Mratibu
wa promosheni ya Pambika na Samsung Bw. Lawrence Andrew akiongea na
mmoja ya washindi wa promosheni ya Pambika na Samsung wakati wa
kuchezesha droo ya tatu ya Pambika na Samsung. Washindi 15 walipataikana
katika droo hiyo ambapo baadhi ya washindi walikuwa ni Issa Richard
Moshi (23), wa Kilimanjaro aliyejishindia deki ya DVD, Agnes John
Mkalango (30) wa Mwanza, Adagoti Komba (57) wa Dodoma, Faustine Kirusya
(45) mkazi wa Mbeya ambae ni askari polisi pamoja na Praygod Amos (39)
wa Arusha wote wameshinda Muziki wa Nyumbani. Kushoto ni Msimamizi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Bw. Humudi Abdulhussein.
Mratibu wa promosheni ya Pambika na Samsung Bw. Lawrence Andrew akijadiliana jambo na Msimamizi
kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Bw. Humudi Abdulhussein Wakati wa
kuchezesha droo ya tatu ya Pambika na Samsung mapema hii leo. Zawadi
kubwa kabisa ya wiki hii ilikuwa ni Jokofu lenye dhamana ya miaka 10
ambapo mshindi wake ni Bi. Bernadeta Peter mkazi wa Dar es Salaam huku
Bi. Anthonia Julius Masele (45) ambae amejinyakulia luninga ya LED ya
Samsung ya inchi 32 wa Dodoma. Hamad Abdallah Hemedi wa Dar es Salaam
ambae amejinyakulia kompyuta mpakato.
Kutoka kulia ni Bw. Humudi Abdulhussein toka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, katikati ni Mratibu
wa promosheni ya Pambika na Samsung Bw. Lawrence Andrew na Chacha
Magege wakifuatilia droo kwa makini wakati wa kuchezesha droo ya Pambika
na Samsung.
No comments :
Post a Comment