JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
MFUKO WA PENSHENI KWA WATUMISHI WA UMMA
(PSPF)
TAARIFA KWA UMMA
Mfuko
wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) unawajulisha kwamba Mkutano
Mkuu wa wadau utakaofanyika tarehe 07 na 08 Machi 2013 kuanzia saa mbili
na nusu asubuhi hadi saa kumi jioni katika Ukumbi wa JB Belmont uliopo
ghorofa ya 6 ya Jengo la Maegesho la PSPF - Golden Jubilee Towers , Dar
es Salaam.
Madhumuni
ya Mkutano huu ni kutoa taarifa ya hesabu ya mwaka na utendaji wa Mfuko
na kutathmini mafanikio na changamoto zinazoukabili Mfuko na Sekta ya
Hifadhi ya Jamii kwa ujumla.
Tafadhali
thibitisha ushiriki wako kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu Makao Makuu, Dar es
Salaam au Ofisi za PSPF mikoani kabla ya tarehe 05 Machi 2013.
“PSPF - Tulizo la Wastaafu”
Kaimu Mkurugenzi Mkuu
Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma,
Golden Jubilee Towers, Ghorofa ya 6-13, Mtaa wa Ohio/Kibo,
Central Area, Kiwanja Na. 8, 9, 12 na 15, S. L. P 4843. Dar-es-Salaam.
Simu: +255 22 2120912/52 au +255 22 2127375 /6
Nukushi: +255 22 2120930.