TIMU itakayoshinda mchezo wa Jumamosi hii utakaowakutanisha mabingwa watetezi, Simba na Yanga ndio itakuwa imejiwekea mazingira mazuri ya kunyakua ubingwa msimu huu.Timu hizo zitakutana katika mchezo wa mzunguko a pili wa Ligi Kuu Bara, ambao utapigwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Japokuwa timu itakayopoteza mchezo huo haitakuwa imejiondoa moja kwa moja katika mbio za kunyakua ubingwa lakini itakuwa na kazi kubwa kuhakikisha inarudi katika nafasi ya kuuchukua.
Katika msimamo Yanga waliocheza michezo 17 ndio wanaongoza wakiwa na pointi 38 huku Simba waliocheza michezo 16 wakishika nafasi ya pili wakiwa na pointi 37 huku Azam ambayo kabla ya matokeo ya mechi yaje ya jana ina pointi 35.
Kama Yanga itafanikiwa kushinda mchezo huu itakuwa imefikisha pointi 41 lakini itakuwa imewazidi Simba mchezo mmoja, wakati mabingwa watetezi wakishinda watafikisha 40.
Mchezo huu ambao utawakutanisha watani wa jadi unatarajiwa kuwa wa aina yake na utatia hukumu ya nani ni mwamba msimu huu.
Yanga itataka kuendeleza rekodi yake ya ushindi katika Ligi Kuu msimu huu, huku Simba ikitaka kulipa kisasi cha kufungwa 1-0 na Yanga katika mechi ya kwanza Mwanza Oktoba 16 mwaka jana.
Lakini Simba ilishinda katika fainali ya Kombe la Mapinduzi Januari 12 mwaka huu kwa kuifunga Yanga 2-0.
Simba ambayo inaingia uwanjani baada ya ushindi mnono wa 4-1 dhidi ya Yanga itatokea Zanzibar huku Yanga walioilaza Ruvu Shooting 1-0 imejichimbia Bagamoyo.
Mchezo huo utakuwa ni mtihani wa kwanza kwa Kocha mpya wa timu hiyo, Mganda Sam Timbe dhidi ya wapinzani wa jadi wa Yanga, Simba.
Kwa upande wake Phiri ambaye alijiunga na Simba kwa mara ya kwanza mwaka 2004, hatokuwa na presha sana na mtanange huo kutokana kuingoza Simba ikikutana na Yanga mara tisa.
Sam Timbe kwa upande wake amesema haihofii Simba japokuwa alikubali kuwa timu hiyo kwa sasa ipo vizuri huku ikiwa na wachezaji wanaojua ipasavyo majukumu yao.
"Tumejiandaa vya kutosha, huu ni kati ya mchezo muhimu kangu kuweza kushinda, natambua juu ya ushindani uliopo kati ya timu hizi,lakini cha msingi hapa ni pointi tatu," alisema Timbe.
Phiri alisema ushindi wa mabao manne waliopata vijana wake dhidi ya Mtibwa ndio utakaowasaidia kuibuka na ushindi katika mchezo wao dhidi Yanga.TFF jana ilitangaza kuwa mechi hiyo itaanza saa 10 za joini na kuchezeshwa na mwamuzi wa kimataifa, Oden Mbaga..Ofisa Habari TFF, Boniface Wambura, alisema kiingilio cha chini kitakuwa ni sh. 3,000 wakati kile cha juu ni sh. 30,000.
Alisema tiketi za mechi hiyo zitaanza kuuzwa Ijumaa saa 2 asubuhi katika vituo vya Shule ya Sekondari Benjanimi Mkapa, Big Bon Msimbazi, mgawahawa wa Steers uliopomtaa wa Samora/Ohio na Uwanja wa Uhuru.
Alifafanua viingilio hivyo kuwa ni viti vya kijani mzunguko ni sh. 3,000, bluu mzunguko sh. 5,000, rangi ya chungwa sh. 7,000, VIP C sh 10,000, VIP B sh. 20,000 na VIP A sh. 30,000.
Alisema Mbaga wa Dar es Salam atasaidiwa na Mohamed Mkono wa Tanga na Maxmiliani Nkongolo wa Rukwa.Alisema mwamuzi wa mezani ni Hashim Abdallah wa Dar es Salaam, kamishna wa mechi ni Mchungaji Army Sentimea wa Dar es Salaam.
Yanga inatarajiwa kupangwa hivi: Yew Berko, Nsajigwa Shadrack, Stephano Mwasika, Nadir Cannavaro, Chacha Marwa, Ernest Boakye, Kigi Makasi, Nurdin Bakari, Davis Mwape, Jerry Tegete na Nsa Job.
Simba: Ally Mustapha, Haruna Shamte, Juma Jabu, Meshack Abel, Juma Nyoso, Jerry Santo, Rashid Gumbo, Patrick Ochan, Mbwana Samatta, Mussa Mgosi na Amri Kiemba.
FEAJ KUTETEA HAKI ZA WAANDISHI
-
*Mwandishi wetu,Kigali*
Shirikisho jipya la Waandishi wa habari Afrika Mashariki(FEAJ) limeanzishwa
ili kusaidia kutetea haki na maslahi ya wafanyakazi ...
10 hours ago
No comments :
Post a Comment