
Safari
hii vita kubwa itafanyika katika nchi ya iliyowahi kujulikana kama
Pwani ya Dhababu au Gold Coast (Ghana) katika jiji la Accrah wakati
bondia anayechipukia kwa kazi Richard Commey wa Ghana anayeishi katika
jiji la London nchini Uingereza atafuana na Mghana mwenzake Bilal
Mohammed ambaye anatoka katika moja na viunga maarufu kwa kutoa mabingwa
wa dunia cha Lenanon katika jiji la Accrah nchini Ghana kugombea mkanda
wa IBF Africa katika uzito mwepesi au lightweight.
Wawili
hao wanakutana katika pambano la utangulizi wakati bondia bingwa wa
dunia wa zamani wa IBF katika uzito wa Bantam Joseph Agbeko
atakapochuana na Luis Melendez kutoka nchini Columbia iliyoko Amerika ya
Kusini kugombea ubingwa wa dunia katika uzito wa Bantam.
Mpambano
mwingine ambao utawakutanisha mabondia wawili wa Ghana wenye uzoefu
mkubwa ni wa kugombea uzito wa Welter wakati bondia maarufu Frederick
Lawson atakapokutana na bondia chipukizi Issac Sowah wakigombea ubingwa
wa IBF katika bara la Afrika.
Ukweli utajulikana wakati huu ni nani kati ya mabondia hawa wanne watakaoibuka na mikanda ya ubingwa wa IBF.
ISSUED BY:
INTERNATIONAL BOXING FEDERATION AFRICA (IBF/AFRICA)
DAR-ES-SALAAM, TANZANIA
No comments :
Post a Comment