WASHINDI
wa Chemsha Bongo ya Brazil ambayo inadhaminiwa na Azam TV, Allen John
Muhuma na Said Mohammed Muba, wamekabidhiwa zawadi zao leo kwenye ofisi
za Global Publishers, Bamaga-Mwenge, Dar.
Washindi
hao ambao walifanikiwa kujibu ipasavyo maswali kwenye swali la Chemsha
Bongo lililokuwa kwenye magazeti ya Championi ya wiki iliyopita,
wamejishidia TV, dekoda ya Azam na dishi.
Wakizungumza
mara baada ya kukabidhiwa zawadi zao walisema kuwa hii ni faraja kubwa
sana kwao kwa kuwa wameweza kuboreshewa maisha yao na Championi. “Ukweli
hii ni faraja kubwa sana kwangu na familia yangu, nimejisikia vizuri
sana na kamwe sitaacha kushiriki kwenye kila toleo,” alisema Muba. Kwa
upande wake Muhuma, alisema awali aliamini kuwa kuna watu huwa
wanaandaliwa kwa ajili ya kushinda zawadi hizi.
“Hili
limenifanya niamini kuwa Chemsha Bongo hizi ni za kweli, nimefarijika
sana na niahidi kuwa nitashiriki kila siku na naamini nitashinda
tena.” Ukitaka kushiriki Chemsha Bongo hii jibu swali ambalo lipo kwenye
gazeti la Championi kisha tuma jibu lako kwenda namba 15564, hapo utakuwa umeingia moja kwa moja kama mshindani.
No comments :
Post a Comment