Mnadhimu wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Tundu Lissu
-----
Kambi ya Rasmi ya Upinzani Bungeni, itafanya
mabadiliko makubwa katika Baraza lake Kivuli wakati wa Mkutano Mkuu wa
14 wa Bunge unaoanza leo mjini Dodoma.
Panga pangua hiyo ambayo imesukumwa na kuvuliwa
nyadhifa zote kwa aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chadema na Naibu
Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Zitto Kabwe itawalenga pia
mawaziri vivuli walioshindwa kutimiza majukumu yao kikamilifu.
Habari zilizopatikana jana mjini Dodoma zilisema
Zitto ni mlengwa mkuu wa mabadiliko hayo ikiwa ni utekelezaji wa
maazimio ya Kamati Kuu (CC) ya chama chake.
Kamati Kuu chini ya Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe
iliagiza kuvuliwa nyadhifa zote, Zitto pamoja na Mjumbe wa Kamati Kuu,
Dk Kitilla Mkumbo kwa kile kilichodaiwa ni kukisaliti chama.Kwa habari zaid
No comments :
Post a Comment