Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Friday, March 25, 2011

HITMA YA KUWAREHEMU WANAMUZIKI WA 5 STARS YAFANYIKA, SERIKALI KUSAIDIA KUPATIKANA WA KUZIBA PENGO


WANAZUONI WAKIENDELEA NA KISOMO
KUSHOTO NI MMOJA YA WASANII WA KUNDI LA 5 STAR WALIONUSURIKA ALI J PAMOJA NA MWENYEKITI WA SHIWATA KASIM TALIB NA KULIA NI KATIBU MTENDAJI WA BASATA GHONCHE MATERAGO
NAIBU WAZIRI WA HABARI VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO DK.FENELA MUKANGARA KULIA NA KULIA NA KUSHOTO NI MKURUGENZI MSAIDIZI WA UTAMADUNI ANGELA NGOWI.



DAKIKA MOJA KUSIMAMA NA KUOMBEA MAREHEMU

SERIKALI imetoa tamko la kusaidia kupatikana kwa wanamuziki wengine watakaounda kundi la taarabu la Five Stars Modern Taarab baada ya wanamuziki 13 wa kundi hilo kupoteza maisha katika ajali iliyotokea hivi karibuni mkoani Morogoro.

Akizungumza katika dua ya kuwaombea wanamuziki hao jioni ya leo katika hoteli ya Starlight, Naibu Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo Dr Fenela Mukangara alisema vijana wasikate tamaa baada ya vijana hao kupoteza maisha katika ajali hiyo.

Mukangara alisema serikali katika jitihada za kufanikisha azma hiyo watajitahidi kuwasiliana na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kuzipiga nyimbo za kundi hilo na kusaidia kuuza kazi zilizofanywa na kundi hilo.

Aidha Mukangara alisema Serikali itaendelea kuwapa ushirikiano kwa muda wote viongozi na familia za marehemu waliokumbwa na msiba huo hapa nchini.

Mukangara alisema watajipanga kuwasaidia vyombo kundi hilo kwa kushirikiana na wadau wa muziki hapa nchini baada ya kundi hilo kupoteza pia vyombo vyake katika ajali hiyo.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Henry Clemence alitoa wito kwa wasanii kutunga tungo za kupigia kelele madereva wazembe kwa sababu ajali ndio mojawapo ya matukio yanayomaliza Watanzania wengi.
Clemence ambaye pia ni Mwenyeji wa wanachama wa Taasisi ya Wasanii Tanzania (SHIWATA), Wilayani Mkuranga alisema pengo la wanamuziki hao halitozibika.
Mwenyekiti wa Shiwata, Taalib Cassim alitoa shukrani kwa viongozi wa Serikali kwa kuonyesha kuwajali wasanii ambako Asilimia kubwa ya viongozi wa serikali kupitia Wizara kuhudhuria katika dua ya kuwaombea marehemu walifariki katika ajali hiyo.
Cassim alisema Shiwata inawapenda viongozi wa Serikali kwa kuonyesha kuguswa na tukio hilo ambalo limetingisha Taifa.
Viongozi waliohudhuria katika dua hiyo ni pamoja na Mkurugenzi wa Utamaduni, Profesa Hermas Mwansoko, Msaidizi wake Anjela Ngowi, Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Ghonche Materego na wadau mbalimbali wa sanaa.

Tuesday, March 22, 2011

PATA NAKALA YAKO YA DAR LEO UPATE HABARI ZAIDI JUU YA FIFO VYA WANAMZIKI WA FIVE STARS


GAZETI LA DAR LEO LIKIWA NA MUONEKANO UPANDE WA MBELE DATE 22/3/2011 JUMANNE

airtel Hands over books to four Dar Schools

Beatrice Singano (left), Airtel Tanzania’s Head of Corporate Communications, handling over books to teaching staffs representatives of Yusuf Makamba Secondary School. Airtel Tanzania today handed over books worth over Tshs 4 Million Shillings as aid to four Dar es Salaam based secondary schools, as part of the company’s corporate social responsibility.


Airtel Tanzania, the mostly available and affordable mobile service provider in the country, today handed over books worth over Tshs four Million as aid to Dar es Salaam based secondary schools, as part of the company’s corporate social responsibility.

The benefiting schools are Barabara ya Mwinyi and Aboud Jumbe secondary schools in Temeke district and Yusufu Makamba and Turiani secondary schools in Kinondoni district.

Speaking during the books handover event at Airtel Head offices in Dar es Salaam, the company’s Corporate Social Responsibility Manager, Tunu Kavishe, said the four schools are amongst 104 schools across the country that will benefit from the unique airtel books project, following a random draw that was held early this year, involving 520 secondary schools.

“We are giving an equal opportunity to schools from all regions in the country to ensure that the books reach students from every part of the country. We have spent 104 million Shillings on buying these books so as to enable each school to get books worth one million Tanzanian shillings”, said Ms. Kavishe.

She further added that each benefiting institution had a unique opportunity to choose their ideal book requirements based on their curriculum and subjects offered at the institution. This will enable Airtel to procure and handover sets of books that adequately meet the need of each school.

“We are highly committed towards supporting communities in Tanzania by improving education levels through availing the most important tools - books - to secondary schools students. Since we started our books support programme, approximately seven years ago, we have reached more than 800 secondary schools that are spread across the country”, said Ms. Kavishe.

Apart from the 104 secondary schools benefiting from books aid, Airtel Tanzania has already adopted a rural primary school in Bagamory District – Coast Region, being a pilot project. The company has completed major refurbishment of existing structures and construction of 10 new ones.

It is expected that after this year, the initiative will be extended to more schools countrywide. Airtel will work closely with the Ministry of Education to identify them and their locations.

wasanii wa five star waliopata ajali na kufariki na wale waliojeruhiwa watajwa


wasanii wa five star waliopata ajali na kufariki na wale waliojeruhiwa watajwawasanii wa five star waliopata ajali na kufariki na wale waliojeruhiwa watajwaBaadhi ya wasamalia wema waliokuwa kwenye foleni ya magari baada ya kutokea kwa ajili ya Basi ndogo la Wasanii wa Kundi la Five Stars Moden Taarab wakichunguza kwa makini iwapo kuna mtu aliyebanwa ama kusahauliwa kuokolewa ama miili wake kubakia eneo hilo baada ya basi hilo kuparamia lori lililosheheni mbao lililokuwa limeharibika njiani , katika barabara kuu ya Iringa- Morogoro , eneo la Hifadhi ya Taifa ya wanyama ya Mikumi, karibu na Kijiji cha Doma, Wilaya ya Mvomero usiku wa kuamkia leo.
Lori lililoparamiana na basi la wanamuziki wa Five Stars

wasanii wa five star waliopata ajali na kufariki na wale waliojeruhiwa watajwaMsanii wa kikundi cha Taarab cha East African Melody Bi Mwanahawa Ally ( 55) akiwa wodini katika Hospitali ya Mkoa wa Morogoro leo baada ya kujeruhiwa kwenye ajali ya basi dogo la wasanii wa Kundi la Five Stars Moden Taarab la Jijini Dar es Salaam. Yeye alikuwa msanii mwalikwa kwenye safari hiyo ya kikazi katika mikoa ya nyanda za juu kusini . Picha zote na habari na John Nditi wa Globu ya Jamii, Morogoro


Majina ya wanamuziki wa bendi ya Five Star Modern Taarab waliokufa katika ajali ya gari Mikumi mkoani Morogoro usiku wa kuamkia leo yamefahamika.

Kwa mujibu wa mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoani Morogoro Be. Ibrahim Mwamakula, marehemu hao ni Issa Kijoti, Nasoro Madenge, Mapande, Fembe Juma, Omary Hashim, Tizo ,Omari Tall,Ngeleza Hasan,Hamisa Omari,Maimuna 'Kisosi', Haji Msaniwa na mcheza show wa kundi la Kitu Tigo Ilala

“ Hii ajali imepoteza watu 13 kati ya hao 12 wamefariki papo hapo na mmoja
amefariki akiwa anapatiwa matibabu Hospitalini.

"Ni ajali mbaya kutokea iliyohusisha magari matatu, ambapo waliokufa wote ni kutoka kwenye basi dogo la wasanii wa kikundi cha Five Stars na kusababisha majeruhu tisa kulazwa” alisema Mwamakula, akifafanua kuwa kati ya waliokufa 10 ni wanaume na watatu ni wanawake.

Amesema majeruhi tisa ambao wote ni wasanii waliolazwa katika Hospitali ya Mkoa wa
Morogoro ni pamoja na Mwanahawaa Ally( 55) kutoka Kundi la East African
Melody, ambaye alikuwa ni msanii mwalikwa, Susana Benedict(32), Zena Mohamed
(27), Samila Rajab (22)na Mwanahawa Hamisi (36)ambao wamelazwa wodi namba
tatu.

Kwa mujibu wa Kamanda huyo wa Kikosi cha Usalama Barabarani aliwataja
wasanii wengine waliolazwa katika Hospitali hiyo ni pamoja na Ally Juma
(25), Rajabu Kondo ( 25), Issa Hamis , Shaaban Hamis (41) na Msafiri Musa
(22).

Kwa mujibu wa Kamanda huyo wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Morogoro, kuwa dereva huyo aliligonga lori hiyo wakati akijaribu kulikwepa Lori jingine lililokuwa likotokea mbele yake lenye namba T 530 BHY lenye tela T 182 BKB aina ya Scania ambapo katika harakati hizo basi hilo lililigonga Lori hiyo mbele pembezoni na kusababisha magari hayo kuanguka.

Alisema kuwa baada ya kuliparamia Lori hiyo , basi hilo liliyumba na kuhama uoande wake na kujibamiza kwenye Lori lililokuwa mbele yake ambalo halikuwa na mzingo kitendo kilichofanya paa la basi hilo kukatwa wa juu ambapo watu 12 waliokuwa ndani ya basi ndogo hilo kufariki dunia papo hapo na wengine saba kujeruhiwa vibaya .

Hata hivyo alisema , majeruhiwa mmoja kati ya saba alifariki dunia wakati alipokuwa akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Mkoa wa Morogoro alipofikishwa kutoka eneo la tukio na kutambuliwa na ndugu zake kuwa ni Haji Mzaniwa ( 38), mwimbaji wa kikundi hicho.

SERIKALI:STUDIO YA JK NI KWA AJILI YA WASANII WALIOIOMBA


Mwakilishi wa Kampuni ya Fleva Unit ambayo ndiyo imekabidhiwa studio ya kurekodia muziki (Mastering Studio) na Mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete, Said Fella (kushoto) akitoa ufafanuzi juu ya vifaa hivyo Jumatatu wiki hii kwenye Jukwaa la Sanaa BASATA. Katikati ni Katibu Mtendaji wa BASATA, Ghonche Materego na Mkurugenzi Msaidizi anayeshughulikia Sanaa Bi. Angela Ngowi
Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi (Kulia) akihoji masuala mbalimbali kwenye Jukwaa la Sanaa BASATA wiki hii kuhusu Studio iliyotolewa kwa wasanii na Rais Jakaya Kikwete miaka mitatu iliyopita. Kulia kwake ni Mratibu wa Jukwaa hilo, Ruyembe C.Mulimba.

Katibu Mtendaji wa BASATA, Bw. Materego akisisitiza jambo kwenye Jukwaa hilo kuhusu Studio ya kurekodia Muziki (Mastering Studio) iliyotolewa kwa wasanii na Rais Jakaya Kikwete.


Mkurugenzi wa Idara ya Utamaduni kitengo cha Sanaa kutoka Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo, Bi. Ngowi akitoa tamko la Rais Jakaya Kikwete kuhusu Studio aliyoitoa kwa wasanii kwenye Jukwaa la Sanaa.Katikati ni Katibu Mtendaji wa BASATA Bw. Materego na Said Fella.

SERIKALI:STUDIO YA JK NI KWA AJILI YA WASANII WALIOIOMBA


Mwakilishi wa Kampuni ya Fleva Unit ambayo ndiyo imekabidhiwa studio ya kurekodia muziki (Mastering Studio) na Mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete, Said Fella (kushoto) akitoa ufafanuzi juu ya vifaa hivyo Jumatatu wiki hii kwenye Jukwaa la Sanaa BASATA. Katikati ni Katibu Mtendaji wa BASATA, Ghonche Materego na Mkurugenzi Msaidizi anayeshughulikia Sanaa Bi. Angela Ngowi
Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi (Kulia) akihoji masuala mbalimbali kwenye Jukwaa la Sanaa BASATA wiki hii kuhusu Studio iliyotolewa kwa wasanii na Rais Jakaya Kikwete miaka mitatu iliyopita. Kulia kwake ni Mratibu wa Jukwaa hilo, Ruyembe C.Mulimba.

Katibu Mtendaji wa BASATA, Bw. Materego akisisitiza jambo kwenye Jukwaa hilo kuhusu Studio ya kurekodia Muziki (Mastering Studio) iliyotolewa kwa wasanii na Rais Jakaya Kikwete.


Mkurugenzi wa Idara ya Utamaduni kitengo cha Sanaa kutoka Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo, Bi. Ngowi akitoa tamko la Rais Jakaya Kikwete kuhusu Studio aliyoitoa kwa wasanii kwenye Jukwaa la Sanaa.Katikati ni Katibu Mtendaji wa BASATA Bw. Materego na Said Fella.

TUZO ZA KIL KUFANYIKA JUMAMOSI

Hapa walisimama pamoja na wanahabari hawapo pichani kuwaombea wasanii 12 wa Five Stars waliotangulia mbele ya haki.
Na Ripota Wetu
Jumanne, Tarehe 22 Machi – Maandalizi kwa ajili ya onyesho la Tuzo za Muziki za Kili yamekamilika ambapo waandaaji wa Tuzo hizo, Kampuni ya Bia Tanzania TBL, kupitia kinywaji chake cha bia ya Kilimanjaro Premium Lager wametangaza wasanii watakaotoa burudani katika onyesho la utoaji wa Tuzo hizo litakalofanyika Jumamosi ya Tarehe 26, Machi 2011 katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam kuanzia saa moja jioni.

Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania TBL, David Minja aliwaambia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana ya kuwa Utoaji wa Tuzo za mwaka huu utapambwa na burudani tofauti kutoka kwa wasanii mbalimbali na kuogezea kuwa mwaka huu onyesho litakuwa katika mwonekano wa kisasa zaidi kulinganisha na miaka ya nyuma.

“Tumekuwa tukidhamini Tuzo hizi kwa miaka kadhaa sasa na kila mwaka tumekuwa tukionyesha staili tofauti katika uboreshaji wa Tuzo hizi. Mwaka huu tumeziboresha zaidi na nina uhakika wale watakaofika kushuhudia onyesho hili watakuwa mashahidi,” Alisema Minja

Minja alisema kuwa wasanii wanaowania tuzo hizo na wale watakaotoa burudani watakaribishwa katika ukumbi huo kwa njia ya kipekee, na kuhojiwa na vyombo vya habari. “Tumeamua kutumia wasanii wa ndani na tuna imani na wanachokifanya katika suala zima la kutoa burudani,” Alisema Minja.

Alisema lengo la Tuzo hizi zinazodhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro Premium Lager ni kufikisha muziki wa Tanzania katika kilele cha mafanikio, na kuongezea kuwa mwaka huu wameona ni vyema kuwapa nafasi kubwa wasanii wa hapa nyumbani kutoa burudani kama sehemu ya kuwapa nafasi ya kuonyesha vipaji vyao katika sanaa ya muziki,” alisema Minja.

Wasanii watakaotumbuiza katika utoaji wa Tuzo hizo ni Ali Kiba, THT, Banana Zoro, Linah, Diamond, Joe Makini, C Pwaa, 20%, Mzee Yusuf pamoja na Mapacha Watatu na Stara Thomas. Halikadhalika kutakuwa na burudani ya pamoja kutoka kwa washindi wa Tuzo za Kili kwa mwaka jana.

Kwa mujibu wa Minja, Tiketi kwa ajili ya onyesho hilo zimeshaanza kuuzwa katika vituo mbalimbali jijini Dar es Salaam kwa bei ya 25,000/- kwa tiketi za VIP na 15,000/- kwa tiketi za kawaida.

Minja alisema kuwa watu watakaolipa kiingio cha VIP watapata bia za Kilimanjaro Premium Lager bure, wakati kutakuwa na bia mia moja za Kilimanjaro Premium Lager kwa watu mia moja wa kwanza kuingia ukumbini.

Tuzo zinazoshindaniwa kwa mwaka 2010/ 2011 ni Msanii wa kike bora wa Muziki, Msanii wa Kiume Bora wa Muziki, Mwibaji bora wa Kike, Mwimbaji Bora wa Kiume, Wimbo Bora wa Taarab, Wimbo bora wa Mwaka.
Nyingine ni Wimbo bora wa Kiswahili (bendi), Wimbo bora R&B, Wimbo bora wa Hip Hop, Wimbo bora wa Ragga, Rapa bora wa Mwaka (Bendi), Msanii bora wa Hip Hop, Wimbo bora wa Africa Mashariki, Mtayarishaji bora wa Muziki, Video bora ya muziki ya Mwaka na Msanii mpya anayechipukia, Wimbo bora wa Kushirikishwa/ Kushirikisha, Wimbo bora wa asili na Wimbo bora wa Rhumba.

Saturday, March 19, 2011

MSONDO SIKINDE ZA DHIHIRISHA KUWA NI MIAMBA YA MUZIKI WA DANSI NCHINI

Mpiga gita la Solo Abdul Ridhiwani 'Pangamawe wa Msondo akiwapagawisha mashabiki wakati wa mpambano wao na Sikinde jana
Mashabiki wa Sikinde wakilisakata lumba
JUma Katundu akiwa sambamba na Nacho Mpendu Mama Nzawisa
Mashabiki wa Msondo wakifuraia magitaa yalivyokuwa yakikungutwa
Hasani Moshi 'Tx Jr' kushoto na Shabani Dede 'Super Motisha'
Waimbaji wa Msondo wakilishambulia jukwaa wakati wa mpambano wao uliofanyika Dar es salaam jana
Wanamziki wa bendi ya Sikinde wakilishambulia jukwaa kulia ni Husein Jumbe, Hassani KUnyata na Abdalah Hemba
Hassani Kunyata na Husein Jumbe wakiimba
Abdalah Hemba akimba sambamba na kucheza na mnenguaji wa bendi ya Sikinde

Thursday, March 17, 2011

JK ATINGA WIZARA YA ELIMU KUKAGUA MAENDELEO


Rais Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Wizara ya Elimu leo
Kikwete akisalimiana na Katibu Mkuu wa Balaza la Mitiani Tanzania JOys Ndarichako walipokutana wizara ya Elimu leo

Tuesday, March 15, 2011

POULSEN ATAJA KIKOSI KIPYA KITAKACHOIVAA AFRIKA YA KATI MACHI 26


Kocha Mkuu wa timu ya Taifa, Jan Poulsen akizungumza na waandishi wa Habari kwenye Ofisi za Shirikisho la mpira wa miguu nchini,( TFF) leo mchana wakati wa kutangaza kikosi cha wachezaji wanaounda timu ya Taifa kwa ajili ya kucheza na timu ya Jamhuri ya Kati katika michuano ya kuwania kufuzu kucheza Fainali za mataifa ya Afrika mwaka 2012 zitakazofanyika Ikweta ya Guinea na Gagon. Kulia ni Ofisa Habari wa Shirkisho hilo, Boniface Wambura na kushoto ni mwakilishi wa wadhamini, kutoka Kampuni ya, Allan Chonjo.
GOALKEEPERS:-
1:- Shaban Kado-Mtibwa Sugar
2:-Juma Kaseja-Simba
3:- Shaaban Dihile-JKT Ruvu
DEFENDERS:-
1:- Shadrack Nsajigwa-Yanga
2:- Aggrey Morris-Azam
3:- Nadir Haroub ‘Cannavaro’-Yanga
4:- Stephano Mwasika-Yanga
5:-Haruna Shamte-Simba
6:- Juma Nyosso-Simba
7:- Idrissa Rajab-Sofapaka (Kenya)
MIDFIELDERS:-
1:- Nurdin Bakar-Yanga
2:- Shaban Nditi-Mtibwa Sugar
3:- Jabir Aziz-Azam Fc
4:- Henry Joseph-Kongsvnger IL, (Norway)
5:- Abdi Kassim-DT Long An, (Vientnam)
6:- Mwinyi Kazimoto-JKT Ruvu
ATTACKERS:-
1:- Dan Mrwanda-DT Long An, (Vientnam)
2:- Nizar Khalfan-Vancouver Whitecaps,(Canada)
3:- Mrisho Ngasa-Azam Fc
4:- Mohamed Banka-Simba
5:- Athuman Machupa-Vasalund IF,(Sweden)

Sunday, March 13, 2011

DVD YA SUPER D BOXING COACH YAINGIA MTAANI JANA


KAVA YA VIDEO YA SUPER D BOXING COACH BONDIA wa Zamani na Kocha wa Ngumi wa Klabu ya ngumi ya Ashanti, Rajabu Mhamila'Super D' ameingiza Video inayozungumzia maisha yake ya mchezo huo.Akizungumza Dar es Salaam leo, Super D alisema video hiyo ilikua sokoni kuanzia sasa ikizungumzia maisha yake tangu alipoanza kucheza mchezo huo mwaka 1984 hadi 2010 sasa.Alisema Video hiyo itaonesha mapambano mbalimbali aliyocheza na dhidi yamabondia Mbwana Matumla, Rashidi Ali na Ajibu Salumu.Alisema lengo la kuandaa video ni kutaka kutimiza malengo yake ya kuendelezamchezo wa ngumi kwa kuwapatia vijana nafasi ya kujifunza kupitia kwake.Alisema kutokana na nchi ya Tanzania kuwana vipaji vingi atashindwa kuwafikiakila mmoja wao na badala yake amewapa fursa ya kujifunza kwa kuangalia video.Alisema Video ya katika kuhaikisha hiyo DVD inafanya vizuri sokoni ameongezeavionjo vingine kutoka kwa mabondia maarufu duniani kama Mike Tyson, Michael Mo,Junior Myweather, Mohamed Ally, Man aqyao na Joe Fleizer ambapo kuanzia sasa ipo mtaani ususani makutano ya barabara ya Uhuru na Msimbazi Dar es salaam

CHIKAWE AKABIDHIWA MSAADA WA HOSPITALI YA WILAYA YA NACHINGWEA



Mbunge wa Jimbo la Nachingwea mkoa,Lindi Bw.Mathias Chikawe wa pili (kushoto) ambaye pia ni waziri wa nchi ofisi ya Rais -utawala bora akipokea msaada wa baiskeli ya walemavu kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya UNDI inayojishughulisha na maswala ya ujenzi, Bw.Philip Makota wa kwanza kulia ikiwa ni sehemu ya vifaa vya hospitalini vyenye thamani ya shilingi milioni 13 kwa ajili ya hospitali ya Wilaya ya Nachingwea,Wengine pichani wakurugenzi wengine wa UNDI Dkt.Saanane Bonaventure katikati na Bakari Shekimweri wa kwanza kushoto hafla ya makabidhiano hayo ilifanyika mwishoni mwa wiki mkoani humo.(Picha na Mpigapicha Wetu)

TAMIMU AMTWANGA ASHIRAFU KILA MMOJA ALAMBA SAKAFU KWA MAKONDE


Awadhi Tamimu akilamba sakafu
Ufundi wa kutupa mawe ukioneshwa
Tamimu akirusha ngumi kwa Ashirafu
Ashirafu akilamba sakafu

tigo wakabidhi nissan hard body kwa mshindi wa promosheni ya bahatika


Ofisa Viwango wa Tigo, David Zakaria akikabidhi funguo ya gari aina ya Nissan Hard Body yenye thamani ya shs milioni 56 kwa mshindi wa promosheni ya Bahatika na Tigo, hafla iliyofanyika katika viwanja vya Coco Beach, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Ofisa Uhusiano wa Tigo Tanzania, Jackson Mmbando akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi ya gari ya promosheni ya Bahatika na Tigo ambako washindi wawili walikabidhiwa magari yao aina ya Nissan Hard body yenye thamani ya shs milioni 56 kila moja jijini Dar es
Salaam mwishoni mwa wiki.
Mwanamuziki wa kizazi kipya Chidi Benz akifanya vitu vyake katika onyesho hilo.
Joe Makini akiwachengua umati wa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam katika onyesho la Bahatika na Tigo katika viwanja vya Coco Beach jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya umati wa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam waliofurika katika viwanja

Thursday, March 10, 2011

WACHEZAJI WA TENNIS WALEMAVU WAKIJIFUA JIJINI DAR


Ernest akicheza
Ernest akicheza
Ernest
Thomas
Ernest
Ernest akicheza
Thomas na Ernest wakicheza dhidi ya Mwalimu wao, Francis Kimati wakati wa mazoezi hayo
Ernest akicheza
Thomas akijiandaa kucheza


Thomas akicheza wakati Mwandishi na Mpiga picha wa ITV, Abdalah Kaniki akifanya kazi yake wakati wa mazoezi hayo.
Thomas (kulia) na Ernest wakiwa kwenye mahojiano na waandishi wa habari
Waandishi wa habari wa ITV ,Abdalah Kaniki na Ester wakifanya mahojiano na wachezaji hao.