Yanga SC imeonesha kukomaa baada ya kuipokea ofa ya Azam FC na kwa mujibu wa mwenyekiti wake Imani Madega, “wao kama Yanga hawana mpango wa kumzuia Ngasa na mchezaji yoyote atakayependa kuhama kwani kuhama kwao kutatoa nafasi kwa Yanga kusajiri wachezaji wengine nyota.
Suala la Ngasa kusajiliwa Azam FC limezuka kama filamu, na sasa limekuwa likifuatiliwa na wapenzi wengi wa Mchezo wa mpira wa miguu, awali leo mchana, Azam FC imepeleka barua ya kuomba kumsajili Ngasa ikiwa na ofa ya 25 Milioni. Kiasi hiki ni kikubwa sana kwa mujibu wa wachambuzi wa masuala ya usajiri wa wachezaji kwani Ngasa amebakisha mwaka mmoja tuu na sheria za FIFA zinamruhusu mchezaji aliyebakisha mwaka mmoja kuunnua mkataba wake kwa kuilipa klabu aliyokuwa akiichezea mshahara wote uliobaki. Lakini Azam FC licha ya kufahamu sheria hiyo bado imeonesha uungwana na nia njema kwa kuamua kutoa ofa nzuri ambayo ni rekodi nchini.
Juma kaseja ndiye anayeshikiria rekidi ya uhamisho ambapo Uhamishowake kwenda Yanga uliigharimu timu hiyo ya Jangwani Milioni 24 na kama deal hili la Ngasa litafanikiwa basi Yanga na Ngasa watakuwa wakishikilia rekodi ya usajiri wa fedha nyingi kwa wachezaji wa ndani.
Gazeti la Mwanaspoti nalo lina habari kuwa, nanukuu “MAMILIONI ya fedha aliyoahidiwa na klabu ya Azam yamemrudisha nyumbani Mrisho Ngassa na jana alitarajiwa kukutana na uongozi wa Yanga na kuwaelezea nia yake ya kutaka kutosajiliwa tena na klabu hiyo msimu ujao.
Ngassa alisema jana kuwa ameamua kurejea nyumbani baada ya kuona kuwa fedha alizopewa na APR ya Rwanda ni ndogo zikilinganishwa na zile alizoahidiwa na Azam.
'' Kweli tulifanya mazungumzo na APR wiki hii, lakini walikuwa wanasuasua kunipa fedha ambayo niliitaka mimi na nilipofuatwa na Azam wakanieleza dau kubwa zaidi, ndipo nikaona nisipoteze muda bora nije kuzungumza nao, '' alisema Ngassa ambaye amekuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom msimu uliopita.
Alisema kuwa alitarajia kukutana na uongozi wa Yanga ili kuwaeleza nia yake ya kutua Azam na kuwaweka wazi fedha anazopata na kuwaomba wamruhusu kwani mpira ni ajira kwa sasa.
'
' Kwa sasa mimi ndio najitengenezea maisha yangu mpira ukiisha hapa sijafanya kitu chochote kesho na kesho kutwa nitavyokuwa naomba omba watu wananisema sana, hivyo naomba viongozi wa Yanga wanielewe na kuniruhusu kuichezea Azam msimu ujao,'' alisema.
Pia, aliongeza kuwa uamuzi wake anaamini kuwa ni sahihi kutokana na fedha alizoahidiwa kuwa ni nyingi na anaamini kuwa Yanga hawawezi kumsajili kwa fedha hizo hata iweje.
"Ni zaidi ya fedha ambazo walitaka kunipa APR ambao katika maongezi ya mwanzo walikubaliana nami Shilingi 20 na Azam wananipa zaidi ya hapo.
"Ninawaomba mashabiki wa Yanga wakubaliane na uamuzi wangu huo kwa ajili ya maisha yangu na ukizingatia nimeitumikia kwa miaka mingi timu hiyo tena kwa moyo mmoja hivyo wasiupokee vibaya uamuzi wangu huo," alisema.
Alisema hana shida na viongozi wake anaamini pindi watakapokutana na wenzao wa Azam watafika muafaka na kumruhusu kwa moyo mmoja kuichezea timu hiyo ambayo imekuwa na upinzani kwenye ligi msimu uliopita.
Hata hivyo, mchezaji huyo alitangaza dau lake kupitia gazeti la Mwanaspoti kuwa yupo tayari kuondoka Yanga endapo klabu inayomtaka iko tayari kutoa Shilingi 40 milioni.
No comments :
Post a Comment