Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Sunday, November 30, 2014

TANZANIA 50 PLUS CAMPAIGN WATEMBELEA WAGOJWA WA SARATANI WALIOLAZWA HOSPITAL YA OCEAN ROAD



Mgeni rasma ambaye ni DR kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Amana DR. Natalius Kapilima akikata utepe kuashilia kugawa zawadi mbalimbali kwa wagojwa wa saratani waliolazwa katika hospital ya ocean road wengine kushoto ni Mkurugenzi wa TTCF. Lutgard Kagaruki na wa tatu kulia ni Mratibu wa kampeni ya manusura wa saratani ya Tezi Dume na Mwanzilishi wa Tanzania 50 Plus Campagn Dr Emanuel Kandusi
DR kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Amana DR. Natalius Kapilima kulia akimkabizi zawadi mgojwa wa saratani Idd Muhode ambaye amelazwa katika hospitali ya ocean road
Baadhi ya wadau mbalimbali wa kujitolea kutoka Tanzania 50 plus campaign wakiwa katika picvha ya pamoja baada ya kutoa misaada mbalimbali kwa wagojwa wa saratani katika hospital ya Ocean Road

DR kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Amana DR. Natalius Kapilima akipokea zawadi za wagojwa zilizoenda kugawiwa katika hospitali ta Ocean Road kutoka kwa
Mratibu wa kampeni ya manusura wa saratani ya Tezi Dume na Mwanzilishi wa Tanzania 50 Plus Campagn Dr Emanuel Kandusi mwingine ni
Mkurugenzi wa TTCF. Lutgard Kagaruki walipokwenda kutoa misaada mbalimbali kwa wagojwa
vitu mbalimbalio vikipakiwa kwenye mfuko kwa ajili ya kugawa kwa wagojwa
vifurushi vikiwa tayali kwa kugawiwa kwa wagojwa wa saratani katika hospitali ya ocean road


Mratibu wa kampeni ya manusura wa saratani ya Tezi Dume na Mwanzilishi wa Tanzania 50 Plus Campagn Dr Emanuel Kandusi kulia akimkabizi zawadi mgojwa Said Kassam aliyelazwa katika hospital ya Ocean Road

MSANII WA NIGERIA ATUWA NCHINI


 Msanii wa komedy kutoka Nigeria,Okopcha Bright Onyekere maarufu kama Basket Mouth (katikati) akiwa na Mkurugenzi wa Kampuni ya Vuvuzela Ltd, Evans Bukuku baada ya kumaliza mkutano wa waandishi wa Habari juzi Dar es Salaam. Msanii huyo alikuja nchini kufanya onesho maalum na wasanii wa komedy wa nchini mwishoni mwa wiki. Picha na Mpigapicha Wetu.
 Msanii wa komedy kutoka Nigeria,Okopcha Bright Onyekere maarufu kama Basket Mouth (kulia) akiwa na Mkurugenzi wa Kampuni ya Vuvuzela Ltd, Evans Bukuku baada ya kumaliza mkutano wa waandishi wa Habari juzi Dar es Salaam. Msanii huyo alikuja nchini kufanya onesho maalum na wasanii wa komedy wa nchini mwishoni mwa wiki. Picha na Mpigapicha Wetu.

DVD MPYA YA MANNY PACQUAIO VS CRIS ALGIERI SASA INAPATIKANA


DVD MPYA YA MASUMBWI AMBAYO WAMEPIGANA MACAU CHINA AMBAPO BONDIA MTANZANIA FADHILI MAJIHA ALICHEZA UTANGULIZI SASA ZINAPATIKANA UHURU NA MSIMBAZI KARIAKOO DAR ES SALAAM PIGA SIMU
0787406938  /  0754406938

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AIWAKILISHA TANZANIA KATIKA MKUTANO WA 3 WA WAKUU WA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI (EAC) KUHUSU MIUNDOMBINU JIJINI NAIROBI, KENYA




 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wa tatu kutoka (kushoto) Makamu wa Rais wa Kenya, William Ruto, (kushoto kwake) Makamu wa Rais kwanza wa Burundi, (kulia kwake) wakijumuika kwa pamoja na viongozi wengine wakionyesha Taarifa ya pamoja waliyoisaini kuhusu majadiliano ya kuimarisha Miundombinu kwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, katika mkutano wa 3 wa Wakuu wa Nchi za Afrika Mashariki (EAC) kuhusu Miundombinu, uliofanyika kwenye Ukumbi wa KICC, jijini Nairobi jana Novemba 29, 2014.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza katika mkutano wa 3 tatu wa wakuu wa Nchi za Afrika Mashariki (EAC) kuhusu miundombinu, uliofanyika katika ukumbi wa KICC jijini Nairobi jana.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisaini taarifa ya pamoja ya majadiliano ya kuimarisha Miundombinu kwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakati wa mkutano wa 3 wa Wakuu wa Nchi za Afrika Mashariki (EAC) kuhusu Miundombinu jijini Nairobi, Kenya jana.
 Baadhi ya washiri wa mkutano huyo kutoka nchini Tanzania......
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na baadhi ya viongozi wakati wakitoka kwenye Ukumbi wa mikutano wa KICC, baada ya kushiriki katika mkutano wa 3 wa Wakuu wa Nchi za Afrika Mashariki (EAC) kuhusu Miundombinu uliofanyika jijini Nairobu, Kenya jana.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wengine walioshiriki katika mkutano huo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifurahia jambo na Makamu wa Rais wa Kenya William Ruto na Waziri wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, wakati wakiondoka katika viwanja vya Ukumbi wa mikutano wa KICC, baada ya kushiriki kwenye mkutano wa 3 wa Wakuu wa Nchi za Afrika Mashariki (EAC) kuhusu Miundombinu, uliofanyika jijini Nairobi, Kenya jana.

Wednesday, November 26, 2014

KAMPUNI YA KONYAGI YANYAKUWA TUZO MBILI ZA ULIPAJI KODI BORA NCHINI



 Mkurugenzi wa Fedha wa TDL, Bwana Michael Brown (KUSHOTO) akipokea Ngao ya ushindi kwa TDL baada ya kuibuka mshindi wa kwanza kama Mlipa Kodi Bora katika kundi la Viwanda, na Naibu Waziri wa viwanda na Biashara Bw Kigoma malima ndie anaemkabidhi tuzo hiyo.  KONYAGI ilinyakuwa tuzo mbili za ulipaji kodi bora
 Waziri Kiongozi mstaafu Vuai Nahodha akimkabidhi Mkurugenzi wa Fedha wa kampuni ya TDL watengenezaji wa KONYAGI bw. Michael Brown Tuzo ya Mshindi wa Jumla ya Mlipa Kodi Bora katika hafla iliyofanyika hivi karibuni katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere Convention centre Wengine katika Picha ni Joseph Chibehe meneja mauzo na Edward Mashingia meneja wa Fedha.

 Mkurugenzi wa Fedha wa kampuni ya TDL watengenezaji wa KONYAGI bw. Michael Brown akiwa na tuzo aliyoipokea


 Maofisa mbalimbali wa makampuni mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kukabidhiwa tuzo za ulipaji kodi bora nchini
 Joseph Chibehe meneja mauzo wa kampuni ya KONYAGI kushoto akibadilishana mawazo na Ofisa wa TBL ambao nao walinyakuwa tuzo
Baadhi ya washiliki walionyakua tuzo za ulipaji kodi bora wakitoka ukumbini na tuzo zao

KONGAMANO LA 31 LA KISAYANSI LAENDELEA MJINI BAGAMOYO




DSC_0825
Maximilian Mapunda kutoka shirika la Afya Duniani (WHO-Country Officer) akiwasilisha mada kwenye kongamano hilo.

Na Andrew Chale, Bagamoyo
Pichani ni baadhi ya picha za matukio ya siku ya pili, jana Novemba 25 kwenye kongamano la Kisayansi la 31, '31th Annual Scientific Conference and Annual General Meeting'.. lililoandaliwa na Tanzania Public Health Association (TPHA).
Mkutano huo unafanyika mjini hapa Bagamoyo katika Ukumbi wa Stella Maris, Bagamoyo, Pwani Tanzania.
Kongamano hilo la kisayansi la 31, limeanza Novemba 24 linatarajia kuwa la siku tano na kutarajia kumalizika Novemba 28 ambapo wataalamu wa afya na wadau watajadilina mambo mbalimbali ya afya hapa nchini.
DSC_0830
Katibu Mtendaji wa TPHA Taifa, Dk. Oberlin Kisanga akiwasilisha mada maalum kwenye kongamano hilo.

KINANA AKAGUA MIRADI YA MAENDELEO NA KUZUNGUMZA NA WANANCHI NANYUMBU


 

2Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiponda mawe wakati aliposhiriki katika ujenzi wa Bwawa la maji linalojengwa katika kijiji cha Sengenya Mangaka wilayani Nanyumbu mkoani Mtwara akiwa katika ziara yake ya kikazi akikagua na kuhimiza utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 inayotekelezwa na serikali pamoja na wananchi kwa ujumla ikiwa ni pamoja na kuhimiza uhai wa chama cha Mapinduzi CCM, Katika ziara hiyo leo Kinana amefanya kazi mbalimbali pamoja na kufanya mikutano kadhaa akiwa ameongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-NANYUMBU-MTWARA) 3Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishirikiana na mafundi kupanga mawe katika ukingo wa bwawa hilo linalojengwa katika kijiji cha Sengenya Mangaka wilayani Nanyumbu.

KITUO CHA KIMATAIFA CHA MICHEZO KUJENGWA MSOGA MKOANI PWANI


Mratibu wa Uhurumarathon Innocent Melleck kulia akizungumza na waandishi habari jijini Dar Es Salaam juu ya Mbio za uhuru kuanzisha mpango wa kuzindua kituo cha michezo eneo la Msoga linalijulikana kwa jina la Jakaya Kikwete Uhuru Sport Accademy ambapo kituo hicho kitagarimu jumla ya shilingi 4.8Bil ambapo kitashirikisha jumla ya michezo kumi na moja na madarasa kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha sita,Kulia ni Katibu mkuu wa chama cha riadha Tanzania Selemani Nyambui.


WAKATI usajili kwa watu wanaotaka kushiriki mbio ndefu za Uhuru, maarufu kama Uhuru Marathon, zinazotarajiwa kufanyika Desemba 7, mwaka huu jijini Dar es Salaam ukiendelea kwa kasi kubwa waandaaji wa mbio hizo wamezindua mpango wa kujenga kituo cha michezo eneo la msoga Mkoani Pwani.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Katibu wa Kamati ya mbio hizo, Innocent Melleck alisema,kamati ya Uhuru Marathon imeona umuhimu wa kuanzisha kituo hicho ambapo jumla ya shilingi bil.4.8 zinatarajiwa kutumika katika kukamilisha mpango huo.
“Tunapenda kutangaza rasmi kwamba Uhuru Marathon imenunua shamba eneo la Msoga Mkoani Pwani lenye ukubwa wa ekari 25 kwa lengo la kujenga kituo kikubwa cha kukuza vipaji vya wanamichezo mbalimbali mkoani pwani eneo la msoga na kitajulikana kwa jina la Jakaya Kikwete Uhuru Sports Accademy na jumla ya michezo 11 itahusishwa katika mkakati huo.
Tunatarajia kumkabidhi mheshimiwa Rais Kikwete mpango huu wenye lengo la kuleta mafanikio makubwa ya michezo nchini ambapo watoto wenye vipaji watapata nafasi ya kusoma na kukuzwa katika utaratibu wa michezo na tunaamini kuwa baada ya miaka mitano hadi kumi tutaweza kuanza kupata mafanikio.
Kituo hiki ndicho kituo pekee katika ukanda wan chi za Afrika Mashariki na Kati ambapo jumla ya wanamichezo 2300 wataweza kuwa katika mpango wa awali.
Tunatarajia kupata nguvu toka katika wahisani mbalimbali wa ndani na nje ya nchi kwa kuwa wapo wanaohitaji kuona Tanzania ikipata mafanikio kupitia michezo.
Wakati huo huo zaidi ya wakimbiaji 2700 wameshachukua fomu kwaajili ya kushiriki mbio za mwaka huu huku malengo makuu yakiwa ni kuhitaji kushirikisha zaidi ya wakimbiaji 15,000.

Vituo vitakavyokuwa vikiuza fomu za ushiriki ni Tripple seven Mikocheni, Maduka ya TSN na Uchumi Supermarket,  Uwanja wa Leaderds Club,Ofisi za RT Taifa,Stendi kuu ya mabasi Moshi Mjini, Arusha pia kwa kutumia tovuti ya www.uhurumarathon.com

Friday, November 21, 2014

MAMIA WAMUAGA MWANDISHI WA HABARI WA NEW HABARI 2006 LTD, MAREHEMU INOCENT MUNYUKU


Baadhi ya waombolezaji wakiwa wamebeba jeneza lililokuwa na mwili wa Mwandishi wa Habari za Michezo wa Kampuni ya New Habari 2006 Ltd marehemu Inocent Munyuku wakati wa kuaga mwili katika hospitali ya Lugalo jijini Dar es Salaam leo.
 Baadhi ya waombolezaji wakiwa wamebeba jeneza lililokuwa na mwili wa Mwandishi wa Habari za Michezo wa Kampuni ya New Habari 2006 Ltd marehemu Inocent Munyuku wakati wa kuaga mwili katika hospitali ya Lugalo jijini Dar es Salaam leo.
 Matinyi akisoma wasifu wa marehemu.
  Katibu Mkuu wa Taswa, Amir Mhando akitoa salama za rambirambi.
 Mhariri Mtendaji Mkuu wa New Habari 2006 Ltd, Absalom Kibanda akitoa salam za rambirambi.

MBUNGE WA JIMBO LA MOROGORO MJINI AENDELEA KUTEKELEZA ILANI YA CCM


 Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood akiongea ofisini kwake wakati akikabidhi Vifaa mbalimbali kwa wananchi wa Jimbo la Morogoro Mjini Ikiwa ni Utekelezaji wa Ahadi zake alizotoa Kipindi Akiomba kura ya Kuwa Mbunge wa Jimbo Hilo Pamoja za Ahadi anazotoa kwenye Mfululizo wa Ziara zake anazofanya Mara kwa mara katika Kata Mbalimbali za Jimbo la Morogoro Mjini.
 Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Azizi Abood akikabidhi Mbao kwa Viongozi wa Msikiti kwajili ya Kumalizia ujenzi wa Msikiti ikiwa ni ahadi aliyoitoa wakati wa ziara zake za mara kwa mara.

Laila Ali 'She Bee Stingin'' BONDIA PEKEE WA KIKE ALIYECHUKUA KIWANGO CHA JUU CHA FEDHA KATIKA WANAMASUMBWI


Laila Ali Curtis Conway Curtis Jr.
Leila ali akiwa na mumewe Curtis Conway pamoja na mtoto wao
Kwa sasa unakadiriwa pia utajiri wake unafikia kiasi cha dola za kimarekani milioni kumi ambazo ni zaidi ya fedha za kitanzania bilioni 16, ambazo ambazo amezitengeneza kutoka katika mchezo wa masumbwi duniani,

Matangazo ya bihashara, pamoja na kazi ya uwanamitindo 
Kutokana na umaarufu wake katika masumbwi , alijikuta akipata mikataba mbalimbali mikubwa ya matangazo ya biashara  katika makampuni na maduka makubwa Duniani, kama maduka ya kuuza vyakula,nguo na vifaa vya michezo hali iliyompatia nafasi ya kujiongezea kipato chake kwa haraka  leila alianza kujihusisha na masumbwi akiwa na umri wa miaka 15, huku msaada wake mkubwa ukitokea kwa baba yake mzazi ambapo baada ya kuonesha uwezo wake kwa mda mfupi arianza kuingia kwenye mapambano ya kimataifa 



Baada ya kupata ubingwa huo mwaka 2005 aliweza kutoa ubingwa mwingine unaotambuliwa na Shirikisho la Kimataifa la ngumi za wanawake ' IWBF kwa kumtwanga Nikki Eplion kwa K,O ya raundi ya nne katika uzito wa female super middleweight title 

Pamoja na uwezo huo, Wapo baadhi ya mabondia wa kike kama Vonda Ward, Leatitia, Robinson na Ann Wolfe wamekuwa wakilalamika kuwa Leila anawakwepa kwa kupangiwa vibonde na kuhofia kupigwa.

Licha ya kufanya vizuri kwenye mchezo wa masumbwi, mitindo na matangazo ya biashara kwenye runinga lakini mara kadhaa amekua akialikwa kwenye vituo mbalimbali vya runinga kwa ajili ya vipindi hali inayomfanya kukusanya kiasi kikubwa cha fedha 

Baadhi ya vipindi hivyo maarufu ni pamoja na agaeorgr Lpez, Dancing with the Stars, American Gladiators,Celebrity Family. The Early Show

Katika historia ya  maisha yake ya ndoa ,leila amesha olewa mara mbili ambapo kwa mara ya kwanza aliolewa na Johnny Mcclain Agost 27,2000,ambaye walikutana kwenye sharehe ya kuzaliwa baba yake mzazi Mohamed Ali wakati anatimiza umri wa miaka 57.

Kabla ya kuoanaMacClain ndiye aliyekuwa promota wake katika michezo ya ngumi za kulipwa jambo ambalo lilimsaidia kufanya vizuri katika mapambano yake yote ambayo ajapigwa wala kutoa droo ata mpambano mmoja akiwa na alama won 24 (KO 21) + lost 0 (KO 0) + drawn 0 = 24  

Baada ya kuoana mwaka 2000 walikuja kuhachana mwaka 2005. mwaka 2007, leila alifunga ndoa na Curtis Conway , ikiwa ni ndoa yake ya pili . wadadisi wa mambo ya kimapenzi wanaeleza kuwa kilichomfanya kuolewa tena ni kutokana na kuwa na mvuto wa kimapenzi alionao mwana dada huyo maili awapo ulingoni,

Leila amefanikiwa kupata watoto watatu akiwa na McClain ambao ni Leilani,Cameron na Kelton. Baada ya kuolewa tena alipata watoto wawili ambao ni Curtis Muhame Conway Aliyezaliwa mwaka 2008 na Sydney  mwaka 2011

Kwa sasa leila amestafu kucheza mchezo wa masumbwi tangu acheze mchezo wake wa mwisho Tareha 3 -2-2007  na Gwendolyn O'Neil na kufanikiwa kumpiga kwa K,O raundi ya kwanza na kutangazwa kuwa bingwa wa mikata miwili ya WBC female super middleweight title
WIBA Women's International Boxing Association super middleweight title
Ingawa kazi kubwa anayofanya kwa sasa ni kutangaza vipindi mbalimbali kwenye television pamoja na mitindo 
Moja ya mambo ambayo yalishangaza ulimwengu katika fani ya mitindo mwaka 2012 akiwa na mimba ya miezi 9, aliweza kushiriki kikamilifu katika maonesho ya mavadhi aliweza kuonesha umahiri wake kwenye jukwaa kwa kupita akiwa kwenye tamasha la mavazi lililofanyika jijini London Nchini Uingereza Novemba 20, 2012

Amestaafu akiwa na rekodi ya kutopigwa ata mchezo mmoja ambapo alicheza michezo  24 alishinda kwa  KO 21 ambapo mabondia watatu pekee ndio aliwashinda kwa point 
huyo ndio leila Muhamed Ali
kwa mahitaji ya DVD ZAKE KWA AJILI YA KUONA MAPAMBANO YAKE MBALIMBALI LIVE TUWASILIANE KUPITIA


Leila ali akiwa na mumewe Curtis Conway pamoja na mtoto wao

MDAU ASIA KINJENGA HAPATA DIGRII YA ELIMU YA JAMII SOSHIOLOJIA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM


Asia Kinjenga kulia akiwa na nyuso ya furaha pamoja na mwenzie Felician Francis baada ya kumaliza digrii ya elimu ya jamii katika sosholojia wakati wa mahafali ya 48 ya chuo kikuu cha Dar es salaam hivi karibuni
Asia Kinjenga wa pili kulia akiwa na wahitimu wenzie wa mahafali ya 48 katika chuo kikuu cha Dar es salaam
Asia Kinjenga
Asia Kinjenga akiwa na familia yake


Asia Kinjenga kulia akipongezwa kwa kuvalishwa shada la mauwa na mama yake mzazi Bi, Anchimole Lutengano
wakati wa mahafali ya 48 ya chuo kikuu cha Dar es salaam hivi karibuni ambapo alipata digrii ya elimu ya jamii katika soshiolojia
Asia Kinjenga katikati akiwa na mama yake mzazi Anchimole Lutengano kulia na bibi yake wakati wa mahafali ya 48 ya chuo kikuu cha Dar es salaam hivi karibuni ambapo alipata digrii ya elimu ya jamii katika soshiolojia

MAADHIMISHO YA SIKU YA UKIMWI DUNIANI KUFANYIKA KITAIFA MKOANI NJOMBE


Mwenyekiti Mtendaji wa Tume ya Taifa ya kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS) , Dkt. Fatma Mrisho akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu Kauli Mbiu ya Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani isemayo, Tanzania Bila Maambukizi Mapya ya VVU, Vifo vitokanavyo na Ukimwi na Ubaguzi na Unyanyapaa inawezekana inayolenga kupunguza maambukizi Mapya ya Ukimwi, kupunguza vifo vitokanavyo na Ukimwi na kukomesha vitendo vya unyanyapaa kwa asilimia Sifuri. 
Mkurugenzi wa ufuatiliaji wa Tathmini wa Ofisi ya Taifa ya kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS) Dkt. Jerome Kamwela akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu utoaji wa huduma na upatikanaji wa dawa za kufubaza makali ya Virusi vya Ukimwi kwa watu wanaoishi na VVU katika maeneo mbalimbali nchini.
Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa TACAIDS akiwaonesha waandishi wa habari (hawapo pichani) mbinu na elimu inayotolewa na TACAIDS katika maeneo mbalimbali ikiwemo matumizi ya mipira ya kike kwa wanawake ili kuzuia maambukizi mapya ya VVU. Picha na Aron Msigwa - MAELEZO
Maadhimisho ya siku ya UKIMWI Duniani kwa mwaka 2014 kitaifa yanatarajiwa kufanyika mkoani Njombe kuanzia tarehe 24 mwezi huu hadi tarehe  moja  Desemba.
Hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Taifa ya kudhibiti UKIMWI (TACAIDS) Dkt. Fatma Mrisho wakati akiongea na waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano uliopo makao makuu ya tume hiyo jijini Dar es Salaam.
Dkt. Mrisho amesema kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni “Tanzania bila maambukizo mapya ya Virusi Vya Ukimwi (VVU), Vifo vitokanavyo na UKIMWI, Ubaguzi na unyanyapaa inawezekana.
“Kauli mbiu hii inalenga kutoa msukumo wa utekelezaji wa mikakati mbalimbali ya kudhibiti UKIMWI kitaifa na kimataifa ili kufikia azma ya sifuri tatu zinazomaanisha maambukizi mapya sifuri, vifo vitokanavyo na UKIMWI sifuri na unyanyapaa sifuri ifikapo mwaka 2018”.
Kauli mbiu hii pia inahimiza utekelezaji wa dhati wa malengo ya Maendeleo ya Milenia na maazimio yaliyowekwa kwenye mkutano maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu UKIMWI uliofanyika mwaka 2001 nchini Marekani”, alisema Dkt. Mrisho.
Amesema kipaumbele cha maadhimisho ya mwaka huu ni upimaji wa hiari wa VVU na ushauri nasaha, na kutoa  wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi ili wapate huduma hii muhimu.
Aidha Mkurugenzi huyo amewataka wananchi kuadhimisha siku hiyo kwa njia ya makongamano, kumbukumbu za waliofariki kwa UKIMWI, midahalo, mikutano ya wazi, vipindi kupitia vyombo vya habari, kutembelea na kutoa misaada kwa watoto yatima na wanaougua ugonjwa huo  na kutoa elimu inayohusu kujikinga na maambukizi.
Akizungumzia kuhusu upatikanaji wa dawa za kupunguza makali ya ugonjwa wa UKIMWI Mkurugenzi wa Sera, Mipango na Utafiti wa TACAIDS Dkt. Raphael Kalinga amesema dawa hizo hutolewa  bila malipo kwa wahitaji wanaostahili kuzipata hii ni kulingana na mfumo wa utoaji kwa wahitaji.
Na Beatrice Lyimo na Aron Msigwa- MAELEZO