
Taarifa kwa vyombo vya Habari
Tigo yazindua suluhu kwa wakulima kupitia mtandau wa simu za mikononi
Agosti
1, 2012, Dodoma. Tigo leo imetangaza uzinduzi wa programu ya majaribio
inayojulikana kama ‘Tigo Kilimo’ ambayo inakusudia kuwapatia wakulima
taarifa stahiki kwa wakati muafaka za kilimo kupitia simu zao za
mikononi.
Tigo Kilimo inatumia teknolojia ya ujumbe wa maadishi (
sms) ambayo itawapatia wakulima wadogo wadogo fursa ya kipekee
kuboresha shughuli zao. Kupitia Tigo Kilimo wakulima watapata taarifa za
hapo kwa hapo kuhusu hali ya hewa na taarifa nyinginezo za kilimo. Hii
itawasaidia kuongeza mavuno na kupunuguza utofauti ya mavuno na sehemu
nyingine za ulimwengu.
“Kwa kutumia mtando wa simu za mikononi
kuleta suluhu kwenye maswala ya Kilimo wakulima wataunganishwa kwa
ukaribu zaidi na italeta ufanisi zaidi katika shughuli za kilimo ,”
alisema Yaha Ndojore , Meneja Mradi wa huduma za Tigo Kilimo , Tigo
Tanzania . “Kutokana na miundombinu na mawailiano hafifu kwenye sehemu
kubwa za nchi zinazoendelea , wakulima wanataabika kupata taarifa muhimu
za kilimo , pamoja na mafunzo na ushauri kuhusu maswala kama wadudu na
magonjwa , hali ya hewa na mbinu tofauti za kilimo . Kupitia huduma hii ,
Tigo itatoa fursa ya suluhu mpya na nafuu yakusaidia hizi
changamoto.” Alisema
Kama mdhamini mkuu wa mawasiliano ya
maonyesho ya Nane Nane na kusheherekea Wiki ya Maonyesho ya Kilimo,Tigo
inawapatia wakulima mawasiliano ya Tigo Kilimo bure kwa mwezi mzima wa
Ogasti.Wakulima wanaweza kupata huduma hii kupitia simu zao za mikononi
kwa kupiga *148*14# na kupata listi ya huduma za Tigo Kilimo. Hapa
watapata lisiti ya taarifa mbali mbali kwa ujumla kuhusu hali ya hewa ,
udani wa menjimenti wa udongo , njia ya kudhibiti wadudu kwa zaidi ya
aina 20 za mboga , matunda na nafaka , taarifa kuhusu utunzaji wa mifugo
nk. Kwenye awamu ya pili ya huu mradi Tigo itaongeza huduma kama vile
bei ya bidhaa sokoni, na kuanzisha huduma kwa wateja wakulima, ambao
wataweza kupiga wakiwa na maswali mbali mbali
Simu za mikononi
zinarahisisha mawasilano. Tigo inaweza kuwafikia wakulima viijini na
taarifa muhimu kupita huduma hii. Kwa kupitia Tigo Kilimo , wakulima
wanapata ujuzi wa kuboresha kazi na stadi zao ambazo zitasaida kuongeza
mazao , kupunguza gharama na kuongeza kipato, na wakati huo huo kupata
faidia kwa kutumia simu za mikononi.
KuhusuTigo
Tigo
ilianza biashara 1994 kama mtandao wa kwanza wa simu za mkononi
Tanzania. Sasa inapatikana katika mikoa yote 26 tanzania Bara na
Zanzibar. Tigo imejitahidi kuwa na ubunifu katika uendeshwaji wa huduma
zake za simu nchini Tanzania kwa kutoa huduma zenye gharama nafuu katika
mawasiliano mpaka katika kutoa huduma za intanet zenye kasi na huduma
za fedha kwa njia ya simu kupitia Tigo Pesa.
Tigo ni sehemu
ya Millicom International Cellular S.A (MIC) na hutoa huduma za simu za
mkononi kwa gharama nafuu na inayopatikana maeneo mengi kiurahisi
kwa wateja zaidi ya milioni 30 katika masoko 13 yanaoibuka
Afrika na Amerika ya Kusini.
Kwa taarifa zaidi tembelea: www.tigo.co.tz