Bondia Idd Mkwera baada ya kupoteza mpambano wake wa nje uliofanyika Riga Ratvia kwa point bondia huyo sasa amesaini mkataba wa kuzipiga na bondia machachari Ramadhani Shauri mpambano wa raundi 10 utakaofanyika Mei 5 katika uwanja wa ndani wa Taifa
akizungumza wakati wa utaiaji saini uho Mkwera amesema kuwa yeye anachojua ngumi ndio kazi yake hivyo kwake kazi ni kazi tu aijalishi anacheza na nani hivyo kuwataka wapenzi wa mchezo wa masumbwi kuja kushudia mpambano uho wa masumbwi siku hiyo
akijibu mapigo Shauri amesema wapenzi wangu na mashabiki zangu mmenikosa tangu mwaka jana nilivyopoteza kwa pointi katika uwanja ule ule sasa nilitoka kidogo nje ya Tanzania hivyo nimerudi na kasi mpya nguvu mpya njoeni mshidie ngumi zinavyopigwa
Nae Promota wa mchezo huo Evalist Ernest alisisitiza kwa kusema mabondia hawa watacheza mpambano wa raundi 10 katika uzito wa kg 62.5 hivyo muje mushudie masumbwi siku hiyo mbali na mpambano uho siku hiyo kutakuwa na mapambano mbalimbali ya ngumi kwa vijana tulio wasainisha
siku hiyo bondia Haidari Mchanjo atazichapa na Amani Bariki 'Manny Chuga' wakati Karimu Ramadhani atakumbana na Jerms Kibazange na Said Chini ataoneshana umwamba na Hamza Mchanjo
Mapambano hayo na mengine yote yatakuwa wakisindikiza pambano kuu kati ya Idd Mkwera na Ramadhani Shauri watakaozipiga Raundi kumi
siku hiyo pia kutakuwa zikiuzwa DVD mpya za masumbwi ambazo zinaonesha mafunzo mbalimbali ya mchezo wa ngumi yanavyoanza hatua kwa hatua
mpaka kujua kitu kamili katika
mchezo huo pia kunakuwa na mapambano ya mabondia mabigwa wa dunia wa mchezo huo kama Floyd
Maywether, Manny Paquaio,mike Tyson, Mohamed Alli pamoja na mabambano ya ngumi ya ndani
Promota wa mpambano wa ngumi Evalist Ernest katikati akiwainua mikono juu mabondia Iddi Mkwera kushoto na Ramadhani Shauri baada ya kusaini mkataba wa kuzipiga Mei 5 katika ukumbi wa Uwanja wa ndani wa Taifa mpambano wa raundi kumi Picha na SUPER D BOXING NEWS |
No comments :
Post a Comment