Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Thursday, February 7, 2013

FFU wa Ngoma Africa band wapo kambini ! kujiandaa na vita vya "kuziba Nyufa"



FFU wakiwa kambini.

Watangaza Vita Mpya ya "KUZIBA NYUFA" katika mpasuko wa Jamii!

Habari za uhakika tena nyeti vimevuja kutoka katika kambi ya bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya "Ngoma Africa Band" aka FFU yenye makazi  yake nchini Ujerumani.

Kuwa bendi hiyo inayofanananishwa na kikosi kazi FFU imeingia kambini katika msimu  wa barafu huko ughaibuni, kwa kujifua na kujiandaa kwa kuwaletea washabiki vitu vipya ! Pia Kiongozi wa bendi hiyo Kamanda Ras Makunja mwanamuziki mwenye mjina mengi ya kutisha tisha kama vile kamanda wa FFU,Kolokoloni namba 1,mfalme Hui Hui wa gagagigikoko n.k,kamanda alikaririwa mwanzoni mwa Januari 2013 kuwa Bendi hiyo inaenda kambini Kujiandaa na vita ! alipoulizwa vita gani? alijibu vita vipya vya "KUZIBA NYUFA" zilezojitokeza katika jamii yetu!

Ndio kusema Kamanda wetu wa FFU Ras Makunja kaingia kambini na kikosi chake kujiandaa na vita? vita venyewe vya kuziba nyufa na mimomonyoko au mipasuko katika jamii yetu! kauli ya kamanda Ras Makunja inaonekana inadarubini ya mtazamo mkali unaoona mbali! katika
mahojiano na jarida la africa analysis la Uingereza,

Ni siku chache tu bendi hiyo yenye tabia za ki-FFU ilionekana katika uwanja wa ndege wa Bremen,wakiwa wanaondoka lakini wakusema wapi wanako elekea, "wanamuziki wa bendi hiyo wakiwa na mizigo" nyusoni wakiwa seriously tena  hawakuwa tayari kujibu chochote wanachoulizwa ! tena katika msimu wa baridi na barafu wanaenda kambini? tena haijulikani nchi gani? kama Serbia au Bosnia ? pengine Israel ! hakuna anayejua !

Kamanda Ras Makunja na ffu wa Ngoma Africa Band wapo kambini,kwa kujiandaa na vita vya kuziba nyufa, na mwaka huu pia bendi hiyo inatimiza miaka 20 tangu izaliwe mwaka 1993 hadi mwaka huu 2013 ni umri mkubwa.

Washabiki wanasubiri kwa hamu kubwa kuona na kujiunga na na vita vilivyotangazwa na bendi hiyo chini ya kamanda Ras Makunja mwenye kichwa kigumu au mkuu wa "Watoto wa Mbwa" Ngoma Africa ukipenda FFU .

No comments :

Post a Comment