Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Sunday, November 3, 2013

Inatisha! Hivi ndivyo alivyojeruhiwa Dk Mvungi




Mtoto wa Dk. Sengodo Mvungi, Deogratius Mwarabu (kushoto) akiwa na baadhi ya wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Joseph Butiku (katikati), na Prof. Paragamba Kabudi walipofika MOI kumjulia hali Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama cha NCCR-Mageuzi ambaye amefikishwa MOI baada ya kuvamiwa na watu wasiojulikana na kukatwa mapanga. 



 Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama cha NCCR-Mageuzi, Dk. Sengodo Mvungi akitolewa katika chumba cha huduma za dharura MOI na kupelekwa katika hospitali ya Aga Khan jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kufanyiwa vipimo.

Wauguzi wakimsaidia kuelekea katika gari la wagonjwa.

Wauguzi wakimsaidia kuelekea katika gari la wagonjwa. 

Dk. Sengodo Mvungi akipata matibabu ndani ya gari la kubeba wagonjwa wakati akipelekwa hospitali ya Aga Khan.



Dk. Sengodo Mvungi akiwa na majeraha kichwani na sehemu za paji la uso.
Na Hapiness Katabazi

MJUMBE wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba nchini na mhadhiri mwandamzi wa Sheria wa Chuo Kikuu cha Bagamayo (UB), Dk. Sengondo Adrian Mvungi, saa saba usiku wa kuamkia leo amevamiwa na watu wasiyojulikana nyumbani kwake Kibamba nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam na kumcharanga mapanga maeneo ya mwilini mwake ikiwemo sehemu za kichwani kwa madai kuwa watu hao wanaosadikiwa kuwa ni majambazi walikuwa wakimshinikiza awapatie fedha na Dk. Mvungi alipowaambia hana fedha ndipo walipoanza kumcharanga mapanga.

Mtoto mkubwa wa Dk. Mvungi, Dk. Natujwa Mvungi ambaye ni Mkuu wa Shule ya Sheria ya Chuo Kikuu cha Bagamoyo Dar es Salaam, saa nane usiku alimdhibitishia mwandishi wa habari hizi kuwa ni kweli baba yake ambaye aliwahi kuwa mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2005 kwa tiketi ya Chama cha NCCR-Mageuzi, lakini kura kwa upande wake hazikutosha na hatimaye aliyekuwa mgombea mwenzie kwa tiketi ya CCM, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, ndiye aliyeshinda na kutangazwa kuwa ndiye Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hadi sasa alivamiwa na kujeruhiwa na mapanga na watu wasiyojulikana.

Dk. Natujwa anasema baada ya watu hao kumjeruhi baba yake na kufanikiwa kuondoka, walimchukua na kumkimbiza katika Hospitali ya Tumbi mkoani Pwani, na kupatiwa matibabu ya huduma ya kwanza na kisha kumkimbiza katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambapo alisema kwanza alipokelewa katika eneo la Emergence na kisha saa kumi na moja asubuhi aliingizwa kwenye wodi ya Taasisi ya Mifupa Moi kwa ajili ya kuanza kupewa matibabu.

HABARI MSETO

NMB YATOA MSAADA WA VYANDARUA HOSPITALI YA LIGULA MKOANI MTWARA




Meneja wa NMB Kanda ya Kusini, Lilian Mwinula akimkabidhi Daktari Mfawidhi wa hospitali ya Ligula-Mtwara, Mohamed Ahmed Gwao sehemu ya msaada wa vyandarua uliotolewa na benki ya NMB kwa hospitali za mkoa wa Mtwara vyenye thamani ya shilingi milioni 10/-. Wanaoshuhudia kutoka kushoto ni matroni wa hospitali ya Ligula, Theofrida Manoti, Mganga Mkuu wa Wilaya, Joseph Mwiru na Meneja wa tawi la NMB Mtwara, Richard lema.

WANAWAKE WAJASIRIAMALI WAASWA KUZINGATIA UBORA WA BIDHAA WANAZOZALISHA




DSC_0394
Mama Tunu Pinda akikaribishwa kufunga maonyesho ya wiki ya Wakinamama Wajasiriamali na Mratibu wa Kitaifa wa Programu ya kuendeleza wajasirimali wanawake Tanzania kutoka ILO, Noreen Toroka. kushoto kwa Mama Pinda ni Mwenyekiti wa MOWE, Bi Elihaika Mrema na
DSC_0354
Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda akifunga rasmi Maonyesho ya Wanawake Wajasirimali (MOWE) katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, maonyesho hayo ya wanawake wajasiriamali yalikuwa ya wiki nzima ambapo wakinamama wanapata nafasi ya kuonyesha na kuuza bidhaa mbalimbali Usindikaji, Mvinyo, Batiki kwa wakazi wa jijini.
DSC_0337
Mratibu wa Kitaifa wa Programu ya kuendeleza Ujasiriamali kwa wanawake Tanzania toka Shirika la Kazi Duniani (ILO) Noreen Toroka akizungumza wakati hafla ya kufunga maonyesho hayo ambapo amesema wiki nzima ilikuwa ni maonyesho wanawake toka sehemu mbalimbali nchini Bara na Visiwani wamepata wasaa wakubadilishana mawazo na mbinu za Kibiashara.
DSC_0324
Mwenyekiti wa Kamati ya MOWE, Mama Elihaika Mrema akizungumza wakati wa kufunga maonyesho hayo ya Wajasirimali wakinamama jijini Dar es Salaam.
DSC_0287
Mama Tunu Pinda akitembelea baadhi ya mabanda katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar.
DSC_0302
Mama Tunu Pinda akipata maelezo kwa mmoja wa Wajasirimali Wanawake walioshiriki maonyeshio hayo.
DSC_0381
Mgeni rasmi Mama Pinda akikabidhi vyeti kwa mmoja wa washiriki wa maonyesho (Certificate of Participation).
DSC_0367
Mgeni rasmi Mama Pinda akiwa katika picha ya pamoja na wenyeji Wake na viongozi wa MOWE.
DSC_0356
Mama Tunu Pinda akiserebuka na baadhi ya Wanawake Wajasiriamali wakati wa sherehe za kufunga maonyesho hayo. .Watanzania wahimizwa kununua bidhaa zinazotengenezwa na wazawa
Na Damas Makangale, MOblog

WANAWAKE Wajasiriamali nchini wameaswa kuzingatia umuhimu wa ubora kwenye bidhaa zao wanazozalisha kwa kuzingatia viwango vya kitaifa na kimataifa ili kupata soko la uhakika ndani na nje ya nchi. Moblog linaripoti.

Akizungumza kwenye kilele cha wiki ya Wajasiriamali Wanawake Tanzania (MOWE) Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda amesema wanawake wanaweza kufanikiwa endapo watazingatia ubora wa vifungashio (Packaging) wanavyotumia kwenye bidhaa zao.

“Nimedokezwa kwamba baadhi ya wajasirimali wamejisajili na kupata kiandishi-anuani yaani Barcodes, hapa Tanzania, mfumo huu umeanza kutumika hivi karibuni na wajasirimali wengi wameshawishiowa kujiunga ili bidhaa zao ziweze kutambuliwa kitaifa na kimataifa,’ amesema
Mama Pinda amesema kwamba watanzania wote wake kwa waume lazima wapende kununua bidhaa zinazotengenezwa hapa nyumbani ili kuweza kuwainua wajasirimali wazawa hasa wakinamama kwa kuunga mkono kampeni ya “Be Tanzanian, Buy Tanzanian” inayohimiza kuwa Mzalendo, Nunua bidhaa za kitanzania.

Amesema hata hivyo, kuna baadhi ya bidhaa zinazozalishwa na baadhi ya vikundi vya hapa nyumbani bado hazijaweza kumudu ushindani wa soko na kukubalika kuuzwa kwenye maduka makubwa yaani supermarkets.

Mama Pinda aliongeza kuwa changamoto nyingine kubwa inayowakabili wajasirimali wenhi ni kutozingatia viwango vinavyotambulika katika soko la ndani la nje ili bidhaa za wazawa ziweze kupenya kwenye soko la kitaifa, kikanda na kimataifa kwa maslahi mapana ya wajasirimali na nchi kwa ujumla.

“kwenu akinamama wajasiriamali na wale waliohidhuria wasio wajasiriamali ni matumaini yangu kuwa mmetumia fursa hii kubadilishana mawazo na kujenga mitandao ya kusaidiana na kuendelezana,” alisisitiza

Kwa upande wake, Mratibu wa kitaifa wa Programu ya kuendeleza Ujasiriamali kwa Wanawake Tanzania kutoka Shirika la Kazi Duniani (ILO) Noreen Toroka amesema shirika la kazi linafarijika kuchangia katika mipango na program za serikali za kuchangia ukuaji wa ajira kwa kupitia program za ILO katika kumuendeleza mjasiriamali mwanamke nchini.

“kwa takribani miongo miwili ILO imekua ikifanya kazi kuhakikisha ujasirimali unachangia ajira na kipato kwa kina mama na tunajivunia kuwa kati ya wadau wengi walio katika kujengea uwezo washirika wetu idara za serikali, asasi za kifedha na zisizo za kifedha katika kuwainua wajasiriamali wakinamama Tanzania,” amesema 

Toroka amesema katika kuendeleza wakinamama nchini ILO imetoa mafunzo ya ujasiriamali kwa wanawake zaidi ya 500 na kuwaunganisha na huduma za kifedha na wataalamu wa ujasiriamali kwa elimu ya biashara na stadi za kazi.

“Kupitia washirika wetu ILO imefikia wakina mama 100 Mkoani Lindi na tunashukuru wadau wtu WAMA Foundation na program yao ya village savings and loan, wakinamama hao walipata mafunzo ya ujasiriamali na tunategemea watapata mikopo nafuu ili waweze kuanzisha, kuboresha na kupanua biashara zao,” aliongeza.

Friday, November 1, 2013

Yanga sasa 'chinjachinja' yaua tena maafande Taifa, Ngassa huyooo!




 Mshambulijia wa Yanga, Hamis Kiiza akiwa katika harakati za kufunga.
Wachezaji wa Yanga wakishangilia.
Beki wa JKT Ruvu akiokoa moja ya hatari langoni mwake.
Kiungo wa JKT Ruvu, Nashon Naftal akimtoka Mrisho Ngasa.
Simon Msuva akichuana na Kessy Mapande wa JKT Ruvu.
Mashabiki wa Yanga wakishangilia timu yao.
Wachezaji wa Yanga wakishangilia bao la tatu lililofungwa na Oscar Joshua. (Picha zote: Francis Dande)
JANGWANI wanacheka! Ndivyo unavyoweza kusema kutokana na Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga kuendelea kutoa dozi kwa timu za majeshi baada ya jioni hii kuivurumusha JKT Ruvu kwa mabao 4-0 na kukalia kiti cha uongozi wa ligi hiyo.
Mabao mawili ya mapema ya Mrisho Ngassa 'Uncle' na mengine ya kipindi cha pili yaliyofungwa na beki wa kushoto, Oscar Joshua na jingine la Jerry Tegete yameifanya Yanga kufikisha pointi 25 kutokana na kucheza mechi 12, huku Ngassa akifikisha jumla ya mabao matano katika orodha ya wafungaji na Tegete kufikisha manne.
Ushindi huo wa Yanga ni wa tatu mfululizo kwa maafande wa Jeshi baada ya awali kuitafuna Mgambo mabao 3-0 kisha kuisulubu Rhino Rangers kwa idadi kaka hiyo kabla ya leo kuisasambua JKT Ruvu.
Mabingwa hao watetezi watamaliza mechi zao za duru la kwanza kwa kuvaana tena na maafande wengine Oljoro JKT pambano lityakalochezwa Alhamis ijayo kwenye uwanja wa Taifa.
Ligi hiyo inatarajiwa kuendelea tena wikiendi hii katika viwanja viwanja vitano kuamliza mechi za raundi ya 12 kabla ya Jumatano na Alhamis kuhitimishwa kwa ligi hiyo ambayo msimu huu imekuwa na msisimko na ushindani mkubwa.


Msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2013-2014                                         P    W   D   L    F    A   GD  PTS
01. Yanga                   12    7    4    1   28  11   17    25
02. Azam                    11    6    5    0   17   7    10    23
03. Mbeya City           11    6    5    0   15   7     8     23
04. Simba                   12    5    6    1   22  11    11    21
05. Kagera Sugar        12    4    5    3   12    9    3     17
06. Ruvu Shooting       11    4    4    3   13   10   3     16
07. Mtibwa Sugar        11    4    4    3   16  15    1     16
08. Coastal Union        11    3    6     2   10   6    4     15
09. JKT Ruvu              12    4    0    8    9   16  -7     12
10.Rhino Rangers         11    2    4    5    9   15  -6     10
11.Ashanti                    11    2    4    5    10  19 -9     10
12.Prisons                    11    1    5    5     5   14 -9      8
13.Oljoro                     11    1    4    6     8    16 -8     7
14.Mgambo                 11    1    2    8     3    21 -18   5

Wafungaji:
9- Tambwe Amisi (Simba)
8- Hamis Kiiza (Yanga)
7- Elias Maguri (Ruvu Shooting), Juma Luizio (Mtibwa Sugar)
6- Kipre Tchetche (Azam)
5- Tumba Sued (Ashanti Utd), Themi Felix (Kagera), Didier Kavumbagu, Mrisho Ngassa (Yanga)
4-Peter Michael (Prisons), Jerry Santo (Coastal Union), Jerry Tegete (Yanga)
3- Haruna Chanongo, Jonas Mkude (Simba), Bakar Kondo (JKT Ruvu), Themi Felix (Kagera), Paul Nonga (Mbeya City), Salum Machaku (JKT Ruvu), Jerry Santo (Coastal Union),
2- Haruna Moshi, Crispian Odulla (Coastal Union), Saady Kipanga (Rhino Rangers), Mwagani Yeya, Jeremiah John, Peter Mapunda,(Mbeya City), Godfrey Wambura (Kagera Sugar), Shaibu Nayopa, Amir Omary (JKT Oljoro), Khamis Mcha (Azam), Shaaban Nditti (Mtibwa Sugar), Betram Mombeki, Ramadhani Singano (Simba), Said Dilunga (Ruvu Shooting)
1- Abdi Banda, Danny Lyanga (Coastal Union), Henry Joseph, Joseph Owino, Gilbert Kazze (Simba), Haruna Niyonzima, Nizar Khalfan, Simon Msuva, Frank Dumayo, Mbuyi Twitte, Oscar Joshua (Yanga), Iman Joel, Salum Majid, Mwalimu Musuku, Kamana Salum, Hussein Abdallah, Abbas Mohammed (Rhino Rangers), Gaudence Mwaikimba, Seif Abdallah,  Aggrey Morris,  John Bocco, Joseph Kimwaga, Faridi Maliki, Hamphrey Mieno, Salum Abubakar, Erasto Nyoni (Azam), Steven Mazanda, Richard Peter, Deo Deus  (Mbeya City), Laurian Mpalile (Prisons-OG), Shaaban Susan, Jerome Lembeli, Cosmas Ader  (Ruvu Shooting), Masoud Ally, Shaaban Kisiga (Mtibwa Sugar), Shaaban Juma, Anthony Matangalu, Paul Maono(OG), John Matei, Mwinyi Ally (Ashanti Utd), Abdallah Bunu, Emmanuel Switta, Amos Mgisa (JKT Ruvu), Fully Maganga, Hamis Msafiri (Mgambo JKT), Seleman Kibuta, Daud Jumanne, Maregesi Marwa, Clement Douglas, Salum Kanoni (Kagera Sugar), Paul Malipesa, Expedito Kidulo, Nurdin Mohammed, Fikiri Mohammed (Oljoro JKT)

Membe: Vifo vya Askari ni chachu kwa Watanzania




Mhe. Bernard K. Membe (Mb), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akizungumzia ushiriki wa Tanzania katika operesheni za kulinda amani za Umoja wa Mataifa popote pale duniani.
Waziri Membe akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya mahojiano na mwandishi Fredy Mwanjala (kushoto) na mpiga picha Bi. Fauzia Yusuph (kulia), wote wanatoka Kituo cha Televisheni cha Channel Ten.

Na TAGIE DAISY MWAKAWAGO

Tanzania itaendelea kushiriki operesheni za kulinda amani za Umoja wa Mataifa popote pale duniani.

Msimamo huo wa Tanzania uliwekwa wazi na Mhe. Bernard K. Membe (Mb), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa katika mahojiano maalum na Mwandishi Fredy Mwanjala wa Kituo cha Televisheni cha Channel Ten, yaliyofanyika leo ofisini kwake jijini Dar es Salaam

Airtel yaipiga tafu Mpinga Cup 2013



Kamanda Msaidizi wa Kikosi cha Usalama Barabarani, ACP Jehansen Kahatano (wa pili kushoto) akipokea mipira itakayotumika kwenye mashindano ya Mpinga Cup 2013 kutoka kwa  Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando (wa pili kulia), pamoja na Rais wa Be forward Tanzania, Hironori Yamakawa (kushoto). Katika makabidhiano hayo Airtel pia ilikabidhi mfano wa hundi ya shilingi milioni tano kudhamini mashindano hayo ya Mpinga Cup. Anaeshuhudia ni Mkuu wa usalama barabarani kanda ya Dar es salaam, ACP Amiri Konja.
  KamandaACP Jehansen Kahatano akipokea mfano wa hundi kutoka kwa Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando iliyotolewa leo kwa dhumuni la kudhamini mashindano ya mpira wa miguu kwa waendesha pikipiki maarufu kama Mpinga cup. 

Kutoka Bungenin Leo



Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiteta na Mbunge wa Arumeru Mashariki na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Goodluck Ole Mideye, Bungeni Mjini Dodoma Novemba 1, 2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Mbunge wa Mwibara, Kangi Lugola akichangia Bungeni Mjini Dodoma Novemba  1, 2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Mizengo  Pinda akiteta  na  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mahusiano na Uratibu, Stephene Wasira (kushoto), Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Bunge na Uratibu, William Lukuvi (wapili kulia) na Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Mathayo David Mathayo, Bungeni Mjini Dodoma Novemba 1, 2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Clouds yadhamini Tamasha la Handeni



Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

KAMPUNI ya Clouds Media Group, imekuwa miongoni mwa wadau waliojitokeza kudhamini Tamasha la Handeni, linalotarajiwa kufanyika Desemba 14 mwaka huu na kusubiriwa kwa hamu wilayani Handeni mkoani Tanga nchini Tanzania.
Mkurugenzi wa Utafiti na Matukio wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba.

Kwa sasa maandalizi kabambe yamekuwa yakipamba moto kwa ajili ya kuhakikisha kuwa tamasha hilo linafanyika kwa mara ya kwanza katika historia ya Taifa kwa mafanikio makubwa, sanjari na kutafuta mbinu za kimaendeleo.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Mratibu Mkuu wa Tamasha hilo linalotambulika pia kama ‘Handeni Kwetu’, Kambi Mbwana, alisema kuwa kuingia kwa kampuni hiyo ni sehemu ya kulifanya tamasha hilo liwe na mvuto mkubwa zaidi.

Alisema kuwa juhudi zao ni kuhakikisha kuwa tamasha hilo linafanyika wilayani humo na kushirikisha mkoa wa Tanga na Tanzania kwa ujumla, hivyo ni wakati wa wadau wengine kujitokeza kuliwekea mguso wazo hilo.

“Tunashukuru kuona Watanzania wote wanaingia humu ili wazo hili lifanikiwe kwa kiwango kikubwa, ingawa tamasha hili linafanyika kwa mara ya kwanza mwaka huu, huku likiwa na changamoto lukuki.

“Naamini huu utakuwa mwanga mzuri kutoka kwa wenzetu Clouds Media Group ambao pia wanamiliki redio ya Clouds FM na Clouds TV, huku wakiwa ni waandaaji wa Tamasha kubwa la Fiesta linalofanyika kila mwaka na kuzunguuka mikoa mbalimbali ya Tanzania na kukonga nyoyo za wapenzi wa muziki wa ndani na ule wa Kimataifa,” alisema Mbwana.

Wadhamini wengine ni Yusuphed Mhandeni, ambaye ni Mchumi wa CCM Kata ya Makumbusho kwa kupitia Kampuni yake ya Phed Trans, Grace Products, Screen Masters na mtandao wao wa Saluti5.com, Dullah Tiles & Construction Ltd, Katomu Solar Specialist, Planbtz  Country Business Directory (CBD) na Michuzi Media Group.

Wengine ni duka la mavazi la Chichi Local Ware, Smart Mind & Arters chini ya Anesa Company Ltd, ikidhamini kwa kupitia kitabu chao cha ‘Ni Wakati Wako wa Kung’aa’, Lukaza Blog, Kajunason Blog, Jiachie Blog na Taifa Letu.com.

UZINDUZI WA REAL UNIQ TZ WAFUNIKA JIJINI DAR



 Mkurugenzi Fabak Fashion, Asia Idarous Khamsin akizungumza wakati wa uzinduzi rasmi wa Kampuni ya Real Uniq Tz jijini Dar es Salaam jana usiku. Uzinduzi huo ambao ulijaza umati wa watu katika ukumbi wa Samaki Samaki uliopo mtaa wa Samora.

Kampuni hiyo itakuwa inashughulisha na shughuli mbalimbali ikiwa ni pamoja na Utengenezaji wa Matangazo ya Biashara, Modeling/Mitindo Uratibu wa Shughuli mbalimbali pamoja na Mabausa.SOURCE: FATHER KIDEVU BLOG.
Asia Idarous alisema kuwa uwepo wa kampuni hiyo ya kwanza nchini inayotoa huduma hizo italeta ufanisi hasa katika tasnia ya mitindo ambapo hutumia zaidi warembo katika maonesho ya mavazi.
 Mmoja wa mamodel wa kampuni ya Real Uniq Tz akipita jukwaani akiwa amevalia kivazi cha Kanga kilichobuniwa na na Asia Idorous wa Fabak Fashion.
 Asia akiwa na Models waliovalia vazi la kanga za Tanzania kutoka Faback Fashion.
 Burudani kutoka Michael Jackson wa Tanzania ilikuwepo.
 Baaadhi ya warembo walioshiriki shindano la Miss Tanzania 2013 wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa uzinduzi huo.
 Hii ndo ilikuwa tatu bora ya Miss Tanzania 2013, Miss Tz, Happiness Watimanywa (katikati) akiwa na Latifa Mohamed (kushoto) na Clara Bayo.

SKYLIGHT BAND MWENDO NI ULE ULE SPIDI 120 NDANI YA THAI VILLAGE-MASAKI LEO USIKU




IMG_1157
Joniko Flower akishambulia jukwaa na kikosi kazi cha Skylight Band Ijumaa iliyopita ndani ya uwanja wao wa nyumbani Thai Village Masaki jijini Dar....Tukutane pale kati leo usiku kama kawaida.....!
IMG_1160
Aneth Kushaba AK47 akitoa burudani sambamba na Mary Lucos pamoja na Digna kwa mashabiki wa Skylight Band Ijumaa iliyopita.
IMG_1191
Sony Masamba wa Skylight Band akijiachia na shabiki wake kwa raha zao.
IMG_1168
Sam Mapenzi a.k.a Asali ya warembo akifanya yake jukwaani juma lililopita ndani Thai Village.
IMG_1211
Mdau David akichiziki na Skylight Band.
IMG_1216
Familia ya Skylight Band ikisebeneka na Style ya "Yachuma chuma"....!
IMG_1221
Twende kazi.......burudani ile ile njoo ushuhudie mwenye leo usiku pale Thai Village.

UNIC YAFURAHI NA WANAFUNZI WA SHULE ZA MSINGI JIJINI DAR



IMG_1869
Pichani juu na chini ni Afisa Habari wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Usia Nkhoma Ledama akizungumza na wanafunzi wa shule za msingi za Zanaki, Diamond, Kisutu na Muhimbili katika siku maalum inayotambulika kama "Fun Thursday" na kufanyika Alhamis ya mwisho wa mwezi.

Bi. Ledama ametumia siku hiyo kuwaelimisha wanafunzi kuhusiana na kazi mbalimbali zinazofanywa na mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini yakiwemo Malengo ya Milenia ambayo ni Kutokomeza umaskini uliokithiri na njaa, Elimu ya Msingi kwa wote, Usawa wa kijinsia na fursa sawa kwa wanawake, kupunguza vifo vya watoto wachanga, Upatikanaji wa huduma bora za uzazi, kupambana na Ukimwi, Malaria na magonjwa mengine, kulinda mazingira pamoja na kujenga mshikamano wa kimaendeleo duniani. Fun Thursday imefanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa ofisi za UNESCO jijini Dar.
IMG_1821 IMG_1887
Wanafunzi wakimsiliza kwa umakini wakati Afisa Habari wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Usia Nkhoma Ledama (hayupo pichani) wakati akiwapiga msasa kuhusiana na kazi mbalimbali zinazofanywa na mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini.
IMG_1962
Msaidizi wa Maktaba ya kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Bi. Harriet Macha akiwaelezea wanafunzi umuhimu wa kuwa na Maktaba mashuleni mwao pamoja na kujijengea tabia za kupenda kujisomea.
IMG_1891
Wanafunzi wakifurahi wakati wa Fun Thursday inayofanyika kila Alhamis ya mwisho wa mwezi na kuratibiwa na Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC).
IMG_1782
Mwalimu Nicholaus Massawe wa shule ya msingi Zanaki akibadilishana mawazo na Mwalimu Rahel Fute wa Shule ya msingi Diamond wakati wa Fun Thursday iliyowakutanisha wanafunzi kutoka shule za msingi mbalimbali za jijini Dar.
IMG_1930
Mratibu wa Mkoa kutoka Asasi ya Vijana wa Umoja wa Mataifa (YUNA) Innocent Mkota akiwasisitiza wanafunzi umuhimu wa kujiunga na vilabu vya Umoja wa Mataifa mashuleni.
IMG_1940
Wanafunzi wa shule za mbalimbali za msingi jijini Dar es Salaam wakifuatilia Documentary fupi iliyomshirkisha msaani wa muziki wa Marekani Beyonce na wimbo wake wa "I was here" inayoenyesha kazi mbalimbali zinazofanywa na mashirika ya Umoja wa Mataifa Duniani.
IMG_2023
Mwalimu Kalabo Mushumbusi kutoka shule ya Msingi Muhimbili akitoa shukrani kwa kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa UNIC kuwa kuwaelimisha wanafunzi wao kuhusiana na kazi mbalimbali ya Umoja Mataifa nchini.
IMG_1980
Wanafunzi wa shule za msingi jijini Dar wakiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) pamoja na walimu wao nje ya ukumbi wa mikutano wa Ofisi za UNESCO.