Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Sunday, June 3, 2012

DAWA YA NGUVU ZA KIUME NA KIKE TATAZO LAKO SASA LIMEKWISHA


DAWA YA NGUVU ZA KIUME NA MSIMKO KWA WANAWAKE WASIO NA HAMU YA TENDO LA NDOA AMBAYO HULETA MSISIMKO KWA WANAUME NA WAKE WAKUTANAPO.KWA SASA INAPATIKANA KWA BEI NAFUU HAPA JIJINI DAR ES SALAAM MAKUTANO YA MTAA WA KIPATA NA BARABARA YA MSIMBAZI
ALLY WA YANGA BOMBA UHURU NA MSIMBAZI 0787230551 AU
SHULE YA UHURU FIKA JENGO LA AZAM BAKHRESA ULIZA NGAEJA 0715110900
0652755838


PIGA NO O713827689, 0755074505 , au 0719 541366
,0652755838 UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM

BUGURUNI LOZANA STENDI YA TAX ULIZIA ADAMU KIBANDANI 0755875884
SHULE YA UHURU FIKA JENGO LA AZAM BAKHRESA ULIZA NGAEJA 0715110900

KARIAKOO SHULE YA UHURU STENDI YA MABASI YA TANDIKA ULIZIA ZUNGU MUHUZA TIKETI 0712743870

NA UKIWA ILALA SHARIF SHAMBA FIKA DSJ BANDA NAMBA 14 SIMU 0718718671

NA UKIWA KOTA ZA BANDARI KARIAKOO FIKA MKUNGUNI KIBANDANI KWA HUSEIN 0753893295

MWANANYAMALA FIKA JABA KLABU ULIZA MACHELLAH 0713470492
ENZOY INALETA HESHIMA

PICHA YA LEO


Barnabas & Ally Kiba

ONESMO NGOWI ATEULIWA KUWA MWENYEKITI WA KAMATI YA MAANDALIZI MKUTANO WA BERLIN UJERUMANI JUNI 2013



Shirikisho la Ngumi la Kimataifa na Chama cha Ngumi cha Marekani (IBF/USBA) limeteua Rais wa Shirikisho hilo katika bara la Afrika, Mashariki ya Kati na Ghuba ya Uajemi,  Mtanzania Onesmo Ngowi kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya kuandaa mkutano wa 30 wa Shirikisho hilo mwakani. Mkutano wa 30 wa IBF/USBA unatarajia kufanyika katika jiji la Berlin nchini Ujerumani kuanzia tarehe 24 hadi 30 Juni mwaka 2013.
 Ngowi alichaguliwa na wajumbe wa mkutano mkuu wa shirikisho la IBF/USBA uliomalizika Hilton Hawaiian Village Resort, jinini Honolulu, Hawaii, Marekani tarehe 2 Juni. Uteuzi wa Ngowi unafuatia juhudi zake alizozifanya kuendeleza shirikisho hilo katika bara la Afrika tangu ateuliwe na Rais wa zamani wa IBF/USBA Robert Lee Sr. mwaka 1999 jijini New Jersey, Marekani. Onesmo Ngowi anakuwa mtu wa kwanza kutoka katika bara la Afrika kushika nyadhifa kubwa katika taasisi ya ngumi duniani na hii inaisaidia sana Tanzania na bara zima la Afrika kijitangaza vyema katika nyanja mbalimbali kama vile Utalii na bishara.
  Katika Kamati hiyo ya maandalizi kuna wajumbe sita nao ni ; Louis Priluker  wa Marekani, Roberto Rea wa Italia, Lahcen Oumghar wa Uholanzina Roberto Ramirez wa  Mexico. Kamati hiyo itafanya shughuli zake katika kipindi cha mwaka mmoja na itakutana mara 4 kwa mwaka. Sekretarieti ya Kamati ya Ngowi itakuwa katika jiji la New Jersey nchini Marekani kuliko na makao makuu ya shirikisho hilo duniani.
  Jiji la Berlin linasifika kwa uzuri wanndari zake pamoja na kuwa jiji la biashara la kimataifa katika bara la Ulaya. Mkutano huo ulianzimia kufanya mkutano wa IBF kwaka 2014 katika bara la Asia na mwaka 2015 IBF itafanya mkutano wake ktika bara la Afrika mahali ambapo patateuliwa.
  Ngowi  anawahimiza Watanzania ambao wako katika uandaaji wa mikutano kuchangamkia nafasi hii ambayo itawaleta watalii zaidi ya 1000 nchini toka nchi zaidi ya 200 duniani. Hii ni nafasi ya nadra sana katika biashara na watanzania ni muhimu wakachangamka kama wenzao wengine katika nchi zinazokuwa wenyeji wa mikutano kama hii.

NMB YAZINDUA PROMOSHENI YA JENGA MAISHA YAKO NA NMB


  Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa NMB, Imani Kajula (kushoto) na Meneja Masoko wa NMB, Shilla Senkoro wakizindua kwa pamoja promosheni mpya ya Jenga Maisha yako na NMB uliofanyika jijini Dar es Salaam leo. (Picha na Mpiga Picha wa Habari Mseto).
 Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa NMB, Imani Kajula akizungumza katika uzinduzi huo. Kushoto ni Ofisa wa wa benki hiyo, Boma Raballa na Meneja Masoko NMB, Shilla Senkoro
Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa NMB, Imani Kajula akionesha zawadi mbalimbali zitakazoshindaniwa.

MKUTANO MKUU WA WANAHISA NMB


  Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya NMB, Misheck Ngatunga (kulia) akibadilishana mawazo na Maofisa wa NMB kabla ya Mkutano Mkuu wa Wanahisa uliofanyika jijini Dar es Salaam.
 Ofisa Mtendaji Mkuu wa NMB, Mark Wiessing akizungumza na Mkuu wa Mahusiano na Jamii wa NMB, Shy-Rose Bhanji na Mwanasheria wa NMB, Lilian Komwihangiro. 
Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya NMB, Misheck Ngatunga (kulia) akibadilishana mawazo na Maofisa wa NMB,  Albert Jonkergouw (kushoto) na Protase Tehingisa wakati wa mkutano huo

LIGHTNESS MICHAEL NDIYE REDDS MISS DODOMA 2012


Mshindi wa Taji la Redds Miss Dodoma 2012 (katikakati) Lightness Michael akiwa katika picha ya Pamoja na Mshindi wa Pili (Kulia)  Berinda Mdogo na Mshindi wa Tatu wa taji la Redds Miss Dodoma 2012 (Kushoto) Nulsa Magambo Mara baada ya Mshindi wa Taji la Redds Miss Dodoma Kumalizika hapo Jana
Washiriki wa Kinyanganyiro Cha Kuwania Taji la Redds Miss Dodoma Wakiwa Katika Picha ya Pamoja kabla ya Kutangazwa Washiriki walioingia Tano Bora
Mshindi wa Kwanza wa Taji la Redds Miss Dodoma 2012 Lightness Michael akiwa katika picha ya pamoja na Washiriki wa Shindano hilo.Picha Zote Na Josephat Lukaza wa Lukaza Blog

Rais Kikwete akutana na Mmiliki wa klabu ya Portsmouth Dkt. Sulaiman Al Fahim Ikulu jijini Dar es Salaam


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Royal Group ya Saudi Arabia, Dkt. Sulaiman Al Fahim wakati walipokutana leo, Jumamosi, Juni 2, 2012, Ikulu Dar es Salaam. Dkt. Al Fahim ambaye ni mwenyekiti wa zamani na mmiliki mwenza wa Klabu ya soka ya Portsmouth ya Uingereza yuko nchini kuangalia uwezekano wa kuwekeza katika uchumi wa Tanzania. Dkt. Al Fahim pia ndiye aliyeongoza mazungumzo na kununuliwa kwa klabu bingwa ya Ligi Kuu ya Uingereza ya Manchester City na Kampuni ya Arabuni. (Picha na fredy Maro).
Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mzungumzo na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Royal Group ya Saudi Arabia, Dkt. Sulaiman Al Fahim
Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Royal Group ya Saudi Arabia, Dkt. Sulaiman Al Fahim mara baada ya  mazungumzo yao Ikulu

Miss Tanzania azindua duka la Mavazi la Michele Fashion Dar es Salaam



Miss Tanzania Salha Israel akikabidhi zawadi kwa mwandishi wa habari wa TBC Angela Michael mara baada ya kufungua duka la nguo la Michelle Fashion lililopo kwenye jengo jipya la PSPF katika mtaa wa Ohio jijini Dar es salaam leo, Duka hilo ndiyo mdhamini wa Miss Tanzania mmwaka huu kwa upande wa mavazi.
Nguo mbalimbali za kike katika duka hilo
Nguo aina tofauti.
Baadhi ya wafanyakazi wa duka hilo wakiwa katika picha ya pamoja.
Katibu Mkuu wa Kamati ya \Miss Tanzania Bosco Majaliwa akizungumza katika duka hilo mara baada ya kuzinduliwa kushoto ni Miss Tanzania Salha Israel.
Miss Tanzania Salha Israel akiangalia nguo mbalimbali katika duka hilo mara baada ya kufungua rasmi.
Miss Tanzania akiwa tayari kwa kugawa zawadi kwa waandishi wa habari mara baada ya kufungua duka hilo.

SHIRIKISHO LA NGUMI LA KIMATAIFA (IBF) LAMKUMBUKA NA KUMLILIA BONDIA MAGOMA SHABAN



SHIRIKISHO la Ngumi la Kimataifa (IBF) pamoja na Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBC) vyatuma salamu za rambirambi na kumlilia bingwa wa IBF wa mabara na bingwa wa dunia wa WBU Magoma Shaban.

Magoma aliyefariki jana katika hospitali ya Bombo jijini Tanga atakumbukwa kwa umahiri wake katika mchezo huo wa ngumi za kulipwa.

Safari ya Magoma Shaban kwenye ngumi za kulipwa ilianzia katika uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga mwaka 1998 wakati Onesmo Ngowi akiwa ndio kwanza ameteuliwa na Rais wa zamani wa IBF Robert Lee Sr, kutoka nchini Marekani kuanzisha shirikisho hilo la IBF katika bara la Afrika.

Katika pambano hilo lililofanyika uwanja huo wa Mkwakwani, Magoma Shaban, alipigana na Joseph Waweru kutoka Kenya na kumshinda kwa KO na kutangazwa kuwa bingwa wa IBF katika bara la Afrika uzito wa Flyweight.

Mwaka 2000 Magoma chini ya kamouni ya Capital Promoters Limited chuini ya mwandishi wa bahari mahiri bwana Gabriel Nderumaki alipigana na bondia Totim Lukunim toka Thailand katika ukumbi wa PTA kugombea mkanda wa IBF wa mabara katika uzito wa Flyweight na kumshinda  kwa KO katika raundi ya 4. Huo ndio ukawa mwanzo wa magoma Shaban kwenye kwenye matawi ya juu katika ngumi.

Magoma Shaban alipigania ubingwa wa dunia wa WBU nchini Italy na kumshinda bondia Ferid Ben Jeddou kwa TKO katika raundi ya 6.

Magoma alikuwa ni bondia aliyeing'arisha Tanzania na bara zima la Afrika katika medani ya ngumi za kulipwa duniani.

Kwa mantiki hiyo leo IBF imetangaza rasmi kuuita mkanda wa uzito wa Fly aliokuwa anachezea Magoma kuwa "Mkanda wa Magoma Shaban" katika mapambano yote yatakayokuwa yanachezezwa katika uzito huu yatajulikana kama "Ubingwa wa IBF Africa wa Magoma Shaban".

Tunafanya hivi ili kuwaenzi mabondia wanaoleta mchango mkubwa katika medani ya ngumi na hivyo majina yao kubakia katika kumbukumbu zetu milele.

Mola alitoa na Mola ametwa, jina lake lihidimiwe milele. Amin!

DAVIS MOSHA AMCHOMOLEA 'ABRAMOVICH'


BAADHI ya wazee wa klabu ya Yanga wakizungumza na aliyekuwa makamu mwenyekiti wa klabu hiyo Davis Mosha nyumbani kwake jana.
WAKATI zoezi la uchukuaji fomu za kuwania uongozi katika klabu ya Yanga likianza leo, aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa klabu hiyo Davis Mosha amesema hana mpango ya kuwania nafasi yoyote katika uchaguzi utakaofanyika Julai 15 mwaka huu.
Mosha alisema hayo jana nyumbani wake Mikocheni jijini Dar es Salaam, akijibu maombi ya baraza la wazee lililomuomba kugombea moja ya nafasi katika uchaguzi huo.
Alisema kwa sasa hayuko tayari kugombea uongozi katika klabu lakini yupo tayari kusaidia kitu chochote kinachohitajika kwa maendeleo ya klabu.
“NAshukuru wazee wangu kwa kuja kuniaona na kunipa pole, pia nashukuru kwa kuona umuhimu wa mimi kuwepo Yanga, lakini napenda niwaeleze kwamba sintoweza kuwania uongozi kwa sasa, ila nipo tayari kuisaidia Yanga kwa lolote litakalokuwa ndani ya uwezo wangu,”alisema.
“Mimi ni mpiganaji kweli, naiopenda Yanga na napenda iwe na maendeleo…nitashirikiana na viongozi watakaochaguliwa lakini mimi siwezi kuongoza Yanga kwa sasa nina mambo mengi ya kufganya,”alisema
Mosha ambaye alijitoa madarakani miezi michache kabla iongeza kuwa wanachama wa Yanga hawana budi kuchagua viongozi ambao wapo tayari kuisaidia klabu hiyo na si kupata chochote.
“Napenda kuwahadharisha wanachama wenzangu nkwamba tusikurupuke, tutafute watu wenye mapenzi ya kweli na si maslahi kwani Yanga ni kwa ajili ya kutumika si kuvuna,”alisema.
Awali Katibu wa baraza hilo Ibrahim Akilimali ‘Abramovich’ kwa niaba ya wazee wengine wa Yanga ambao walikwenda nyumbani kwa Mosha kwa ajili ya kumpa pole kutokana na kufiwa na Mkwewe, aliwasilisha ombi la kumtaka Mosha kurejea kundini.
Mzee Akilimali alisema kuwa wameamua kumuomba Mosha arejee kuongoza Yanga kutokana na umahiri mkubwa aliouonesha kipindi alichoongoza ambapo alikuwa mstari wa mbele kuisaidia timu hiyo na hatimaye kwa kipindi kifupi iliweza kupata mafanikio.
“Mwanetu sisi wazee wako tumekuja kukupa pole lakini pamoja na hilo tunakuomba urejee kuongoza kwani bado tunakumbuka ushupavu wako katika kuongoza…kuna kombe la Kagame linakuja ambalo wewe ulichangia kwa kiasi kikubwa kupatikana, sasa uje ulibakize tena kombe hilo,”alisema Mzee Akilimali.
Aidha , Mzee Akilimali aliongeza kuwa wanataka Yanga iingie kwenye mashindano na kushiriki hivyo mchango wa Mosha katika hilo ni muhimu sana.
Uuchaguzi huo utajaza nafasi za viongozi waliojiuzulu na ile ya mjumbe mmoja aliyefariki dunia, ambapo viongozi watakaochaguliwa watakaa madarakani kwa muda uliosalia kama katiba inavyoelekeza na kwa mantiki hiyo viongozi hao watamaliza muda wao wa miaka minne mwaka 2014.
Uchaguzi huo unafuatia kujiuzulu kwa aliyekuwa Mwenyekiti Lloyd Nchunga baada ya kushinikizwa na baadhi ya wanachama wakiongozwa na baraza la wazee wa klabu hiyo kutokana na kushindwa kuiletea mafanikio klabu hiyo chini ya uongozi wake.
Pia nafasi ya Makamu mwenyekiti iliyokuwa inashikiliwa na Davis Mosha ambaye alijitoa miezi michache baada ya kuchaguliwa kutokana na kutoelewana na Nchunga, huku mjumbe Theonest Rutashoborwa akitangulia mbele ya haki.
Uchaguzi huo pia utajaza nafasi za Wajumbe walioachia ngazi ambao ni pamoja na Mzee Yusuf, Charles Mgondo na Ally Mayay.
Kwa sasa Yanga imebaki na wajumbe wanne, Mohammed Bhinda, Sarah Ramadhan, Tito Osoro na Salum Rupia ambao baada ya uchaguzi wataungana na viongozi wapya na kuteua wajumbe wengine watatu kwa mujibu wa katiba, hiyo inatokana na wajumbe hao wa kuteuliwa Seif Ahmed, Mbaraka Igangula na Pascal Kihanga kujiuzulu.
Katika hatua nyingine, wagombea wawili jana walijitokeza kuchukua fomu za kuwanmia nafasi ya ujumbe katika, wanachama hao ni pamoja na Jumanne Mwamamwenye na Salehe Hassan na Ayoub Nyenzi anayewania nafasi ya Makamu Mwenyekiti.

Mkuu wa Mkoa wa Tabora azindua Tamasha la Mtemi Milambo


Mkuu wa mkoa wa Tabora Mhe.Fatma Mwassa amezindua Tamasha la ngoma za utamaduni la kila mwaka liitwalo Mtemi Milambo leo hii tarehe 1/6/2012 katika uwanja wa shule ya Uyui mkoani Tabora.
Katika Picha Kulia Mkuu wa mkoa wa Tabora akirusha upinde ishara ya uzinduzi wa Tamasha hilo,pembeni yake kushoto ni Bwana.Amon Mkoga Mkurugenzi Mtendaji wa Chief Promotions ambao ndiyo waandaaji wa Tamasha hilo.

Pichani ni Mkuu wa mkoa mhe.Fatma Mwassa akirusha mshale juu kama uzinduzi rasmi wa Tamasha hilo pembeni ni Chief Promotions MD Bw.Amon Mkoga.

Friday, June 1, 2012

REAKING NEWS: BONDIA MAGOMA SHAABAN AFARIKI DUNIA





BINGWA wa zamani wa dunia wa ngumi za kulipwa uzito wa Super Fly, aliyekuwa akitambuliwa na WBU, Magoma Shaaban Ngereza amefariki dunia usiku huu katika hospitali ya Bombo, mkoani Tanga, imeelezwa.
Bondia maarufu wa zamani nchini, Ally Bakari ‘Championi’ amesema, Magoma aliyezaliwa Oktoba 21, mwaka 1980 mjini Tanga, amefariki majira ya saa 12 jioni.
Championi alisema kwamba Magoma alikuwa anaumwa kwa muda mrefu na siku nne zilizopita alizidiwa na kukimbizwa katika hospitali hiyo, kabla ya umauti kumfika leo.
Hadi anafariki dunia, Magoma (pichani kushoto) alikuwa amepigana jumla ya mapambano 16, akishinda 13, manane kati ya hayo kwa Knockout (KO), amepigwa matatu na yote kwa KO na hakuwahi kutoka sare.
Magoma alipanda ulingoni kwa mara ya mwisho Julai 21, mwaka 2006 na Eugen Sorin Tanasie mjini Timisoara, Romania katika pambano ambalo alipigwa kwa Technical Knocout (TKO) raundi ya pili.
Taji lake la kwanza kutwaa lilikuwa ni la IBF Afrika, Septemba 12, mwaka 1998 akimpiga Mkenya Joseph Waweru kwa KO raundi ya kwanza, Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
Mei 11, mwaka 2000 alimpiga bondia ‘matata sana’ Totin Lukunim wa Thailand na kutwaa taji la IBF Intercontinental, uzito wa Super Fly kwenye ukumbi wa PTA, Temeke, Dar es Salaam.
Agosti 3, mwaka 2001 ndipo alitwaa ubingwa wa dunia wa WBU baada ya kumpiga Ferid Ben Jeddou wa Tunisia kwa TKO raundi ya sita mjini Avezzano, Abruzzo, Italia, kabla ya kupoteza taji hilo kwa kupigwa na Gabula Vabaza Julai 26, mwaka 2002 katika ukumbi wa Hemingways Casino, East London, Eastern Cape, Afrika Kusini kwa KO raundi ya kwanza.
Mei 25, mwaka 2003 alipigwa na Mtanzania mwenzake, Mbwana Matumla kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam kwa TKO raundi ya nne.
Alijiunga rasmi na ngumi za kulipwa mwaka 1996, pambano lake la kwanza akicheza Juni 3, mwaka huo na kumpiga Athumani Omari kwa pointi, Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
Mungi aiweke pema peponi roho ya marehemu. Amin.

MABONDIA WA TANZANIA WAWEKWA KATIKA VIWANGO VYA KIMATAIFA



Shirikisho la Ngumi la Kimataifa na Chama Cha Ngumi cha Marekani (IBF/USBA) limewaweka mabondia wa Tanzania katika orodha ya viwango .
 
Mabondia hawa ambao watakuwa miongoni mwa mabondia 15 bora duniani katika uzito wao ni:
 
Francis Miyeyusho, Fadhili Ramadhani, Mbwana Matumla, Seba Temba, Allan Kamote, Pascal  Bruno na Francis Cheka.
 
Katika kikao cha Kamati ya Viwango (Ratings Committee) ambacho kilikaa jana chini ya Uenyekiti wa William James, IBF/USBA iliridhishwa na viwango vya mabandia wa Kitanzania na kutoa ahadi kuwa watawaangalia kwa karibu zaidi katika kipindi cha mwaka mmoja ujao ili kuwaongeza katika orodha ya viwango.
 
Hii ina maana kuwa mabondia hao waliowekwa kwenye orodha ya viwango vya IBF vya mabara wanaweza kupigania ubingwa wa IBF wa Afrika na mabara wakati wowote.
 
Afrika, Mashariki ya Kati ya Ghuba ya Uajemi iliwakilishwa kwenye kikao hicho na Rais wake Onesmo Ngowi toka Tanzania. Katika vikao hivi vya viwango ni Marais wa mabara na viongozi wakuu wa IBF wanaohudhuria peke yao.
 
Ngowi aliwapendekeza pia mabondia kadhaa wa Kenya, Uganda, DRC, Afrika ya Kusini, Namibia, Zimbabwe, Mali, Gabon, Benin, Bukina Faso, Ghana, Nigeria, Morocco, Cameroon, Ivory Cost, Tunisia, Misri, Dubai na Jordan.
 
Kumekuwepo na uchakachuaji mkubwa wa rekodi za mabondia katika bara la Afrika kwa mapromota na mawakala wa ngumi kuweka viwango vya mapambano ya uongo katika rekodi za mabondia wao kweney mtandao wa Boxrec. Hii inawapa wakati mgumi sana mabondia wa Kiafrika kupata mapambano ya ngumi ya kimataifa.
 
Afrika, Mashariki ya kati na Ghuba ya Uajemi inaongozwa na rais wake Onesmo Ngowi wa Tanzania.

SUALA LA AFYA YA UZAZI SALAMA LIPEWE KIPAUMBELE MCHAKATO WA KATIBA MPYA



Mkurugenzi wa Chama cha Wanasheria wanawake TAWLA Mwanasheria Tike Mwampipile akizungumza na washiriki wa semina ya mapendekezo ya kuwepo kwa   sheria ya Afya ya Uzazi Salama  katika mchakato wa maoni ya kuandikwa kwa Katiba Mpya iliyomalizika jana kwenye ukubi wa hoteli ya Blue Pear Ubungo Plaza jijini Dar es salaam.
 
NA MAGRETH KINABO- MAELEZO

JAMII iimeshauriwa kulipa kipaumbele suala ya mapendekezo ya kuwepo kwa   sheria ya Afya ya Uzazi Salama  katika mchakato wa kuwepo kwa Katiba Mpya , ambayo itawezesha watumishi wa afya ambao watasababisha vifo vya wakinamama wajawazito  au watoto wachanga kwa sababu za uzembe.
Kauli hiyo iliyoilitolewa (jana) na Mkurugenzi wa Mtendaji  wa Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania(TAWLA), Tike Mwampipile,   wakati  akifafanua ya mapendekezo  hayo  iliyoandaliwa  na chama hicho kwa waandishi wa habari kwenye semina ya siku mbili iliyofanyika , Ubungo Plaza jijiini Dares Salaam.Semina ya mafunzo hayo  ambayo iliyoanza jana  (juzi) na kumalizika leo(jana)
“ Wito wangu katika jamii ni ni ina wajikubu mkubwa wa kujua haki zao za msingi na kufahamu wapi pa kuzipata. Afya ya Uzazi Salama ni kitu muhimu ambacho hakijangaliwa kwa umakini. Hivyo katika mchakato wa Katiba Mpya suala hili liangaliwe kwa uzito kwa  na upana wake kujali mama ambaye analemta mtoto hapa duniani  ambaye anaweza kuwa na  Rais au Waziri Mkuu wa kesho,” alisema   Mwampipile.
 Aliongeza kuwa kuwepo kwa sheria hiyo kutasaidia kupunguza  idadi ya vifo vya wakinamama wajawazitio na watoto wachanga.
Kwa upande wake mtoa mada wa mapendekezo hayo,  Bernadetha Mkandya ambaye pia ni mjumbe wa bodi ya TAWLA na Wakili wa Kujitegemea alisema  kuwa mwanamke ana haki ya   kuishi na kulindwa ,hivyo sheria hiyo italuiwezesha taifa kupata watoto waliolelewa katika mazingira bora na afya njema.   .
“ Tunataka tuwe na sheria ya iyatomlinda mwanamke wakati wa ujauzito na siku 42 baada ya kujifungua,”  ikiwepo kupanga idadi ya watoto atakaoweza kuwalea na muda wa kupata mtoto mmoja baada ya mwingine alisema.  
 Akifafanua zaidi kuhusu sheria hiyo alisema  itamwezesha mamamjamzito kupata huduma za afya ya uzazi salama bora na ambazo zitamwezesha kupata vifaa tiba vinavyotakiwa bila gharama yeyote.
Aidha Mkandya aliongeza katika sheria hiyo wamapendekeza kuwa umri wa uti mzima uwe ni miaka 18 ili kuwezesha mtoto wa kike kuolewa katika umri unaotakiwa hatua ambayo itasaidia kupunguza athari za afya ya uzazi  zinazotokana na umri mdogo. Alisisitiza kuwa ni muhimu kwa makundi yote katika jamii kushiriki katika kutoa maoni ya mchakato huo.
Mkandya aliongeza kuwa mapendekezo hayo  hayo yanaelekeza kuwepo kwa sheria ambayo itamwezesha mama mjamzito kusitisha ujauzito pale itakapogundulika kuwa unasabbaisha athari za kiafya kwa ruhusa ya daktari na ridhaa yake  au endapo atakuwa amebakwa na  kwa ridhaa yake kuwa hana uwezo wa kuendelea hudumia ujauzito huo na kumlea mtoto  pale atakapojifungua.
Pia ridhaa hiyo inaweza kutolewa na ndugu zake endapo mama huyo ni mlemavu wa

MKUTANO WA 29 WA SHIRIKISHO LA NGUMI LA KIMATAIFA (IBF) WAANZA RASMI NCHINI MAREKANI.



Rais wa IBF duniani Daryl Peoples wa Marekani katikati akiwa amesimama na Rais wa IBF katika bara la Afrika, Mashariki ya Kati na Ghuba ya Uajemi Onesmo Ngowi wa Tanzania pamoja na promota maarufu wa ngumi wa Thailand Jimmy  Chaichotchuang walipotembelea Pearl Habour tarehe 30 May, 2012.

Mkutano wa 29 wa Shirikisho la Ngumi la Kimataifa (IBF) umeanza rasmi katika Hotel ya Hawaii Hilton Village Resort jijini Honolulu, Hawaii, Marekani tarehe 29 May, 2012. Mkutano huu ulianza rasmi saa 3 za asubuhi katika ukumbi wa kimataifa wa Atlatic International Conference Center, kwenye jengo la Rainbow Towers katika hotel hii ya nyota tano.
Tarehe 29 ilianza kwa wajumbe wa mkutano huo kujiandikisha kuanzia saa 3 za asubuhi mpaka saa 11 jioni. Jioni wajumbe wote walikuwa na cocktail party ya get together katika ukumbi wa Rainbow Towers.
Mkutano huu unahudhuriwa na wajumbe 6000 toka nchi 204 duniani kote. Ujumbe wa Afrika ni moja ya ujumbe unaoshiriki katika mkutano huu maalum wa kuafiki programu ya Utalii wa Michezo itakatowakilishwa na Rais wa IBF katika bara la Afrika, Mashariki ya Kati na Ghuba ya Uajemi Mtanzania Onesmo Ngowi.
Akiwakaribisha wajumbe walioanza kumiminika katika mkutano huo Rais wa IBF duniani Daryl Peoples wa Marekani aliwataka wakaribie Marekani na kutumia muda walionao katika jiji la Honolulu kufahamiana na kutembelea jiji hili.
Ratiba ya siku tano itajumuisha kuwa tarehe 29 ni siku ya kuanza kwa mkutano huo kwa wajumbe kujiandikisha. Jioni kutakuwa na party ya kukutana na kufahamiana. Tarehe 30 kutakuwa na ziara ya kutembelea Pearl Habour bandari iliyoharibiwa na majeshi ya Japan mwaka 1941na kuifanya Marekani ijiingize kwenye vita ya pili ya dunia.
Tarehe 31 ni siku rasmi ya ufunguzi wa mkutano huo ambapo Rais wa IBF duniani Daryl Peoples wa Marekani ataufungua rasmi. Wajumbe wengine watakaohutubia ni pamoja na Rais wa IBF katika bara la Afrika, Mashariki ya Kati na Ghuba ya Uajemi Mtanzania Onesmo Ngowi.
Wengine ni Lindsey Tucker ambaye ni mwenyekiti wa Kamati ya Ubingwa wa IBF,  William James ambaye ni mwenyekiti wa Kamati ya Viwango wa IBF.
Nao Lou Priluka ambaye ni Katibu wa bodi ya wakurugenzi wa IBF atazungumza pia. Aidha Al Maiyer ambaye ni Mwakamu wa Rais wa IBF atazungumza. Ray Wheatler ambaye anaiwakilisha IBF katika bara la Asia atazungumza.
Rarehe 1 Juni kutakuwa na semina ya Utibabu pamona na Marefari. Tarehe 2 kutakuwa na semina ya Majaji pamoja na programu maalum kwa IBF zitawakilishwa. Mkutano huu utafungwa rasmi tarehe 2 Juni na Mstahiki Meya wa jiji la Honolulu.
Imetumwa toka Honolulu, Hawaii, Marekani na;
Onesmo A.M.Ngowi
IBF/USBA President for Africa
President, Tanzania Professional Boxing Commission(TPBC)
Director, Commonwealth (English Empire) Boxing Council (CBC)
Coordinator, Moshi Sister Cities Committee
Coordinator, International Education and Resources Network (iEARN) to TANZANIA

BAADHI YA WAREMBO WATAKAOPANDA JUKWAANI KATIKA SHINDANO LA MISS NYAMAGANA JIJINI MWANZA LEO



Aisha.
HIZI NI BAADHI YA SURA  ZITAKAZOPANDA JUKWAANI USIKU WA LEO IJUMAA,  KATIKA SHINDANO LA  MISS NYAMAGANA 2012. KATIKA UKUMBI WA GOLD CREST JIJINI MWANZA.
SHUGHULI NZIMA INASIMAMIWA NA STOPPERS ENTERTAINMENT.
BURUDANI ITATOLEWA NA LINAH, DITTO NA HAFSA KAZINJA.
MSHEHERESHAJI MKUU AU MC WA SHUGHULI NZIMA NI MASANJA MKANDAMIZAJI KUTOKA KUNDI LA ORIGINAL KOMEDI.
Amina.
Brenda.
Cecy.
You might also like:

MKUTANO WA SHIRIKISHO LA NGUMI LA DUNIA IBF WAENDELEA HUKO HONOLULU MAREKANI



 
Rais wa IBF/USBA duniani Daryl Peoples wa Marekani kushoto akiwa amesimama na Rais wa IBF bara la Afrika, Mashariki ya Kati na Ghuba ya Uajemi Mtanzania Onesmo Ngowi siku ya ufunguzi wa mkutano huo tarehe 31 May, 2012.
Rais Peoplers aliwakaribisha wajumbe na kuwasomea taarifa ya mwaka ya IBF/USBA ambapo zaidi ya mapambano ya ubingwa 349 yalifanyika chini ya IBF/USBA mwaka jana. 
 
Mkutano huo ulihutubiwa pia na Rais wa IBF katika bara la Afrika, Mashariki ya Kati na Ghuba ya Uajemi Mtanzania Onesmo Ngowi. Aidha mwakilishi wa IBF katika bara la Ulaya Roberto Reya wa Italia naye alihutubia mkutano huo.
 
Katika mkutano huo taarifa ya kifo cha bondia wa Thailkand Thangthong Kiattaweesuk aliyekuwa na miaka 35 kilitolewa rasmi. Bondia Kiattaweesuk alikufa katika ajali ya gari akiwa na mkewe, mtoto mmoja na ndugu yake baada tu ya kushinda pambano lililompa nafasi ya kupigana na bingwa wa IBF wa dunia katika uzito wa Feather Geoffrey Mathebula wa Afrika ya Kusini.
 
Kiattaweesuk alimpiga bondia wa Kenya Geofrey Munica kwa KO raundi ya 10 katika pambano la kugommbea mkanda wa mabara wa IBF.
 
Pamoja na ufunguzi huo leo kutakuwa na semina ya utibabu pamoja na semina ya majaji. Mkutano huo utamalizika tarehe 2 Juni.
 
Mkutano huu unahudhuriwa na wajumbe 6000 toka nchi 204 duniani kote. Ujumbe wa Afrika ni moja ya ujumbe unaoshiriki katika mkutano huu maalum wa kuafiki programu ya Utalii wa Michezo itakatowakilishwa na Rais wa IBF katika bara la Afrika, Mashariki ya Kati na Ghuba ya Uajemi Mtanzania Onesmo Ngowi.

Msondo kukamua Kitunda Juni 10



NA MWANDISHI WETU

BENDI kongwe ya muziki wa dansi ya Msondo ngoma inatarajia kuwapa burudani kabambe wakazi wa Kitunda na maeneo jirani kwa kufanya onyesho kwenye ukumbi mpya wa Msige Pub Juni 10, mwaka huu.
Mratibu wa onyesho hilo, George Msige, alisema kuwa maandalizi yamekamilika na amewataka wapenzi wa burudani kujitokeza kwa wingi kupata vionjo vya wakongwe hao.
Alisema amevutiwa kuialika bendi hiyo kutumbuiza kwenye ukumbi huo uliopo Kitunda Kibeberu, kutokana na maombi aliyopewa na mashabiki wengi baada ya kufurahishwa na 'shoo' ya kwanza ya kundi la taarab la Five Stars wiki mbili zilizopita.
"Kwa hiyo wakazi wa Kitunda Kibeberu kuanzia sasa watakuwa wanapata burudani ya kila aina kwa nia ya kukata kiu yao hivyo, wajiandae kucheza nyimbo za bendi ya Msondo," alisema Msige.
Alisema kuwa Msondo itapiga vibao vya zamani na vipya ambavyo ni Suluhu wa Shabani Dede, Nadhiri ya Mapenzi wa Juma Katundu na Baba Kibene wa Eddo Sanga.
Mwimbaji nguli Maalim Gulumo 'Kamanda' na Saidi Mabela na wengineo watafanya vitu vyao siku hiyo ili kukonga nyoyo za mashabiki wao.
Msemaji wa bendi hiyo, Rajabu Mhamila 'Super D' amethibitisha Msondo itaangusha burudani ya nguvu katika ukumbi huo ikitokea Masasi, Mtwara kuzindua ukumbi wa Emirate.

MISS MTWARA KUFANYIKA JUMAMOZI JUNI 2 MJINI MTWARA



Warembo watakaopanda jukwani kushiriki katika shindano la  kumtafuta Miss Mtwara 2012 siku ya jumamosi juni 2 katika ukumbi wa Makonde Beach mjini Mtwara, ambapo wamekuwa wakiendelea na mazoezi katika ukumbi huo kujiweka tayari kwa ajili ya shindano hilo.
Warembo watakaopanda jukwani kumtafuta Miss Mtwara 2012 Wakimsikiliza mkufunzi wao Isabela mpada (MISS RUVUMA 2006) siku ya jumamosi Juni2 katika ukumbi wa makonde beach
Warembo watakaopanda jukwani kumtafuta Miss Mtwara 2012 Wakimsikiliza mkufunzi wao Isabela mpada (MISS RUVUMA 2006),Pamoja na muandaaji wa shindano Rajab Mchatta. siku ya jumamosi Juni 2 katika ukumbi wa makonde beach

SAFARI LAGER YATANGAZA TAREHE NA ZAWADI ZITAZOKABIDHIWA KWA WAJASILIAMALI WASHINDI WA “WEZESHWA NA SAFARI LAGER”.



  Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo akionyesha baadhi ya vifaa vitavyokabidhiwa kwa wajasiliamali waliofuzu katika grogramu ya ruzuku ya “Wezeshwa na Safari Lager” Dar es Salaam jana.Vifaa hivyo vitakabidhiwa mwishoni mwa wiki katika viwanja  vya CCM Ilomba Mkoani Mbeya.
  Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo akizungumza na waandishi wa habari.
KAMPUNI ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager leo imetangaza rasmi tarehe na zawadi zitakazokabidhiwa  kwa wajasiliamali  ambazo ni vitendea kazi kwa wajasiriamali walioshinda katika shindano la “Wezeshwa na Safari Lager”.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam leo, Meneja wa bia ya Safari Lager Bw. Oscar Shelukindo alisema wajasiriamali watakabidhiwa ruzuku zao kwenye kanda walizofanyia mafunzo ya ujasiriamali. Bwana Oscar alisema, “Tutaandaa matamasha ya kuwazawadia wajasiriamali wetu ambapo tunawaalika pia wafanyabiashara wengine wa eneo lao ili kufurahi pamoja na wajasiriamali wetu”. Aliendelea, “Kituo cha Mbeya tamasha litafanyika siku ya Jumamosi tarehe 02 June katika kiwanja cha CCM Ilomba, kituo cha Arusha tamasha litafanyika siku ya Jumamosi tarehe 09 June katika viwanja vya Soweto, kituo cha Mwanza tamasha litafanyika siku ya Jumamosi tarehe 16 June katika kiwanja cha Furahisha na tutamaliza na kituo cha Dar Es Salaam ambapo tamasha litafanyika siku ya Jumapili tarehe 23 June kwenye viwanja vya leaders Club.”
Akielezea mchakato wa kuwapata wajasiriamali hawa Bwana Shelukindo alisema baada ya kutangaza kuanza kwa shindano hili mwishoni mwa mwaka jana, jumla ya fomu za maombi 9,738 zilikusanywa. Fomu hizi zilikaguliwa na majaji wenye ujuzi wa mambo ya biashara na wajasiriamali 80 walichaguliwa kuingia katika hatua ya pili. Wajasiriamali waliochaguliwa walitembelewa na wataalamu ili kuthibitisha uwepo wa biashara zao, jumla ya wajasiriamali 54 walifaulu na ndio waliopatiwa mafunzo. Wajasiriamali 26 waliondolewa katika hatua hii kutokana na mapungufu mbalimbali kama kuomba kuwezeshwa wakati biashara sio za kwao, kutokuwa na biashara inayoendelea .
Akionyesha baadhi ya ruzuku zitakazotolewa kwa wajasirimali walioshinda bwana Oscar alisema, “wajasiriamali wetu wamepatikana kutoka katika mikoa mbalimbali ya Tanzania, wako wajasiriamali katika fani tofauti pia kama Mafundi wa kushona nguo za aina tofauti,  mafundi seremala, magari nk wako pia wajasiriamali wa kusindika vyakula, ufugaji wa samaki, ufugaji wa kuku, kutengeneza mizinga ya nyuki nk, wako wajasiriamali katika biashara za vyakula, kuuza vinywaji, umeme jua, teknolojia ya mawasiliano .
Bwana Shelukindo aliwataja tena wajasiriamali watakaopatiwa ruzuku ya vitendea kazi ili kupanua biashara zao. Katika kituo cha Dar Es Salaam wajasiriamali watakaokabidhiwa ruzuku ni Catherine Urio, Josephine Kisiri, Zainabu Juma Zayumba, Elizabeth Chami, Richard Kwiligwa, Hilary Meck Mremi, Damas Daniel Msoka, Innocent Mbelwa, Stumai Namanga, Dasina J Buzuka, Christabela Lymo, Dadan J Munisi, Faraji Bakary Mgwegwe, Issa Lema na Valerian Tigano Luzangi. Shelukindo aliwataja pia washindi wa kituo cha Arusha kuwa ni Ansilla Danny, Bibie Msumi, Rogers Msangi, Simon Kinabo, Sophia Khalfan, Yuda Mbando, Amani Lymo, Adam Akilinyingi, Joseph M. Mnemwa, Rose Tesha na Victoria Riwa.
Bwana Shelukindo aliendelea kuwataja wajasiriamali watakaojipatia ruzuku katika kituo cha Mwanza ambao ni Bora Mganda, Brighton Dismas Maricell, Mangana Kilahanya Kigombe, Prudence Mubito, Musa Mahushi George, Innocent K. Doi, Amos Edward Mwambola, Edith Mudogo, Aron Magembe, Yusuph A. Kawaga, Zamda Shabban, Oscar Bosco Kabobo, Yahaya Fundisa, Dainess Ngaiza na Boniface Joseph Minja. Na katika kituo cha Mbeya wajasiriamali waliofaulu kupata ruzuku baada ya mafunzo ni Rose Eliudi Maruila, Benedict Abel Matandiko, Vumilia Mtweze, Bahati Mbata, Hellen A. Mwanguku, Felix Phillip Kamuhabwa, Festo Mwakasege, Phares Richard Lymo, Iradi A. Msemwa, Gabriel Mwalugaja na Tatu Ngemela. Jumla ya ruzuku ya vitendea kazi vya thamani ya shilingi milioni 200 vitatolewa kwa wajasiriamali hawa.
Bwana Shelukindo alimaliza kwa kuwashukuru watanzania wote kwa kushiriki shindano la Wezeshwa na Safari Lager, alisema “Shukrani nyingi ziende pia kwa wanywaji wetu wa bia ya Safari Lager, bila wao hakika zoezi zima la Wezeshwa na Safari Lager lisingewezekana, tunawaomba waendelee kufurahia bia yetu”. Aliwakaribisha kuhudhuria matamasha haya na aliwaomba radhi wajasiriamali ambao hawakufaulu, na wale wanaoendelea kutuma fomu wasitume tena, wajiandae kushiriki shindano lijalo la Wezeshwa na Safari Lagerbaadae mwaka huu
 .
Meneja akizungumza na waandishi wa habari
You might also like:

DOGO ASLAY, ORIJINO KOMEDY WAPAMBA UZINDUZI WA KAMPENI YA 'TUKO WANGAPI?TULIZANA!



Mwenyekiti Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS) Dk.Fatma Mrisho wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kimataifa ijulikanayo kama ‘Tuko Wangapi?, Tulizana’.
 Dk.Mrisho ambayea likuwa mgezi rasmi katika uzinduzi huo uliofanyika leo kwenye hoteli ya Golden Tulip amesema kwamba kampeni hiyo imelenga kuongeza idadi ya Watanzania wanaojua maana ya mtandao wa ngono, hatari ya kuambukizwa VVU kutokana na kuwa mmoja ya wanamtandao wa kuwa na wapenzi wengi kwa wakati mmoja.
 Dogo Aslay jukwaani
 Original Komedy wakiwa kazini


Bondia wa kike,Lulu Kayege ajifua kwa ajili ya kuwakabiri wapinzani wake



 Kocha wa Mchezo wa ngumi Kambi ya Ilala Kondo Nassoro akimfundisha bondia chipkizi wa kike,Lulu Kayege Dar es salaam leo kwa ajili ya kujiandaa  na mashindano ya kumi bora yatakayofanyika june 15 katika ukumbi wa panandi panandi Ilala Bungoni Dar es salaam.picha na www,superdboxingcoach.blogspot.com

Bondia wa kike,Lulu Kayege akiwa katika pozi bondia huyo  anaenolewa katika Kambi ya Ilala na Makocha wazowefu wa mchezo wa Masumbwi Nchini Habibu Kinyogoli 'Masta, Rajabu Mhamila 'Super D' na Kondo Nassoro kwa sasa yupo fiti kwa ajili ya masindano mbalimbali nchiniwww,superdboxingcoach.blogspot.com