Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Sunday, May 25, 2014

SAFARI YA MWISHO YA MAREHEMU AMINA NGALUMA



Mwili wa marehemu Amina Ngaluma ukishushwa tayari kuingia kaburini kwa maziko, Machimbo Mnarani.
Mwili wa marehemu Amina Ngaluma ukiingizwa kaburini.
Mume wa marehemu Amina Ngaluma akisoma dua kwa mkewe.
Kaburi la marehemu Amina Ngaruma aliyezikwa leo maeneo ya Machimbo, Mnarani.
Waombelezaji wakitoka msikitini tayari kwa kwenda kwenye maziko.
Picha na Global WhatsApp +255 753-715 779

MASHINDANO YA DATS YAZINDULIWA MKOANI MOROGORO, MIKOA TISA KUSHIRIKI




Mwenyekiti wa chama cha Dats Tanzania Gesase Waigama akiongea wakati wa ufunguzi wa mashindano ya mchazo huo unaoshirikisha mikoa  ya Dar es Salaam, Dodoma, Mwanza, Mbeya, Kilimanjaro, Kagera, Arusha na wenyeji wao Morogogoro ambapo katika mashindano hayo yaliodhaminiwa na bia aina ya Safari mshindi wa kwanza atatoka na kitita cha shilingi 600,000 hapo kesho.

Baadhi ya washiriki wa mchezo huo wakifanya mazoezi kabla ya kuanza kwa shindano hilo linalofanyika katika ukumbi wa Magunila  Kihonda Mjini Morogoro.

Wahsiriki wa shindano hilo kutoka mikoa mbailimbali wakiwa katika ukumbi  huo wakishuhudia pambano hilo.

Irene Kihupi mchezaji kutoka mkoa wa Dar es Salaam akiwa katika pambano hilo.

Joyce Laize mchezaji kutoka mkoa wa Arusha akiwa katika pambano hilo.

 Mwenyekiti huyo wa Dats akizindua mchezo huo ili kuruhusu pambano kuanza rasmi.

 Baadhi ya wachezaji wakiwa katika pambano hilo

Frolida Namajojo katibu wa Dats mkoa wa Morogoro akiwa katika mazoezi kabla ya kuanza mchezo huo.


WANACHAMA wa chama cha Darts Taifa (TADA) wameyaomba makampuni yanayodhamini michezo mbali mbli nchini kuwekeza kwenye chama hicho ili kuweza kukuza uchumi,michezo pamoja na kuongeza pato la taifa. 
Wanachama hao waliyasema hayo Mei 24 mwaka huu   kwa nyakati tofauti watika  wa mashindano ya mabingwa wa chama hicho yanayofanyika mkoani hapa.

Walisema kuwa mchezo huo ni mzuri lakini unachangamoto ya gharama ambapo alisema kuwa mara zote yanapoandaliwa mashindano hayo kila mwanachama anatakiwa kujitegemea mwenyewe.  Aidha waliwaomba kopa Coca Cola kuandaa utaratibu wa kupeleka mchezo huo mashuleni ili kuweza kuibua vipaji vya mchezo huo kuanzia ngazi ya shule.

Kwa upande wake katibu mkuu wa chama hicho Kale Mwigonja alisema kuwa shindano hilo ambalo limedhaminiwa na kampuni ya bia ya Safari Lager linalenga kunua mchezo huoikiwa I pamoja na kujiandaa na Afrika Mashariki linalotarajia kufanyika mwezi juni mwaka huu Mkoani Dodoma. 

Alisema kuwa mashindano hayo yanashirikisha virabu 32 kutoka katika mikoa mbali mbali nchni ambapo alisema kuwa washindi watapata zawadi mbalimbali ikiwemo ikombe pamoja na zawadi za pesa taslimu ambapo alisema kuwa mshindi wa kwanza atapata sh.laki 6 na kikombe ,wa pili laki 4 na kikombe na watatu laki 3.

KWENYE TAASISI ZA DINI ZAIDI 80 JIMBONI KWAKE



DSC_0025
Mbunge wa Singida Mjini, Mh. Mohammed Dewji (MO), akizungumza na viongozi wa Mahakama ya Qadhi wakati alipotembelea Mahakama hiyo kuona namna inavyohudumia waumini wa Dini ya Kiislamu katika kutatua migogoro ya ndoa.
DSC_0029
Sheikh wa Mahakama ya Qadhi, Ramadhani Kaoja akimweleza Mheshimiwa Mbunge shughuli za Mahakama hiyo pamoja na changamoto mbalimbali zinazowakabili, Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Singida Mjini , Hamis Nguli, wa pili kulia ni Katibu wa Mahakama ya Qadhi, Alhajj B. Mlau.
DSC_0133
Mbunge wa jimbo la Singida Mjini MO akisalimiana na waumini wa Msikiti wa Kata ya Mtipa wakati alipofanya ziara ya kukagua ujenzi wa Msikiti huo, ambapo mara baada ya kuona hatua zilizofikia za ujenzi huo aliahidi kutoa Mabati 50 pamoja na mifuko 50 ya Saraji kwa ajili ya kukamilisha ujenzi huo.
DSC_0171
MO akitoka kukagua ujenzi wa Msikiti wa kijiji cha Mangwanjuki kata ya Mtipa.
DSC_0237
Waumini wa Msikiti wa kijiji ch Mangwanjuki wakimsikiliza Mbunge wao Mheshimiwa MO.
DSC_0262
Baadhi ya wapiga kura wa kijiji cha Mangwanjuki wakipeana mikono ya Kheri na Mbunge wao.
DSC_0287
Baadhi ya waumini wa dini ya Kiislamu wa Msikiti wa Mwankonko darajani wakimsikiliza Mbunge wao (hayupo pichani) wakati alipoendelea na zoezi la kutembelea nyumba za kuabudu zilizopo jimboni kwake.

Saturday, May 24, 2014

MABONDIA WAPIMA UZITO KUTWANGANA JUMAMOSI MAY 24 MANZESE





Bondia Said Mbelwa akipima uzito kwa ajili ya mpambano wake  leo na Karama Nyilawila wa kugombania ubingwa wa UBO katika ukumbi wa frends corner manzese Dar es salaam picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
 Mabondia Abdalla Pazi kushoto na Seleman Galile wakitunishiana misuli baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambani wao wa leo jumambosi ya may 24 katika ukumbi wa frend corner manzese dar ea salaam picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
BONDIA SELEMAN GALILE AKIPIMA UZITO
Mabondia Abdalla Pazi kushoto na Seleman Galile wakitunishiana misuli baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambani wao wa leo jumambosi ya may 24 katika ukumbi wa frend corner manzese dar ea salaam picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
 BONDIA SELEMAN GALILE
  BONDIA SELEMAN GALILE AKIPIMA AFYA KWA DAKTARI
BONDIA SELEMAN GALILE AKIPIMA AFYA KWA DAKTARI
Bondia Khalid Chokolaa kushoto akitunishiana misuli na Abdul Manyenza wakati wa upimaji uzito kwa ajili ya mpambano wao leo jumamosi ya may 24 katika ukumbi wa frends corner manzese Dar es saklaam picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

MPIGA PICHA WA MLIMAN TV MAXIMILLIAN NGUBE AFARIKI DUNIA


MPIGA PICHA MKONGWE WA PICHA ZA TELEVISHENI,MAXIMILIAN NGUBE (PICHANI) AMEFARIKI DUNIA LEO ASUBUHI BAADA YA KUSUMBULIWA KWA MARADHI KWA MUDA MREFU.

MAREHEMU MAXIMILIAN AMBAYE ALIFAHAMIKA SANA KWA JINA LA PAPAA MAX,ALIKUWA NI MPIGA PICHA HODARI WA KITUO CHA TELEVISHENI CHA MLIMANI TV.

GLOBU YA JAMII IMEPOKEA TAARIFA ZA MSIBA HUU KWA MASIKITIKO MAKUBWA SANA NA TUNAMUOMBEA KWA MWENYEZIMUNGU AIWEKE ROHO YA MAREHEMU MAXIMILIAN NGUBE MAHALI PEMA PEPONI.

-AMIN.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL ATEMBELEA KIWANDA CHA KUKAMUA MAFUTA YA UFUTA CHA TAKEMOTO, NAGOYA JAPAN




 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohammed Gharib 
Bilal, mkewe Mama Asha Bilal, Balozi wa Tanzania nchini Japan, Salome Sijaona 
(wa pili kushoto) na Balozi wa Japan nchini Tanzania, Masaki Okada, wakiongozana 
wakati walipokuwa wakielekea kutembelea kiwanda cha kukamua mafuta ya Ufuta cha Takemoto kilichopo Nagoya nje kidogo ya Jiji la Tokyo Japan, jana Mei 22, 2014, 
akiwa katika ziara yake ya kikazi nchini Japan.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib 
Bilal na ujumbe wake wakipata maelezo kuhusu kiwanda hicho kinavyofanya kazi 
hadi kupatikana mafuta ya Ufuta, wakati walipofika kiwandani hapo kujionea kutembelea na kujionea shughuli za uzalishaji, jana Mei 22, 2014.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib 
Bilal, akipata maelezo kutoka kwa Ofisa wa Kiwanda cha kukamua mafuta ya Ufuta 
cha Takemoto, Akira Ogawa, jinsi mbegu za ufuta zinavyoanza kuandaliwa kuelekea katika mashine za kukamua mafuta. Hapa ni hatua ya kwanza zinaposhushwa mbegu hizo na kuingia moja kwa moja kwenye mitambo.
  akiendelea kupata maelezo....

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib 
Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Ofisa wa Kiwanda cha Mafuta ya Ufuta cha 
Takemoto, Akira Ogawa, jinsi mbegu za ufuta zinavyosafiri hadi kufika katika Kinu cha kuzisaga hadi kupatikana mafuta hayo, wakati alipotembelelea kiwanda hicho kilichopo Nagoya nje kidogo ya Jiji la Tokyo nchini Japan, jana
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib 
Bilal na mkewe Mama Asha Bilal, wakionyeshwa mbegu za ufuta na Ofisa wa Kiwanda cha kukamua mafuta ya Ufuta cha Takemoto, Akira Ogawa, wakati alipotembelelea kiwanda hicho kilichopo Nagoya nje kidogo ya Jiji la Tokyo nchini Japan
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na mkewe Mama Asha Bilal, wakionyeshwa mafuta ya ufuta na Ofisa wa Kiwanda cha kukamua mafuta ya hayo cha Takemoto, Akira Ogawa, wakati alipotembelelea kiwanda hicho kilichopo Nagoya nje kidogo ya Jiji la Tokyo nchini Japan, jana

 Wakiendelea kutembelea kiwanda hicho.

BENKI YA CRDB YACHANGIA MILIONI 20 UJENZI WA KANISA LA KKKT JIMBO LA HAI





Mkurugenzi wa MasokoUtafiti, Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa akiwasili katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Jimbo la Hai kwa ajili ya ibada maalumu ya kuchangisha fedha kwa ajili ya ujenzi wa Kanisa la KKKT jimbo la Hai. Katika harambee hiyo Benki ya CRDB ilitoa shilingi milioni 20 kufanikisha ujenzi wa Kanisa na Kituo cha Watoto wanaoishi katika mazingira magumu.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika Kanisa la KKKT jimbo la Hai.
 Baadhi ya waumini wakiingia kanisani wakati wa ibada maalumu ya iliyofanyika katika Kanisa la KKKT jimbo la Hai, iliyokwenda sambasamba na harambee ya kuchangia kanisa hilo pamoja na Kituo cha Watoto wanaoishi katika mazingira magumu.
 Askofu wa Jimbo la Kaskazini Dk. Martin Shao akiongoza ibada ya katika Kanisa la KKKT jimbo la Hai.
 Maofisa wa Benki ya CRDB wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Dk. Charles Kimei wakiwa katika ibada maalumu ya kuchangisha fedha kwa ajili ya Kanisa la KKKT jimbo la hai.
  Askofu wa Jimbo la Kaskazini Dk. Martin Shao akiongoza ibada ya katika Kanisa la KKKT jimbo la Hai.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akipeana mkono na Askofu wa KKKT jimbo la Kaskazini, Dk. Martin Shao.