Watalii wakipiga picha katika
wanyama katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti mkoani Mara leo kama
walivyokutwa na wanahabari kutoka mkoa wa Iringa
Mhifadhi mkuu wa hifadhi ya Taifa ya
Serengeti mkoani Mara Bw Wiliam Mwakilema akizungumza na
wanahabari wa mkoa wa Iringa ambao wametembelea hifadhi hiyo leoIMEELEZWA kuwa siasa za vurugu vinazoendeshwa na baadhi ya vyama vya siasa katika mikoa ya kaskazin zimeendelea kushusha idadi ya watalii katika hifadhi za kaskazin.
Kauli hiyo imetolewa leo na mhifadhi mkuu wa hifadhi ya Serengeti mkoani mara Bw Wiliam Mwakilema wakati akizungumza na timu ya wanahabari 16 kutoka mkoa wa Iringa ambao wametembelea hifadhi ya Taifa ya Serengeti kwa ajili ya kujifunza na kutangaza zaidi vivutio vya utalii
Mwakilema alisema kuwa moja kati ya mambo yanayokwamisha watalii kufika katika hifadhi ni pamoja na wanasiasa kuendesha siasa za vurugu ambazo zinawatisha watalii hao ambao wengi wanapenda maeneo yasiyo ya vurugu kwa ajili ya kutembelea.
Bila kuvitaja vyama ama wanasiasa wanaofanya siasa za vurugu Mwakilema aliwataka wanahabari na vyombo vya habari nchini kuendelea kutoa elimu zaidi kwa vyama vya siasa na wanasiasa ili kuepuka kuendesha siasa za vurugu.
Wakati huo huo Mwakilema alikanusha upotoshwaji unaofanywa na nchi ya Kenya juu ya wanyama aina ya Nyumbu kuwa ni wanyama ambao wanapatikana kenya na kuwa wanyama hao si raia wa Kenya ni wanyama wenye uraia wa Tanzania ambao Kenya wamekuwa wakifika kwa msimu kwa ajili ya malisho na baada ya hapo huzaliana katika hifadhi hiyo ya Serengeti .
No comments :
Post a Comment