Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Saturday, December 8, 2012

MIYEYUSHO VS NASSIBU WAPIMA UZITO LEO




Bondia Said Mundi wa Tanga kushoto akitunishiana misuri na Ibrahimu Class 'King Class Mawe' baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao utakaofanyika kesho jumapili Desemba 9 katika ukumbi wa PTA Sabasaba Dar es salaam picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' akipimwa Afya na Dkt, Kalaga wakati wa maandalizi ya mwisho kwa ajili ya mpambano wake na Saidi Mundi wa Tanga wa pili kulia wengi kulia ni Promota wa mpambano huo Mohamed Bawazir na wa pili Kushoto ni Mratibu wa Mpambano huo Paul kunambi picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Promota ya mpambano wa masumbwi Mohamed Bawazir katikati akiwa na baazi ya mabondia
Baazi ya mashabiki wakishangilia wakati wa upimaji uzito wa mabondia watakaopambana katika ukumbi wa PTA sabasaba siku ya 9 desemba


Bondia Fransic Miyayusho akipima uzito kwa ajili ya kumkabiri Nassibu Ramadhani kushoto mpambano wao wa ubingwa wa WBF utakaofanyika kesho 9 desemba katika ukumbi wa PTA Sabasaba picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Bondia Nassibu Ramadhani kushoto akitunishina Msuri na bondia Fransic Miyeyusho wakati wa uipimaji uzito kwa ajili ya mpambano wao wa 9 Desemba Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' akipima uzito kwa ajili ya kumkabili mpinzani wake Said Mundi kushoto mpambano utakaofanyika Desemba 9 Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Bondia Said Mundi wa Tanga kushoto akitunishiana misuri na Ibrahimu Class 'King Class Mawe' baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao utakaofanyika kesho jumapili Desemba 9 katika ukumbi wa PTA Sabasaba Dar es salaam picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Bondia Said Mundi wa Tanga kushoto akitunishiana misuri na Ibrahimu Class 'King Class Mawe' baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao utakaofanyika kesho jumapili Desemba 9 katika ukumbi wa PTA Sabasaba Dar es salaam picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

NEEMA YAISHUKIA MWANZA TENA, MWAKYEMBE AZINDUA USAFIRI WA TRENI YAKWENDA HUKO.



Waziri wa Uchukuzi,Dk. Harrison Mwakyembe akipeperusha bendera kuashiria uzinduzi wa kuanza tena kwa safari za treni ya abiria kwenda Mwanza.


Waziri wa Uchukuzi Dk Harrison Mwakyembe mwenye suti akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji Mhandisi Kipallo Aman Kisamfu kabla kuzindua safari ya treni ya abiria kwenda Mwanza leo mchana katika Stesheni ya Dar es Salaam.
 
WAZIRI wa Uchukuzi leo mchana amezindua rasmi usafiri wa treni za abiria toka Dar es Salaam hadi Mwanza, hivyo kutimiza ahadi ya Serikali iliyotolewa Bungeni kipindi cha Bajeti mwaka huu kuhusu
kurejesha huduma hiyo.
Dkt. Harrison Mwakyembe akiwa amefuatana na viongozi wa Wizara akiwemo Katibu Mkuu wa Wizara, Injinia Omar Chambo na Mtendaji Mkuu wa TRL, Injinia Kipallo kisamfu aliruhusu treni hiyo kuondoka stesheni ya Dar es Salaam Saa 8:30 mchana huku abiria wakishangilia na kudai huduma hiyo iendelezwe zaidi na zaidi.
Usafiri wa treni ya abiria kati ya Dar na Mwanza ulisitishwa Desemba 2009 kufuatia maamuzi ya iliyokuwa menejimenti ya Kampuni ya  RITES kutoka India .
Treni hiyo ikiwa imefunga Mabehewa 16 yenye abiria wapatao elfu moja inatarajiwa kuingia Mwanza Jumapili asubuhi na kupokewa na Mhe. Naibu Waziri wa UCHUKUZI, Dkt. Charles Tizeba na viongozi mbalimbali wa mkoa wa Mwanza.
Akiongea na viongozi na Wafanyakazi baada ya ufunguzi huo, Dkt. Mwakyembe aliwapongeza Wafanyakazi wa TRL hasa mafundi wa karakana za Dsm na Morogoro kwa kazi kubwa ya kufufua Injini na Mabehewa hivyo kulikolea Taifa mabilioni ya pesa ambazo zingetumika kukodisha vifaa hivyo kutoka Afrika ya Kusini, India ama nchi nyingine.
Treni ya abiria ya Mwanza itakuwepo kwa kuanzia mara mbili kwa wiki Jumanne na Ijumaa kama ilivyo kwa treni ya Kigoma na baadaye kuongezeka jinsi injini na mabehewa yatakavyokuwa yanaongezeka kutengenezwa.

TIGO, MPANGO WA TAIFA WA DAMU SALAMA WAHAMASISHA KUJITOLEA DAMU, Kuna umuhimu wa kuchangia mara kwa mara kwasababu damu haiwezi kuhifadhiwa zaidi ya siku 35. Kumbuka Damu yako inakua mwilini kwa siku 90 tu! baada ya hapo inakufa nakutengeneza nyingine.








Mwanasheria wa Kampuni ya Tigo Tanzania, Kay Ngalomba, akitolewa damu kwenye zoezi hilo la uchangiaji Damu.
Utulivu muhimu wakati wa zoezi la uchangiaji damu.
Afisa Muuguzi kutoka Mpango wa Taifa wa Damu Salama akimchoma sindano mmoja wa wau waliojitokeza kwenye zoezi hilo linalofanyika kwenye ofisi za Makao Makuu ya Kampuni ya Tigo Kijitonyama jijini Dar es Salaa

Wednesday, December 5, 2012

TIGO ILIPOSHIRIKI KATIKA SIKU YA UKIMWI DUNIANI

Baadhi ya wakazi wa Mkoa wa Lindi waliojitokeza kutoa damu wakisubitri kutoa damu katika banda la damu salama katika mpango uliodhaminiwa na kampuni ya simu ya mikononi ya Tigo
Mhamasishaji wa Damu salama Hawa akitoa maelezo kwa mtu kabla ya kutoa damu

Monday, December 3, 2012

Mkutano Mkuu wa TASWA kufanyika Desemba 21 mjini Bagamoyo





Katibu Mkuu wa Taswa, Amir Mhando
MKUTANO Mkuu wa Mwaka wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) utafanyika Desemba 21 na 22 mwaka huu Kiromo View Resort Hotel, Bagamoyo mkoani Pwani.

Mkutano huo unatarajiwa kushirikisha wanachama 100, na pia watakuwepo wadau mbalimbali wa TASWA wakiwemo waandishi wakongwe wa habari za michezo wambao watapewa nafasi ya kuzungumza kwenye mkutano huo.

Wanachama wa TASWA watapata fursa ya kupokea na kujadili Ripoti ya Utendaji ya chama, Mapato na Matumizi, maendeleo ya chama na masuala mbalimbali yanayohusu waandishi wa habari za michezo kwa ujumla.

Pia kutakuwa na semina maalum itakayoendeshwa kwa washiriki wa mkutano huo ili wawe na uelewa kuhusiana na ajenda ya kuinua kipato kwa wanachama ambayo itajadiliwa kwenye mkutano huo.

Kamati ya Utendaji ya TASWA imekubaliana iwasaidie wanachama wake waweze kujitegemea kwa kuanzisha Chama cha Akiba na Mikopo (SACCO’S), lakini imeamua kwanza iwaite wataalamu wa vyama vya ushirika watoe elimu juu ya jambo hilo na kukishakuwa na uelewa wa kutosha suala hilo lipelekwe kama ajenda kamili ya kuanzisha chama hicho kwenye Mkutano Mkuu.

Nia yetu ni kuona tunapiga hatua za kimaendeleo na kuwafanya wanachama wetu wafurahie kujiunga na chama hiki na waweze kupata mikopo ya kuwasaidia katika masuala mbalimbali.

Tunawaomba wanachama wote ambao wanatarajia kuhudhuria mkutano huo wathibitishe ushiriki wao kwa Katibu Mkuu wa TASWA kwa njia ya email: mgosius@yahoo.com au taswatz@yahoo.com. Mwisho wa kuthibitisha ni Desemba 15, 2012 saa kumi alasiri ili maandalizi mengine yaendelee na uwepo wao katika mkutano uthaminike.

Wanachama ambao wanajua hawajalipa ada ni vyema wakafanya hivyo,  kwa kuwasiliana na Mhazini Mkuu wa TASWA, vinginevyo chama kitafanya utaratibu mwingine wa kuhakikisha ada zao zinapatikana siku ya mkutano.

TASWA inaendelea na mazungumzo na wadhamini mbalimbali na Jumatatu Desemba 10, 2012 saa tano asubuhi katika mgahawa wa City Sports Lounge Dar es Salaam itatangaza mdhamini wa mkutano huo.

Imetolewa na:
Amir Mhando
Katibu Mkuu TASWA

KILIMANJARO STARS KUPAMBANA NA ZANZIBAR HEROES KATIKA NUSU FAINALI YA CECAFA CHALLENGE





 Kiungo mshambuliaji wa timu ya Kilimanjaro Stars inayadhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, Amri Kiemba na beki wa timu ya Rwanda, Michel Rusheshangoga wakiwania mpira wakati wa mchezo wa Robo  Fainali ya kwanza uliochezwa leo katika Uwanja wa KCC uliopo Lugogo nchini Uganda. (Na Mpiga Picha Wetu)
 Kiungo mchezeshaji wa Kilimanjaro Stars inayodhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, Mwinyi Kazimoto akizuiwa na beki wa Rwanda, Ismail Nshutiyamagara wakati wa mchezo wa Robo Fainali ya kwanza ya michuano ya Cecafa Chalenge uliochezwa katika Uwanja wa KCC uliopo Lugogo
 Kipa wa Rwanda aliyelala chini akijitahidi kuokoa goli lililofungwa na Amri Kiemba baada ya kazi nzuri iliyofanywa na Mwinyi Kazimoto ya kuwapita mabeki wa timu ya Rwanda
 Mashabiki wa Kilimanjaro Stars inayodhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, wakishangilia wakati wa mchezo wa Robo Fainali ya kwanza ya michunao ya Cecafa Challenge dhidi Rwanda uliochezwa katika Uwanja wa KCC uliopo Lugogo nchini Uganda. Kilimanjaro Stars ilishinda 2-0
 Mshambuliaji wa timu ya Kilimanjaro Stars inayodhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, Mrisho Ngasa aliyelala chini na wachezaji wenzake wakishangilia kwa staili ya aina yake baada ya kuwafunga Rwanda 2-0 katika mchezo wa Robo Fainali ya kwanza ya michuano ya Cecafa Challenge uliochezwa leo katika Uwanja wa KCC uliopo Lugogo nchini Uganda
Wachezaji wa Kilimanjaro Stars inayodhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro Premium Lager wakitoka Uwanjani baada ya kipindi cha kwanza kumalizika katika mchezo wa Robo Fainali ya kwanza ya michuano ya Cecafa Challenge uliochezwa katika Uwanja wa KCC uliopo Lugogo

ROSE MUHANDO KUTAMBULISHA MPYA KUPITIA TAMASHA LA SHANGWE ZA KAGERA






MWIMBAJI maarufu wa muziki  wa Injili nchini, Rose Muhando amewataka wadau kujitokeza kwa wingi katika tamasha la ‘Shangwe Kagera’ linalitarajiwa kufanyika Desemba 9 kwenye Ukumbi wa Linas mjini Bukoba na uwanja wa Kaitaba.
Muhando na Enock Jonas ‘Zunguka’ watapamba katika maalum la kuchangia watoto yatima lenye lengo la kuielimisha jamii na kuamsha mwamko wa kusaidia watoto yatima na wanaoishi katika maisha magumu. 
Akizungumzia tamasha hilo Rose alisema amejiandaa kusherekea  Uhuru kwa aina yake tofauti na watu wengi walivvozoea kwa kuwashirikisha watoto yatima na wale wanaoishi katika mazingira magumu. 
“Nimefurahi kupata nafasi ya kutumbuiza katika tamasha hili la aina yake hasa katika  mkoa wa Kagera ambapo itakuwa mara ya kwanza kuonekana live katika mji wa Bukoba”, alisema . 
Muhando aliwamba wananchi wa Bukoba kufika kwa wingi katika tamasha hilo la kipekee katika ukuonyesha moyo wa upendo kushirikiana na kusaidia jamii ya watu wengine wasio jiweza.
Alisema kupitia tamasha hilo anatarajiwa kuwapa uhondo wa nyimbo zake za zamani sambamba na kutambulisha nyimbo zake mpya ambapo wakazi wa huko watapata fursa ya kuzisikiliza kwa mara ya kwanza. 
 Naye Zunguka amewataka wakazi wa Kagera kukaa mkao wa kula kwa ajili ya tamasha hilo na watarajie kupata burudani ya kutosha na ya kipekee kutoka kwake  ambayo itawajenga roho ya imani, kupendana na kusaidia watu yatima na watoto wanaoishi katika mazingira magumu ili nao waweze kufaraia maisha. 
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Kampuni ya Beula Communications Ltd, ambao ni waandaji wa tamasha hilo,Melkizedeck Mutta alisema maandalizi yanakwenda vizuri na kuwataka wadau kujitokeza kwa wingi siku hiyo.
Aliongeza kuwa mbali ya wasanii hao, pia tamasha hilo litapambwa na burudani kutoka  bendi ya muziki ya wazawa mkoa huo, Kakau Band pamoja na vikundi vingine vya wanakwaya  wa makanisa mbalimbali na  kikundi cha watoto yatima.

JULIUS KIHAMPA NA GRACE KINGARAME, WALIVYOMEREMETA MWISHONI MWA WIKI





Mwandishi wa Habari za michezo Mwandamizi wa Gazeti la Jambo Leo, na mchezaji wa timu ya TASWA Fc, Julius Kihampa, akimvisha pete ya ndoa Mke wake Grace Kingarame, ambaye pia ni  Mtangazaji wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC), wakati wa ibada ya Ndoa yao iliyofanyika kwenye Kanisa la Anglikana la St Albano jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita.

LUNDENGA, JE WAMJUA MISS TANZANIA HUYU?





 MATAPELI wa Dunia, Miss huyu "MAGGIE R  MUNTHALI" akiwa amevalia taji lake linalosomeka Miss Tanzania, akiwa katika moja ya shindano la urembo huku akiwaakilisha nchi yetu ya Tanzania katika mashindano hayo kama mwakilishi aliyeteuliwa na wahusika kuwakilisha katika shindano hilo lililokuwa likifanyika Washngton DC hivi karibuni.

Je Mkurugenzi wa Kamati ya MIss Tanzania, Hashim Lundenga, unamtambua Mrembo huyu? na je unaweza kutufahamiasha wadau wa urembo kuwa aliwahi kushiriki katika shindano lako la mwaka gani?, Na je uliwahi kutangaza kumteua mrembo huyu kuiwakilisha nchi katika shindano lolote na urembo kwa kutumia Taji la Miss Tanzania? 

Dunia ya sasa ni Kijiji, inawezekana pamoja na kuishi huko majuu, mdada huyu pamoja na waliomshauri hawajui mambo ya mtandao na hawatambui hilo kuwa hivi sasa duni ni kijiji, na ndiyo maana wakaamua kuwatapeli wasiojua na kuwadanganya kuwa huyu ndiye Miss Tanzania ili waweze kupata kile walichokikusudia.

Wadau wanahitaji Tamko rasmi kutoka kwa wahusika Kamati ya Miss Tanzania na majibu kamili kuhusiana na jambo hilo la Miss Tanzania FEKI.


KAULI YA WADAU WA UREMBO KUTOKA WASHNGTON DC
NA TUNAOMBA UTWAMBIE JE ALISHINDA NA KUTWAA TAJI HILO?.....WAPO MAMISS WENGI AMBAO WANAFANYA KAZI KUBWA SANA KUWEZA KUFIKIA KUITWA MISS,WAMEVIJA JASHO KUPITIA VIKWAZO HADI KUSHINDA NA KUIWAKIRISHA NCHI VYEMA....TUNAOMBA MTU ANAPOAMUA KUIBEBA BENDERA YA NCHI ASIWE MTU WA KUFOJI.....HUU NI WIZI WA KUMUITA MTU MISS TANZANIA WAKATI HAJAWAHI KUWA..TUNAOMBA PIA SWALA HILI MHESHIMIWA LUNDENGA KAMA SIO LA HALALI BASI LIFIKISHWE KWA WAANDALIZI WA MISS AFRICA USA KWANI INAWEZEKANA KABISA WAMERUBUNIWA..AU LABDA WANAVIGEZO VYAO.TUNAOMBA WATANZANIA MLIOKO NJE YA NCHI MSITUDANGANYE NA KUTUIBIA KWANI WATANZANIA SIKUIZI TUKO KWENYE MITANDAO....HABARI HIIZI PIA TUTAZIPELEKA WIZARA YA MABO YA NJE KWANI HUWEZI KUIWAKIRISHA NCHI PASIPO HALALI..!
AHSANTE.....MUNGU IBARIKI TANZANIA !
WADAU WASHINGTON
ZAID  TEMBELEA

RAIS KIKWETE AZINDUA MABWENI YA WASICHANA SHULE YA SEKONDARI NACHINGWEA





Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kuzindua rasmi mabweni ya Wasichana katika shule ya sekondari ya Nachingwea leo.Wengine katika picha kutoka kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi Ludovick Mwananzila,Mkuu wa Shule ya Wasichana Lindi Bi.Rahma Zedi (Wapili kushoto),Mkurugenzi wa wilaya ya Nachingwea,Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Bibi.Regina  Chonjo na Mbunge wa Jimbo Nachingwea  Bwana Mathias Chikawe.Picha na Freddy Maro

MH. SHY ROSE BANJI ATETA NA KIONGOZI MTUKUFU WA ISMAILIA AGA KHAN






Kiongozi Mtukufu Aga Khan ambaye ndiye Mwenyekiti wa Mtandao wa Maendeleo wa Aga Khan (AKDN) na Kiongozi wa Waislamu wa Ismailia akizungumza mawili matatu ya kimaendeleo na Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki kutoka Tanzania Mh. Shy-Rose Bhanji wakati wa ufunguzi wa Makao Makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki mkoni Arusha. Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Masuala ya Kidiplomasia ya AKDN Dkt. Shafik Sachedina. ( Picha zote kwa Hisani ya Ikulu).

TBL YAADHIMISHA SIKU YA UKIMWI DUNIANI. 400 WAJITOKEZA KUPIMA VIRUSI VYA UKIMWI






 Watoto wanaolelewa katika Kituo cha Walioathirika kwa Ukimwi cha Tocha +, Saad Ramadhan (kulia) na Arnold Goha wakiwasha mshumaa na Mratibu Mkuu wa Kifua Kikuu na Ukimwi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Dk. Hakimu Mwaikasu, wakati wafanyakazi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), ikiadhimisha Siku ya Ukimwi Duniani, Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa TBL, Keneth Wanyoto. Zaidi ya watu 400 walipima Virusi vya Ukimwi siku hiyo. PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG.
 Watoto wanaolelewa katika Kituo cha Walioathirika kwa Ukimwi cha Tocha +, Saad Ramadhan (kulia) na Arnold Goha pamoja na Meneja Uhusiano Mambo ya Nje wa TBL, Emma Orio wakiwasha mishumaa wakati wa maadhimisho hayo
Wafanyakazi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), wakiwasha mishumaa wakati wa maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani, Dar es Salaam
Banda lililowekwa na TBL  katika Soko la Ilala Mchikichini, Dar es Salaam ili wafanyabiashara washiriki kupimwa virusi vya Ukimwi
 Mkazi wa Ilala Mchikichini, Abdalah Lukali (58), kushoto, akichukuliwa damu na Mshauri Nasaha kutoka Amref, tayari kupimwa virusi vya Ukimwi katika banda lililowekwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), katika Soko la Ilala Mchikichini, Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani.
 Fundi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Shabani Kilango (kushoto) akichukuliwa damu na Mshauri Nasaha kutoka Amref, Elizabeth Sangu  tayari kupimwa virusi vya Ukimwi wakati wafanyakazi wa kampuni hiyo wakiadhimisha ya Siku ya Ukimwi Duniani, Dar es Salaam juzi.
 Mtalaamu wa upishi wa TBL, Edward Mvula akichukuliwa damu tayari kupimwa virusi vya Ukimwi

TTCL ILIVYOSHIRIKI KATIKA MADHIMISHO YA SIKU YA UKIMWI KITAIFA - LINDI




Wafanyakazi wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) wakiwa  katika picha ya pamoja kwenye maonesho hayo.

 Meneja Biashara Mkoa wa Lindi, Omari Mbogo akipokea cheti cha ushiriki wa maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani yaliyofanyika kitaifa mkoani Lindi, kutoka kwa mmoja wa waratibu wa maadhimisho hayo aliyekabidhi kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa huo, Ludovick Mwananzila. Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), walikuwa miongoni mwa wadhamini wa maadhimisho hayo. (Na Mpiga Picha Wetu)
  Wafanyakazi wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) wakiwa  katika picha ya pamoja kwenye maonesho hayo.
 Rais Jakaya Kikwete akipata maelezo kuhusu Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano kutoka kwa Bi. Anifa Chingumbe.

Sunday, December 2, 2012

NGUMI ZAAMASISHWA KWA KISHINDO BAGAMOYO MKOA WA PWANI




Bondia Zumbe Kikuru kushoto akipambana na Toma Kato wakati wa mpambano wao uliofanyika katika ukumbi wa Saadan High Way Bagamoyo mwishoni mwa wiki iliyopita Kikuru alishinda kwa  K'O raundi ya pili Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Mashabiki waliojitokeza kushudia mpambano wa masumbwi uliofanyika katika ukumbi wa Saadan High Way Bagamoyo mwishoni mwa wiki iliyopita Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Zumbe Kikuru kushoto akipambana na Toma Kato wakati wa mpambano wao uliofanyika katika ukumbi wa Saadan High Way Bagamoyo mwishoni mwa wiki iliyopita Kikuru alishinda kwa  K'O raundi ya pili Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Refarii wa mpambano wa masumbwi Said Chaku katikati akimwinua mkono juu bondia Obete Ameme baada ya kumtwanga mpinzani wake katika raundi ya kwanza kwa K,O uliofanyika katika ukumbi wa Saadan High Way Bagamoyo mwishoni mwa wiki iliyopita Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Mashabiki waliojitokeza kushudia mpambano wa masumbwi uliofanyika katika ukumbi wa Saadan High Way Bagamoyo mwishoni mwa wiki iliyopita Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com


Na Mwandishi Wetu
Kocha wa Kimataifa wa mchezo wa Masumbwi nchini anaefundisha Timu ya Ashanti pamoja na timu ya Mkoa wa Ilala Kimichezo Rajabu Mhamila 'Super D' amevutiwa na mashabiki wa mchezo huo mkoa wa Bagamoyo Pwani

Baada ya kuvutiwa na umati mkubwa uliojitokeza katika mpambano uliofanyika Bagamoyo mkoa wa pwani mwishoni mwa wiki iliyopita mpambano uliofanyika katika ukumbi wa Saadan High Way ambapo uliudhuliwa na mashabiki wengi wa bagamoyo

Kocha huyo anaefundisha kwa njia mbalimbali ikiwemo DVD amevutika kwa wapenzi wa ngumi bagamoyo kuchangamkia DVD hizo zenye kuelimisha mchezo wa masumbwi pamoja na kujua shelia mbalimbali za ngumi Duniani

Mpambano huo ulioandaliwa na Sharif Muhsin na kuratibiwa na bondia wa siku nyingi Said Yazidu umefungua ukurasa mpya kwa wakazi wa bagamoyo kuukubali mchezo huo na kuendelea kuupenda na kuwapa sapotimabondia wanaowakilisha Bagamoyo

Baazi ya mabondia waliopigana katika mpambano huo ni Maneno Zele alipata kichapo kutoka kwa Baisa Juma wakati Zumbe Kikuru alimtwanga kwa K,O Tomo Kato katika raundi ya kwanza huku Kadani Rhamwana alimchapa Ndumbo Hassani kwa point 

Mpambano huo ni wa pili kufanyika kwa mwaka huu umendelea kuwa chachu ya kupata vipaji vipya vya mchezo wa ngumi hapa nchini

PROFESIONAL KIBAO NDANI YA NDONDO DAR ES SALAAM




Mshambuliaji wa Mpumalanga Adam Kingwande (Anachezea African Lyon)  mwenye mpira akijaribu kumtoka mshambuliaji wa Vuguvugu Husein Kicheche (Anachezea Bandari ya Kenya) kwenye mchezo wa fainali ya mashindano ya jezi uliochezwa juzi uwanja wa Chuo cha Bandari, Vuguvugu ilitwaa kombe baada ya kuifunga Mpumalanga mabao 4-2





Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Kata ya Tandika wilaya ya Temeke akikabidhi zawadi ya mbuzi nahodha wa timu ya Mpumalanga amabo ni washindi wa pili wa mashindano ya jezi yaliyokuwa yameandaliwa na Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi kata ya Tandika kwenye uwanja wa Chuo cha Bandari, Temeke jijini Dar es Salaam.

Mshambuliaji wa Kimataifa anayechezea Bandari ya Kenya inayoshiriki ligi kuu nchini humo Husein Kicheche jana aliisaidia timu ya mtaani kwake ijulikanayo kama Vuguvugu kutwaa kombe la jezi lililochezwa uwanja wa Chuo cha Bandari.


Mchezo huo ambao ulikuwa wa fainali ya mashindano ya kuwania jezi uliandaliwa na Umoja wa Vijana Kata ya Tandika wilaya ya Temeke na ulizikutanisha timu zaidi ya 30.

Fainali ilichezwa katti ya Vuguvugu na Mpumalanga, mchezo ambao ulivuta hisia za mashabiki kiasi cha kujaza uwanja wa Chuo cha Bandari kutokana na timu zote kuwa na wachezaji wa wanaocheza ligi kuu Bara na Zanzibar.

Timu ya Vuguvugu ambayo ilikuwa ikicheza mchezo wa kasi iliifunga wapinzani wake timu ya Mpumalanga mabao 4-2.

Mabao ya Vuguvugu yalifungwa na Babu Deo dakika ya 8 ya mchezo baada ya kupokea pasi toka kwa Husein Kicheche na la pili lilifungwa na Oseja Said dakika ya 30.


Kipindi cha pili kilianza kwa kasi sana iliwachukua dakika mbili kuongeza bao la tatu lililofungwa na Kimbu Musa anayechezea Toto African kwa shuti la mbali na karamu ya mabao ilihitishwa na Mponda Nurdin dakika ya 78.

Mpumalanga walipata bao la kwanza kwa njia ya penalti lililofungwa na Adam Kingwande dakika ya 58 na bao pili lilifungwa na Muhaji Kampala dakika ya 82.

Wachezaji wanaochezaji ligi kuu wamekuwa wakichezea timu za mtaani kwa kipindi hiki cha mapumziko.

Baada ya mchezo kumalizika mgeni rasmi Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Kata ya Tandika alitoa zawadi ambapo timu ya Vuguvugu walikabidhiwa seti ya jezi na Mpumalanga walipewa zawadi ya mbuzi.

Pia aliwaasa wachezaji kutumia michezo kama ajira hivyo nidhamu ni muhimu ili kufikia malengo yao.
"Mnatakiwa mcheze michezo mkijua ndio ajira yenu hivyo nidhamu ni muhimu ili kufikia malengo mliojiwekea", alisema.