Mkuu
wa Kitengo cha Affluent Banking wa benki ya Barclays Tanzania Ms Neema
Rwehumbiza akiongea na waandishi wa habari waliofika katika ofisi za
Benki hiyo katika tawi lililopo Alpha House barabara ya Ali hassan
Mwinyi kwaajili ya kushuhudia washindi wa Droo ya Pili ya "Double your
Saving"kutoka benki ya Barclays.
Mmoja
wa Wafanyakazi wa Benki ya Barclays tawi la Alpha house Barabara ya Ali
Hassan Mwinyi akizungusha pipa lenye kuponi za washiriki wa droo ya
pili ya "Double Your Saving" kwaajili ya kupata washindi wa tano wa
Mwezi November, huku akiongozwa na afisa kutoka Bodi ya Michezo ya
Kubahatisha
Mkuu
wa Kitengo cha Affluent Banking wa benki ya Barclays Tanzania Ms Neema
Rwehumbiza akisoma jina la Mshindi wa Kwanza aliyepatikana mara baada ya
pipa hilo kuzungushwa katika droo ya pili ya "Double your saving'
kutoka Benki ya Barclays Tanzania iliyochezeshwa leo katika Ofisi ya
Benki hiyo katika tawi lililopo barabara ya Ali Hassani Mwinyi
Mmoja
wa Wafanyakazi wa Benki ya Barclays tawi la Alpha house Barabara ya Ali
Hassan Mwinyi akichukua moja ya kuponi za washiriki wa droo ya pili ya
"Double your Saving" kwaajili ya kumtaja mshindi wa Pili katika droo
iliyochezeshwa leo na Kupelekea kupatikana kwa washindi watano ambao
kila Mmoja ataondoka na Kitita Cha shilingi Milioni Moja
.................................
5
Disemba 2013 , Baclays Bank Tanzania leo imefanya droo yake ya Pili kwa
wateja wake katika kampeni ijulikanayo kama "Double Your Saving".
Kampeni hii ilianza rasmi tarehe 16 septemba 2013 na itaendelea hadi
tarehe 16 Januari 2014.
Kila
Mwezi, droo hii itawapatia wateja watano nafasi ya kujishindia hadi
shilingi milioni moja za kitanzania kila mmoja kwa kipindi chote cha
kampeni. Droo za mwezi, zitakuwa zinafanyika wiki ya mwisho ya mwezi
husika.
Akiongea
na waandishi wa habari Mkuu wa Kitengo Cha Affluent cha Benki ya
Baclays Ms Neema Rwehumbiza amesema; "Ushiriki upo wazi kwa wateja wote
binafsi(waliopo na wapya) kupitia akaunti zao za akiba na za hundi.
Wanachotakiw
kufanya ni kuongeza na kutunza akiba zao kwa kiwango cha Shilingi laki
tatu (300,000) za kitanzania au zaidi. Kiwango hiko kitampa mteja nafasi
ya kushiriki katika droo ya mwezo husika tu. Baada ya kuongeza akiba
kwa kiwango husika, mteja ataingia kwenye droo ya mwezi na kupata nafasi
ya kujishindia hadi shilingi milioni moja za Kitanzania. Kila ongezeko
la shilingi laki tatu litampatia mteja nafasi moja ya kushiriki.
Wateja
wote watakaoongeza salio kwenye akaunti zao kwa shilingi laki tatu au
zaidi katika kipindi hiki cha kampeni wanajipatia nafasi ya kushinda
zawadi kubwa kabisa ya shilingi za kitanzania Milioni Thelathini
(30,000,000) mwishoni mwa kampeni hii.
Aliongeza
kuwa, "hii ni droo ya pili ambao tunapata washindi wengone watano.
Baclays inawapongeza washindi wote na kuhamasisha watanzania wote
kushiriki katika kampeni hii hususani katika kipindi hiki cha sikukuu za
mwisho wa Mwaka
No comments :
Post a Comment