Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Friday, December 9, 2011

RAIS DK. JAKAYA KIKWETE AONGOZA WATANZANIA KATIKA SHEREHE ZA MIAKA 50 YA UHURU WA TANZANIA

Rais Dk. Jakaya Kikwete akisalimiana na viongozi wa nchi mbalimbali waliohudhuria katika maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru wa Tanzania yanayofanyika kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam mchana huu hapa akisalimiana na Rais wa Namibia Mhshimiwa Hifikepunye Pohamba. FULLSHANGWE inakumuvuzishia moja kwa moja matukio ya maadhimisho hayo kutoka kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam ili kukujuza mambo mbalimbali yaliyojiri katika sherehe hizo.
Rais Jakaya Kikwete akielekea Jukwaa kuu mara baada ya kukagua gwaride katika sherehe za miaka 50 ya uhuru wa Tanzania kwenye uwanja wa Uhuru huku akiwa ameongoza na na Mkuu wa Majeshi nchini Jenerari Davis Mwamunyange.
Rais Jakaya Kikwete akikagua vikosi vya ulinzi na usalama wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru wa Tanzania kikosi hiki ni cha Jeshi la Wananchi wanawake
Rais Jakaya Kikwete akikagua vikosi vya ulinzi na usalama wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru wa Tanzania kikosi hiki ni cha Jeshi la Wananchi wanaume.
Rais jakaya Kikwete akipokea heshima wakati mizinga ikipigwa na jeshi la wananchi kwa heshima ya Rais.
Hiki ni kikosi cha Jeshi la wananchi wanamaji kikiwa tayari kutoa heshima kwa amiri jeshi mkuu na Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tamnzania Dk. Jakaya Kikwete.
Rais Dk. Jakaya Kikwete akipungia mkono wananchi wakati alipowasili kwenye uwanja wa uhuru kwa ajili ya kuongoza sherehe za miaka 50 ya Tanzania.
Msafara wa Rais Dk Jakaya Kikwete ukiwasili kwenye uwanja wa Uhuru tayari kwa kuongoza watanzania katika sherehe za miaka 50 ya Tanzania.
Walinzi wa rais walikuwa kivutio katika sherehe.wakati msafara wa Rais Dk. Jakaya Kikwete ukiwasili katika uwanja wa Uhuru leo.

MHESHIMIWA HAMAD RASHID NDANI YA RANGI ZA NJANO NA KIJANI



Mbunge wa Jimbo la Wawi Pemba kupitia Chama cha Wananchi CUF, Hamad Rashid, akijumuika na vijana wa CCM pamoja na Msindai kucheza miondoko ya Taarab, ikiwa ni sehemu ya kusherehekea mkesha wa maadhimisho ya sherehe za miaka 50 ya Uhuru zilizofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo.
Wasanii wa kundi la Sanaa la Safi Theatre, wakimpagawisha Mbunge Msindai, jukwaani wakati wakishambulia jukwaa.
Wasanii wa Kundi la Safi wakiwapagawisha wananchi waliohudhuria sherehe hizo.
Kapten John Komba, akiongoza kundi lake la Kwaya kuimba wimbo maalum wa Maadhimisho ya Sherehe hizo jukwaani.
Wasanii wa Kundi la Sanaa la Safi Theatre, wakionyesha umahiri wao jukwaani wa kucheza Sarakasi.
Baadhi ya Wabunge na wananchi wakimtunza Kaptein John Komba wakati akiimba jukwaani.

HATIMAYE ULIFIKA MUDA WA KUANZA RASMI SHAMBRASHAMBRA ZA MAFATAKI.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akibonyesha Rimoti kufyatua Mafataki ikiwa ni sehemu ya kuzindua rasmi Mkesha wa Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 50 Uhuru zilizofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja usiku wa kuamkia leo. Kutoka (kushoto) ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Idd, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Mke wa Makamu wa Rais, Mama Zakhia Bilal na (kulia) ni Mke wa Makamu wa Rais, Mama Asha Bilal.
Mafataki yakifyatuka baada ya kuzinduliwa rasmi na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal.
Mafataki yakifyatuka baada ya kuzinduliwa rasmi.
Mafataki yakifyatuka baada ya kuzinduliwa rasmi.
Makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamanda Suleiman Kova, baada ya kuzindua rasmi sherehe hizo kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam usiku wa kuamkia

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL, MGENI RASMI MKESHA WA SHEREHE ZA MIAKA 50 YA UHURU MNAZI MMOJA DAR



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza kuwahutubia wananchi waliohudhuria mkesha wa sherehe za Maadhimisho ya Miaka 50 ya Uhuru, zilizofanyika usiku wa kuamkia leo kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck sadick, akizungumza jukwaani kutoa salam za sherehe hizo kwa wananchi.
Baadhi ya Viongozi wa Kisiasa na wananchi waliohudhuria sherehe hizo.
Baadhi ya Viongozi wa Kisiasa na wananchi waliohudhuria sherehe hizo.
Vijana wakishangia burudani iliyokuwa ikitolewa jukwaani na makundi mbalimbali ya sanaa, wakati wa sherehe hizo.
Wasanii wa Kundi la Safi wakiwapagawisha wananchi waliohudhuria sherehe hizo.
Wanamuziki wa Bendi ya Msondo Ngoma, wakiimba jukwaani ikiwa ni sehemu ya kutoa burudani maalum ya kusherehekea sherehi hizo.
Rapa na mwimbaji wa Bendi ya TOT Plus, Jua Kali, akighani rap zake jukwaani wakati wa mkesha wa sherehe hizo.
Wanenguaji wa Bendi ya Msondo Ngoma, wakishambulia jukwaa wakati wa mkesha wa sherehe hizo.
Wasanii wa Kikundi cha Sanaa cha JKT Mgulani, wakishambulia jukwaa kwa kucheza ngoma ya Bugobogobo ya Kabila la Wasukuma, wakati wa sherehe hizo.
Mbunge, John Shibuda, akipagawishwa na ngoma ya Kisukuma ya Bugobogobo, iliyokuwa ikipigwa na wasanii wa kundi la JKT Mgulani.
Wasanii wa Kundi la Taarab la Culture kutoka Zanzibar, wakitoa burudani jukwani.

Wednesday, December 7, 2011

MTONI KIJICHI KUTAWAKA MOTO DESEMBA 25 RASHIDI MATUMLA NA MANENO OSWARD



MLEZI wa mchezo wa ngumi 'Masimbwi 'Mawe' Tanzania kamanda wa Polisi
wa kanda maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova anatarajia kuwa mgeni
rasmi katika pamabano kati ya Rashid Matumla ‘Snake Man’ na Maneno
Osward ‘Mtambo wa Gongo’ linalotarajia kufanyika Desemba 25 katika
ukumbi wa Heinken, Mtoni Kijichi Dar es Salaam.

Pambano hilo lisilo la ubingwa linatarajia kuwa katika uzito wa middle
weihgt raundi 10.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Maneno Osward alisema atahakikisha
anamtwanga mpunzani wake ili kufuta machungu ya kumzidi kwa pointi
katika pambano lao walilocheza hivi karibuni.

"Matumla alinizidi kwa pointi sasa nataka kumonyesha kama ninauwezo wa
kumuangusha katika hatua za awali za pambano letu kwani nimejiandaa na
bado naendelea kujifua kwa ajili ya pambano hilo," alisema Maneno.

Naye kwa upande wake Rashid alisema, anaendelea kujifua ili kuweza
kuwapa raha mashabiki wake ikiwa na kuwapa zawadi ya Christimas kwa
kumtwanga kwa mara nyingine Maneno.

"Ushindi wangu ndio utakuwa zawadi kwa mashabiki wangu kwani
sinachazaidi cha kuwapa," alisema Rashid.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Adios Promotion, Shabani Adios 'mwayamwaya'
ambaye ndiye muandaaji wa pambano hilo, alisema kabla ya kufanyika kwa
pambano hilo mabondia hao watapima vipimo mbalimbali vikiwemo ukimwi
na madawa ya kuongeza nguvu ili kuweza kuwatayari kwa ajili ya
mpambano.

Mapambano ya utangulizi yatakuwa kati ya mabondia Venas Mponji
atakayezichapa na Tumaini Maguno 'SMG' na bondia Rashidi Ally
atazichapa na Kulwa Mbuchi, Selemani Jumanne na Ibrahimu Madeusi
wakati Shabani Zunga atavaana na Mohamedi Kashinde, na bondia Sweet
Kalulu na Saleh Mtalekwa

Katika Mchezo huo kutakua na DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi pamoja
na kutambua sheria zake mbalimbali zitakazokua zikisambazwa na kocha
wa mchezo huo mkoa wa kimichezo wa Ilala Rajabu Mhamila 'Super D' kwa
ajili ya kuwapa mambondia mbalimbali mbinu za mchezo na mashabiki
kujua sheria za masumbwi.


--
Super D Boxing Coach
Photojournalist at Majira, Business Times
Email.superdboxingcoach@gmail.com
www.burudan.blogspot.com
Mob;+255787 406930
+255774406938
Po.Box. 15493
Dar es Salaam Tanzania

CASTLE LITE YADHAMINI MASHINDANO YA MPIRA WA KIKAPU



CASTLE LITE YADHAMINI MASHINDANO YA MPIRA WA KIKAPU
Dar es Salaam, 07,DECEMBER 2011:
Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia Bia yake ya Castle Lite, leo imetangaza udhamini wa mashindano ya mpira wa kikapu yatakayofanyika jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 11/12/2011 hadi tarehe 17/12/2011.
Akizungumzia udhamini huo Meneja wa Bia ya Castle Lite Bi. Pamela Kikuli alisema; “Tunafurahi sana kupata nafasi hii ya kudhamini mashindano haya muhimu, tumeamua kushirikiana na Shirikisho la mpira wa Kikapu Tanzania (TBF) kuhakikisha mashindano haya yanafanyika katika hali ya ufanisi mkubwa. Mchezo wa mpira wa kikapu umekuwa na mvuto mkubwa na kuendelea kujizolea mashabiki wengi hapa nchini na Ulimwenguni kwa ujumla. Zaidi ya kuwa chanzo kizuri cha ajira kwa vijana, mchezo huu pia unatoa fursa kwa washiriki kufanya mazoezi ya kutosha na hivyo kuwa na afya bora wakati wote”.
Bia ya Castle lite ambayo inawalenga na kuhamasisha zaidi watu wanaojali afya zao, imeamua kuonesha hayo kwa vitendo kwa kudhamini mashindano haya na kuhakikisha inashirikiana na vyombo husika kuhakikisha kuwa mchezo wa mpira wa kikapu unakuwa hapa nchini. Aliongeza Bi. Pamela.
Akizungumzia thamani ya udhamini, Bi Pamela alisema; Castle Lite imetoa jumla ya shilingi Milioni Ishirini na Nane (28,000,000/-) ili kufanikisha mashindano haya. Tuna imani kuwa fedha hizi zitatumika vema katika maeneo yaliyokusudiwa ili kuleta tija katika mchezo huu wa mpira wa kikapu na tutaendelea kuwa mstari wa mbele kuendeleza mchezo wa kikapu hapa nchini.
Nae meneja mahusiano na habari wa Tbl Bi Edith Mushi akitaja mikoa itakayoshiriki alisema mashindano hayo kwa mwaka huu yatashirikisha mikoa kumi na nane ya Tanzania ambayo
ni.Ilala,Pemba,Tabora,Manyara,Kinondoni,Mwanza,Kilimanjaro,Morogoro,Temeke,Tanga,Iringa,Arusha,Unguja,Mara,Rukwa,Lindi,Shinyanga na mbeya.
Alisema mashindano hayo yatashirikisha timu za wanaume na wanawake na yanatarajia kuwa na msisimko mkubwa miongoni mwa jamiii ya wanamichezo kote nchini.
Kwa upande wake katibu mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania Bw. Mike Maluwe, alitoa shukurani na pongezi nyingi kwa Bia ya Castle Lite kwa ushirikiano mkubwa waliotoa kwa kudhamini mashindano haya ya mwaka 2011 yatakayoshirikisha mikoa 18 ya Tanzania. “Castle Lite imeonesha moyo wa Uzalendo kwa kuwa mstari wa mbele kudhamini mashindano haya, kwa kushirikiana na mdhamini huyu tuna imani kubwa kuwa mchezo wa mpira wa kikapu utapata msukumo mkubwa utakaoleta maendeleo ya kweli katika mchezo huu hapa nchini; Alisema Maluwe.
Sisi viongozi wa shirikisho na wapenzi wa mpira wa kikapu hapa nchini, Tuna imani kubwa kuwa udhamini huu utaongeza chachu ya ushindani kwa timu zitakazoshiriki na hivyo kuongeza tija katika mchezo huu hapa nchini. Tunawaomba wapenzi na mashabiki wa mpira wa kikapu kujitokeza kwa wingi katika viwanja viliyvotajwa ili kuja kushuhudia na kushangilia timu zao wakati wote wa mashindano.

DVD MPYA ZA MWEZI HUU HIZI HAPA







MIAKA 50 YA UHURU YAENDEREA KUFANA VIWANJA VYA SABASABA


Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano na Matangazo wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) Bi, Sarah Kibonde (kushoto) na Ofisa uhusiano wa mamlaka hiyo wakitoa maelekezo, mbalimbali kutoka kwa wananchi waliofika katika banda lao wakati wa Mahadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara katika viwanja vya Mwalimu nyerere sabasaba Dar es salaam

mabondia kupima uzito kesho


MABONDIA Ramadhani Nasibu na Antony Kairuki wa Kenya wanatarajia kupima uzito kesho kwa ajili ya pambano lao la maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanganyika litakalofanyika kesho kutwa katika ukumbi wa DDC, Keko Dar es Salaam.

Pamabno hilo lisilo la ubingwa litakuwa katika uzito kg 51 la raundi nane .

Akizungumza Dar es salaam jana, Mratibu wa pambano hilo Pius Agaton alisema lengo hasa ni kusheherekea miaka 50 ya Uhuru ikiwa ni sambamba na kuwapima ubavu mabondia hao.

Alisema, maandalizi yamekamilika ambapo mabondia wote wanaendelea kujifua ambapo pia bondia huyo kutoka Kenya yupo nchini kwa ajili ya kujiweka sawa ikiwa ni pamoja na kukamilisha taratibu zote za kimashindano.

"Naimani mashindano yatakuwa mazuri kwani mabondia wote ni wazuri na wamejiandaa hivyo mashabiki wa subiri kupata burudani hiyo ikiwa ni pamoja na kuadhimisha miaka 50 ya Uhuru

RAIS DK JAKAYA KIKWETE AKISALIMIANA NA MKURUGENZI WA FULLSHANGWE AFURAI KUSHIKWA MKONO NA JK LEO



Pamoja na majukumu yangu magumu nimefurahi kwani leo nilipata wasaa wa kusalimiana na Rais Mh. Dk. Jakaya Kikwete mara baada ya kulifungua rasmi jengo la Golden Jubilee Towers, ilikuwa ni fursa nzuri kwangu na niliifurahia, Ninamtakia Afya njema na kazi njema katika majukumu yake ya kuongoza watanzania kwa ujumla na namtakia kila mafanikio katika kazi zake na Serikali yake.

SERENGETI YADHAMINI TIMU ZA WABUNGE NA WAWAKILISHI NA KUKABIDHI VIFAA VYA MICHEZO

Katikati ni Mkurugenzi wa Mawasiliano kampuni ya SBL.Teddy Mapunda akikabidhi kombe kwa viongozi wa timu ya Bunge na Timu ya Baraza la Wawakilishi.Pichani kulia ni Kapteni wa timu ya Bunge,Mh Amos Makala na kushoto ni Mwenyeki wa timu ya Baraza la Wawakilishi,Mh Hamza Hassani Juma.
Mkurugenzi wa Mawasiliano kampuni ya SBL.Teddy,Mapunda akizungumza mbele ya wanahabari mapema leo Makao Makuu ya ofisi hizo zilizopo Oysterbay,jijini Dar,kuhusiana na udhamini wa mechi kati ya Timu ya Wabunge na Timu ya Baraza la Wawakilishi kutoka Zanzibar,itakayofanyika 9 Desemba kwenye Uwanja wa Uhuru,ikiwa ni sehemu mojawapo ya kusherehekea miaka 50 ya Uhuru,aidha Teddy amesema kuwa udhamini wa timu hizo umegharimu kiasi cha zaidi ya milioni 65.
Mkurugenzi wa Mawasiliano kampuni ya SBL.Teddy,Mapunda (katikati), akizungumzia namna udhamini wao utakavyokuwa kwa timu hizo, wengine kulia na kushoto ni Nahodha wa timu ya Bunge, Mh Amos Makalla na Mwenyekiti wa timu ya Baraza la Wawakilishi, Mh Hamza Hassani Juma.
Wawakilishi nae akifafanua zaidi namna watakavyowakabili wapinzani wao Desemba 9 mwaka huu ndani ya Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Kapteni wa Timu ya Wabunge,Mh Amos Makala akizungumza ni namna gani wamejipanga kuhusiana na mechi hiyo itakayokuwa ya kusisimua dhidi ya mahasimu wao Timu ya Baraza la Wawakilishi kutoka Zanzibar.

Mwenyekiti wa timu ya Baraza la wawakilishi Mkurugenzi wa Mawasiliano kampuni ya SBL.Teddy Mapunda akikabidhi kombe kwa viongozi wa timu ya Bunge na Timu ya Baraza la Wawakilishi.Pichani kulia ni Kapteni wa timu ya Bunge,Mh Amos Makala na kushoto ni Mwenyeki wa timu ya Baraza la Wawakilishi,Mh Hamza Hassani Juma.

Monday, December 5, 2011

Miguel Cotto achakaza Antonio Margarito na kulipiza kisasi baada ya mara ya kwanza kudundwa


Miguel Cotto (right) connects against Antonio Margarito during their fight at Madison Square Garden. Cotto won by TKO before the 10th round when the ring doctor stopped the fight.
Antonio Margarito akionekana jicho lake limevimba kutokana na masubwi aliyokua anatupiwa

Benki ya Twiga kutumia miundombinu ya Benki Ya Posta kutoa huduma za fedha


C E O wa Twiga Bank, Hussein Mbululo.
KATIKA jitihada za kuboresha huduma za kibenki na kusogeza huduma zaidi kwa wateja, Benki ya Twiga Bancorp Limited inaanzisha ushirikiano na Benki ya Posta Tanzania kutoa huduma ya kusafirisha pesa (monygram).

Akiongea na gazeti hili, katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere (sabasaba) ambako benki ya Twiga inashiriki maonesho ya miaka 50 ya uhuru, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Twiga, Hussein Mbululo alisema katika juhudi za benki ya Twiga kuboresha huduma na kuzifanya kuwa za uhakika, benki hiyo imeamua kwa kanzia kutumia miundombinu ya benki ya Posta Tanzania kuwafikia wateja wake.

Amesema utaratibu huo utaanza kutumika mapema mwaka ujao.

“Kufuatia kuongezeka kwa ushindani katika biashara ya kutuma pesa, benki yetu imeamua kujizatiti kwa kutumia mtandao wa benki ya posta kufikisha huduma kwa wateja wote kote nchini, hii itasaidia kufanya huduma zetu kuwa nzuri na za uhakika,” alisema Mbululo.

Alisema utaratibu wa kutuma pesa kwa njia ya moneygram ni huduma ya pekee inayotolewa na benki ya Twiga na kwamba unamuwezesha mteja kutuma na kupokea pesa akiwa nje na ndani ya nchi.

Benki ya Twiga pia inatoa huduma za fedha kwa kutumia mtndao wa Umoja Switch Automatated Teller Machine.

Kwa mujibu wa Mbululo, benki ya Twiga ilianzishwa mwaka 1992, wakati huo ikiitwa National Bureau De Change.

Hata hivyo mwaka 1998, beni ya Twiga ilibadilishwa na kuwa benki isiyopokea amana lakini ikajikita zaidi katika kutoa huduma za kibenki.

Akielezea mafanikio ya benki hiyo, Mbululo alisema Twiga imekuwa benki pekee ya wazawa ambayo imeweza kustahimili changamoto mbalimbali katika ushindani pasipo kutegemea ruzuku kutoka serikalini.

Alisema mbali na kutengeneza faida kubwa kila mwaka, kufikia Sepemba, 2011 benki ilikuwa imepokea kiasi cha Sh 50 billioni kutoka kwa wateja na kutoa mikopo ya kiasi cha Sh 30 billioni.

Mbululo aaliongeza kuwa, benki ya Twiga ambayo kwa sasa ina matawi manne, Dar es Salaam, Mwanza na Arusha inafanya mandalizi ya kufungua matawi zaidi katika mkoa wa Dodoma na Kigamboni jijini Dar es Salaam.

Aidha, Mbululo alihaidi kuwa benki yake itaendelea kusimamia na kuwasaidia wajasiriamali wadogowadogo (SMEs) kwa kuwapatia mikopo yenye masharti nafuu naya uhakika kwani ndio hasa kichocheo cha ukuaji wa uchumi nchini.

Kwamujibu wa Mbululo benki inajipanga kuzidi kujiimarisha kwa kuboresha huduma mbalimbali ili kuendana na wakati na kuhimili ushindani kutoka kwa benki zaidi 40 za kibiashara hapa nchini.

Ameongeza kuwa, benki inawashauri na kuwataka wananchi kufungua na kutumia akaunti za watoto yaani ‘Twiga Kids Account na ile ya Holiday Account’ ambazo zimeanzishwa hivi karibuni kwa madhumuni ya kuwasaidia wazazi na walezi kuwawekea akiba watoto wao pamoja na kuweka fedha kwaajili ya safari za mapumzikoni na wakati huu wa siku kuu.

TIGO WAGAWA VITABU UDOM PAMOJA NA KUPROROMOSHA BONGE LA PARTY NDANI YA CLUB LA AZIZ, DOM


Meneja wa Tigo mkoa wa Morogoro Noel Maktauwa (kulia) akikabidhi vitabu kwamwakilishi wa makamu mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma Dkt. Adam Mwakalobo (katikati). Kushoto ni Dr. Rex Kidyalla ambaye ni mkurugenzi wa Maktaba chuoni hapo. Tigo ilikabidhi vitabu pamoja na vifaa vya michezo kwa ajili ya fainali za mashindano ya Tigo Inter-College yaliyofanyika mwishoni mwa wiki chuoni hapo.
Dkt. Rex Kidyalla ambaye ni mkurugenzi wa Maktaba katika Chuo Kikuu cha Dodoma akiongea katika hafla fupi ya makabidhiano ya Vitabu kutoka kampuni ya Simu za mkononi ya Tigo iliyofanyika hivi karibuni chuoni hapo. Katikati ni mwakilishi wa makamu mkuu wa chuo hicho Dkt. Adam Mwakalobo. Kulia ni Meneja wa Tigo mkoa wa Morogoro Noel Maktauwa. Tigo ilikabidhi vitabu pamoja na vifaa vya michezo kwa ajili ya fainali za mashindano ya Tigo Inter-College yaliyofanyika mwishoni mwa wiki chuoni hapo.
Msanii wa Muziki wa Kizazi kipya Nick Wa Pili akitoa burudani mjini Dodoma wakati wa hafla ya kuwakaribisha wanafunzi wa mwaka wa kwanza wa Chuo Kikuu cha Dodoma iliyofanyika juzi katika Ukumbi wa Club La Aziz chini ya udhamini wa kampuni ya Tigo.
Msanii wa Muziki wa kizazi kipya Rogers Lucas akitoa burudani mjini Dodoma wakati wa hafla ya kuwakaribisha wanafunzi wa mwaka wa kwanza wa Chuo Kikuu cha Dodoma iliyofanyika juzi chini ya udhamini wa kampuni ya Tigo.
---
Timu ya soka ya College of Informatics and Virtual Education ya chuo kikuu cha Dodoma, juzi iliibuka mabingwa wa mashindano ya Tigo-Inter-colleges yaliyofikia kilele chake katika viwanja vya Chuo Kikuu hicho mjini Dodoma, baada ya kuwafunga wenzao wa College of Health Sciences kwa bao 1-0 katika mechi ya fainali.

Halikadhalika katika mchezo wa kikapu timu ya Informatics and Virtual Education iliwabukiza tena College of Health Sciences kwa jumla ya vikapu 43-37 katika mchuano wa fainali pia. Mashindano hayo yalishirikisha vyuo vilivyoko chini ya Chuo kikuu cha Dodoma.

Mechi ya soka ilikuwa ya upinzani wa hali ya juu kutokana na viwango vilivyoonyeshwa na timu zote. Katika kipindi cha kwanza kila timu ilionyesha hali ya kukosa nafasi ya kupata magoli dhidi ya mwenzake. Goli la ushindi la Informatics lilitiwa kimiani na mchezaji Sidne Mbele baada ya kuiadaa ngome ya College of Health Science kabla ya kukwamisha mpira wavuni.

Mashindano hayo yamekuwa yakifanyika katika chuo kikuu hicho kwa muda wa siku sita chini ya udhamini wa kampuni ya simu za mkononi ya Tigo. Washindi wa michuano hiyo wote walikabidhiwa vikombe.

Awali fainali hizo ziliambatana na makabidhiano ya vitabu kutoka kampuni ya Tigo kwa uongozi wa chuo hicho ambapo mwakilishi wa makamu mkuu wa chuo kikuu cha Dodoma, Dkt. Adam Mwakalobo aliishukuru kampuni ya Tigo kwa kusaidia chuo hicho na pia kudhamini michezo chuoni hapo.

Mashindano hayo ambayo yaliambatana na sherehe maalum ya kuwakaribishwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza chuoni hapo iliyofanyika jioni baada ya kukamilika kwa mechi za
fainali chuo hapo, yalikuwa yamegawanya timu katika makundi mawili, kwa kila kundi kuwa na timu nne.

Kundi A lilikuwa na timu za School of Curriculum and Teacher Education, School of Education Studies, College of Earth Sciences, College of Natural and Mathematical Sciences.

Kundi B lilikuwa na timu za School of Social Sciences, School of Humanities, College of Informatics and Virtual Education, College of