Mabasi ya mwendo kasi 2014 kimara kivukoni. Picha kwa hisani ya Deo Mutta Mwanatanga |
Mtendaji
mkuu wakala wa mradi wa mabasi yaendayo kasi Bi Asteria lambo amesema
basi hilo ni miongoni mwa mabasi madogo yatakayoingia nchini yenye uwezo
wa kubeba zaidi ya abiria 40 na makubwa yatabeba abiria zaidi ya 150 na
kuwataka wakazi wa jiji la Dar es Salaam kuendelea kuwa na subira na
kuwahakikishia mradi huo sio ndoto na adha ya usafiri itapungua mapema
mwaka kesho.
Nao
baadhi ya wakazi wa jiji walioshuhudia gari hilo wameelezea kufurahishwa
na kuanza kuwa na imani na serikali yao ambapo wamesema kama mradi huo
utakamilika kwa muda uliopangwa utakuwa faraja sana kutokana na adha
kubwa ya usafiri wanayokumbana nayo huku wakitoa wito kwa mamlaka
husika kupanga mikakati ya kupunguza nauli za mabasi hayo pindi
yatakapoanza kufanya safari zao.
No comments :
Post a Comment