Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Wednesday, June 19, 2013

Shindano la Epiq Bongo Star Search 2013 lazinduliwa leo




 Ofisa Biashara Mkuu wa Zantel, Sajid Khan ambao ndio wadhamini wakuu wa shindano la Epiq Bongo Star Search 2013, akifafanua jambo wsakati wa uzinduzi wa shindano hilo. (Picha zote Habari Mseto Blog)
Mshindi wa shindano la Epiq Bongo Star Search 2012, Walter Chilambo akizungumza na waandishi habari jijini Dar es Salaam. 
 Mshindi wa shindano la Epiq Bongo Star Search 2012, Walter Chilambo (katikati) akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa BenchMark Production Rita Poulsen na Ofisa Biashara Mkuu wa Zantel, Sajid Khan.
Mkurugenzi Mtendaji wa BenchMark Production Rita Poulsen akifafanua jambo wakati wa uzinduzi wa shindano la Epiq Bongo Star Search jijini Dar es Salaam leo.

DAR ES SALAAM, Tanzania
SHINDANO la Epiq Bongo Star Search linatarajia kuanza kutimua vumbi Juni 29 mwaka huu huku likiwashilikisha wadau wakubwa wa muziki hapa nchini kwa lengo la kuwajenga washiriki kwa kuwapa ujuzi zaidi utakaowasaidia kukua kimuziki.

Akizungumza katika makao makuu ya Kampuni ya simu za Mkononi ya Zantel ambao ni wadhamini wakuu wa shindano hilo, Mkurugenzi Mtendaji wa BenchMark Production Rita Poulsen alisema, shindano hilo linatarajiwa kufanyika usajili katika Mikoa Sita ambayo ni Mwanza, Mbeya, Arusha, Zanzibar, Dodoma na Dar es Salaam.

Rita alisema, Mwaka huu kauli mbiu ‘Kamua’ na kudai kuwa wamejipanga kuwafikia vijana wengi hapa nchini, na pia kutengeneza nyota wengi wa muziki mbali na mshindi na kudai kuwa wataanzia Mkoani Dodoma Juni 29-30, katika ukumbi wa Maisha klabu, Julai 5-6 Zanziba Hotel ya Bwawani, Mbeya Julai 10-11 Klabu Vybes, Mwanza Julai 14-15 Klabu Fassion, Arusha Julai 20-21 Tripple A na kumalizia Dar es Salaam Julai 26-28 uwanja wa Taifa.

Naye Ofisa Biashara Mkuu wa Zantel, Sajid Khan alisema, Zantel wanajivunia kufanya kitu kikubwa kama hiki ambacho kinawapatia vijana ajila, na kudai kuwa, wanatarajia kufungua laini ya kurekodi kwa simu kuanzia siku ya kwanza ya usaili Mikoani ambapo washiriki watapiga namba 0901551000 au kutuma neno Kamua kwenda 15530.

Epiq BSS, imekuwa ikiwatoa vijana katika hali ya umasiki na kuwapa ajili kama ilivyo kwa wasanii kama Kala Jeremaya ambaye anatikisa katika muziki wa Hiphop pamoja na Walter Chilambo aliyetwaa taji hilo mwaka jana.

TABORA WAPATA BINGWA WA MASHINDANO YA BALIMI NGOMA


:



Kushoto meneja wa matukio wa kampuni ya Bia Tanzania - tbl kanda ya ziwa  Bwana Erick Mwayela akimkabidhi Meya wa Manispaa ya Tabora Mstahiki Meya Gulamhussein Remtullah kitita cha shilingi laki sita ikiwa ni zawadi ya mshindi wa kwanza wa mashindano ya Ngoma za asili kwa mkoa wa Tabora mashindano hayo yamedhaminiwa na kampuni ya Bia Tanzania kupitia Bia yake ya Balimi Extra kulia aliyevaa fulani ya balimi ni kiongozi wa kundi la Mwenge la manispaa hiyo ambao ndio wameibuka washindi wa shindano hilo.
  Mgeni rasmi katika mashindano ya ngoma za asili kwa Mkoa wa Tabora Mstahiki Meya wa manispaa ya Tabora Gulamhussein Remtullah akizungumza na wakazi wa Mkoa huo katika mashindano hayo chini ya udhamini wa kampuni ya Bia Tanzania kupitia bia yake ya Balimi Extra , mashindano hayo yamefanyika katika shule ya sekondari Iyungi

BAKWATA v/s ISTIQAAMA ZATOKA SARE, SHEIKH MKUU WA MKOA WA DAR, AL-HAD MUSSA, NYOTA WA MCHEZO




 Mshambuliaji na Nahodha wa timu ya Bakwata, Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Al-had Mussa Salum (kulia) akimtoka beki wa timu pinzani ya Istiqaama ya Dar es Salaam, wakati wa mchezo wa kirafiki uliochezwa kwenye Uwanja wa Dar es Salaam Zuu, Kigamboni jijini mwishoni mwa wiki iliyopita. Katika mchezo huo timu hizo zilitoka sare ya 1-1.
 Kamanda kwa Polisi wa Kanda maalum, Suleiman Kova, akizungumza na waandishi wa habari wakati wa utambulisho wa mchezo huo mwishoni mwa wiki.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mecky Sadick, akimkabidhi Jezi, Nahodha wa timu ya Bakwata, Sheikh Al-had Mussa, wakati wa hafla ya kukabidhiwa vifaa vya michezo kwa ajili ya mchezo huo wa kirafiki uliochezwa mwishoni mwa wiki iliyopita. Katikati ni Nahodha wa timu ya Istiqaama, Saleh Omar Saleh.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mecky Sadick, akimkabidhi Jezi, Nahodha wa timu ya Istiqaama, Saleh Omar Saleh, wakati wa hafla ya kukabidhiwa vifaa vya michezo kwa ajili ya mchezo huo wa kirafiki uliochezwa mwishoni mwa wiki iliyopita. Kushoto ni Nahodha wa timu ya Bakwata,  Sheikh Al-had Mussa,
 Sheikh Al-had Mussa, akionyesha umahiri wake wa kuchezea soka.
 Kikoso cha timu ya Bakwata




 Mwenyekiti wa Mfuko wa Sikoseli Tanzania, Grace Rubambey (katikati) akizungumza wakati wa maadhimisho ya Siku ya ugonjwa wa  Sikoseli Duniani jijini Dar es Salaam leo. Wengine kutoka kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Mfuko huo, Dk Julie Makani,  Balozi wa Canada nchini, Alexandre Leveque na mmoja wa watu wanoishi na ugonjwa huo, Arafa Salim Said.
  Balozi wa Canada nchini, Alexandre Leveque (katikati) akizungumza wakati wa maadhimisho ya Siku ya ugonjwa wa Sikoseli Duniani jijini Dar es Salaam leo. Wengine kutoka kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Mfuko wa Sikoseli Tanzania Dk Julie Makani na Mwenyekiti wa mfuko huo, Grace Rubambey na mmoja wa watu wanoishi na ugonjwa huo, Arafa Salim Said.
  Makamu Mwenyekiti wa Mfuko wa Sikoseli Tanzania, Dk Julie Makani (kushoto) akizungumza wakati wa maadhimisho ya Siku ya ugonjwa wa Sikoseli Duniani jijini Dar es Salaam leo. Tanzania ni nchi ya nne duniani kwa kuwa na idadi kubwa ya watu wanaougua ugonjwa wa sikoseli.
   Meneja wa Benki ya KCB Tawi la Msimbazi, Philipo Pilla (kulia) akizungumza wakati wa maadhjimisho hayo. Benki ya KCB ni mmoja wa wadhamini wa Mfuko wa Sikoseli Tanzania.
 Mratibu wa Huduma za Ugonjwa wa sikoseli katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Dk. Deogratias Soka (kulia) akizungumza kuhusu hali ya ugonjwa huo katika hospitali hiyo katika maadhimisho hayo. Inakadiriwa kuwa katika ya watoto 8,000 hadi 10,000 kuzaliwa na ugonjwa huo nchini Tanzania kila mwaka.
Baadhi wa watu walioshiriki maadhimisho jijini Dar es Salaam leo. Ugonjwa wa sikoseli ni ugonjwa wa kurithi unaosababisha mabadiliko yasiyo ya kawaida katika chembechembe nyekundu za damu hivyo mtu hawezi kuambukizwa kwa njia yoyote ile kama vile kuishi au kuwa karibu na mgonjwa wa sikoseli.

MASHINDANO YA TIKA CUP 2013 YAANZA KUTIMUA VUMBI JUNI 6 VIWANJA VYA SHUJAA NA KILAKALA MAKABURINI MORO.




Mshambuliaji wa timu ya soka ya kata ya Kauzeni, Juma Bangule kushoto akimiliki mpira dhidi ya mlinzi wa timu ya kata ya KongaSufian Dikongola wakati wa mashindano ya TIKA CUP 2013 katika michezo. PICHA JUMAMTANDA.BLOGSPOT.COM
Mshambuliaji wa timu ya soka ya kata ya Kauzeni Omari Kaeza (katikati) akiwatoka wachezaji wa kata ya Kong

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA MKUTANO MKUU WA MWAKA WA SIKU 4 WA MAWAKALA WA USAFIRISHAJI WA MAJINI KWA NCHI ZA MASHARIKI YA KATI KWA AFRIKA JIJINI DAR




 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati akifungua rasmi Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Mawakala wa Usafirishaji wa Majini kwa nchi za Mashariki ya Kati kwa Afrika, uliaoanza jijini Dar es Salaam leo Juni 19, 2013 unaofanyika kwa siku nne
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Waziri wa Uchukuzi, Dkt. Harrison Mwakyembe, wakati alipowasili kwenye Hoteli ya Double Tree, kwa ajili ya kufungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Mawakala wa Usafirishaji wa Majini kwa nchi za Mashariki ya Kati kwa Afrika, uliaoanza jijini Dar es Salaam leo Juni 19, 2013 unaofanyika kwa siku nne.
  Baadhi ya washiriki wa mkutano huo wakimsikiliza Mheshimiwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati akisoma hotuba yake ya ufunguzi rasmi wa mkutano huo.
  Baadhi ya washiriki wa mkutano huo wakimsikiliza Mheshimiwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati akisoma hotuba yake ya ufunguzi rasmi wa mkutano huo.
 Rais wa FIATA, Stanley Lim, akizungumza wakati waka wa ufunguzi wa kutano huo.

 Waziri wa Uchukuzi, Dkt. Harrison Mwakyembe, akizungumza kabla ya kumkaribisha Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal, kufungua mkutano huo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Waziri wa Uchukuzi, Dkt. Harrison Mwakyembe,wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa mkutano huo.

SHIWATA WAKUTANA NA VIONGOZI WAKUU WA MKURANGA



Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Bi. Mercy Silla (kulia) akizungumza na Mwenyekiti wa Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) baada ya ujumbe huo kumtaarifu kuhusu tamasha la Wasanii litakalofanyika Juni 29, 2013, Mkuranga.
Mwenyekiti wa Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA), Caasim Taalib akikaribishwa ofisini na Ofisa Utamaduni Utamaduni wa Wilaya ya Mkuranga, Bw. Lucas Kamwavah alipokwenda kuomba kibali cha Tamasha la Mastaa Chipukizi litakalofanyika kijiji cha wasanii Mwanzega, Mkuranga Juni 29 mwaka huu.

Tuesday, June 18, 2013

'YOHANA MTAKATIFU' KUZIPIGA MANZESE







Kwa mara nyingine limeandaliwa pambano la ngumi  aina yake ni kati ya mabondia wakimya na wapole usoni  na wasiopenda kabisa kuongeaYohana Robert  aliekuwa bondia wa taifa na mkongwe katika masumbwi atakapopigana na Yohana Mathayo katika ukumbi wa friends corner manzese siku ya jumapili  tarehe 30 mwezi huu.

Pambano hilo linakuwa la kiana yake kwa sababu ya sifa za hao mabondia kuwa  ni wacha mungu wazuri kiasi cha yohana Robert  kuitwa  na wapenzi wa masumbwi “mtakatifu  ngumi jiwe” ni mtu mwenye ngumi mojamoja ambazo ni nzito sana  na hatari kwa mpinzani  nae bondia Yohana Mathayo wapenzi  humwita  “Tembo mtoto”  kutokana na umbo lake kubwa, pia humwita “Yohana mbatizaji” kwani mara nyingi huwaachisha ngumi wapinzani  wake kwa kipigo au kubadilisha majina yao, mathayo ana ngumi kali za kuvizia, hutulia muda mrefu na akiachia ngumi moja ikikupata vizuri mchezo umekwisha ni mtaalamu wa kuvizia.

Pambano hili limeandaliwa na mwalimu Hatibu ambae ni mdau wa karibu wa ngumi na tunaliita pambano la aina yake kwa mabondia wote kufanana majina na matendo na huwa na tabia ya kubeba na kusoma biblia kabla na baada ya pambano ni wapole watulivu lakini ni watu hatari sana ulingoni na lolote laweza tokea wanapocheza.

 Pambano hilo ambalo litasimamiwa na PST  chini ya Anthony ruta na mapambano ya utangulizi kuratibiwa na Ibrahim kamwe bigright.

 Mwalimu Hatibu anaripoti ya  kuwa maandalizi yanakwenda vizuri  vibali vyote tayari na mabondia watakaowasindikiza kina  Yohana  na mikataba yao imekwisha kamilika ni Fabian lyimo ambae pambano la mwisho alifanya vizuri Indonesia  atazipiga na  musa sunga nae Bakari ustadh atazipiga na frank zagarino, wakati huohuo Tasha mjuaji na Rama johncena watatoana jasho.

 Pia Yule bingwa wa PST uzito mdogo (minimum weight) goldsilver anaumana vikali na herman Richard. Nae Ibrahim kamwe anathibitisha hilo na linaweza kuwa pambano kali sana la vunja jungu ambalo halijawahi kutokea kutokana na sifa za mabondia hao.
 IBRAHIM KAMWE
+255 -713 / 767 / 784 - 501991
kamwe@hotmail.com

FOMU ZA UONGOZI BFT ZADODA






Na Elizabeth John
WADAU wa Shirikisho la Ngumi za Ridhaa Tanzania (BFT) wameshauriwa kujitokeza kuchukua fomu za kuwania nafasi mbali mbali za uongozi wa chama hicho baada ya viongozi waliopo madarakani kumaliza muda wao.

Hadi jana hakuna mgombea aliyejitokeza kuchua fomu za ugombea katika chama hicho ambapo zilianza kutolewa Juni 4 mwaka huu katika Ofisi za Baraza la Michezo la Taifa (BMT) jijini Dar es Salaam.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Ofisa Michezo wa BMT, Benson Chacha alisema hadi jana hakuna mwanachama yeyote aliyejitokeza kuchukua wala kuulizia fomu za kuwania uongozi katika chama hicho kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Julai 7 jijini Mwanza . 

Alisema usaili kwa wagombea ambao watajitokeza kuwania nafasi za uongozi utafanyika Julai 5 kabla ya kuanza kwa taratibu za uchaguzi wa chama hicho ambapo wanachama na wadau mbalimbali watashiriki uchaguzi huo.

“Nawaomba wadau wajitokeze kuwania nafasi za uongozi pamoja na kushiriki uchaguzi ili baadae wasije kulalamika maana hii ni fursa pekee kwao wanapaswa kuitumia,” alisema Chacha.

Fomu zinazotolewa ni kwa nafasi ya Rais, Makamu, Katibu Mkuu, Mweka Hazina na wajumbe tisa na gharama za fomu hizo kwa  nafasi ya Rais sh 150,000, Makamu, Katibu Mkuu, Mweka Hazina ni sh 100,000 na 50,000 kwa wajumbe.

TENISI KUCHAGUANA JUNI 22





Na Elizabeth John
WAKATI zoezi la kuchukua na kurudisha fomu za kugombea uongozi wa Chama Cha Tenisi Tanzania (TTA), lilifika tamati tarehe Juni 17, Mwenyekiti anayemaliza muda wake, Denis Makoi amechukua fomu ya kutetea kiti hicho.

Wagombea 14 wamejitokeza kuwania nafasi mbalimbali za uongozi katika chama hicho na ucahaguzi mkuu unatarajiwa kufanyika Juni 22 jijini Dar es Salaaam.


Kwa mujibu wa Ofisa Michezo wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Benson Chacha, wagombea wengine waliochukua fomu ni Mtangazaji wa Magic FM, Fina Mango na Mathisut Sele Mbajo ambao pia wanawania Uwenyekiti wa chama hicho.


Alisema wagombea wengine waliojitokeza kuchukua fomu ni Joyce Marwa akiitaka nafasi ya Uhasibu, William Kallaghe aliyejitosa ukatibu mkuu, Josima Mutale anawania ukatibu msaidizi huku wanaowania ujumbe wa Kamati ya Utendaji ni Kiango Kipingu, Swalehe Malimbo, Gilbert  Peter, Majaliwa Majuto, Nico Jonas, Morris Loje na Ismail Ngulingo.


“Zoezi hili limeenda salama, mimi nawasisitiza tu wadau mchezo huu wawachague viongozi ambao wanaamini watawapa ishirikiano wa kutosha                      katika kipindi chake cha uongozi, siku ya usaili kwa wagombea hao itatangazwa mapema kabla ya siku ya uchaguzi,” alisema Chacha.

Polisi wafafanua sababu ya kulipua mabomu ya machozi leo Arusha





Jeshi la polisi limekipiga marufuku chama cha demokrasia na maendelo(CHADEMA)kufanya shughuli zozote za kuaga miili ya marehemu kwenye viwanja vya Soweto kwani zoezi la uchunguzi bado linaendelea kwenye viwanja hivyo .

Akizungumza ofisini kwake kamanda wa polisi mkoani Arusha, Liberatus Sabas amesema kutokana na uchunguzi unaoendelea wa tukio la bomu kwenye viwanja hivyo imeonelea kuwa si busara kuweka mkusanyiko wa watu kwani kutaharibu upelelezi.


Kamanda Sabas amedai  kuwa  jeshi la polisi  liliwataka viongozi wa chama hicho kuwaeleza wafuasi wao mahali sahihi watakapoweza kufanyia shughuli hiyo lakini si kwenye viwanja hivyo.

Hali kwenye viwanja hivyo imekuwa ya pilika pilika tangu juzi kwa wafuasi wa chama hicho kujikusanya tokea asubuhi hadi jioni kwa madai ya kuomboleza ..

Hata hivyo viongozi wa chama cha demokrasia na maendeleo walikaidi agizo hilo na  kuanza  kujikusanya uwanjani hapo pamoja na wafuasi wa CHADEMA , hali iliyoleta  mvutano kati ya viongozi  wa jeshi la polisi na  wafuasi hao.
Wakati mabishano hayo yakiendelea, Askari Polisi mmoja  alijichanganya na kuingia katikati ya wafuasi wa Chadema pembeni mwa uwanja huo ambao walikua wanasubiri kujua utaratibu wa kuaga miili ya Marehemu waliolipuliwa na bomu June 15 2013.

Baada ya hapo,Wafuasi hao hawakupenda kitendo cha Polisi kujichanganya nao hivyo ikazuka ugomvi huku wakitaka atoke, baada ya dakika kadhaa  mabumu yalianza kusikika.

Baadhi ya viongozi wa juu wa chama hicho waliokuwepo uwanjani haponi mbunge wa jimbo la ubungo John Mnyika,Ezekia Wenje,Tundu lissu, Halima Mdee...

IDD AZAN, HALIMA MDEE WAJIANDAA KUZIPIGA NA WOLPER NA JB

.




Halima Mdee na Idd Azan wakijifua mkoani Dodoma.
Mazoezi yakiwa yamepamba moto.
 
Mdee akijiimarisha kwa ajili ya kumkabili Wolper.
Mbunge wa Kawe, Halima Mdee na Idd Azan ambaye ni Mbunge wa Kinondoni, wameanza kujichua kwa ajili ya mapambano yao ya ndondi katika Tamasha la Matumaini 2013 litakalofanyika Julai 7 katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Halima Mdee atazipiga na Jacqueline Wolper wakati Idd Azan akionyeshana ubabe na Jacob Steven 'JB'

Klabu Thailand yaja kusaka wachezaji wa kulipwa




Nembo ya klabu ya Thai Port FC
Na Boniface Wambura
KLABU ya Thai Port Football ya Thailand inatafuta wachezaji nchini Tanzania kwa ajili ya kucheza mpira wa miguu nchini humo na katika nchi nyingine barani Ulaya.

Kupitia kwa wakala wake, klabu hiyo imetuma taarifa kupitia Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ikitaka wachezaji wenye umri kuanzia miaka 15 hadi 28 kwa ajili ya kuwafanyia majaribio ambapo watakaofuzu watacheza nchini humo na katika klabu nyingine za Ulaya ambazo wana ushirikiano nazo.

Wachezaji wenye nia ya kufanya majaribio wanatakiwa kutuma taarifa za wasifu wao (CV) kwa klabu hiyo kwa njia ya emaili, wawe na pasi ya kusafiria pamoja na pasi ya mchezaji (player passport).

Wakala atapitia vitu hivyo, na kwa wachezaji atakaowahitaji atawatumia tiketi za ndege na viza kwa ajili ya kwenda kufanya majaribio nchini humo, na watakaofanikiwa kabla ya kusaini nao mikataba watawasiliana na klabu zao nchini (kwa wale wenye klabu).

'NYOTA NJEMA' YA SALMA SEGERE YAANZA KUTESA






Na Elizabeth John

MWANADADA anayetamba katika tasnia ya muziki wa Taarabu nchini, Salma Swed ‘Salma Segere’ ameachia wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la ‘Nyota Njema’ ambao umeanza kufanya vizuri katika vituo mbalimbali vya redio.

Mbali na kibao hicho mwanadada huyo alishawahi kutamba katika vibao vya Segere, Lindima, Alongore na vinginevyo ambavyo vimeimbwa na kundi la muziki huo la Wazazi Culture Troup ‘Segere Original’.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Salma Segere alisema anamshukuru mungu kazi hiyo inafanya vizuri katika tasnia ya muziki huo ikiwa ni pamoja na kupokelewa vizuri na mashabiki wa Taarabu nchini.

“Namshukuru mungu kazi hii imepokelewa vizuri na mashabiki wangu, kwani tasnia ya muziki sasa ina wasanii wengi sana hadi kazi yako ikikubalika ujue umefanya kazi nzuri na umeumiza sana kichwa,” alisema.

Alisema kwasasa yupo katika mchakato wa kuachia video ya kazi hiyo ambayo anaamini itafanya vizuri pia kutokana na mazingira ambayo ameyatumia kutengeneza kazi hiyo

Siitaki Tanzania ya Ugaidi na Mauaji, naitaka Tanganyika ya Amani na Utulivu!




Na Bryceson Mathias
SI UTANI; nimesema siitaki Tanzania ambayo viongozi na Watawala wake hawataki kuimba wimbo wa, Ili Tuendelee, tunahitaji vitu vinne; Watu, Ardhi, Siasa Safi na Uongozi Bora.
Kiongozi lazima atokane na Watu, wasipokuwepo watu hakuna Kiongozi, ataongoza Mawe? Kiongozi asiyejali watu si Kiongozi; Hivyo siitaki Tanzania itakayoruhusu watu wake wauawe ovyo kama ndege, watekwe, wajeruhiwe na kuwindwa kama Wanyama au ndege.
RASHID KAWAWA
Siitaki Tanzania ambayo Viongozi wake hawatajali Uridhi wa Vizazi vya watu wake ikiwemo Ardhi. Mtawala atakayeacha watu wake wanyang’anywe na kudhulumiwa Ardhi, huyo hawapendi watu wake na wala hatokani nao. Watu wanaweza kukusaidia.
Sitaki hata kuiona Tanzania yenye siasa Chafu, Siasa ya Kuhasimiana, ya kulipizana Visasi, Siasa ya kumfurahisha mtu na kuwaumiza wengine, ya Kung’angania Madaraka, Siasa ya Nyangumi,  Mamba na ya Sumu ya Nyoka.
Sipendi kunusa, kuiona hata kuisema, Siasa ya kuviziana, kutekana na Kutupana Mabwepande, kutoana Meno, Kucha, kutoboana Macho, Kumwagiana Tindikali, ya Mabomu ya Machozi, Siasa ya Maji ya Kuwasha.
Kama Siasa ya namna hiyo itaendelea kujiri; ni heri kuishi chini ya Mkoloni, ni heri tusigambe kuwa tuna Uhuru, na ni Kheri tuitwe wanyama kama walivyotuita Wazungu, kwamba tu Masokwe watu, kutokana na tabia hiyo ya kutesana wenyewe!
Naichukia sana Siasa ya Makundi na Usultani, inayodharau watu wengine na kuwafanya waonekane kama Kinyaa, kiasi cha kuwaita huzungumzi na Mbwa, ila Mwenye Mbwa! Maana kama kilichoumbwa na Mungu kikapuliziwa Pumzi ya Uhai ni Mbwa!.........
Sithubutu kuinusa hata kuipa Mawazo Siasa ya wasiokubali kushindwa, wanaoona wako sawa, hata wanapokosea, wanaoona pekee yao ndio wanafaa kutawala, kumbe hata uwezo wa kutawala hawana! Wanaotaka wasikilizwe wao tu! Wao wasisikilize!
Natamani Mungu angerejesha, Utawala wa Tanganyika ambao ndani mwake alikuwemo Baba wa Taifa na Mwasisi wake Mwalimu Julius Nyerere, ambapo tulionekana kama tunachelewa lakini tuliheshimiwa! Na watu waliishi miaka Mingi!
Naitaka Tanganyika hiyo iliyokuwa haina Ufisadi, tofauti na wa leo wa kupindukia. Siku hizi anaweza akauawa Mtu mchana kweupe na watu wanaona na  Polisi wakishuhudia ukiporwa kila kitu, lakini wasiseme chochote!
Naipenda Tanganyika ya Bibi Titi Mohamed, ambayo ilikuwa haina Udini, iliyovaa Utu! Uadilifu na Uzalendo wa Taifa hili. Naitaka Tanganyika ya Waziri Mkuu Rashid Mfalme Kawawa (Simba wa Yuda), ambaye hata akikosolewa alikuwa anakubali!
BIBI TITI
Naitaka Tanganyika ya waliosema, Madini ardhini hayaozi hadi wazao wao wapate Akili na vifaa vya kuvunia yakiwa nchini Tanganyika, kuliko kukodi watu wayachimbue kwa madai watu wetu hawana uelewa lakini yanatoroshwa na kuwapa faida wageni.
Siitaki Tanzania ya Viongozi wanaochaguliwa kwa Rushwa na Ufisadi, wanaochukia wandishi ambao wakiwa madarakani wanarudisha kwanza fedha walizotumia kupata Uongozi, na hatimae kuwakumbuka Watanganyika kwa kuwabagua kwa Udini, na kurithishana Uongozi Kiu-koo.
Pia Sitaki hata kusikiliza, Bunge la Tanzanaia ya Leo, ambalo wabunge wake  wanasema Ndiyooo! hata kwenye Elimu Chafu! hawaungani kusema siyo kwenye siyo na ndiyo kwenye Ndiyo kama Enzi ya Tanganyika ya Spika Adamu Sapi Mkwawa.
Siitaki Tanzania ya Viongozi wanaotuhumiwa kuwa na Vyeti Bandia, au vilivyoungwaungwa kama Nywele Bandia za kuunganisha, ilihali zenyewe ni za Kipilipili, na wanaoporomosha Matusi bungeni kama Mabomba ya Maji.

Makala hii imeandikwa na

MARIA TUBETI ATWAA TAJI LA REDD'S MISS KAGERA 2013




Mshindi wa taji la Redds Miss Kagera 2013 Maria Tubeti (Katikati) akiwa na nyuso ya furaha mara baada ya kamati ya majaji kumtangaza mshindi katika kinyanganyiro kilichoshirikisha walimbwendwe 14, Wa pili ni Hilda Athanas na mshindi wa tatu ni Arodia Mahatane
Mshindi wa taji la Redds Miss Kagera 2013 Maria  Tubeti akifurahia kutwaa taji hilo lililokuwa limeshikiliwa na  Miss Talent Tanzania Babylove Kalalaa aliyeshinda mwaka jana 2012.
Eeeee jamani Hongera kwa kushinda...
Warembo wote 14 wa Redd's Miss kagera 2013 wakitambulishwa

Washiriki wa Shindano la redd's miss Kagera 14 wakiwa kwenye picha ya pamoja.
Majaji walianza kutaja Tano Bora hapa.(Kutoka kulia ni jaji Abella Kamala mtangazaji wa Radio Kasibante fm, jaji wa katikati ni Bi Beata na wa kushoto ni Jaji Edgar)
Tano Bora
Maria  Tubeti akijibu swali
Warembo waliochagulia tano bara wakiwa na tabasamu baada ya kutajwa na kusonga mbele
Miss aliyeachia taji lake leo hii ambaye pia ni Miss Talent Tanzania Babylove Kalalaa
Majaji wakitaja Mshindi wa tatu, wa pili na