Mwenyekiti
wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora nchini Tanzania (THBUB),
Jaji Mstaafu Amir Manento akizungumza na waandishi wa habari wakati
mdahalo wa Siku ya Kimataifa ya Haki za Binadamu kuelekea maadhimisho ya
siku hiyo ambayo hufanyika tarehe 10 mwezi Disemba kila mwaka.
.Jaji Manento asema ni uvunjifu wa sheria kwenda na watoto harusini
Na Damas Makangale, MOblog
WAZAZI
na Walezi wameaswa kuacha mara moja tabia ya kwenda na watoto katika
sherehe na harusi mbalimbali za kwa sababu ni kosa la Jinai kwa mujibu
wa sheria na Haki za Mtoto. MOblog inaripoti.
Akizungumza
kwenye mdahalo wa Siku ya Kimataifa ya Haki za Binadamu ambao
huadhimisha kila tarehe 10 mwezi Disemba kila mwaka, Mwenyekiti wa Tume
ya Haki za Binadamu na Utawala Bora nchini Tanzania, Jaji Mstaafu Amir
Manento amesema kwa mujibu wa sheria na Haki za Mtoto wazazi au walezi
hawaruhusi kwenda na watoto katika sherehe za usiku.
“wazazi
na walezi na watu wa kawaida wanamazoea ya kwenda na watoto kwenye
sherehe za harusi na majumba ya starehe lakini kwa mujibu wa sheria na
haki za mtoto na marekebisho yake ya 2009 ni uvunjifu wa sheria na haki
za mtoto,” amesema Jaji Manento.
Meza
Kuu kati kati ni msimamizi (moderator) Dkt Khoti Kamanga toka UDSM,
kushoto kwake ni Bw, Godfrey Mulisa toka UN, kushoto mwisho ni
Mwakilishi Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) Bw, Harold
Sungusia na kulia kwa msimamizi ni Francis Nzuki kutoka Tume ya Sheria
na Haki za Binadamu na Utawala Bora na mwisho kulia ni Bi, Felistas
Mushi toka Wizara ya Sheria na Katiba.
Amesema
kuwa Tanzania iliridhia tamko rasmi la Haki za Binadamu ili pamoja na
mambo mengine kulinda Uhuru na Haki za Binadamu pamoja na haki ya
kuishi.
“Tarehe
10 Disemba imeainishwa kuwa Siku ya Kimataifa ya Haki za Binadamu.
Kuainishwa siku ya Kimataifa ya Haki za binadamu kunakumbusha juhudi
kubwa zilizofanywa kwa lengo la kuwafanya watu waheshimu Haki za
Binadamu kote duniani,” alisisitiza.
Jaji
Manento amesema suala la kuheshimiwa haki za binadamu lilipewa
kipaumbele cha kwanza wakati wawakilishi wa nchi mbalimbali walipokuwa
wakibuni Hati ya Umoja wa Mataifa.
Aliongeza
kuwa Januari mwaka 1947 iliundwa kamati ya haki za binadamu na hati ya
kamisheni hiyo ilipasishwa katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa tarehe
10 Disemba 1948.
Jaji
manento amesema kuwa kwa msingi huo siku hiyo ya tarehe 10 Disemba
ilitambuliwa kuwa ni Siku ya Kimataifa ya Haki za Binadamu duniani kote.
Mwakilishi
kutoka Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Bw. Harold Sungusia
akiwasilisha mada yake kuhusu historia na chimbuko la Haki za Binadamu
katika bara la Afrika tangu enzi za miaka 1200 kwenye nchi ya Mali (Mali
Empire).
Amesema
kuwa imepita zaidi ya miongo sita sasa tangu kutolewa Azimio la Haki za
Binadamu ambalo linakusanya thamani za pamoja kwa ajili ya kuondoa
ubaguzi, kueneza uhuru na kupambana na dhuluma dhidi ya binadamu
duniani.
Alilisitiza
kwamba hapana shaka kuwa kutetea haki za binadamu kwa ajili ya kutimiza
lengo hilo ni kazi yenye thamani kubwa. Hata hivyo aliongeza kadhia
hiyo inayumbishwa na nchi za Magharibi ambazo zinatumia haki za binadamu
na ripoti zinazotolewa na taasisi za haki za binadamu kama nyenzo na
fimbo ya kisiasa kwa baadhi ya nchi zinazoendelea.
Kauli
mbiu ya Siku ya Kimataifa ya Haki za Binadamu ni “mafanikio na
changamoto katika kuhamasisha na kulinda Haki za Binadamu Tanzania” .
Juu na chini ni Baadhi ya vijana wa shule za sekondari mbalimbali na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
Mjumbe
kutoka Tume ya Sheria na Haki za Binadamu na Utawala bora Bw, Francis
Nzuki (wa pili kulia) akizungumzia uzoefu wake katika kuhamasisha Haki
za binadamu katika Magereza nchini Tanzania hasa kwa Wafungwa.
Mwakilishi
kutoka Wizara ya Sheria na Katiba, Bi.Felistas Mushi akiwasilisha mada
kuhusu kwanini kuna mpango mkakati wa serikali katika kutekeleza Haki za
Binadamu nchini Tanzania.
Mtaalamu
wa mambo ya Utawala bora , Grainne Kilcullen kutoka UNDP akiwahamasisha
vijana waliohudhuria mdahalo huo kuwa mstari wa mbele katika kusimamia
Haki za Binadamu na kuwaelimisha jamii inayowazunguka kuzitambua Haki
zao za msingi.
Mwenyekiti
wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora nchini Tanzania, Jaji
Mstaafu Amir Manento (wa pili kushoto), Mkurugenzi wa Huduma za sheria
wa Tume ya Sheria na Haki za Binadamu na Utawala bora, Bw. Nabor Assey (
wa pili lulia), Mtaalamu wa mambo ya Utawala bora , Grainne Kilcullen
kutoka UNDP na Afisa Habari wa Kitengo cha Umoja wa Mataifa cha Habari
(UNIC), Bi. Usia Nkhoma Ledama wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa
zikizungumziwa kwenye mdahalo huo.
Pichani
Juu na chini ni baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
wakitoa maoni na kuchangia mada mbalimbali zilizokuwa zikijadiliwa
kwenye mdahalo huo.
No comments :
Post a Comment