Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Thursday, November 29, 2012

NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI CHARLES TIZEBA ATEMBELEA UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA JULIUS NYERERE.




Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dk. Charles Tizeba akipata malezo kutoka kwa Afisa wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga(TCAA), Bw. Elieza Mwalutende, wakati Naibu Waziri huyo alipotemmbelea Uwanja Wa Ndege wa Kimataifa wa Mwl . Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa katika kiwanja hicho.

Hayo ni Majenereta yanayotumika endapo Umeme wa TANESCO unapokatika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijjini Dar es Salaam.

BODI YA UTALII (TTB) YAPEWA CHETI KWA MCHANGO WAKE DHIDI YA MAPAMBANO YA MALARIA KATIKA UZINDUZI WA MPANGO WA KUTOKOMEZA MALARIA UNAOITWA “MALARIA SAFE”





Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda akimkabidhi cheti Geofrey Meena Meneja Masoko wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) kuitambua kwa mchango wake katika mapambano dhidi ya Malaria wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kupambana na ugonjwa huo inayoitwa (Malaria Safe Companys) uliofanyika kwenye hoteli ya Hyatt Regency Dar es Salaam jijini dar es salaam usiku huu ambapo Wizara ya afya inashirikiana na pamoja na taasisi za kimataifa na Makampuni mbalimbali pamoja na Sekta ya michezo, ambapo wadau mbalimbali wameshiriki katika uzinduzi huo.
PICHA NA FULLSHANGWEBLOG.COM
Waziri wa Afya na Ustawi wa jamii Mh. Hussein Mwinyi akimpongeza Bw. Geofrey Meena baada ya kupokea cheti hicho kwa niaba ya Bodi ya Utalii Tanzania (TTB).
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda akimkabidhi cheti Mzee CHrisant Mzindakaya Mwenyekiti wa Kampuni ya Kuzalisha nyama ya mkoani Rukwa kwa mchango wake katika kupambana na Malaria nchini.
Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda akiwa katika picha ya pamoja na wadau makampuni na taasisi mbalimbali wanaopambana na ugonjwa wa malaria nchini mara baada ya uzinduzi huo.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mh. Mizengo Pinda akizungumza na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Hussein Mwinyi wakati akiwasili kwenye hoteli ya Hyatt Regency Dar es Salaam kwa ajili ya kuzindua rasmi kampeni ya kupambana na Malaria inayoitwa "Malaria Safe Companys" , kulia ni Kaimu Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh. Raymond Mushi.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mh. Mizengo Pinda akizungumza na Rais Washirikisho la Mpira wa miguu nchini TFF Bw. Leodger Tenga wakati alipowasili katika hoteli ya Hyatt Regency Dar es Salaam kwa ajili ya uzinduzi wa kampeni ya kupambana na ugonjwa wa Malaria, kushoto ni Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Hussein Mwinyi.
Wadau waliohudhuria katika uzinduzi wa kampeni ya kupambana na ugonjwa wa malaria kutoka kulia ni Mkurugenzi wa michezo katika Wizara ya Habari, Vijana , Michezo na Utamaduni Bw. Leonald Thadeo, Assah Mwmbene Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo, Mbunge wa Jimbo la Temeke Mh. Abbas Mtemvu na Mbunge na Waziri wa zamani Mh. Chrisant Mzindakaya.
Wadau mbalimbali wakiwa katika uzinduzi huo katika Hyatt Regency Dar es Salaam
Mkurugenzi wa Sahara Media Bw. Samwel Nyala kushoto akiwa na wadau wengine katika uzinduzi huoHyatt Regency Dar es Salaam.
Wadau mbalimbali waliohudhuria katika uzinduzi huo kwenye hoteli ya Hyatt Regency Dar es Salaam
Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda akiandika kitu huku Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Mh. Hussein Mwinyi akipiga makofi katika uzinduzi huo.
Meneja Mkuu wa Kampuni ya Azam Mzee Salim Mohamed Abeid Bakhressa akitoa ushuhuda kuhusu malaria ilivytokomezwa katika viwanda vyao.
Rais wa Shirikisho la mpira wa miguu nchini TFF Bw, Leodger Tenga akizungumza katika hafla ya uzinduzi huo jinsi sekta ya michezo ilivyosaidia kutokomeza malaria nchini.
 
Mwimbaji nguli wa muziki wa Taarab Khadija Kopa pamoja na kundi lake wakitumbuiza katika hafla hiyo iliyofanyika usiku huu kwenye hoteli ya Hyatt Regency Dar es Salaam

RAIS WA ZANZUBAR DK.ALI MOHAMED SHEIN AREJEA NCHINI AKITOKEA VIETNAM ALIKOKUWA KWA ZIARA YA KISERIKALI..




Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,akivalishwa Shada la mauwa alipowasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume wa Zanzibar,akirejea Nchini kutoka ziara ya Kiserikali nchini Vietnam.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,akiwasalimia Vijana wa Chama cha Mapinduzi CCM
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi,wakati wa mapokezi alipowasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume wa Zanzibar,akirejea Nchini kutoka ziara ya Kiserikali nchini Vietnam.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,akizungumza na Waandishi wa Habari wa Vyombo mbali mbali nchini alipowasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume wa Zanzibar,akirejea Nchini kutoka ziara ya Kiserikali nchini Vietnam.

DK.SHEIN AENDELEA NA ZIARA NCHINI VIETNAM.




Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akiwapungia mkono wanachama wa Chember of Commerce and Industry wa nchini Vietnam baada ya kuzungumza nao katika jumba la jumuiya hiyo Mjini Hanoi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akizungumza na Mabalozi wa Nchi zilizo katika jangwa la Sahara SADC wakati walipofika kumsalimia Rais katika Hoteli ya Melia Mjini Hanoi nchini Vietnam.

TIGO NA REACH FOR CHANGE YAKABIDHI DOLA 75,000 KWA WASHINDI.




Wadau mbalimbaliT wa masuala ya mawasiliano na maendeleo wakifuatilia hafla ya makabidhiano ya $75,000/ kwa washindi watatu wa mpango wa Tigo wa Reach For Change kwa kila mmoja kutekeleza miradi yao kupitia Shindano lhilo la wajasiriamali la.
 

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tigo, Andrew Hodgson (Kushoto) akiwa na washindi watatu wa shindano la Tigo Reach For Change, Bi. Brenda D. Shuma, Nyabange Chirimi na Thadei Msumanje, kulia ni Mkurugenzi wa Reach For Change Bi. Sarah Damber

Tigo na Reach For Change yakabidhi $75,000 kwa washindi watatu kila mmoja kutekeleza miradi yao kupitia Shindano la wajasiriamali la Reach for ChangeDar es Salaam, Tanzania, 28 Novemba, 2012. Mwezi Septemba mwaka huu, Tigo kwa kushirikiana na Shirika la kujitolea la Reach For Change kwa mara ya kwanza nchini Tanzania walizindua programu iliyodhamiria kutambua na kuendeleza mawazo madhubuti ya wajasiriamali  yenye lengo la kuboresha maisha ya watoto. Baada ya kampeni ya mwezi mmoja ya kutoa wito kwa watanzania wote wenye mawazo madhubuti kujitokeza kwa ajili ya ajili ya kuwasilisha maombi yao, tulipokea maombi 2480, ambapo waombaji 15 walifika fainali  ikifuatiwa na mchujo mkali ambao ulijumuisha wafanyakazi wa Tigo na Reach For Change pamoja na wataalamu wengine wa nje. Hawa waliendelea kuchujwa hadi tulipofanikiwa kupata washindi watatu  baada ya mawazo yao kupitishwa na jopo la majaji.
"Mpango wa kurejesha kwa Jamii sehemu ya faida yetu, ni moja ya nguzo ya kampuni yetu na tuna nia ya dhati na mpango huu wa Reach for Change, ambao ni sehemu ya mpango wetu kimataifa. Tigo Tanzania imepokea maombi yenye mvuto na ushindani wa hali ya juu. Washindi wa nafasi tatu za juu ambao wamechaguliwa leo si tu walishinda mioyo za majaji bali waliwavutia na ubunifu wa mipango yao dhubuti. Sasa waanapokea ufadhili wa $25,000 kama mshahara wa mwaka, kwa miaka mitatu mfululizo ili kuweza kuzingatia na kutimiza malengo yao," alisema Andrew Hodgson, Kaimu Mkurugenzi Mkuu Tigo.
Washindi wa shindano la wajasiriamali la Tigo Reach For change mwaka 2012 ni Brenda-Deborah Shuma, Nyabange Chirimi na Thadei Msumanje. Miradi yao watakayo ianzisha italenga katika kuwawezesha watoto wenye ulemavu na vijana wenye ujuzi wa kiufundi, kusaidia elimu ya watoto wa mitaani na kuboresha elimu kupitia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT).
'Tigo Reach for Change' imelenga katika kuainisha na kusaidia wajasiriamali kwenye miradi ya kijamii na wenye mawazo yakinifu juu ya kuboresha maisha ya watoto wa Tanzania. Washindi hawa watatu sasa wanajiunga na programu ya miaka mitatu ya kuboresha miradi yao, ambapo mawazo yao yatabadilishwa kuwa miradi endelevu. Mbali na hayo, watapata mshahara wa dola 25,000 kwa mwaka kwa miaka mitatu mfululizo pamoja na  ushauri wa kitaalamu kutoka kwa wafanyakazi waandamizi wa Tigo.
Reach for Change ni Shirika la kujitolea lililoanzia Sweden ambalo lilianzishwa na Kinnevik, ambaye ndiye aliyeunda kampuni ya Millicom (shirika anzilishi la Tigo). Kampeni ya kutafuta wajasiriamali kwa mkakati wa Reach for Change kwa mara ya kwanza ulianzia huko Sweden mwaka 2010 ikifuatiwa na Russia 2011 kabla mwaka huo huo kuanzishwa barani AfriKa katika nchi ya Ghana. Hadi sasa imeweza kuboresha maisha ya watoto wapatao 140,000 nchini Ghana.
Tigo na Reach For Change imeanza rasmi utafutaji wa wajasiriamali kwenye miradi ya kijamii,  katika nchi zinazotoa huduma yake barani  Afrika, kwa kuzinduliwa kwanza Rwanda ikifuatiwa na Tanzania, halafu Ghana,  Congo DRC, Senegal na mwishomi itakuwa Chad miezi michache ijayo.

Wednesday, November 28, 2012

KALI YA MWAKA: MTOTO AMUUA MAMAYAKE KWA KUMPIGA NGUMI!




Akina mama waombolezaji wakisawazisha kaburi la marehemu Sinjembele Julius(62) aliyeuawa kwa kupigwa na mwanae Ndele Julius(25)

Baadhi ya waombolezaji wakishuhudia mazishi ya Sinjembele yaliyofanyika Nyumbani kwake katika kitongoji cha Igawilo kata ya Swaya Mbeya
 
UKISTAAJABU ya Musa utayaona ya firauni, unaweza kusema hadithi kumbe nikweli ,Mkazi wa  Swaya jijini Mbeya Ndugu Ndele  Julius amemuua mama yake mzazi kwa kumpiga mateke na ngumi kisha kutoroka pasipo julikana Novemba 25 mwaka huu.

Tukio hilo limetokea majira ya saa 10 jioni nyumbani kwa mama huyo mara baada ya kutokea kwa ugomvi kati ya mtoto wake na kijana  mwingine hali iliyopelekea mama huyo kuingilia ndipo alipo kutwa na mauti huo.
Akizungumzia tukio hilo Kamanda wa Polisi  Mkoani humo Ndugu Diwani Athumani amesema kuwa Chanzo cha tukio hilo ni ugomvi uliokuwepo kati ya mtoto wake na kijana  mwenzake kitendo ambacho kilipelekea mama huyo kuingilia ugomvi huo .

Amesema wakati  mama huyo akijaribu kuamulia ugomvu huo mtoto wake alicha kupigana na mwenzake na kuanza kumshambulia mama yake kwa kumpiga ngumi na mateke mwilini.

Amesema mama huyo alifariki muda mchache kutokana na kupigwa sehemu mbalimbali za mwili wake na kusababishiwa majeraha makuibwa yaliyopeleka kupoteza uhai wake.

Awali akizungumzia tukio hilo Mtoto wa Kwanza wa mama huyo Ndugu Razaro Mbwiga amesema kuwa mdogo wake alikuwa na tabia ya kugombana na mama yake marakwamara .

Hata hivyo teyari mwili huo umekwisha chukuliwa hospitali na kuzikwa ambapo katika maziko hayo Chama cha Muungano wa kijamii (Mujata) umewataka vijana kujiepusha na vitendo viovu kama uvutaji bangi na pombe za kienyeji kwani ndio chanzo cha kutokea kwa vurugu nyingi. Mjengwa.

BONDIA TYSON FURY KUMVAA WLADIMIR KLITSCHKO MWAKANI





LONDON, England
“Nimezungumza mara kadhaa na kocha wa Wladimir, Bernd Boente kuhusu pambano hilo na Tyson yu tayari sasa kwa hilo. Ni mpambano ambao unaweza kuwa katika uwanja wa soka katika kipindi cha kuanzia Mei, Juni au Julai
BONDIA mahiri Tyson Fury amepania kupanda ulingoni kupimana ubavu na Wladimir Klitschko kuwanuia ubingwa wa dunia kiangazi kijacho.
Fury, 24, bondia asiyepigika katika uzani wa ‘heavyweight,’ Jumamosi hii anapanda ulingoni kumvaa Mmarekani Kevin Johnson jijini Belfast, Ireland ya Kaskazini.
Na promota wa pambano la Jumamosi Mick Hennessy amedai kuwa, ushindi kwa Fury mwenye urefu wa futi 6.9, utampa fursa ya kuandaliwa pambano dhidi ya Klitschko - bingwa wa mikanda ya WBA, IBF, na WBO.
Hennessy alisema: “Nimezungumza mara kadhaa na kocha wa Wladimir, Bernd Boente kuhusu pambano hilo na Tyson yu tayari sasa kwa hilo.
“Ni mpambano ambao unaweza kuwa katika uwanja wa soka katika kipindi cha kuanzia Mei, Juni au Julai.
“Ujerumani ni nchi inayoweza kuwa kipaumbele chetu kupigwa pambano hilo, lakini nimeshazungumza na wamiliki wa Uwanja wa Old Trafford au Croke Park,” alisema Hennessy.

NAPE AONGOZA MAELFU MAZISHI YA SHARO MILIONEA, MUHEZA‏





Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye (Watatu kulia, waliobeba jeneza) akishiriki kubeba jeneza lenye mwili wa aliyekuwa msanii wa muziki wa kizazi kipya na filamu, Hussein Ramadhani maarufu kwa jina la Sharo Milionea, alipokiwakilisha Chama Cha Mapinduzi, kwenye mazishi ya msanii huyo, leo kwenye Kijiji cha  Lusanga, Muheza Tanga. (picha na Bashir Nkoromo)
 Mwana FA akitoa salam kwa niaba ya Wanamuziki wa Bongofleva, wakati wa mazishi hayo
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwa na Rais wa Bongo Movies Simon Mwakifyamba na Ofisa Habari wa Airtel Jackson Mbando, alipokiwakilisha Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwenye mazishi ya aliyekuwa msanii wa muziki wa kizazi kipya na filamu, Hussein Ramadhani maarufu kwa jina la Sharo Milionea,leo kwenye Kijiji cha  Lusanga, Muheza Tanga. (Picha na Bashirb Nkoromo).
Mwili wa Marehemu ukiswaliwa kabla ya kwenda kuzikwa.
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akitoa pole za Chama Cha Mapinduzi (CCM) alipokiwakilisha Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwenye mazishi ya aliyekuwa msanii wa muziki wa kizazi kipya na filamu, Hussein Ramadhani maarufu kwa jina la Sharo Milionea,leo kwenye Kijiji cha  Lusanga, Muheza Tanga. (Picha na Bashir Nkoromo).
 
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akimpa pole  Zaina Mkieli, Mama wa aliyekuwa msanii wa muziki wa kizazi kipya na filamu, Hussein Ramadhani maarufu kwa jina la Sharo Milionea, alipokiwakilisha Chama Cha Mapinduzi kwenye mazishi ya msanii huyo, leo kwenye Kijiji cha  Lusanga, Muheza Tanga. (Picha na Bashir Nkoromo).

WAREMBOWATAKAOSHIRIKI SHINDANO LA MISS EAST AFRICA 2012 WAKIWA JIJINI DAR ES SALAA


 


Miss East Africa 2012-Eritrea. Grand Finale to be held on 07th December at Mlimani City, Dar es salaam
Miss East Africa 2012-Rwanda. Grand Finale to be held on 07th December at Mlimani City, Dar es salaam

Miss East Africa 2012-Burundi. Grand Finale to be held on 07th December at Mlimani City, Dar es salaam Warembo wa Miss East Africa 2012 wakiwa katika vazi la ufukweni, jijini Dar es salaam.
 
shindano hilo litafanyika tarehe 7 ijumaa wiki ijayo, kwenye ukumbi wa Mlimani City, Dar es salaam.Yanaandaliwa na kumilikiwa na kampuni ya Rena Events Ltd na kudhaminiwa na TANAPA, Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro, Ethiopian Airlines, Seascape Hotel, Darlings Hair, Ako Catering, DTP, Satguru, na Clouds FM.
Miss East Africa 2012-Ethiopia. Grand Finale to be held on 07th December at Mlimani City, Dar es salaam
Miss East Africa 2012-Kenya. Grand Finale to be held on 07th December at Mlimani City, Dar es salaam
Miss Esat Africa 2012-Somalia. Grand Finale to be held on 07th December at Mlimani City, Dar es salaam
Miss East Africa 2012-Uganda. Grand Finale to be held on 07th December at Mlimani City, Dar es salaam.
Miss East Africa 2012-Tanzania. Grand Finale to be held on 07th December at Mlimani City, Dar es salaam

MREMBO ANAESHIKILIA TAJI LA MISS UNIVERSE TANZANIA AKABIDHIWA BENDERA NA BASATA LEO JIJINI DAR ES SALAAM, Mashindano kuunguruma Disemba 19 nchini Marekani.



Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa nchini(BASATA) Ghonche Materego(kushoto) akimkabidhi bendera ya Taifa Mrembo wa Tanzania anaeshikilia taji la Miss Universe Winfrida Dominic, kwenye ofisi za Baraza hilo jijini Dar es Salaam leo, mrembo huyo anaiwakilisha Tanzania kwenye fainali za mashindano hayo nchini Marekani yanayotarajiwa kufanyika December 19 mwaka huu.

Mrembo huyo akizungumza na katibu mtendaji wa Basata kabla ya kukabidhiwa bendera hiyo.

fastjet yazinduliwa na Naibu Waziri wa Uchukuzi na kukamilisha makubaliano ya Ubia na Swissport



Shirika la kwanza la ndege la nauli nafuu Afrika, fastjet, limeizundua ndege yake ya kwanza ikiwa nachapa yake kamili, siku mbili tu kabla ya kuanza safari za anga Tanzania. Kwenye hafla iliyofanyikakwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Kamabarage (JKIA),Dar es Salaam, maafisa wa serikali, watendaji wa fastjet na wataalamu wa safari za anga walishuhudia ndege aina ya Airbus A319 ikipaa kwenye anga ya Dar es Salaam kwa mara ya kwanza.

Kuanzia Alhamisi, 29 Novemba, fastjet itafanya safari mbili kutwa kwenye ruti zake mbili za mwanzo – Dar es Salaam-Kilimanjaro na Dar es Salaam-Mwanza, zote zikiwa ni safari zenye wasafiri wengi wa ndani. Tiketi zilianza kuuzwa wiki mbili zilizopita na fastjet imeshuhudia mahitaji makubwa, zaidi kuliko matarajio ya awali. Mpaka sasa idadi ya tiketi zilizonunuliwa ni sawa na safari 60 za ndege iliyojaa, na mauzo yanaendelea kwa safari za mwakani. Nauli zitakuwa za wastani wa dollar $80, lakini zinaanzia bei ya chni kabisa ya $20 kwa safari ya kwenda, kabla ya kodi za serikali kwa wateja watakowahi kununua tiketi.

Akizungumza mjini Dar es Salaam, Afisa Mtendaji Mkuu wa fastjet, Ed Winter, alisema:

“Leo ni siku ya kusisimua sana, na siyo tu kwa fastjet, bali kwa Tanzania na Afrika kwa ujumla. Kwa miaka mingi tasnia ya safari za anga Afrika imekosa huduma bora, na kulegalega nyuma ya kwingine duniani. Ustawi wa mapato umeongeza fursa za watu kuwa na mapato ya ziada, na pamoja na kwamba hilo limeambatana na mahitaji makubwaya usafiri wa anga, bado watu baraniAfrika wamekosa fursa za usafiri wa anga wanaoumudu na kuuamini. fastjet sasa itaziba pengo hilo na kwakuwaletea Watanzania, na hasa bara zima la Afrika, shirika la kwanza la ndege la nauli nafuu, likiwa na safari za kituo hadi kituo, na lenye kujiendesha kwa viwango vya kimataifa vya usalama na ubora.”

Akizungumzia uzinduzi huo, Afisa Mwendeshaji Mkuu wa Airbus – Wateja, alisema:

Uamuzi wa fastjet kujikita kwenye ndege aina ya A319 pekee ni kidhihirisha ufanisi, kuaminika na kustahili kwa ndege za aina hiyo kwa ajili ya safari za nauli nafuu barani Afrika na haswa kusini mwa Jangwa la Sahara. Ndege hiyo itakayotumiwa na fastjet inaoongoza kwenye mauzo ya ndege aina ya Airbusna inayo safu mbili za viti,, fastjet imezingatia kuleta viwango vipya vya starehe na unafuu wa gharamakwenye soko la Afrika ambalo linatarjiwa kuongezeka mara dufu karikakipindi cha miaka 20 ijayo .”

Fastjet itakuwa ikiendeshwa na timu yenye uzoefu wa safari za ikiongozwa na Ed Winter, Afisa Mwendeshaji Mkuu wa zamani wa kampuni ya easyjet na mkurugenzi mwanzilishi wa shirika la ndege ya bei nafuu la Go, Afisa Biashara Mkuu Richard Bodin, Mkurugenzi wa zamani wa Mikataba wa easyJet na Mkurugenzi wa Biashara wa shirika la ndege la bei nafuu la Jet2.com, Mkurugenzi wa Uendeshaji Rob Bishton, Rubani Kiongozi & Mkuu wa Shughuli za Ndege wa easyJet na Meneja Mkuu wa Afrika Kyle Haywood, amabye aliwahi kuwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Air Uganda.

Shirika hili la ndege linaendeshwa chini ya leseni ya chapa ya easyGroup Holdings Limited na Sir Stelios Haji-Ioannou, mwanzilishi wa shirika la ndege kinara kwa nauli nafuu, easyJet.

Akizungumzia uzinduzi, Mwenyekiti wa easyGroup Holdings, Sir Stelios alisema:

Sasa ni zamu ya Afrika! Nimefurahi kuwa nimeshiriki, japo kidogo, kwenye kuanzishwa kwa mapinduzi mengine tena. Ninawatakia wahusika wote safari njema!”

Shirika hili la ndege linabashiri kwamba idadi ya abiria wa Fly540, ambayo kwa sasa ni abiria 750,000 kwa mwaka, itaongezeka mara dufu ndani ya miezi sita kuanzia uzinduzi huu. Fastjet imepanga ndani ya mwaka mmoja itakuwa na idadi ya ndege 15 aina ya A319.

Kituo cha kwanza cha fastjet niDar es Salaam, na cha pili kitakua niNairobi,ambacho kinatarajiwa kuzinduliwamwakani. Baada ya kujizatiti Afrika Mashariki, shirika hilo la ndege linatarajia kuzinduliwa Accra, Ghana na Luanda, Angola.

astjet pia inafurahi kutangaza kwamba leo imetiliana saini mkataba na Swissport International, shirikia linaloongoza kwenye huduma za sekta ya anga viwanjani, ambapo itakuwa ikihudumia mtandao wote wa shirika hilo la ndege kwa mahitaji yake kwenye viwanja vya ndege.

Kupitia makubaliano hayo ya kipekee ya ubia, Swissport ambayo hutoa huduma mbalimbali kwenye viwanja vya ndege, itawajibika kwa usambazaji na usaidizi wa mlolongo wa ugavi kwenye mtandao wote wa fastjet.

Juan Jose Alvez, Makamu wa Rais Mtendaji wa Uhudumiaji kwenye Viwanja vya Ndege Ulaya, Mashariki ya Kati, Asia na Afrika alidokeza:

“Swissport ina uzoefu mkubwa wa kutoa huduma kwenye mfumo wa usafiri wa bei nafuu katika bara laUlaya na tuko tayari kushirikianakuisaidia kuijenga chapa ya fastjet katika bara laAfrika, kwa kutumia  uelewa na michakato yetu. Ubia huu unahusisha changamoto zote zinazohusiana na uanzishwaji wa mtandao wa kushughulikia ndege kwenye viwanja vya ndege na mifumo ya usimamizi, na hivyo ubia huu ni wa kipekee na unawakilisha aina mpya ya uhusiano kati ya mtoa huduma na shirika la ndege na kutoa firsa kwaSwissport kuendelea kujenga mtandao wake Afrika kwa ubia na fastjet.”

Afisa Mtendaji Mkuu wa fastjet Ed Winter alidokeza:

“Swissport ina hadhi inayong’ara kimataifa na historia ya kutoa huduma bora kwa mashirika ya ndege kwenye viwanja vya ndege kote duniani. fastjet inajenga shirika la ndege la bara la Afrika likiwa na viwango vya kimataifa vya usalama, ubora, ulinzi na kuaminika na hivyo ni muhimu kwetu kuwa na mbia ambaye atoakipaumbele cha juu kwa viwango vya ubora kulingana na malengo yetu ya kababmbe ya kustawi barani Afrika.”

KUMUONA JB MPIANA 100,000





 JB Mpiana akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu shoo yake itakayofanyika Leaders Club Novemba 30.
Mtangaji wa Kituo cha Televisheni cha Channel Ten, Said Kilumbanga (kulia) akiwa amepozi na wanenguaji wa  mwanamuziki kutoka Congo, JB Mpiana
DAR ES SALAAM, Tanzania
MSANII nguli wa muziki wa dansi Afrika, JB Mpiana amewataka Watanzania kujitokeza kwa wingi na kushuhudia shoo yake itakayopigwa kwenye viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam Ijumaa hii, ambapo kiingilio kwa VIP A itakuwa sh 100,000 na kawaida sh 25,000.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, JB Mpiana alisema, anajikubali na kuithamini kazi yake ambayo anaifanya na kuahidi kuwapa raha wapenzi na wadau mbalimbali wa muziki hapa nchini ambao watajitokeza siku hiyo.

“Kwanza nimefurahia sana mapokezi ya jana, hivyo basi nitawapa raha siku hiyo na pia nawapongeza waandaaji kwa kuona umuhimu na kuniteua mimi kufanya nao kazi siku hiyo, nimekuja na kikosi changu kamili cha watu 25, hivyo basi nina imani siku hiyo itakuwa raha sana,” alisema Mpiana.

Mpiana aliwataka wanamuziki wa hapa nchini, kujituma na kufanya kazi zao kwa ufanisi zaidi na kuziheshimu pia, ili waweze kufikia mafanikio ambayo wamejipangia kuyafikia, kwa kuwa hata yeye alianzia huko na ndio sababu amefikia hapa alipo.

Naye Mkurugenzi wa QS J Mhonda Entertainment, Joseph Mhonda, alisema kila kitu kimekamilika na kudai kuwa, kwa sasa wanasubiri siku ifike ili watanzania wapate raha na kile ambacho wamekitarajia.
Mhonda alisema, viingilio siku hiyo itakuwa sh 25,000 kwa atakayenunua tiketi mapema, huku 30,000 kwa watakaonunulia mlangoni na sh 100,000 VIP A kwa watakaonunua mapema huku kwa mlangoni ni sh 150,000.

Aliongeza kuwa, Mpiana ataanza kufanya shoo ukumbi wa Triple A, jijini Arusha na baadaye jijini Mwanza katika ukumbi wa Villa Park huku wasanii mbalimbali wakitarajiwa kutumbuiza siku hiyo ambao ni Ney Wamitego, H Baba, Mashujaa pamoja na Mb Dog.

SHARO MILIONEA PUMZIKA KWA AMANI