa Mahusiano na Mawasiliano wa Kampuni ya bia ya Serengeti Bi. Teddy Mapunda, akifafanua juu ya gharama halisi za mradi huo. 
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti, anaemaliza muda wake Richard Wells akizungumza wakati wa uzinduzi huo.

SHINDA BABU KUBWA NA ECO BANK


  Balozi wa Eco Bank, Joyce  Mrema akizungumza na wateja wakati wa promosheni ya Shinda Babkubwa na EcoBank Mlimani City Dar es Salam.
Joyce Mrema akizungumza na Wateja
Shinda Babkubwa Promo na Ecobank Promo, enhancing personal,
family and business lives..
Shinda Babkubwa na Ecobank promotion is creating lots of excitement in Dar es Salaam. The first set of winners emerged in the June draw and they are right now redeeming their prizes amidst celebration and jubilations. Being one of the most exciting promotions in Dar es Salaam right now, the promotion mechanics is simple and easy to understand. The prizes are functional and intended to add value to a winner’s life, personally, as a family or even as a business owner.

Taji Kaaya a student of Kampala University who won an Ipad said ‘I came back from Kampala to hear I had won a laptop. It put some sunshine into my holiday’. The story of Kelvin Kipenge . who won a laptop was equally touching when he said ‘I have longed to own a brand new laptop to help me get information around the world that I need to do my business’. Another winner, CEO of Federal Trading Company Limited, was excited about giving his wife the opportunity to shop in Mariedo. ‘I will give the voucher to my wife to shop and I will watch her pick those lovely clothes she has been dreaming of’.

While some winners opted to redeem their prizes same day, others said they will take their time, shop around and eventually settle for what they want. Some winners went to Clocktower Shopping Centre while others went to Home Shopping Centre. This is the beauty of the Shinda Babkwuba na Ecobank promo. You have options with your prize and you can redeem it at your convenience.

Mr. Sam Ayim, Executive Director of the Ecobank Tanzania, said …‘Our branches have seen tremendous growth in traffic from June 4th when the promotion started. This is a clear indication that the objectives of the promotion which included fostering a saving culture in Tanzania, is being achieved. Saving is an essential tool in planning for the future. Thanks to Shinda Babkubwa na Ecobank na Ecobank Promo. He further explained.. ‘We have exciting products and services that have been carefully developed to deliver endearing value to our customers’ and encouraged potential customers to visit any of Ecobank branches to avail themselves of more information.

For those who did not win in the first draw, the promotion continues until November, so there is still time to win. Simply open an account with Ecobank and grow your deposit to Tsh 100,000 each month to qualify for a chance to win. Prizes include a brand new Hyundai Tucson grand prize and monthly prizes including Ipads, Laptops, Air Tickets and more. Visit an Ecobank branch today to open your account. Ecobank, The Pan African bank.

Sunday, July 29, 2012

KIDUNDWA ADUNDWA OLIMPIKI



Bondia wa Tanzania, Selemani Kidunda (kulia) akiwa hoi baada ya kudundwa kirahisi kwa pointi 20-7 dhidi ya bondia wa Moldova, Vasilii Belous katika pambano la uzito wa welter (69kg) mzunguko wa 32 kwenye Ukumbi wa ExCeL katika michuano ya Olimpiki ya London 2012 leo Julai 29, 2012. Picha: REUTERS

Bondia wa Tanzania, Selemani Kidunda (kushoto) akishambuliwa na bondia wa Moldova, Vasilii Belous wakati wa pambano lao la uzito wa welter (69kg) mzunguko wa 32 kwenye Ukumbi wa ExCeL katika michuano ya Olimpiki ya London 2012 leo Julai 29, 2012. Picha: REUTERS

Bondia wa Tanzania, Selemani Kidunda (kushoto) akiendelea kuadhibiwa na bondia wa Moldova, Vasilii Belous wakati wa pambano lao la uzito wa welter (69kg) mzunguko wa 32 kwenye Ukumbi wa ExCeL katika michuano ya Olimpiki ya London 2012 leo Julai 29, 2012. Picha: REUTERS