Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Monday, June 30, 2014

NGUMI ZILIVYOPIGWA MWANANYAMALA NDANI YA MFUNGO WA RAMADHANI


Bondia JuliasKisarawe kushoto akipambana na Patrick Nne wakati wa mchezo wao uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita Kisarawe alishinda kwa point Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Mwinyi Mzengela  kushoto akimtupia konde la kushoto bondia Georege Manywele wakati wa mpambano wao wa kumaliza ubishi uliofanyika katika ukumbi wa CCM Mwijuma Mwananyamala mwishoni mwa wiki iliyopita Mzengela alishinda kwa K,O ya raundi ya nne picha na 
Bondia Josepher Mbowe akipambana na Mfaume Alkaida wakati wa mpambano wao mbowe alishinda katika raundi ya pili picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

dj films company kutoa filamu mbili mpya


Na Mwandishi Wetu


David Jastin
KIKUNDI cha filamu nchini kimezinduliwa kwa ajili ya kuendeleza na kuibua vipaji vipya katika tasinia hiyo kundi hilo lililoweka makazi yake Mbezi beach jijini Dar es salaam linaongozwa na David Jastin limepewa jina la dj films company

kampuni hiyo inayohusika na utengenezaji wa filamu mbalimbali nchini linatarajia kutoa kazi yake mpya hivi karibuni itakayokwenda kwa jina la Dunia aina siri itakayotoka hivi karibuni

wakati wa uzinduzi wa kundi hilo walimtambulisha rasmi meneja wa kundi anaejulikana kwa jina las Paul Marandu ambaye atakuwa ana husika na kazi mbalimbali za kampuni hiyo pamoja na kundi lake

Jastin aliongeza kwa kusema wameanzisha kundi hilo kwa lengo moja tu kuja kuwainua vijana chipkizi na kuendeleza wale wanaofanya vizuri zaidi 

kundi hili limeshafanya kazi mbalimbali ambazo zipo mtaani kwa sasa  kama Opportunity Love,Binadamu kigeugeu na nyingine nyingi zikiwashilikisha wasanii mbalimbali kama

WastaraJuma,Ndumbagwe Misajo,Chales Magari na wasanii mbalimbali wanaotamba katika anga ya sanaa kwa sasawasanii wa kundi la dj films company

GLOBAL PUBLISHERS YAKABIDHI MEZA MBILI KWA CHAMA CHA MAGAZETI MKOA WA DAR ES SALAAM


Afisa Tawala wa Global Publishers, Soud Kivea kulia akimkabidhi meza mbili za ofisini kwa makamu mwenyekiti wa wauza magazeti mkoa wa Dar es salaam  zilizotolewa na kampuni yake ya
Global Publishers
 Afisa Tawala wa Global Publishers, Soud Kivea kulia akimkabidhi meza mbili za ofisini kwa makamu mwenyekiti wa wauza magazeti mkoa wa Dar es salaam  zilizotolewa na kampuni yake ya
Global Publishers
Afisa Tawala wa Global Publishers, Soud Kivea kulia akimwangalia makamu mwenyekiti wa wauza magazeti mkoa wa Dar es salaam jinsi anavyo andika taharifa mbalimbali baada ya kupokea meza mbili  zilizotolewa na kampuni  ya
Global Publishers

WANARIADHA WAAHIDI KURUDI NA MEDALI NA KULINDA HESHIMA YA TANZANIA KATIKA MASHINDANO YA JUMUIYA YA MADOLA NCHINI SCOTLAND


 Kocha wa wachezaji wa Riadha waliokuwa nchini Ethiopia kwa ajili ya maandalizi ya mashindano ya Olympic yanayotarajia kufanyika kuanzia 23, Julai, 2014 jijini Glasgow Scotland Bw. Shaban Hiiki (mwenye suti nyeusi) akiwa na baadhi ya wanamichezo hao mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam jana.
Kocha wa wachezaji wa Riadha waliokuwa nchini Ethiopia kwa ajili ya maandalizi ya mashindano ya Olympic yanayotarajia kufanyika kuanzia 23, Julai, 2014 jijini Glasgow Scotland Bw. Shaban Hiiki (mwenye suti nyeusi) akiwa na baadhi ya wadau wa mchezo wa Riadha waliojitokeza kuwapokea wachezaji wa mchezo huo mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam jana.
 Kocha wa wachezaji wa Riadha waliokuwa nchini Ethiopia kwa ajili ya maandalizi ya mashindano ya Olympic yanayotarajia kufanyika kuanzia 23, Julai, 2014 jijini Glasgow Scotland Bw. Shaban Hiiki (mwenye suti nyeusi) akiwa na baadhi ya wanamichezo hao mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam jana. Picha na Frank Shija, WHVUM
**********************
Na Frank Shija, WHVUM
Wanamichezo waahidi kuleta medali katika mashindano ya Olympic yanayotarajia kuanza tarehe 23 Julai jijini Glasgow Scotland.
Akizungumza mara baada ya kuwasili nchini jana wakitokea Ethiopia Kocha wa Timu ya Riadha aliyeambatana na wachezaji 8 Bw. Shaban Hiiti alisema kuwa ana imani kubwa na wachezaji wake walioteuliwa katika Timu ya Taifa kuwa watailetea heshima Taifa kwa kuwa mazoezi waliyoyapata wakiwa nchini Ethiopia yamewajengea uwezo mkubwa.
Hiiki aliongeza kuwa walipokuwa nchi Ethiopia kwa mazoezi wamejifunza mbinu mbalimbali kutokana na kuwa na program za kuwajengea uwezo wachezaji wake.
“Nimatumaini yangu wachezaji hawa walioteuliwa kujiunga na wenzao waliokuwa mazoezini katika nchini zingine ambapo wanamichezo wetu walienda kwa ajili ya mazoezi wataliletea Taifa letu heshima kubwa kwani wamepikwa wakapikika”. Alisema Kocha huyo.
Aidha kocha huyo amesema kuwa uwepo mazingira mazuri na vifaa bora vya mazoezi kumechangia kwa kiasi kikubwa kuinua ubora wa wanariadha hao ambao wamefanya mazoezi kwa takribani miezi miwili nchini Ethiopia.
Kwa upande wake mmoja wa wanariadha ambaye amebahatika kuitwa kwenye kikosi kitakachoshiriki mashindano hayo Bw. Alphonce Felix amesema kuwa anajisikia faraja kuwa miongoni mwa wanamichezo watakao iwakilisha nchi katika mashindano ya Olympic kupitia mchezo wa riadha.
Alphonce amesema kuwa atatumia ujuzi alioupata nchini Ethiopia walipokuwa wameweka kambi kwa ajili ya maandalizi ya mashindano hayo.
Jumla ya wanariadha 9 na kocha wao waliweka kambi nchini Ethiopia ikiwa ni jitihada zinazofanywa na Serikali za kukuza na kuendeleza Sekta ya Michezo nchini kupitia mpango wa Diplomasia ya Michezo, ambapo wanamichezo mbalimbali wameweka kambi ambao wanamichezo wengine waliweka kambi katika nchi za Uturuki, China na New Zealand

Sunday, June 29, 2014

KANISA LA YESU KRISTO LA WATAKATIFU WA SIKU YA MWISHO WAKARIBISHA WATU MBALIMBALI KATIKA KANISA



Kiongozi wa shule ya jumapili wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa siku za mwisho,Dr, Emanuel Kandusi akiwapatia maelezo mbalimbali kwa watu waliotembelea kanisa hilo wakati wa siku ya wazi kwa ajili ya watu mbalimbali kuangalia shughuli zinazofanywa na kanisa hilo
Baadhi ya watu waliotembelea kanisa hili wakipata maelekezo mbalimbali
Mwakilishi wa Darasa la Mkono msaidizi wa akina mama Happy Ayubu akitoa maelezo kwa watu waliotembelea kanisa hilo
Baadhi ya watu waliotembelea kanisa hili wakipata maelekezo mbalimbali
Mhumini waKanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa siku za mwisho Framers Ngosha akijibu maswali ya watu waliojitokeza katika siku hiyo


Kiongozi wa shule ya jumapili wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa siku za mwisho,Dr, Emanuel Kandusi 'kulia' akionesha vitabu vinavyotumika kwa ajili ya mafunzo kushoto ni Rais wa tawi la Mbezi Beach, Malabi Kyubi
Rais wa tawi la Mbezi Beach, Malabi Kyubi akitoa maelezo
Baadhi ya watu mbalimbali waliotembelea katika kanisa hilo lililopo Mbezi Beach
Baadhi ya watoto wa waumini wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za mwisho wakicheza na kuimba wakati wa siku ya wazi kwa watu kutembelea na kuona mambo mbalimbali iliyofanyika katika kanisa lao la Mbezi Beach jijini Dar es salaam
Baadhi ya watoto wa waumini wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za mwisho wakicheza na kuimba wakati wa siku ya wazi kwa watu kutembelea na kuona mambo mbalimbali iliyofanyika katika kanisa lao la Mbezi Beach jijini Dar es salaam
Baadhi ya watoto wa waumini wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za mwisho wakicheza na kuimba wakati wa siku ya wazi kwa watu kutembelea na kuona mambo mbalimbali iliyofanyika katika kanisa lao la Mbezi Beach jijini Dar es salaam
watu waliotembelea wakipata mahelezo mbalimbali
Baadhi ya watu waliotembelea katisa hilo

NGUMI ZILIVYPIGWA MANZESE KATIKA UKUMBI WA KOBELO PUB



Bondia Mohamed Mussa kushoto akipambana na Shomary Punzi wakati wa mchezo wao uliofanyika katika ukumbi wa Kobelo Pub Manzese Dar es salaam Punzi alishinda kwa point Mchezo huo picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Mvukeni, Muhidini Kassimu kulia akimkabizi kiongozi wa mabondia, Ramadhanu Uhadi pesa kwa ajili ya mabondia kununua maji wakati wa mashindano yaliyofanyika katika ukumbi wa Kobelo Pub
Bondia Omary Gumbo kushoto akimrushia konde Japhert Pascar wakati wa mchezo wao uliofanyika katika ukumbi wa Kobelo manzese Gumbo alishinda kwa point mpambano huo picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Mwenyekiti wa Sertikali ya Mtaa wa Mvuleni, Muhidini Kassimu akiwapatia zawadi mabondia Omary Gumbo na Japhert Pascar

Bondia Shomari Punzi kushoto akipambana na Mohamed Mussa wakati wa Mpambano wao Punzi alishinda mpambano huo kwa point picha na
www.superdboxingcoach.blogspot.com

TAMWA kutoa elimu kupambana na ulevi kupindukia


Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Valerie Msoka akisisitiza jambo katika mkutano na wahariri wa vyombo vya habari jijini Dar es Salaam leo. 
Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Valerie Msoka akisisitiza jambo katika mkutano na wahariri wa vyombo vya habari jijini Dar es Salaam leo.Mkutano wa wahariri wa vyombo vya habari na TAMWA ukiendelea. Mkutano wa wahariri wa vyombo vya habari na TAMWA ukiendelea.Baadhi ya wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari jijini Dar es Salaam wakiwa kwenye mkutano na Chama cha Wanahabari Wanawakecha (TAMWA) leo. Baadhi ya wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari jijini Dar es Salaam wakiwa kwenye mkutano na Chama cha Wanahabari Wanawakecha (TAMWA) leo.Sehemu ya wahariri wa vyombo anuai vya habari jijini Dar es Salaam wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Valerie Msoka (hayupo pichani). Sehemu ya wahariri wa vyombo anuai vya habari jijini Dar es Salaam wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Valerie Msoka (hayupo pichani)Baadhi ya wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari jijini Dar es Salaam wakiwa kwenye mkutano na Chama cha Wanahabari Wanawakecha (TAMWA) leo. Baadhi ya wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari jijini Dar es Salaam wakiwa kwenye mkutano na Chama cha Wanahabari Wanawakecha (TAMWA) leo.Baadhi ya wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari jijini Dar es Salaam wakiwa kwenye mkutano na Chama cha Wanahabari Wanawakecha (TAMWA) leo. Baadhi ya wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari jijini Dar es Salaam wakiwa kwenye mkutano na Chama cha Wanahabari Wanawakecha (TAMWA) leo.

 KITUO cha Usuluhishi (CRC) kinachofanya kazi chini ya Chama cha Wanahabari Wanawakecha (TAMWA) kimejipanga kutoa elimu kwa jamii kuhakikisha kinapambana na matumizi ya pombe kupindukia kwa jamii suala ambalo limezidisha vitendo vya ukatili wa jinsia unaofanywa na watumiaji pombe kupindukia.

AIRTEL YAZINDUA SIMU MPYA AINA YA IPHONE 5S


Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel, Bi. Beatrice Singano Mallya (wa pili kulia) akizungumza na waandishi wa habari wakati Kampuni ya Airtel kwa kushirikiana na Apple ilipofanya uzinduzi wa simu mpya ya iPhone 5s pamoja na ofa kabambe kwa wateja wa Airtel, katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Ofa hiyo itawawezesha wateja wa Airtel kupata sms 5000, muda wa maongezi dakika 1500 pamoja na kifurushi cha internet cha 3GB. Wanaoshuhudia ni Meneja Masoko wa Airtel, Prisca Tembo (kulia) na wafanyakazi wa kitengo cha huduma kwa wateja wa kampuni ya Apple.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel, Bi. Beatrice Singano Mallya (kulia) akizungumza na waandishi wa habari wakati Kampuni ya Airtel kwa kushirikiana na Apple ilipofanya uzinduzi wa simu mpya ya iPhone 5s pamoja na ofa kabambe kwa wateja wa Airtel, katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Ofa hiyo itawawezesha wateja wa Airtel kupata sms 5000, muda wa maongezi dakika 1500 pamoja na kifurushi cha internet cha 3GB. Wanaoshuhudia ni Meneja Masoko wa Airtel, Prisca Tembo ( wa pili kulia) na wafanyakazi wa kitengo cha huduma kwa wateja wa kampuni ya Apple.

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam.
·Ni kampuni ya kwanza ya mawasiliano nchini kuingia mkataba wa ushirikiano na Apple.

KAMPUNI ya simu za mkononi ya Airtel inayoongoza kwa huduma bora na nafuu leo imetangaza ushirika wake na kampuni kubwa inayotengeneza simu za mkononi ya Apple.Airtel imeweka historia kwa kuwa kampuni ya kwanza ya mawasiiliano nchini Tanzania kuingia mkataba na Apple kupitia simu ya iPhone S5.

Akiongea wakati wa uzinduzi wa simu huo jijini Dar es Saalam Meneja Masoko wa Airtel Bi Prisca Tembo alisema” leo tunazindua  simu ya iPhone 5s na kuwapatia wateja wetu ofa kabambe ya vifurushi vya muda wa maongezi , ujumbe mfupi na internet. Mteja atakaponunua simu ya iphone S5 atapata kifurushi cha internet cha 3GB, dakika 1450 za maongezi na SMS 5000 kwa mwezi. Natoa wito kwa watanzania na wateja wetu kutumbelea maduka yetu na mawakala wetu ili kuweza kujipatia simu hii.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mawasiliano Bi, Beatrice Singano alisema “Uzinduzi huu leo utato fulsa kwa wateja wetu  kupata uzoefu tofauti wa huduma zetu na kuwawezesha  kuendelea kufurahia huduma yetu ya SWITCH on, huduma ambayo imezinduliwa ili kuwawezesha wateja wetu kupata internet yenye kasi zaidi bila kikomo kupitia mtandao wa Airtel”

“Simu hii ya iPhone 5s itawawezesha wateja wetu pia kupiga picha, kutuma video na kuwaunganisha na marafiki na familia . Ili kupata maelezo zaidi kuhusu ofa hii ya simu ya iPhone 5s tembelea tovuti yawww.apple.com/phone “aliongeza mmbando.

HOSPITALI YA MUFINDI YAPATA MSAADA WA VITI VYA KUBEBA WAGONJWA


 Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Mufindi, Dk Goodluck Mlimbila akijaribu kusukuma moja kati ya viti 33 vilivyotolewa na asasi ya MUVIMA kwa ajili ya hospitali ya wilaya ya Mufindi. Anayefurahi katikati ni mkurugenzi mwenza wa MUVIMA, Albert Chalamila akipongezwa na Katibu wa Afya wa Wilaya hiyo, Atupekisye Mwakifamba
Albert Chalamila na baadhi ya wanahabari wakiangalia hali ilivyo ndani ya wodi ya wazazi ya hospitali hiyo; hapa wanaonekana baadhi ya wajawazito wanaolala chini kutokana na ukosefu wa vitanda

Na Denis Mlowe,Mufindi

ASASI ya Mufindi Vijana kwa Maendeleo (MUVIMA) imetoa msaada kwa hospitali ya wilaya ya Mufindi yenye matatizo mbalimbali  kwa lengo la kusaidia kutoa huduma bora kwa kutoa viti 33 vya kubeba wagonjwa.
Akikabidhi msaada huo hivi karibuni Kaimu Mkurugenzi wa MUVIMA, Albert Chalamila alisema asasi yao imeguswa na kero mbalimbali zinazoikabili hospitali hiyo na kwa kuanzia ililazimika kutafuta viti hivyo kwa lengo la kusaidia hospitali hiyo yenye matatizo mbalimbali  yanayofifisha utoaji wa huduma bora za afya, zikiwemo zile za wajawazito na watoto,
Alisema kwa msaada wa asasi ya kimataifa ya Rafiki Surgical Mission ya Australia waliomba msaada huo baada kuomba msaada wa vitanda kwa ajili ya hospitali hiyo hivyo vitanda 23 vimekwishawasili bandari ya Dar es Salaam na tumeanza na viti vya kubeba wagonjwa.
Alisema Mkurugenzi Mkuu wa MUVIMA, Cosato Chumi anaendelea na utaratibu wa kuvitoa vitanda hivyo bandarini na mara baada ya shughuli hiyo kukamilika vitakavifdhiwa kwa uongozi wa hospitali hiyo.

Kaimu Mganga wa Hospitali ya Wilaya ya Mufindi, Dk Goodluck Mlimbila kwamba vitapunguza adha waliyokuwa wanapata watoa huduma wa hospitali hiyo ya kupokea na kubeba mikononi, wagonjwa wanaohitaji huduma hiyo.
 Akishukuru kwa msaada huo, Dk Mlimbila alisema hospitali hiyo ina upungufu mkubwa wa vifaa tiba na dawa na akalitaja eneo lenye tatizo zaidi kuwa ni lile la huduma kwa mjamzito na watoto.
Alisema katika kuboresha huduma za uzazi, jengo lenye uwezo wa kulaza wajawazito zaidi ya 100 na lenye chumba cha upasuaji na kile cha kuhifadhia watoto wanaozaliwa kabla ya muda lilijengwa katika hospitali hiyo ambayo awali ilikuwa ikitumia jengo lenye uwezo wa kuweka vitanda 27 tu.
Alisema msaada uliotolewa na MUVIMA una umuhimu mkubwa katika hospitali hiyo kwani utarahisisha huduma za ubebaji wagonjwa kutoka eneo moja hadi lingine na utapunguza idadi ya wajawazito wanaolala chini baada ya vitanda vilivyoahidiwa kuwasili.
Naye Katibu wa Afya wa wilaya hiyo, Atupakisye Mwakifamba aliwataka MUVIMA na wadau wengi kujitokeza kuzimaliza kero za utoaji huduma zinazoikabili hospitali hiyo na vituo vingine vingi vya huduma wilayani humo.
 Mwakifamba alisema pamoja na wilaya hiyo kuwa na idadi ya kuridhisha ya watoa huduma wenye ujuzi, inakabiliwa na upungufu mkubwa wa vifaa tiba, dawa na magari ya kubeba wagonjwa.

Friday, June 27, 2014

NGUMI KUPIGWA JUMAMOSI PUGU KIRUMBA ZULU PARADAISE


Bondia Jems Martn kushoto akitunishiana misuli na Hamza Mchanjo baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao wa jumamosi utakaofanyika katika ukumbi wa Zulu Paradaise uliopo Pugu Kirumba Road Picha na www.superdboxing coach.blogspot.com


Dr, Mohamed Hassani 'Bula' akimpima Afya bondia Twalibu Mchanjo baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano na Adamu Ngange jumamosi hii
Bondia Twalibu Mchanjo akipima uzito

MTEMVU AKAGUA MADHARA YA MOTO SOKO LA KEKO, ATOA POLE KWA WAATHIRIKA


 Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu akiingia eneo lililopata madhara kutokana na kuungua moto usiku wa kuamkia leo, katika soko la Keko, katika jimbo hilo jijini Dar es Salaam. Mtemvu amewapa pole walipoteza mali zao kutokana na moto huo ambao chanzo cha ke hakijajulikana.  Hadi inakisiwa imepatikana hasara ya zaidi ya sh. milioni 97.
 Naibu Katibu wa soko la Keko, Hassan Gitigi (kushoto) akimpa maelezo Mbunge wa Temeke Abbas Mtemvu kuhusu madhara yaliyosababishwa na moto huo
 Baadhi ya wafanyabiashara katrika soko hilo akieleza hasara walizopata. Wameeleza kwamba mbali na waliopata hasara ya kuunguliwa bidhaa na mabanda yaop ya biashara, pia wapo waliopata hasara kwa maduka na mabanda yaop ya biashara kuporwa na vibaka wakati wa tukio hilo la moto.
 Mtemvu akizungumza na waliopatwa na madhara kuhtokana na moto huo
Mtemvu akizungumza na baadhi ya viongozi waliofika kutoa pole kwa walipatwa na madhara kwenye soko hilo. Picha zote na Bashir Nkoromo,

SHIRIKA LA UTANGAZAJI LA TBC LAKABIDHIWA RASMI GARI LA KURUSHIA MATANGAZO NA SERIKALI YA CHINA



 Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara( wa pili kutoka kushoto) akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa matumizi ya Gari la kurushia matangazo la TBC, kutoka kulia ni Makamu Waziri wa Biashara wa Jamhuri ya watu wa China Li Jingzao, Makamu wa Rais wa China Li Yunchao  na wa mwisho kushoto ni Mkurugenzi wa TBC Bw. Clement Mshana
 Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara akikabidhiwa mfano wa Ufunguo wa gari la kurushia matangazo la TBC mara baada ya kuzinduliwa leo jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Waziri wa Biashara wa Jamhuri ya Watu wa China Li Jingzao.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara akimkabidhi zawadi ya Kinyago cha mnyama Twiga Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China Li Yunchao mara baada ya kuzindua gari la kurushia matangazo la TBC leo jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Mkurugenzi wa TBC Clement Mshana
 Gari la kisasa la kurushia matangazo ya moja kwa moja lililokabidhiwa kwa TBC likiwa katika viwanja vya Shirika hilo Mikocheni jijini Dar es Salaam.

Kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Sihaba Nkinga, Waziri wa Nchi ofisi ya Rais Utawala Bora Kapteni George Mkuchika na Mkurugenzi Mtendaji wa TBC Clement Mshana wakifuatilia mazungumzo baina ya Makumu wa Rais wa China Li Yunchao na Mwakilishi wa Startime (hawapo pichani) alipotembelea ofisi za Kampuni hiyo leo jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China Li Yunchao akiangalia picha zinazoonyesha vipindi vinavyorushwa na Startimes alipotembelea ofisi za Kampuni hiyo leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China Li Yunchao akisalimiana na baadhi ya Wafanyakazi wa Startimes na TBC mara baada ya kuwasili katika Viwanja vya Ofisi za Shirika la Taifa la Utangazaji (TBC) alipokuwa mgeni rasmi katika hafla ya Kukabidhi na kuzindua gari la kurushia matangazo (OB Van) leo jijini Dar es Salaam.Gari hilo limetolewa kwa Msaada wa Serikali ya China.Katikati ni Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wa Tanzania Dkt. Fenella Mukangara.
 Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara akijadiliana na jambo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Sihaba Nkinga, katikati ni Mwakilishi wa Kampuni ya Startimes Bw. Jack Zhou.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Sihaba Nkinga akimsikiliza kwa makini Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Assah Mwambene (katikati) wakati wa hafla ya makabidhiano na uzinduzi wa Gari la kisasa la kurushia matangazo ya moja kwa moja (OB Van) ambalo Serikali ya China ili kutoa msaada kwa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC). Kushoto ni Mkurugenzi wa TBC Bw. Clement Mshana.
 Msafara wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China Li Yunchao ukiwasili katika Viwanja vya Ofisi za Shirika la Taifa la Utangazaji (TBC) alipotembelea kwa ajili ya hafla ya Kukabidhi na kuzindua gari la kurushia matangazo (OB Van) lililotolewa kwa Msaada wa Serikali ya China jana jijini Dar es Salaam.