Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Wednesday, November 6, 2013

NSSF KUENDELEA KUKABILIANA NA CHANGAMOTO ZA MAKAZI




Meneja Uhusiano na Huduma kwa Wateja wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Bi. Eunice Chiume akieleza kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) mpango wa Shirika hilo kuendelea kutatua changamoto za makazi kwa wanachama wake,wakati wa mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari(MAELEZO) Leo Jijini Dar es Salaam.Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bi Zamaradi Kawawa. Picha na Hassan Silayo-MAELEZO
********************************************
Na Georgina Misama
Shirika la Taifa la hifadhi ya jamii (NSSF) linaendelea na mikakati wa kutatua changamoto za makazi kwa wanachama wake.

Hayo yamesemwa na Meneja Uhusiano na Huduma kwa Wateja wa shirika hilo Eunice Chiume wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam.

Eunice alisema kuwa kutokana na kuwepo kwa  hitaji kubwa ya makazi shirika limejipanga kukabiliana na changamoto hiyo kwa kuendelea kujenga nyumba za bei nafuu zitakazouzwa kwa wanachama wake ili kuweza kuwapatia makazi ya kudumu.

“baada ya kukamilika kwa awamu ya kwanza naya pili ya ujenzi wa nyumba 297, NSSF tumeona kuna haja ya kuendelea kukukabiliana na hali hii kwa kuanzisha awamu ya tatu ya mradi wa nyumba za bei nafuu itakayohusisha ujenzi wa nyumba 900 zitakazo gharimu  takriban shilingi bilioni 23.” alisema Eunice.

Aidha Eunice aliongeza kuwa kuanzia November 11 mwaka huu Shirika linatarajia kuanza kutoa fomu za maombi ya kununua  viwanja 498 vilivyopimwa katika eneo la kiluvya A madukani, viwanja hivyo vitauzwa kwa ushirikiano wa shirika na Halmashauri ya wilaya ya kisarawe, ambapo  eneo hilo litakuwa makazi mapya nay a kisasa litakalokuwa na huduma muhimu za kijamii.

Viwanja hivyo vitauzwa kwa wanachama wa NSSF na jamii kwa ujumla kwa bei inayoanzia Shilingi 15,000 hadi Shilingi 20,000 kwa mita ya mraba kulingana na matumizi.

No comments :

Post a Comment