Naibu Waziri wa Kazi na Ajira Mhe,Makongoro Mahanga akitoa hotuba yake. HABARI PICHA NA PHILEMON SOLOMON WA FULLSHANGWE DAR ES SALAAM
SERIKALI
imezindua mfumo maalumu wa kielektroniki wa taarifa za soko la ajira,
ambao utamuwezesha mtafuta kazi kufahamu nafasi mbalimbali za kazi
zinazotangazwa ndani na nje ya nchi.
Mtandao
huo ambao umeelezwa kuwa utakuwa msaada mkubwa hususani kwa vijana,
utamuwezesha muomba kazi kuomba nafasi hizo moja kwa moja katika
makampuni husika kulingana na vigezo vitakavyokuwa vikihitajika.
Akizundua
mtandao pamoja na maonyesho ya shughuli za huduma za ajira jana jijini
Dar es Salaam, Naibu Waziri wa Kazi na Ajira Makongoro Mahanga alisema,
mbali na kutangaza nafasi za ajira pia mfumo huo utawawezesha watu wenye
nia ya kuwekeza hapa nchini kutambua aina ya ujuzi unaopatikana nchini
na kuwarahisishia katika kuajiri.
“Hii
itapunguza waajiri kuajiri wageni zaidi katika zile nafasi ambazo zina
wataalumu nchini kutokana na kufahamu mapema. Pia kwa wanafunzi wqa vyuo
vikuu watafahamu mapema ujuzi na taalumu wanazopaswa kusoma kwa kuwa
utatoa taarifa zitakazowezesha mtu kujua mahitaji ya sasa na ya siku za
usoni katika soko la ajira,” aliongeza.
Kwa
upande wa waajiri mfumo huo utawawezesha kutangaza nafasi za kazi
walizonazo ikiwa ni pamoja na sifa za mtafuta kazi wanayemhitaji.
“Wataweza kupata wafanyakazi wenye viwango wanavyovitaka kwa urahisi kwa kujiunga na mtandao huu,” alisema.
Alisema
hatua ya mtandao huo utasaidia kupunguza ukosefu vwa ajira kwa vijana
kwani kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2006 tatizo la ukosefu wa ajira kwa
vijana lilikuwa kwa asilimia 13.4 hivyo ni matarajio kiwango hicho
kitapungua baada ya waajiri wengi kutangaza ajira kupitia mtandao huo.
Mahanga
ametoa wito kwa waajiri wote nchini kutumia mfumo huo kutangaza ajira
na watafuta kazi na kuutumia kupata taarifa sahihi ili kuweza kuomba
nafasi hizo.
Mtandao huo ambao umezinduliwa ni www.ajiralmis.go.tz, vijana wametakiwa kuutumia kwa usahihi zaidi ili kunufaika na ajira zinazotangazwa
Huu ndio mtandao uliozinduliwa.
Wanafunzi
na wahitimu wa vyuo mbalimbali wakiwa kwenye kongamano la siku mbili
jinsi ya kuandika barua ya maombi ya kazi katika ukumbi wa Mw. Julius
Kambarage Nyerere jijin dar es Salaam. Naibu
Waziri wa Kazi na Ajira Mhe Makongoro Mahanga, akimsikiliza Kaimu
Mtendaji Mkuu wakala wa Huduma za Ajira Tanzania (TaEsA), Boniface Chandaruba wakati akielezea kazi wanazofanya kuhusiana na ajira kwa vija mara baada ya kutembelea banda hilo, Wafanyakazi wakala wa Huduma za Ajira Tanzania (TaEsA), wakiwa kwenye picha ya pamoja katika kongamano
la siku mbili jinsi ya kuandika barua ya maombi ya kazi katika
ukumbi wa Mw. Julius Kambarage Nyerere jijin dar es Salaam.
No comments :
Post a Comment