Pichani juu na chini ni Afisa
Habari wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Usia Nkhoma
Ledama akizungumza na wanafunzi wa shule za msingi za Zanaki, Diamond,
Kisutu na Muhimbili katika siku maalum inayotambulika kama "Fun
Thursday" na kufanyika Alhamis ya mwisho wa mwezi.
Bi. Ledama ametumia siku hiyo
kuwaelimisha wanafunzi kuhusiana na kazi mbalimbali zinazofanywa na
mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini yakiwemo Malengo ya Milenia ambayo
ni Kutokomeza umaskini uliokithiri na njaa, Elimu ya Msingi kwa wote,
Usawa wa kijinsia na fursa sawa kwa wanawake, kupunguza vifo vya watoto
wachanga, Upatikanaji wa huduma bora za uzazi, kupambana na Ukimwi,
Malaria na magonjwa mengine, kulinda mazingira pamoja na kujenga
mshikamano wa kimaendeleo duniani. Fun Thursday imefanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa ofisi za UNESCO jijini Dar.
Wanafunzi wakimsiliza kwa
umakini wakati Afisa Habari wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa
(UNIC) Usia Nkhoma Ledama (hayupo pichani) wakati akiwapiga msasa
kuhusiana na kazi mbalimbali zinazofanywa na mashirika ya Umoja wa
Mataifa nchini.
Msaidizi wa Maktaba ya kitengo
cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Bi. Harriet Macha akiwaelezea
wanafunzi umuhimu wa kuwa na Maktaba mashuleni mwao pamoja na kujijengea
tabia za kupenda kujisomea.
Wanafunzi wakifurahi wakati wa
Fun Thursday inayofanyika kila Alhamis ya mwisho wa mwezi na kuratibiwa
na Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC).
Mwalimu Nicholaus Massawe wa
shule ya msingi Zanaki akibadilishana mawazo na Mwalimu Rahel Fute wa
Shule ya msingi Diamond wakati wa Fun Thursday iliyowakutanisha
wanafunzi kutoka shule za msingi mbalimbali za jijini Dar.
Mratibu wa Mkoa kutoka Asasi
ya Vijana wa Umoja wa Mataifa (YUNA) Innocent Mkota akiwasisitiza
wanafunzi umuhimu wa kujiunga na vilabu vya Umoja wa Mataifa mashuleni.
Wanafunzi wa shule za
mbalimbali za msingi jijini Dar es Salaam wakifuatilia Documentary fupi
iliyomshirkisha msaani wa muziki wa Marekani Beyonce na wimbo wake wa "I
was here" inayoenyesha kazi mbalimbali zinazofanywa na mashirika ya
Umoja wa Mataifa Duniani.
Mwalimu Kalabo Mushumbusi
kutoka shule ya Msingi Muhimbili akitoa shukrani kwa kitengo cha habari
cha Umoja wa Mataifa UNIC kuwa kuwaelimisha wanafunzi wao kuhusiana na
kazi mbalimbali ya Umoja Mataifa nchini.
Wanafunzi wa shule za msingi
jijini Dar wakiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa Kitengo cha
Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) pamoja na walimu wao nje ya ukumbi wa
mikutano wa Ofisi za UNESCO.
No comments :
Post a Comment