
Mwakilishi wa Kampuni ya Fleva Unit ambayo ndiyo imekabidhiwa studio ya kurekodia muziki (Mastering Studio) na Mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete, Said Fella (kushoto) akitoa ufafanuzi juu ya vifaa hivyo Jumatatu wiki hii kwenye Jukwaa la Sanaa BASATA. Katikati ni Katibu Mtendaji wa BASATA, Ghonche Materego na Mkurugenzi Msaidizi anayeshughulikia Sanaa Bi. Angela Ngowi

Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi (Kulia) akihoji masuala mbalimbali kwenye Jukwaa la Sanaa BASATA wiki hii kuhusu Studio iliyotolewa kwa wasanii na Rais Jakaya Kikwete miaka mitatu iliyopita. Kulia kwake ni Mratibu wa Jukwaa hilo, Ruyembe C.Mulimba.

Katibu Mtendaji wa BASATA, Bw. Materego akisisitiza jambo kwenye Jukwaa hilo kuhusu Studio ya kurekodia Muziki (Mastering Studio) iliyotolewa kwa wasanii na Rais Jakaya Kikwete.

Mkurugenzi wa Idara ya Utamaduni kitengo cha Sanaa kutoka Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo, Bi. Ngowi akitoa tamko la Rais Jakaya Kikwete kuhusu Studio aliyoitoa kwa wasanii kwenye Jukwaa la Sanaa.Katikati ni Katibu Mtendaji wa BASATA Bw. Materego na Said Fella.
No comments :
Post a Comment