Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Saturday, June 22, 2013

KALA PINA 'NABII KOKO' APIGA BONGE LA SHOO



 Chid Benz akikonga nyoyo za mashabiki wake wakati wa shoo ya Kikosi cha Mizinga kutimiza miaka 13 iliyofanyika katika ukumbi wa New Msasani jijini Dar es salaam. (Picha zote na Habari Mseto Blog).
 Chid Benz
 Fukuda akichana mistari
 Katibu wa CUF, Julius Mtatiro ambaye alikuwa mgeni rasmi  akizungumza wakati wa shoo maalumkundi la muziki wa Hip Hop la Kikosi cha Mizinga kutimiza miaka 13.
Baadhi ya watu waliotoa mchango mkuwa kwa wasanii wa Kikosi cha Mizinga walipewa vyeti, hapa mwandishi Joseph Zablon akionesha cheti chake baada ya kukabidhiwa ba mgeni rasmi. 
 Mwakilishi wa Clouds Radio akipokea cheti.
   
 Kala Pina 'Nabii Koko' akitumbuiza
 
 Afande Sele akipagawisha  mashabiki.

KAULI YA PINDA; ASIYETII PIGA TUMECHOSHWA ITAMLIZA TENA?




‘Ngariba ukimpa mtoto atamfanya vyoyote atakavyo’

Na Bryceson Mathias

KUTOKANA na watanzania nchini kupoteza Imani na Jeshi la Polisi kila Kona ya nchi, kuwa linakisaidia Chama Tawala (CCM), huenda Kauli ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ya kulipa Jeuri Jeshi hilo kuwa, liwapige tu wasiotii amri waumechoshwa; litamsababishia kulia Tena!.

Kauli ya Pinda imesemewa mahali palepale aliposemea awali kuhusu wanaoua walemavu wa Ngozi (Albino) kuwa nao wauawe, na alipogeuziwa kibao na watoa hoja wa eneo hilo hilo aliloko, alilia kwa uchungu na kujutia Kauli ya Ulimi wake, jambo linaloonesha litamrejea!

Kwa kuwa Pinda ni Msimamizi Mkuu wa Shughuli za Serikali bungeni, wananchi hawaoni kama Pinda kasema, ila wanatafsiri kwamba hiyo ndiyo Kauli ya Serikali ya sasa na Muundo wake (Mfumo), na kuwa sasa itakuwa mtu asipotii Sheria bila Shuruti ni kupiga tu! Tumechoka!.

Lakini kibaya kinachojitokeza, Pinda katamko kauli hiyo nzito kwenye chombo kikuu cha kutunga sheria kati ya Mihimili mitatu (Utawala, Mahakama na Bunge), hivyo watu wanahisi Taswira hii; ‘Kama anaweza kutoa Kauli hiyo nzito hadharani, akiwa kwenye vikao vya siri Je!

Wadau wengi wanapohojiwa Sirini ni wapi wanadai, Kwenye Vikao vya Mikakati ya Uongozi ndani ya Itikadi yake, Halmashauri Kuu, Kamati Kuu, huku wengine wakisema, Pinda hajui Ugeugeu wa Polisi, linaweza kuanza utekelezaji kwa nguvu wakisingizia kasema Waziri Mkuu.

Jambo kubwa linalowauma watanzania wengi waliosikia Kauli ya Pinda na Michanngo mbalimbali, hasa baadhi ya Wasomi na Watalaam wa Uchumi wanasema,”Pinda katoa Kauli hiyo wazi mno, na kwamba, Vyombo vya Habari na vya Haki vya Kimetaifa vimemsikia.

“Awali Waziri, Bernard Membe, alilalai ati kuna watu wanadiriki kushawishi Wawekezaji Nje, ili inyimwe misaada kwa kukosa uzalendo na nchi yao”. Wanahoji, kwa tamko la Pinda, Wawekezaji wakisitisha Misaada Tanzania, Mchawi ni Nani?
Pia ni hofu ya watanzania kwamba, Kama mtu ukimkabidhi Ngariba mtoto; humfanya anavyotaka, hata mtoto akilalamika kufanyiwa sivyo ndivyo, huambiwa hatii sheria za Jandoni!

Upo uwezekano mkubwa na hata Polisi huenda wakaitumia vibaya amri ya Pinda wakidai, wao ni ndio Afande hakuna kuuliza, na kwa hiyo watawapiga wananchi ovyo, kwa madai wanatekeleza maagizo, mtu asipotii sheria pasi shuruti, Pinda aliagiza Piga tumechoshwa!

Utekelezaji mbaya wa kauli hiyo, itafika mahali utaleta madhara, kwa sababu wananchi watapigwa na baadaye nao watachoshwa na vipigo vya Polisi, na kusema inatosha, tumepigwa kiasi cha kutosha, tumeonewa kiasi cha kutosha, na unyonge wetu ndio uliotufikisha hapo, basi! Enough is enough.

Baaadhi ya wasomi wa Uchumi Mzumbe Morogoro walisema, Awali walizoea kusikia Ugonjwa wa Upofu wa Macho upo Mikoa miwili nchini! Lakini wanadai, sasa nchi nzima watu watakuwa vipofu, wenye miwani.

Wanadai sababu kubwa macho ya watoto Shule yataharibiwa kwa mabomu ya machozi, Maji ya kuwasha na Moshi, kutumika na kuhatarisha afya zao bila sababu za msingi, ambapo matibu ya uwingi wao, yatayumbisha uchumi kimatibabu.

Waliongeza, ni kweli akili ni nywele kila mtu ana zake, lakini akili za kuharibu uchumi kwa mabomu, na baadaye kuanza kuhangaikia tiba ya magonjwa yatakayosababishwa na vuruguru za tamaa ya baadhi ya watawala kung’ang’ania madaraka iletayo adha ya kuutweza uchumi, Ipo mlangoni.

Timu nane kushiriki bonanza la Breake Point Jumapili



JUMLA ya timu nane zimethibitisha kushriki katika bonaza la soka klabu ya Break Point lililopangwa kufanyika Jumapili Juni 23 kwenye viwanja vya Survey (Chuo Kikuu cha Ardhi).
Mkurugenzi wa Breake Point Outdoor Distributors, Daudi Machumu alizitaja timu ambazo ambazo zitashiriki katika bonanza hilo lililodhaminiwa na kampuni ya bia ya Seregeti (SBL) kuwa ni, Rose Garden, Survey, Mbezi Beach na Boko Veterans.
Machumu alisema kuwa timu nyingine ni Clouds Media Group, Magogoni, Umoja na waaandaaji, Break Point ambayo itakuwa chini ya Rodrick “Neymar” Mwambene. Alisema kuwa bonanza hilo  limepangwa kuanza saa 2.30 asubuhi na madhumuni yake ni kuwakutanisha wadau wa michezo na kubadilishana mawazo.
“Lengo kubwa ni kupromoti michezo na kujadili mambo mbali mbali, kampuni ya Break Point Outdoor Distributors ni wadau wakubwa wa michezo na sanaa, tumedhamini mashindano ya urembo na shughuli nyingine, bonanza hili ni fursa pekee kwa wadau kukutana na kustarehe kwa pamoja huku wakipata vinywaji ambavyo vitauzwa kwa bei ya promotion na nyama choma,” alisema Machumu.
Alisema kuwa pia kutakuwa na bia za bure kwa timu shiriki na kuwataka kuzingatia muda kwani wachezaji wa Ligi Kuu na Ligi nyingine hawaruhusiwi na usimamizi utakuwa mkali. “Hii ni fursa kwa wachezaji walioachana na mpira wa miguu wa ushindani, tunataka timu kuzingatia hayo,” alisema.
Machumu alisema kuwa wameandaa burudani mbali mbali ili kunogesha siku hiyo muhimu sana kwa wadau wa michezo. “ Natoa wito kwa mashabiki kufika na timu kuzingatia muda, kwani mtindo utakaotumika utakuwa wa ligi,” alisema.

Wateja watano wajizolea Milioni 2 kila mmoja za Cheka Nao



Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Bw.Matina Nkurlu akimpigia mmoja wa washindi miongoni ya watano waliojishindia shilingi milioni mbili  kila mmoja kwenye droo kubwa ya Promosheni ya Cheka Nao,inayowezesha  wateja kuongea na mitandao yote bila mipaka kwa bei nafuu. Ili kujiunga mteja anatakiwa kupiga *149*01#.wanaoshuhudia   ni Meneja wa Idara ya Malipo ya Kabla wa kampuni hiyo, Yvonne Maruma (kati kati)pamoja na  Ofisa wa bodi ya michezo ya kubahatisha Tanzania Bi.Chiku Saleh.
     HAWA NDIYO WASHINDI WA PROMOSHENI YA CHEKA NAO - 21/06/2013
WAMEJINYAKULIA KITITA CHA  MILIONI TSH 2,000,000 KILA MMOJA
  



JINA
UMRI
ANAKOISHI
KAZI YAKE
Majija Amos Kidara
24
Shinyanga - Kahama
Peasant
Mkude Idd
30
Msamvu - Morogoro
Peasant
Isaya Edward Sengo
35
Mbeya
Petty Trader
Alexander Vinson
33
Mbinga - Ruvuma
Peasant
Derick Charles Cosmas
25
Karagwe - Bukoba
Peasant







Friday, June 21, 2013

YOHANA ROBERT VS YOHANA MATHAO KUPAMBANA JUNE 30



Bondia Yohana Robart kushoto akitunishiana misuri na Yohana Mathayo wakati wa utambulisho wa mpambano wao utakaofanyika june 30


Bondia Yohana Robart kushoto akitunishiana misuri na Yohana Mathayo wakati wa utambulisho wa mpambano wao utakaofanyika june 30

MPAMBANO WA MABINGWA



Japhet Kaseba, Mada Maugo kumaliza ubishi Septemba 7





https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiCJ875kXCjT27WYdmiEcPdGQW6TKJ8lXRFDJb8EfCGDNEK8jBpPjeucfEAlb_TMY77LGU7b5GYxWORiAZIyANCQqjBRY46msvNiiVS_VnUG6HUqaIpUftwkFG36AADCAacHUKOq5XXH-SX/s1600/7.JPG
Mada Maugo (kushoto) akichuana na Kaseba katika pambano lao la kwanza April 16, 2011
MABONDIA machachari wa ngumi za kulipwa wenye upinzani mkubwa nchini, Japhet Kaseba 'Champion' na Mada Maugo 'King maugo Jr' wanatarajiwa kuvaana Septemba 7 mwaka huu katika pambano la kumaliza ubishi baina yao litakalofanyika jijini Dar es Salaam.
Wanamasumbwi hao walipambana mara ya mwisho April 16, 2011 na Maugo kuibuka kidedea kwa TKO  ya raundi ya saba baada ya wapambe wa Kaseba kuingia ulingoni na kumvua bondia wao glovu ikiwa bado raundi moja kabla ya pambano hilo kumalizika.
Akizungumza na mwandishi hivi punde, Kaseba alisema pambano hilo litakuwa la kuwania taji lililo wazi la WBF kwenye ukumbi kati ya Diamond Jubilee au PTA na litasimamiwa na Shirikisho la Ngumi za Kulipwa Tanzania (PST).
Kaseba alisema anaamini pambano hilo ndilo litakalomaliza ubishi kati yake na Maugo baada ya kutoridhishwa na ushindi aliopewa walipoumana mara ya mwisho.
Bondia huyo aliyetoka kumnyuka Mmalawi, Rasco Simwanza kwa KO ametamba kuibuka na ushindi mbele ya Maugo ambaye kwa sasa yupo katika maandalizi ya kwenda Russia kuzipiga na mwenyeji wake Movsur Yusupov Julai 27 kwa sababu amebaini ili kumaliza ubishi ni lazima ashinde kwa KO kitu alichoanza kutumia sasa katika mapambano yake.
"Nimebaini ukimpiga mtu kwa KO hakuna malalamiko tofauti na kumaliza pambano na kushinda kwa pointi, hivuo Maugo ajiandae kukumbana na KO ya hatari kwa vile kiu yangu ni kutwaa ubingwa wa dunia kama nilivyofanya kwenye Kick Boxing," alisema Kaseba.
Maugo mwenyewe hakupatikana kueleza tambo hizo za mpinzani wake, ingawa imefahamika kuwa tayari kila kitu juu ya pambano hilo ikiwemo kusainishwa kwa mikataba kumeshafanyika.

'SUJUTII KWA NILIEKUWA NAE' YA BARNABA VIDEONI






Na Elizabeth John

MKALI wa muziki wa kizazi kipya nchini, Barnaba Elias ‘Barnaba’ ameachia video ya kibao chake kipya kinachokwenda kwa jina la ‘Sijutii kwa niliekuwa nae’ ambacho kinafanya vizuri katika vituo mbalimbali vya redio.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Barnaba alisema wimbo huo kaupeleka sokoni wiki iliyopita na kwamba umeshaanza kufanya vizuri katika soko hilo, kitu ambacho kinampa moyo wa kufanya kazi hiyo bila kuchoka.
“Kama kawaida yangu nyimbo zangu nyingi huwa haziwachukizi mashabiki wangu ni jambo ambalo namshukuru mungu kwani ni wasanii wachache ambao nyimbo zao zinafanya vizuri mtaani,” alisema.
Barnaba alisema anawaomba mashabiki wa muziki huo kuendelea kumpa sapoti katika kazi zake ikiwa ni pamoja na kukaa mkao wa kula kwaajili ya kupokea kazi nyingine ambazo zinakuja.
Mbali na kibao hicho, Barnaba alishawahi kutamba na vibao vyake kama, Magubegube, Wrong number, Tulizana, Milele daima, Sorry na vinginevyo ambavyo vinafanya vizuri katika tasnia ya muziki wa kizazi kipya nchini.

FILAMU YAMFANYA IRENE PAUL AJIFUNZE KUENDESHA BAJAJI







Na Elizabeth John

AKIWA bado anafanya vizuri katika filamu, mwanadada  Irene Paul amesema kwamba filamu ya kibajaji  ilimfanya ajifunze kuendesha chombo hicho kwa lazima ili kuleta uhalisia.

Japo awali alisema aliona kama ingekuwa ni kazi ngumu sana kwake lakini ilimbidi kukaza roho kwa kuwa yeye ni msanii ambaye angependa kuwaonesha mashabiki wake vitu vya ukweli na si vya kuongopea.


Katika filamu hiyo ambayo safu hii iliichambua wiki iliyopita, Irene ameweza kuitendea haki akiwa sambamba na mchekeshaji Salum Haji’Mboto’ ambapo kumejaa vituko vitakavyokufanya ucheke hata  kama umemka vibaya siku hiyo.

Mwanadada huyo ni kati ya wasanii ambao wanakuja juu katika tasnia hiyo ambapo mwaka huu amefanikiwa kuchukua tuzo ya msanii bora wa kike anayechipukia, zilizotolewa katika ukumbi wa Ubungo Plaza wiki iliyopita jijini Dar es Salaam.

LUIZA MBUTU KUJA NA 'MAISHA BAADA YA NDOA'





Na Elizabeth John 
BAADA ya miaka michache kutoka na wimbo wa Kuolewa, mwanamuziki Luiza Mbutu, anatarajia kuachia single nyingine ya ‘Maisha baada ya kuolewa’.
Akizungumza na Habari Mseto, Mbutu alisema anakuja na kitu hicho baada ya kupata uzoefu wa muda sasa katika maisha ya ndoa jambo litakalomfanya kuimba jambo analolijua.

Luiza Mbutu aliolewa mwaka 2000 na kwa sasa ndiye  kiongozi wa bendi ya Twanga Pepeta huku akiwa kati ya wanamuziki waliodumu katika bendi hiyo takribani miaka 12.

mwanadada huyo ni kati ya wasanii wakongwe wa bendi hiyo tamgu kuanzishwa kwa bendi hiyo.
You might also like:

CRDB YAMPA SHAVU MATALUMA





 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akipokea mic kutoka kwa msanii wa muziki wa kizazi kipya, Mataluma baada ya kumtaka aanza kuimba kabla ya msanii huyo kuanza kutoa burudani wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya Wakala wa benki hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akiimba kibao cha Mataluma kinachokwenda kwa jila la ‘Tunasonga Mbele’. 
 Mataluma akiimba kwa hisia wimbo wa CRDB 'Tunasonga Mbele'
 Wacheza shoo wakionesha manjonjo yao.
DAR ES SALAAM, Tanzania
MSANII wa Bongo fleva kutoka Nyumba ya Vipaji Tanzania (THT), Mataluma na wacheza shoo wa kundi hilo, walishindwa kuamini baada ya Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei kueleza nia ya kununua kibao cha ‘Tunasonga Mbele’.

Kibao hicho kilichotungwa na Mataluma kwa ajili kupamba uzinduzi wa mfumo mpya wa kuhudumia wateja wa CRDB wa FahariHuduma, kilimvutia mno Dk. Kimei na kuagiza idara husika kukaa na msanii huyo kufanya mazungumzo ya kukinunua.

“Nimevutiwa mno na ubunifu uliofanywa na mtunzi katika kibao hiki na ningependa kuona CRDB inakimiliki na kukitumia katika matangazo yetu tofauti, hivyo naiagiza idara husika kukaa na Mataluma na kumlipa, ili asije kukitumia mahali pengine,” alisema Dk. Kimei.
Uamuzi huo ulipokelewa kwa shangwe kutoka kwa waalikwa wa uzinduzi huo, uliofanyika hoteli ya Kempinski, huku wacheza shoo wa THT na Mataluma wakipagawa kutokana na agizo hilo ambalo hawakulitegemea.

Akizungumza baada ya agizo hilo la Dk. Kimei, Mataluma alikiri kufurahishwa kuona utunzi huo umewavutia wengi ukumbini kiasi cha mkurugenzi huyo kukihitaji moja kwa moja, na kwamba anaamini mazungumzo baina ya pande mbili yatafikia muafaka.

 “Nina kila sababu ya kufurahi, kutokana na siku hii kuwa ya aina yake kwangu kama msanii. Namshukuru Dk. Kimei kwa kuvutiwa na kuthamini kilichofanywa katika kibao hiki maalumu kwa ajili ya hafla hii ya uzinduzi wa FahariHuduma ya CRDB,” alisema Mataluma.

Katika uzinduzi huo, Mataluma alikonga vilivyo nyoyo za waalikwa kwa kuimba mashairi yanayoelezea ubora wa huduma za benki ya CRDB, huku wacheza shoo wakionesha umahiri mkubwa wa kumiliki jukwaa. 

CHEKIBUDI ASHUKURU MAPOKEZI YA 'DIKTETA'






Na Elizabeth John

MUIGIZAJI wa filamu nchini, Mohamed Nurdin ‘Chekibudi’ amewashukuru wadau na wapenzi wa kazi zake baada ya kumpokea vizuri na kazi yake inayokwenda kwa jina la ‘Dikteta’, ambayo imeanza kufanya vizuri sokoni.
Filamu hiyo inayoonesha ukandamizaji wa familia, imekamilika na kuingizwa sokoni hivi karibuni, ambapo tayari imeanza kufanya vizuri katika  mauzo baadhi ya maeneo ya jijini  Dar es Salaam, ikisambazwa na kampuni ya steps Entertaiment.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Chekibudi alisema, filamu hiyo ameiandaa ili kuonesha ukandamizaji uliopo baadhi ya familia katika maisha ya kila siku, na amefarijika kuona iko katika wakati mzuri sokoni.
Alisema baada ya kuangalia hilo, aliamua kuweka wazo lake katika filamu ili kuwafikishia ujumbe watu wengi zaidi na ikawa kama ni moja ya kazi za wasanii kuelimisha na kufundisha jamii.
“Unajua unapokuwa msanii unatakiwa kuwa mbunifu katika mambo mengi na ndiyo maana kila kukicha tunaangalia ni jinsi gani tutawakumbusha wenzetu matatizo ambayo yanaepukika,” alisema Chekibudi.
Chekibudi alishawahi kufanya vizuri alipokuwa katika kundi la sanaa la ‘Splendid’, na katika filamu hiyo ya ‘Dikteta’ amewashirikisha nyota wengine kama, Cojack, Philipo, Munira Sultan, Snura Mush, Coletha Reymond pamoja na nyota wengine.

AMINI 'HAYUPO NAE'






Na Elizabeth John

BAADA ya kufanya vizuri na kibao chake cha ‘Ni wewe’, Mkali wa muziki wa kizazi kipya nchini, Amin Mwinyimkuu ‘Amini’ anajipanga kuachia video ya kibao chake cha ‘Sipo nae’ kinachofanya vizuri katika vituo mbalimbali vya redio.
Akizungumza na Habari Mseto jijini Dar es Salaama, Amini alisema anamshukuru mungu kazi hiyo imefanya vizuri na anaamini itafanya vizuri kutokana na ujumbe uliopo ndani ya kibao hicho.
Alisema wimbo huo kautengeneza katika studio ijulikanayo kwa jina la Shany chini ya mtengenezaji mahiri Mr. T ambaye anauhakika amemtendea haki katika kazi hiyo.
“Mtayarishaji wangu namuamini sana, hivyo najua wadau wengine wataupenda wimbo kulingana na vionjo ambavyo amevitumia mbali na ujumbe uliopo katika kazi hiyo.” alisema Amini.
Pia aliwaomba wadau na mashabiki wa muziki nchini kumpa sapoti katika kazi zake na wasicheze mbali na yeye kuna vitu vingi ambavyo amewaandalia.  
Licha ya kutaka kutoka na kibao hicho, Amini alishawahi kutamba na kibao chake cha ‘Robo saa’ ambacho kilimtambulisha na kufanya vizuri katika vituo mbalimbali vya redio na runinga.

TIBA YA UKOSEFU WA NGUVU ZA KIUME NA KIKE UVUMBUZI WAKE KITABU HIKI HAPA






KITABU AMBACHO KINATOA TIBA ZA UKOSEFU WA NGUVU ZA KIUME NA KIKE KWA KUTUMIA VYAKULA VYA ASILI IKIWEMO MATUNDA NA MBOGA MBOGA ZA MAJANI SASA KIPO MITAANI KINAPATIKANA MITAA YA UHURU NA MSIMBAZI KWA MAITAJI YA KITABU HIKI NA DAWA MBALIMBALI ZA KUTIBU MARADHI PAMOJA NA MATATIZO PIGA SIMU  0787406938

TANGAZO LA DAWA YENYE NGUVU ENZOY






DAWA YA NGUVU ZA KIUME NA MSIMKO KWA WANAWAKE WASIO NA HAMU YA TENDO LA NDOA AMBAYO HULETA MSISIMKO KWA WANAUME NA WAKE WAKUTANAPO.KWA SASA INAPATIKANA KWA BEI NAFUU HAPA JIJINI DAR ES SALAAM MAKUTANO YA MTAA WA KIPATA NA BARABARA YA MSIMBAZI
ALLY WA YANGA BOMBA UHURU NA MSIMBAZI 0787230551 AU 0652755838


PIGA SIMU KWA MR.MKUNJE O713827689, 0755074505 , au 0719 541366
,0652755838 UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM

BUGURUNI LOZANA STENDI YA TAX ULIZIA ADAMU KIBANDANI 0755875884
SHULE YA UHURU FIKA JENGO LA AZAM BAKHRESA ULIZA NGAEJE 0713873412


MWANANYAMALA FIKA JABA KLABU  ULIZA MACHELLAH 0713470492
ENZOY INALETA HESHIMA

Uhuru Seleman athibitishia kutua Coastal Union






KIUNGO mchezeshaji wa aliyekuwa akiichezea Azam kwa mkopo kutoka Simba, Uhuru Seleman ametua Coastal Union ya Tanga pia kwa mkopo kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Uhuru aliithibitishia MICHARAZO kwamba ametua Coastal kwa ajili ya ligi ijayo na kwamba anajifua vilivyo ili kuwapa raha mashabiki wa klabu hiyo aliyowahi kuichezea msimu wa 2007-2008 na kufikia kuzigombanisha Simba na Coastal wakimgombea kila mmoja alipodai ni mchezaji wake.
Kiungo huyo ambaye amewahi pia kutamba na Mtibwa Sugar, alisema amefurahi kutua Coastal kwa kuamini atapata nafasi nzuri ya kuonyesha kipaji chake baada ya kushindwa kupata fursa hiyo ndani ya Simba na hata Azam walipomchukua msimu uliopita.
"Ni kweli nimetua Coastal kwa mkopo na najiandaa kuichezea kwa msimu ujao, nimefurahi kwa sababu naamini nitarejesha makali yangu," alisema Uhuru.
Uongozi wa Coastal kupitia Mkurugenzi wake wa Ufundi, Nassor Binslum amethibitisha suala la kumnyakua kiungo huyo akidai wamezungumza na Simba ili wamchukue kwa mkopo na watasaidiana nao kulipa mshahara wa mchezaji huyo wakati akiichezea timu yao ambayo ilimaliza msimu wa ligi iliyopita katika nafasi ya 6.
Mabingwa hao wa zamani wa kandanda nchini mbali na kumnyakua Uhuru pia imewanasa wachezaji wengine wapya katika kukiimarisha kikosi chao baadhi yao ni beki Juma Nyosso na Haruna Moshi (wote Simba), Kenneth Masumbuko toka Polisi-Moro, Marcus Ndeheli na Said Lubawa (JKT Oljoro) na Abdallah Ally kutoka visiwani Zanzibar.

Thursday, June 20, 2013

KONYAGI YAGAWA VIFAA VYA KISASA VYA KUHIFADHIA TAKA

Meneja Mauzo na USAMBAZAJI WA kiwanda cha Konyagi cha Tanzania Distilleries Limited (TDL), Mwesige Mchuruza Akionesha kifaa cha kuifazia takataka ambapo jumla ya

Vifaa vya  kisasa 130 vya Kuhifadhia Taka vilitolewa na kampuni hiyo

Meneja Mauzo na USAMBAZAJI WA kiwanda cha Konyagi cha Tanzania Distilleries Limited (TDL), Mwesige Mchuruza (kushoto), akimkabidhi Meneja wa Baa ya Calabash iliyoko Mwenge, JUMA Kihoma, kifaa cha kuhifadhia taka zinazotokana na kinywaji aina ya kiroba kwa lengo la kudumisha usafi wa mazingira. Hafla hiyo ya kugawa vifaa 80 kwenye baa mbalimbali wilayani Kinondoni, Dar es Salaam, ilifanyika leo. Katika Wilaya ya Ilala waligawa vifaa 50.

Meneja Mauzo na Usambazaji wa Kiwanda cha Konyagi cha Tanzania Distilleries Limited (TDL), Mwesige Mchuruza (kushoto), akimkabidhi Meneja wa Baa ya Mama Kamche's iliyoko Mwenge, Patrick Mrema, kifaa cha kuhifadhia taka zinazotokana na kinywaji aina ya kiroba kwa lengo la kudumisha usafi wa mazingira. Hafla hiyo ya kugawa vifaa 80 kwenye baa mbalimbali wilayani Kinondoni, Dar es Salaam,
Meneja Mauzo na Usambazaji wa Kiwanda cha Konyagi cha Tanzania Distilleries Limited (TDL), Mwesige Mchuruza (kushoto), akimkabidhi Meneja wa Baa ya Etina iliyoko Mwenge,Egbert Mtunza, kifaa cha kuhifadhia taka zinazotokana na kinywaji aina ya kiroba kwa lengo la kudumisha usafi wa mazingira. Hafla hiyo ya kugawa vifaa 80 kwenye baa mbalimbali wilayani Kinondoni, Dar es Salaam, ilifanyika. Katika Wilaya ya Ilala waligawa vifaa

Meneja Mauzo na USAMBAZAJI WA kiwanda cha Konyagi cha Tanzania Distilleries Limited (TDL), Mwesige Mchuruza Akizungumza na wana habari wakati wa kugawa vifaa vya kuhifadhia takataka

Shindano la Epiq Bongo Star Search 2013 lazinduliwa



 Ofisa Biashara Mkuu wa Zantel, Sajid Khan ambao ndio wadhamini wakuu wa shindano la Epiq Bongo Star Search 2013, akifafanua jambo wsakati wa uzinduzi wa shindano hilo. (Picha zote Habari Mseto Blog)
Mshindi wa shindano la Epiq Bongo Star Search 2012, Walter Chilambo akizungumza na waandishi habari jijini Dar es Salaam. 
 Mshindi wa shindano la Epiq Bongo Star Search 2012, Walter Chilambo (katikati) akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa BenchMark Production Rita Poulsen na Ofisa Biashara Mkuu wa Zantel, Sajid Khan.
Mkurugenzi Mtendaji wa BenchMark Production Rita Poulsen akifafanua jambo wakati wa uzinduzi wa shindano la Epiq Bongo Star Search jijini Dar es Salaam leo.

DAR ES SALAAM, Tanzania
SHINDANO la Epiq Bongo Star Search linatarajia kuanza kutimua vumbi Juni 29 mwaka huu huku likiwashilikisha wadau wakubwa wa muziki hapa nchini kwa lengo la kuwajenga washiriki kwa kuwapa ujuzi zaidi utakaowasaidia kukua kimuziki.

Akizungumza katika makao makuu ya Kampuni ya simu za Mkononi ya Zantel ambao ni wadhamini wakuu wa shindano hilo, Mkurugenzi Mtendaji wa BenchMark Production Rita Poulsen alisema, shindano hilo linatarajiwa kufanyika usajili katika Mikoa Sita ambayo ni Mwanza, Mbeya, Arusha, Zanzibar, Dodoma na Dar es Salaam.

Rita alisema, Mwaka huu kauli mbiu ‘Kamua’ na kudai kuwa wamejipanga kuwafikia vijana wengi hapa nchini, na pia kutengeneza nyota wengi wa muziki mbali na mshindi na kudai kuwa wataanzia Mkoani Dodoma Juni 29-30, katika ukumbi wa Maisha klabu, Julai 5-6 Zanziba Hotel ya Bwawani, Mbeya Julai 10-11 Klabu Vybes, Mwanza Julai 14-15 Klabu Fassion, Arusha Julai 20-21 Tripple A na kumalizia Dar es Salaam Julai 26-28 uwanja wa Taifa.

Naye Ofisa Biashara Mkuu wa Zantel, Sajid Khan alisema, Zantel wanajivunia kufanya kitu kikubwa kama hiki ambacho kinawapatia vijana ajila, na kudai kuwa, wanatarajia kufungua laini ya kurekodi kwa simu kuanzia siku ya kwanza ya usaili Mikoani ambapo washiriki watapiga namba 0901551000 au kutuma neno Kamua kwenda 15530.

Epiq BSS, imekuwa ikiwatoa vijana katika hali ya umasiki na kuwapa ajili kama ilivyo kwa wasanii kama Kala Jeremaya ambaye anatikisa katika muziki wa Hiphop pamoja na Walter Chilambo aliyetwaa taji hilo mwaka jana.