Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Tuesday, December 3, 2013

RAIS KIKWETE AKIWA MGENI RASMI SHEREHE YA SIKU YA WATU WENYE ULEMAVU DUNIANI



 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokewa na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt Hussein Mwinyi alipowasili katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam leo Novemba 3, 2013 kuwa mgeni rasmi kwenye sherehe ya Siku ya Watu Wenye Ulemavu Duniani
 Makamu Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Watu Wenye Ulemavu (SHIVYAWATA) Bw. Amon Anastaz akisoma risala kwa kutumia braille katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam leo Novemba 3, 2013 kwenye sherehe ya Siku ya Watu Wenye Ulemavu Duniani
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipongeza baada ya kupokea risala toka kwa Makamu Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Watu Wenye Ulemavu (SHIRYAWATA) akisoma risala kwa kutumia Braille huku mkalimani wa lugha ya alama akifanya kazi hiyo (kulia) katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam leo Novemba 3, 2013 kuwa mgeni rasmi kwenye sherehe ya Siku ya Watu Wenye Ulemavu Duniani
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam leo Novemba 3, 2013 akiwa  mgeni rasmi kwenye sherehe ya Siku ya Watu Wenye Ulemavu Duniani
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mikono na  Makamu Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Watu Wenye Ulemavu (SHIRYAWATA) akiwa na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt Hussein Mwinyi pamoja na Mwenyekiti wa (SHIVWATA) baada ya kuhutubia  katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam leo Novemba 3, 2013 kwenye sherehe ya Siku ya Watu Wenye Ulemavu Duniani
Rais Jakaya Mrisho Kikwete  akitoa cheti kwa  Bw. Frederick Msigallah wa CCBRT katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam leo Novemba 3, 2013 kwenye sherehe ya Siku ya Watu Wenye Ulemavu Duniani

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpa cheti kwa niaba ya TBC Mtangazaji mahiri wa stesheni hiyo ya Taifa Bi. Amina Mollel  katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam leo Novemba 3, 2013 kwenye sherehe ya Siku ya Watu Wenye Ulemavu Duniani
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi hati mwakilishi na Mtangazaji wa ITV  katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam leo Novemba 3, 2013 kwenye sherehe ya Siku ya Watu Wenye Ulemavu Duniani

MAKINDA AONGOZA KIKAO CHA KAMATI YA UONGOZI KUPITIA RATIBA YA SHUGHULIZA BUNGELA LA MKUTANO WA 14 ULIOANZA LEO MJINI DODOMA



 Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akiongoza kikao cha Kamati ya Uongozi Bungeni Dodoma leo.Kamati hiyo imekaa kupitia ratiba ya shughuli zitakazokuwemo kwenye mkutano wa 14 wa Bunge ulioanza leo. Kushoto ni Katibu wa Bunge Dkt. Thomas Kashililah.
Wajumbe wa Management ya Bunge ambao ni Maafisa wa Bunge wakifuatilia kwa umakini kikao hicho cha kamati ya Uongozi. Picha na Owen Mwandumbya

NAIBU WAZIRI MHE. UMMY MWALIMU ASHIRIKI SEMINA YA WASANII KUADHIMISHA SIKU YA UKIMWI DUNIANI



P4-2

Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Ummy Mwalimu (kulia), akiteta jambo na Mwakilishi wa Bongo Movie, Devota Mbaga, wakati wa semina hiyo.P5Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Ummy Mwalimu, akichangia mada ya ‘Ukimwi na Vijana’, mara baada ya kuifungua semina ya wasanii katika kuadhimisha Siku ya Ukimwi duniani, iliyoandaliwa na Taasisi ya Benjamin William Mkapa HIV/AIDS Foundation kwa uratibu wa Kampuni ya Motage, Dar es Salaam jana. Wa pili  kulia ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa taasisi hiyo, Dk. Ellen Mkondya, Mwakilishi wa Bongo Movie, Devota Mbaga (kulia)  na msanii wa maigizo, Aisha Amani ‘Walonge’.
P6Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto,  Ummy Mwalimu (wa tatu kulia) na Ofisa Mtendaji Mkuu wa  Taasisi ya Benjamin William Mkapa, Dk. Ellen Mkondya (wa  pili kulia) pamoja na wasanii, Salama salmin ‘Sandra’  (kushoto), Aisha Amani ‘Walonge’ (wa pili kushoto) na  Mwakilishi wa Bongo Movie, Devota Mbaga, wakisikiliza  mada juu ya Ukimwi na Vijana, iliyokuwa ikiwasilishwa na mtaalamu huyo.
P8Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto,  Ummy Mwalimu na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya  Benjamin William Mkapa, Dk. Ellen Mkondya, wakiwa katika  picha ya pamoja na baadhi ya wasanii mbalimbali wakati wa  ufunguzi wa semina hiyo

RAIS WA ZANZNIBAR DKT. SHEIN AZUNGUMZA NA UONGOZI WA OFISI NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI



 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(kulia) akizungumza na Uongozi wa Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,katika kikao cha kujadili utekelezaji wa Mpango kazi wa Ofisi hiyo,wa mwaka wa fedha 2012-2013 na robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2013-2014,katika Ukumbi wa Mikutano Ikulu Mjini Zanzibar,(wa pili kulia)  Katibu Mkuu  Kiongozi Dk.Abdulhamid Yahaya Mzee.
 Baadhi ya Viongozi mbali mbali wa Ofisi ya Rais, na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,wakiwa katika cha kujadili utekelezaji wa Mpango kazi wa Ofisi  hiyo,wa mwaka wa fedha 2012-2013 na robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2013-2014,chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DK.Ali Mohamed Shein,(hayupo pichani) katika Ukumbi wa Mikutano Ikulu Mjini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,  (katikati) akizungumza na Uongozi wa Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,katika kikao cha kujadili utekelezaji wa Mpango kazi wa Ofisi hiyo,wa mwaka wa fedha 2012-2013 na robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2013-2014,katika Ukumbi wa Mikutano Ikulu Mjini Zanzibar. Picha na Ramadhan Othman Ikulu

DK MIGIRO APONGEZWA KUTEULIWA NA RAIS KUWA MBUNGE



 Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro akipongezwa na Katibu wa NEC-Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye kwa kuteuliwa na Rais Jakaya Kikwete kuwa Mbunge, jioni mjini Mbalizi, jijini Mbeya. Viongozi hao wamo kwenye ziara ya kuimarisha chama na kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa kuata Ilani ya Uchaguzi ya CCM.
Akizungumzia uteuzi huo, mjini Mbalizi jioni hii,

Dk. Migiro amemshukuru Rais Jakaya Kikwete kwa uteuzi huo ambao ameupokea kwa furaha, na kueleza kuwa kitendo hicho kinadhihirisha jinsi Rais Kikwete alivyo na imani naye pamoja na imani kwa Wanawake wa Tanzania





 Dk. Migiro (kulia), akipongezwa na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana kwa uteuzi wake huo.
 Dk. Migiro akizungumza na vyombo vya habari, jinsi alivyopokea kwa furaha uteuzi wake huo.
 Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro akimpongeza Dk. Migiro kwa kuteuliwa na Rais Kikwete kuwa Mbunge.PICHA NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG

Mnadhimu wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Tundu Lissu: Kambi ya Rasmi ya Upinzani Bungeni, itafanya mabadiliko makubwa katika Baraza lake Kivuli wakati wa Mkutano Mkuu wa 14 wa Bunge unaoanza leo mjini Dodoma.




Mnadhimu wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Tundu Lissu
-----
Kambi ya Rasmi ya Upinzani Bungeni, itafanya mabadiliko makubwa katika Baraza lake Kivuli wakati wa Mkutano Mkuu wa 14 wa Bunge unaoanza leo mjini Dodoma.

Panga pangua hiyo ambayo imesukumwa na kuvuliwa nyadhifa zote kwa aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chadema na Naibu Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Zitto Kabwe itawalenga pia mawaziri vivuli walioshindwa kutimiza majukumu yao kikamilifu.
Habari zilizopatikana jana mjini Dodoma zilisema Zitto ni mlengwa mkuu wa mabadiliko hayo ikiwa ni utekelezaji wa maazimio ya Kamati Kuu (CC) ya chama chake.
Kamati Kuu chini ya Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe iliagiza kuvuliwa nyadhifa zote, Zitto pamoja na Mjumbe wa Kamati Kuu, Dk Kitilla Mkumbo kwa kile kilichodaiwa ni kukisaliti chama.Kwa habari zaid

Monday, December 2, 2013

HAYA NDIYO MAMBO MANNE MUHIMU YA KUFANYA BAADA YA KUFANYA KAZI NGUMU YA TENDO LA NDOA KWA MWANAUME NA MWANAMKE.



man and woman wallpaper tattaat
NASHUKURU Mwenyezi Mungu kwa kunijaalia siha njema na pia kwa kunipa mwangaza wa kuandika hiki ninachokusudia.

Pia niwashukuru wapenzi wasomaji wa safu hii ambao tumekuwa tukiwasiliana na kushauriana hili na lile katika tasnia hii adhimu ya mapenzi. Nawakaribisha sana !.

Labda kwa wale wasiofahamu niwaambie tu kwamba dhana ya mapenzi ni dhana yenye wigo mpana sana na ndiyo maana hutasikia hata siku moja tumepumzika kuizungumzia.

Hata hivyo, tunachofanya siku zote ni kukumbushana kwa yale tunayoyafahamu na kushauriana kwa pale tunapohisi wengi hufanya makosa. 

Baada ya kusema hayo sasa nigeukie mada yangu ya leo ambayo kwa kiasi kikubwa inawahusu wale walio kwenye ndoa na kikubwa nazungumzia yale ambayo wawili waliotokea kupendana kwa dhati wanatakiwa kuyafanya mara baada ya kumaliza kufanya tendo la ndoa.


Nalazimika kuandika makala haya baada ya kubaini kuwa wengi wamekuwa wakifanya makosa na kujikuta wakishamaliza kufanya tendo hilo takatifu, kila mmoja anageukie kwake kisha kuuchapa usingizi.

Sisemi kwamba ni lazima kuyafanya haya nitakayoyaeleza leo ila yakifanywa huwa na manufaa yake na mara nyingi yanaboresha uhusiano.


Kuoga pamoja
Mtakuwa ni watu wa ajabu kama mtamaliza kufanya tendo hilo kisha kila mmoja kulala na majasho yake. Wapo wasiojali katika hili na kuona kuoga au kutooga ni uamuzi wa mtu. Elewa linapokuja suala la usafi inashauriwa mkimaliza lazima muoge.



Wapo wanawake ambao wakishamaliza hukimbilia kuwaandalia maji wenza wao, wakishaoga ndipo nawo huenda kuoga. Hivi unaona ugumu gani kwenda kuoga na mwenza wako? Unaijua raha ya kuoga na huyo wako wa maisha ?.


Wanaofanya hivyo wanajua raha yake na wewe ambaye hujawahi, anza leo. Mmemaliza mambo yenu, chukuaneni kimahaba, elekeeni bafuni kisha ogeshaneni kimahaba.


Baada ya hapo rudini chumbani, mkishajifuta maji pandeni kitandani mkiwa wapesi.


Kusifiana
Hakuna muda maalum uliotengwa kwa ajili ya wanandoa kusifiana. Hilo linaweza kufanyika wakati wowote lakini pale mnapomaliza kufanya tendo la ndoa ni lazima utakuwa na jambo zuri la kumuambia mwenza wako.


Msifie kwa utundu na ubunifu wake. Msifie pia kwa mapenzi matamu anayokupa na ikibidi mpe sifa ya uzuri wake kiasi cha kukufanya kila unapokuwa karibu yake ujisikie amani ya kupitiliza.


Wapo ambao hawana kabisa kasumba ya kuwasifia wala kuwashukuru wenza wao kwa mazuri wanayofanyiwa. Yaani wao wanachukulia kila kitu poa tu bila kujali kwamba kusifiana kunanogesha mambo.


Kuelekezana
Kwenye kale kamchezo, wapo ambao wanakosea, kuelekezana na kukosoana kwa wapenzi ni jambo la kawaida. Yawezekana mwenza wako alifanya kitu ambacho hakikukufurahisha wakati mkiendelea na burudani yenu, mnapomaliza mwambie lakini kwa lugha ya kimahaba na ya upole. Naamini kwa kufanya hivyo atakuelewa na kubadilika.


Zungumzieni maisha
Huu ni wakati muafaka wa kujadili changamoto na malengo katika maisha yenu. Hapa akili zinakuwa zimetulia na kila mmoja anakuwa na mawazo chanya kwa mwenza wake. Jadilini mambo yenu, wekeni mikakati ya kuliboresha penzi na maisha yenu kwa ujumla. 


Hayo ni baadhi ya mambo ambayo mnashauriwa kuyafanya pale mnapomaliza kufanya tendo la ndoa. 


Yapo mnayotakiwa kuyaepuka ili kutotibua furaha iliyopatikana. Hayo nitakuja kuyaeleza katika makala zinazokuja kupitia ukurasa huu.

KOCHA MPYA WA AZAM FC JOSEPH OMOG AKUTANA NA TIMU



 Kocha mpya wa Azam FC akiwa na msaidizi wake Kali Ongalla.
 .....Akizungumza na wachezaji...


KOCHA MPYA SIMBA AWASILI NA KUKAGUA UWANJA WA KINESI, APOKELEWA NA MASHABIKI KIBAO








KOCHA mpya wa Simba Zdravko Logarusic amewasili nchini majira ya 2:15 asubuhi na Kenya Airways jana huku akitoa ahadi kemkem kwa mashabiki wa klabu hiyo yenye makao makuu mtaa wa Msimbazi jijini Dar es Salaam.

Logarusic raia wa Croatia ambaye awali alikuwa anaifundisha Gor Mahia ya Kenya na kuisaidia kuchukua Ubingwa baada ya ukame wa miaka 18 amesema yeye falsafa yake ni  ya kucheza mpira wa kushambulia haraka wakitokea nyuma (Counter attack) kwani ndio wenye kuleta matokeo mazuri.

Akizungumza baada ya kuwasili Logarusic ambaye anatarajia kusaini mkataba wa miezi sita leo amesema kuwa hatafanya mabadiliko ya wachezaji katika kikosi hicho zaidi ya kuhakikisha Simba inachukua ubingwa kama alivyofanya kwa Gor Mahia.

“Mimi kazi yangu ni kujenga timu ili icheze mchezo wa ushindani wenye kuonekana bayana hasa kufanya mashambulizi  ya haraka kwani nategemea Simba itabadilika na kutwaa ubingwa ili icheze kombe la mabingwa barani Afrika”, alijigamba Logarusic kocha nayeonekana kuwa muongeaji sana.

Kocha huyo amefikia Rombo View hotel iliyoko Shekilango, Urafiki  ambako amefikia golikipa Yaw Berko aliyesajiliwa na Simba kwa mkataba wa miezi sita kuitumikia Simba katika mzunguko wa pili wa ligi Kuu Tanzania bara.

Mara baada ya kufika hotelini na kupewa chumba na kupata kifungua kinywa alikwenda moja kwa moja kukagua uwanja wa Kinesi ambao unatumiwa na Simba kufanyia mazoezi na kuridhika nao japo alionekana kutaka kupata uwanja mwingine ambao anautumia anapokaribia kuwa na mechi.
Pia ametoa mapendekezo ya kupata mechi ya kirafiki kila wiki ili aweze kujenga timu yake katika ushindani wakati wote.
Kocha huyo alipokelewa na wajumbe watatu wa kamati ya Utendaji wa klabu ya Simba wakiongozwa na Saleh Pamba, Swedy Nkwabi na Damian Manembe na mashabiki waliokuwa kwenye Coaster tatu.

Logarusic amewahi kuzifundisha timu za King Faisal Babies FC Kumasi toka mwaka 2009/2010 na  Ashanti Gold SC toka 2010 hadi 2012 zote za nchini  Ghana na baadae alichukuliwa na Gor Mahia ya Kenya toka  Aprili 2012 hadi Novemba 2013.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AKUTANA NA KATIBU MTENDAJI WA SADC DKT. STAGOMENA TAX IKULU DAR ES SALAAM LEO



 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkaribisha Katibu Mtendaji wa SADC, Dkt. Stagomena Tax, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo kwa mazungumzo
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika mazungumzo na Katibu Mtendaji wa DADC, Dkt. Stagomena Tax, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, kwa mazungumzo leo, Dec 2, 2013
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika mazungumzo na Katibu Mtendaji wa DADC, Dkt. Stagomena Tax, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, kwa mazungumzo leo, Dec 2, 2013. Kushoto ni Ofisa Mawasiliano, Charles Mubita. Picha na OMR

Watanzania wanaonunua Bidhaa halisi waendelea kupongezwa katika Promosheni ya Pambika na Samsung



Mratibu wa promosheni ya Pambika na Samsung Bw. Lawrence Andrew akiongea na mmoja ya washindi wa promosheni ya Pambika na Samsung wakati wa kuchezesha droo ya tatu ya Pambika na Samsung. Washindi 15 walipataikana katika droo hiyo ambapo baadhi ya washindi walikuwa ni Issa Richard Moshi (23), wa Kilimanjaro aliyejishindia deki ya DVD, Agnes John Mkalango (30) wa Mwanza, Adagoti Komba (57) wa Dodoma, Faustine Kirusya (45) mkazi wa Mbeya ambae ni askari polisi pamoja na Praygod Amos (39) wa Arusha wote wameshinda Muziki wa Nyumbani. Kushoto ni Msimamizi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Bw. Humudi Abdulhussein.
 Mratibu wa promosheni ya Pambika na Samsung Bw. Lawrence Andrew akijadiliana jambo na Msimamizi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Bw. Humudi Abdulhussein Wakati wa kuchezesha droo ya tatu ya Pambika na Samsung mapema hii leo. Zawadi kubwa kabisa ya wiki hii ilikuwa ni Jokofu lenye dhamana ya miaka 10 ambapo mshindi wake ni Bi.  Bernadeta Peter mkazi wa Dar es Salaam huku Bi. Anthonia Julius Masele (45) ambae amejinyakulia luninga ya LED ya Samsung ya inchi 32 wa Dodoma. Hamad Abdallah Hemedi wa Dar es Salaam ambae amejinyakulia kompyuta mpakato.
Kutoka kulia ni Bw. Humudi Abdulhussein toka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, katikati ni Mratibu wa promosheni ya Pambika na Samsung Bw. Lawrence Andrew na Chacha Magege wakifuatilia droo kwa makini wakati wa kuchezesha droo ya Pambika na Samsung.

COASTAL UNION ULIVYOIGAGADUA YANGA NA KUTWAA UBINGWA WA UHAI CUP







RAIS wa Shirikisho la Soka nchini (TFF) Jamal Malinzi amesema watakaa na wadhamini wa mashindano ya Uhai ili yachezwe kwa mfumo wa ligi, sambamba na ligi Kuu ya Tanzania Bara
Malinzi aliyasema hayo juzi wakati akifunga fainali za mashindano ya kombe la Uhai zilizofanyika katika Uwanja wa Chamazi ulionje ya jijini la Dar es Salaam.

“Tunawapongeza Uhai kwa kufadhili mashindano haya ambayo yanalengo la kuibua vipaji ila shirikisho litakwenda kuzungumza nao ili mashindano haya yachezwe kwa mfumo wa ligi sambamba na ligi kuu ya Tanzania ili kutoa wigo mpana kwa vijana kuonyesha uwezo wao”, alisema Malinzi.

Pia alisema mfumo wa sasa wa makundi unazikosesha fursa timu zingine kuendelea mbele kwani inawezekana kabisa kama mchezo wa kwanza timu inafungwa mchezo wa pili inafanya vizuri.

Katika fainali hizo timu ya Coastal Union ilitwaa ubingwa kwa kuifunga Yanga mabao 2-0 na kuzawadiwa kikombe na fedha taslimu 2, 500, 0000 huku Yanga wakiambulia 1,500,000.
Pia Azam Fc ilichukua nafasi tatu na kuzawadiwa 1,000,000 baada ya kuifunga Mtibwa Sugar penati 4 kwa 3 baada ya kutoka sare ya mabao 3-3 katika muda wa dakika 120.


Kocha wa Mtibwa Sugar, Zuberi Katwila alipata zawadi ya kocha bora huku Ally Kabunda wa Ashanti United akipata zawadi ya mfungaji bora baada ya kufunga mabao 9 na Ruvu Shooting ikipewa zawadi ya timu bora.

KINANA NA UJUMBE WAKE WAWASILI WILAYANI MBARALI LEO,KUIMARISHA UHAI WA CHAMA MKOANI MBEYA.



 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Ujumbe wake wakisalimiana wananchi na wanachama wa CCM wakati wa mapokezi Igawa, alipoanza ziara ya kuimarisha uhai wa chama katika Wilaya ya Mbarali, mkoani Mbeya asubuhi leo.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akisalimiana na wafuasi wa CCM wakati wa mapokezi Igawa, alipoanza ziara ya kuimarisha uhai wa chama katika Wilaya ya Mbarali, mkoani Mbeya asubuhi leo.
 Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye (kushoto) akiwasalimia wananchi wakati wa mapokezi, eneo la Igawa, wilyani Mbarali, Mbeya.
 Kinana akikata utepe kuzindua jengo la ofisi za CCM Tawi la Ihanga, wilayani Mbarali leo.
Jengo jipya la CCM Tawi la Ihanga, wilayani Mbarali
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Ujumbe  wake wakizungumza na Wajumbe wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali, mkoani Mbeya asubuhi leo.

Sunday, December 1, 2013

MASHINDANO YA TANZANIA BOXING AWARDS YAZINDULIWA KWA WANAMASUMBWI KUZIPIGA MWENGE





Bondia John Christian kushoto akipambana na Gervas Rogasiano wakati wa uzinduzi wa tunzo za Tanzania Boxing Awards  iliyofanyika katika kituo cha mabasi ya mwenge Dar es salaam Christian  alishinda kwa pointi mpambano huo, wananchi watatakiwa kupiga kula kwa mabondia waliochaguliwa kugombea tunzo hizo kilele chake kitakuwa desemba 28 ambapo washindi watatangazwa  Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Baadhi ya viongozi na waau wa mchezo wa masumbwi wakifatilia mashinano hayo ya ngumi kwa ajili ya kuhamasisha tuzo za Boxing AWARD zitakazofikia kirere Desemba 28 mwaka huu wa 2013
Mabondia wa uzito wa juu Kulwa Makenzi kushoto akipambana na Haruna Swanga wakati wa mashindano ya wazi ya kutangaza tuzo za Tanzania Boxing Awards ambazo kilele chake kitakuwa Desemba 28 Swanga alishinda kwa pointi mpambano huo Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Bondia Hamad Furahisha kushoto akimsukumiza konde la kulia George Costantino wakati wa uzindunzi  wa Tuzo za Tanzania Boxing Awards iliyofanyika katika kituo cha mabasi mwende Dar es salaam Furahisha alishinda kwa point mpambano huo Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com



Matangazo ya kuamasisha tuzo za ngumi

mmoja ya wadau wa mchezo wa masumbwi akibandika tanzazo la kuhamasisha masumbwi

Bondia Haruna Swanga akipiga picha kwenye bango

Bondia John Christian kushoto akipambana na Gervas Rogasiano wakati wa uzinduzi wa tunzo za Tanzania Boxing Awards  iliyofanyika katika kituo cha mabasi ya mwenge Dar es salaam Christian  alishinda kwa pointi mpambano huo  wananchi watatakiwa kupiga kula kwa mabondia waliochaguliwa kugombea tunzo hizo kilele chake kitakuwa desemba 28 ambapo washindi watatangazwa  Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Bondia John Christian kushoto akitupa ngumi ya kulia wakati wa mpambano wake  na Gervas Rogasiano wakati wa uzinduzi wa tunzo za Tanzania Boxing Awards  iliyofanyika katika kituo cha mabasi ya mwenge Dar es salaam Christian  alishinda kwa pointi mpambano huo  wananchi watatakiwa kupiga kula kwa mabondia waliochaguliwa kugombea tunzo hizo kilele chake kitakuwa desemba 28 ambapo washindi watatangazwa  Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com