Na Mwandishi Wetu
BONDIA Vicent Mbilinyi baada ya kukuu benchi mwaka mzima kwa kukimbiwa na kuogopewa na wambinzani wake mbalimbali katika uzito wake sasa amerudi tena kwa kasi ya ajabu baada ya mwanzo wa mwezi mei kumtwanga bila ya huruma bondia Hussein Shemdoe na kufanya taaruki kwa mashabiki waliojitokeza kwa kumshangilia
Mbilinyi ambae ni bingwa wa kg 61.5 amekuwa akikimbiwa na wapinzani wake waliopo katika renki moja baada ya kuona vipondo anavyowapa wapinzani wake awapo ulingoni baada ya ushindi uho mbilinyi alijinasabu kwa kusema sasa kazi kazi kwani mabondia wengi kwenye uzito wangu wamekuwa wakinikimbia wali sijui sababu za wao kunifanyia hivyo
kwani kama ngumi ni zile zile tunacheza wote ila sio kesi sasa nipo tayali kucheza na yoyote atakaejitokeza kwa sasa kwani mabondia wengi wanachaguana na awana viwango vya juu kama nilivyo mimi
Mbilinyi katika uzito wake anashika nafasi ya tatu katika mabondia 69 wa Tanzania na ni wa 300 duniani katika uzito wake kwa mabondia 1,949
kwa Tanzania katika uzito wa Lightweight namba moja kwa sasa ni Benson Nyilawila wa pili Mohammed Kambuluta
hata hivyo Mbilinyi anamtamana sana kupambana na Benson Nyilawila ili amuondoe pale alipo akae yeye Nyilawila anaefanya shughuli zake mkoa wa mbeya anaonekana kushinda mapambano yake yote 10 kwa K,O ndio mana amekuwa juu mapambano yote akichezea uko uko mkoani Mbeya
Mbilinyi ambae yupo katika kambi moja na Mabondia Idd Mkwela, Mohamedi Muhunzi, Shomari Milundi, Ibrahimu Class, Kelvin Majiba na wengine walio chini ya kocha wa Kimataifa wa mchezo wa masumbwi Nchini Rajabu Mhamila 'Super D
ambaye amewafanya wavume mabondia hawo na kuwa moto wa kuotea mbali kwani mabondia hawo wana nguvu na spidi ya ajabu kwa mazoezi wanayopewa na kocha wao
Mabondia wote wapo katika mazoezi wakati wote kwa ajili ya mapambano yatakayo wakabili popote Duniani
No comments :
Post a Comment