Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Wednesday, December 10, 2014

BFT WAKABIDHIWA ULINGO RASMI WA MASUMBWI


Bondia Zulfa Macho kushoto akipambana na Vumilia Kalinga wakati wa maskabidhiano ya ulingo mpya wa masumbwi Picha na SUPER D BOXING NEWS
Bondia Zulfa Macho kulia akipambana na Vumilia Kalinga wakati wa maskabidhiano ya ulingo mpya wa masumbwi Picha na SUPER D BOXING NEWS
Baadhi ya wadau wa mchezo wa masumbwi wakifatilia afla ya makabidhiano hayo
Waziri wa Habari,Vijana Utamaduni na Michezo DR. Fenela Mkangara akivishwa glove na
Mjumbe wa maendeleo ya wanawake  BFT Aisha Voniatis kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Zantel Patap Ghose wakati wa makabidhiano ya ulingo mpya wa masumbwi uliotolewa na kampuni ya Zantel Picha na SUPER D BOXING NEWS
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Zantel Patap Ghose kushoto akipeana mkono na Waziri wa Habari,Vijana Utamaduni na Michezo DR. Fenela Mkangara baada ya kukabidhi ulingo mpya wa masumbwi kulia ni Mjumbe wa maendeleo ya wanawake  BFT Aisha Voniatis  na wa pili kushoto ni Makamu wa Rais wa Shirikisho la ngumi za Ridhaa nchini 'BFT' Lukelo Willilo na Katibu mkuu wa chama hicho Makore Mashaga
Bondia Fransic Cheka kushoto akipeana mkono na Waziri wa Habari,Vijana Utamaduni na Michezo DR. Fenela Mkangara wakati wa hafla ya makabidhiano ya ulingo mpya kutoka Zantel
Bondia Fransic Cheka akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Zantel Patap Ghose
BAADHI YA WADAU MBALIMBALI WA MCHEZO WA MASUMBWI NCHINI WAKIWEMO MABONDIA WAKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA

RAIS WA ZANZIBAR DKT. SHEIN KUWA MGENI RASMI TUZO ZA TASWA


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohammed Shein anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika utoaji wa tuzo za Wanamichezo Bora Tanzania Ijumaa wiki hii.
Tuzo hizo zinaandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) na mwaka huu zimedhaminiwa na Selcom Wireless, Said Salim Bakhresa & Co Ltd - Bakhresa Group, IPTL, mifuko ya hifadhi ya jamii, PSPF na NSSF.
TASWA inaishukuru Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa ushirikiano wake na kukubali Rais Dk. Shein aje katika tuzo zetu, ambazo zitafanyika ukumbi wa Diamond Jubilee, VIP Dar es Salaam.
Kukubali kwa Dk. Shein kuwa mgeni rasmi kunaonesha jinsi gani alivyokuwa mwanamichezo wa kweli na mwenye nia ya dhati ya kushirikiana na wadau wa michezo nchini.
Katibu wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo (TASWA) Amir Mhando (kulia) akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuhusu tuzo za TASWA zinazotarajiwa kufanyika jumamosi hii katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam. Katikati ni Makamu Mwenyekiti wa TASWA, Egbert Mkoko na mjumbe wa Kamati ya Utendaji, Mwani Nyangasa 
******************************
Wanamichezo 44 wanatarajiwa kupewa tuzo siku hiyo baada ya kufanya vizuri katika michezo mbalimbali kuanzia Juni 2013 hadi Juni 2014. Pia itatolewa Tuzo ya Mwanamichezo Bora wa jumla na Tuzo ya Heshima.
TASWA imewahi kutoa Tuzo ya Heshima kwa Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa, pia imewahi kutoa Tuzo ya Heshima kwa timu ya soka ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ iliyokuwa ikicheza mechi za kufuzu fainali za mataifa ya Afrika mwaka 1980 zilizofanyika Lagos, Nigeria.
Tunaamini zitakuwa tuzo za aina yake, ambapo tayari Kamati ya Kusimamia Tuzo hizo imeshatangaza majina ya wanamichezo zaidi ya 100 wanaowania tuzo mbalimbali.

Monday, December 8, 2014

PAMBANO LA MAOKOLA NA MKALAKALA





CHAMA cha Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBC),
limeidhinisha pambano la ubingwa wa taifa uzani
wa kilo 69 litakalowakutanisha Ibrahim Maokola
dhidi ya Selemani Mkalakala.
Kwa mujibu wa Rais wa TPBC, Chaurembo Palasa,
pambano hilo limepangwa kufanyika Desemba 19,
mwaka huu kwenye Ukumbi wa Vigae Pub,
Mbagala jijini Dar es Salaam.
Palasa alisema pambano hilo litasindikizwa na
mapambano mengine ya utangulizi kati ya Abdallah
Mohamed dhidi ya Salehe Mkalekwa.
Alisema maandalizi kuelekea kwenye pambano hilo
ni mazuri na kwamba wanategemea mashabiki
wengi watajitokeza kuwaunga mkono vijana hao.
“Tumekuwa tukihamasisha mchezo wa ngumi
sehemu mbalimbali ili kuleta mvuto kwa wakazi wa
jiji na sehemu nyingine ili kuvutia wadhamini,”
alisema Palasa.
Alisema ngumi sio mchezo wa fujo kama baadhi ya
watu wanavyodhani, bali ni mchezo wa
wastaarabu ambao wanapigana kwa kufuata
sheria. Alisema atakayebainika kukiuka sheria
zilizowekwa awe ni bondia au promota
atachukuliwa hatua za kisheria.

BENKI YA CRDB YAIBUKA KIDEDEA TUZO ZA NBAA


 Naibu waziri wa fedha Adam Malima akimkabidhi meneja wa fedha wa benki ya CRDB Sosteness Biseko  tuzo  ya NBAA ya ushindi  katika  uandaaji wa taarifa bora za fedha mwaka 2013-2014,jumla ya benki tisa zilishiriki ambapo Benki ya CRDB iliibuka mshindi wa kwanza katika kundi la mabenki, hafla hiyo ilifanyika juzi katika hotel ya Mount Meru jijini Arusha
*********

Mashirika binafsi ,taasisi na idara mbalimbali za serikali zimehimizwa kushiriki katika mashindano ya tuzo zinazotolewa na bodi ya wahasibu na wakaguzi wa hesabu nchini NBAA katika uandaaji bora wa taarifa za fedha za mwaka ili kuboresha hesabu za mashiriki hayo na kuongeza uwazi katika shughuli za biashara za ndani ya nchi na kimataifa 

Mwenyekiti wa bodi ya wahasibu na wakaguzi wa hesabu nchini NBAA Profesa Issaya Jairo ametoa kauli hiyo jijini Arusha wakati wa kufunga  mkutano mkuu wa mwaka wa bodi hiyo ulio enda sambamba na utoaji wa tuzo na vyeti kwa washindi  katika uaandaaji  bora wa taarifa za fedha za mwaka ambapo kwa mwaka 2014 jumla ya washiriki 40 walishiriki ambao waligawanywa katika makundi 11 kulingana na huduma wanayo itoa

Katika kundi la mabenki, benki ya crdb ilibuka mshindi  wa kwanza kwa mwaka2013-2014 na kupata tuzo maalumu ya uandaaji  wa taarifa bora  za fedha za mwaka iliyokabidhiwa na naibu waziri wa fehda Adam Malima  kwa meneja wa fedha wa benki hiyo Sosthenes Biseko ambaye akizungumzia ushindi huo amesema ni njia mojawapo ya kuudhihirishia umma wa watanzania kuendelea kuwa na Imani na benki.
Wafanyakazi mbalimbali wa benki ya CRDB wakiwa katika picha wakati wa makabidhiano hayo.

FAINAL YA MASHINDANO YA WAZI YA TAIFA YA NGUMI YALIVYO MALIZIKA MWISHONI MWA WIKI UWANJA WA NDANI WA TAIFA



 
 Mabondia latifa Halidi  kushoto wa Kigoma na Vumilia Kalinga wa JKT wakioneshana umwanmba wa kutupiana makonde wakati wa mashindano ya taifa ya wazi yaliyomalizika mwishoni mwa wiki iliyopita picha na SUPER D BOXING NEWS
Makamu wa Rais wa Shirikisho la ngumi za Ridhaa nchini 'BFT' Lukelo Willilo akimvisha medali ya dhaabu bondia Robert Kyaruzi baada ya kushinda katika fainal ya mashindano ya taifa ya wazi iliyomalizika mwishoni mwa wiki iliyopita
Mabondia Siwatu Elieta kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Zulfa Macho wakati wa fainali za mchezo wa masumbwi Macho alishinda kwa point mpambano huo
 Mabondia latifa Halidi  kushoto wa Kigoma na Vumilia Kalinga wa JKT wakioneshana umwanmba wa kutupiana makonde wakati wa mashindano ya taifa ya wazi yaliyomalizika mwishoni mwa wiki iliyopita picha na SUPER D BOXING NEWS

 Mfanya biashara na mdau na promota maarufu nchini Zahoro Maganga akisalimiana na bondia 
 wakati wa fainali
ya mashindano ya taifa

DAKITARI KANJANJA AMBANBWA MUHIMBILI



aSKARI WA HOSPITALI YA tAIFA YA MUHIMBILI AKIMUEKA SAWA KOT ANAEDAIWA DAKITARI FEKI BAADA YA KUDAKWA LEOAL,IEJITAMBULISHA KWA JINA LA DISMAS MACHA

DAKITARI FEKI AKIONYESHA MIPIRA YA KUVAA WAKATI WA KUMUHUDUMIA MGOJWAAMBAYO ALIKUTWA NAYO KWENYE BEGI LAKE

DAKITARI FEKI AKIONYESHA NYARAKA ZA MBALIMBALI ZIZOTUMIKA WAKATI ANAPOTOA HUDUMA PAMOJA NA KARATASI ZA KUANDIKIWA MGONJWA BAADA KUMUONA DAKITARI

ANAEDAIWA DAKITARI FEKI  AKIONYESHA VITU VILIVYOKUTWA KATIKA BEGI LAKE WA OPILI KUSHOTO NI MKURUGENZI WA HOSPOTALI YA MOI AMBAKO ALIKOKAMATWA DAKITARI HUYO LEO

MAAFISA WA USALAMA PAMOJA NA MADAKITARI WA MUHIMBILI WAKIMUHOJI DAKITARI FEKI

MKURUGENZI WA HOSPITALI YA MOI DK OTHMAN AKIWAELEZA WANDISHI WA HABARI KUHUSU DAKITARI FEKI LEO

DAKITARI FEKI AKIWA NA DAFTARI ALILOKUWA ANAPITA WODINI KUWACHANGISHA WAFANYAKAZI  PESA KWANI MKE WAKE AMEFARIKI NCHINI INDIA ALIKOPELEKWA KUTIBIWA

DAKITARI FEKI  AKIWAONYESHA WANDISHI WA HABARI MOJA YA KITABU CHA MASWALA YA MAGONJWA YA AKINA MAMA AMBAYO DAKITARI HUYO ALIKUA ANADILI NAYO

AKIWAELEZEA WANDISHI WA HABARI




ASKARI WA USALAMA WAKIMSINDIKA DAKITARI FEKI KUMPELEKA KITUONI KWA UCHUNGUZI ZAIDI

AKIWA CHINI YA ULINZI MKALI

AKISUBIRI GARI
AKIINGIZWA KWENYE GARI NA KUELEKEA KITUO CHA POLISI CHA SALANDA

BAADHI YA WATU MBALIMBALI WALIOFIKA KUMUONA

WALIOFIKA KUMUONA DAKITARI FEKI

DANNY MRWANDA ASAINI YANGA AWAMWAGA SIMBA USIKU HUU


HABARI zilizotufikia usiku huu, zinasema kuwa Mshambuliaji wa timu ya Polisi Moro, Danny Mrwanda, amesaini mkataba wa mwaka mmoja kuitumikia Klabu ya Yanga ya jijini Dar es salaam, usiku huu.

Imekuwa ni tofauti na mategemeo ya mashabiki walio wengi wa soka kutokana na habari zilizozagaa kuanzia juzi kuwa mchezaji huyo 'eti' alikuwa tayari ameshakamilisha taratibu zote za kujiunga na Klabu ya Simba, ambao walimtaka na kufanya naye mazungumzo.

Kama ambavyo imekuwa kwa timu hizi watani wa jadi kufanyiana 'Kitu Umafia', mara kadhaa kwa kuchukuliana wachezaji na kupandiana dau kama ilivyokuwa kwa baadhi ya wachezaji akiwamo, Mbuyu Twite, na wengineo na ndivyo Yanga walivyofanya tena kwa Mrwanda usiku huu.

Ikumbukwe kuwa Simba, walikuwa wameshatangaza dau la kumsajili mchezaji huyo katika kipindi hichi cha dirisha dogo na tayari taratibu zilikuwa zimekwishaanza.

Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya Klabu ya Yanga kinasema kuwa,Yanga imeamua kumsajili Mrwanda ili kuchukua nafasi ya Said Bahanuzi aliyetolewa kwa mkopo kwenda Polisi Morogoro wakati Jerry Tegete akiwa ni majeruhi, na mshambuliaji pekee wa ndani aliyebaki tegemeo akiwa ni Hussein Javu.

Friday, December 5, 2014

SUPER D BOXING COACH KARIKA HARAKATI ZA KUINUA MCHEZO WA MASUMBWI NCHINI


Kocha kimataifa  wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' akionesha baadhi ya nakala za DVD ambazo utumia kufundishia mbinu za mataifa mbalimbali wakiwemo mabondia wanaotamba Duniani kwa sasa ambazo anaziuza kwa ajili ya vijana kupata hamasa zaidi ya kufanya mazoezi kwa bidii
super d


Kocha kimataifa  wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' akionesha baadhi ya nakala za DVD ambazo utumia kufundishia mbinu za mataifa mbalimbali wakiwemo mabondia wanaotamba Duniani kwa sasa ambazo anaziuza kwa ajili ya vijana kupata hamasa zaidi ya kufanya mazoezi kwa bidii





super d akifuraia ushinda wa shabani kaoneka

MANJU MSITA KUPEPERUSHA BENDERA MOZAMBIQUE FASHION WEEK 'MFW-2014'


Mbunifu wa Mavazi nchini Manju Msita kulia akizungumza na waandishi wa habari juu ya ushiriki wake katika Mozambique Fashion Week yatakayoanza desemba 10 mpaka 14 ambapo atakuwa akipeperusha bendera ya taifa
Mwanamitindo Matukio Chuma kulia akizungumza na wahandishi wa habari wakati wa kutangaza  upeperushwaji wa bendera ya tanzania katika nchi ya mozambique fashion week ambayo mbunifu wa mavazi Manju Msita atashiriki na kupeperurusha bendera ya Tanzania kushoto ni mwanamitindo Vivian Williams ambaye anafanya shughuli zake za uwanamitindo nchini Barcelona .Spain
Mwanamitindo anaefanya shughuli zake nchini Barcelona Spein Vivian Williams kushoto akizungumza na waandishi wa habari juu ya ujio wake nchini kwa ajili ya kushiriki maonesho ya SwaHILI fASHION WEEK yatakayoanza ijumaa ya Desemba 5 mpaka 7 kulia ni Mwanamitindo Matukio Chuma
Mbunifu wa Mavazi nchini Manju Msita katikati akiwa na wanamitindo
anaefanya shughuli zake nchini Barcelona Spein Vivian Williams na Ieva Stropule anaeishi ujerumani

Kocha wa kimataifa wa mchezo wa ngumi nchini Rajabu Mhamila kushoto  akiangalia zawadi  aliyopewa na mwanamitindo Matukio Chuma iliyotoka kwa Manju Msita
Kocha wa kimataifa wa mchezo wa ngumi nchini Rajabu Mhamila kushoto  akipokea zawadi kutoka kwa mwanamitindo Matukio Chuma iliyotoka kwa Manju Msita
Kocha wa kimataifa wa mchezo wa ngumi nchini Rajabu Mhamila kushoto  akipokea zawadi kutoka kwa mwanamitindo Matukio Chuma iliyotoka kwa Manju Msita