Na Fatma
Salum-Maelezo
Serikali kutumia
takriban dola za marekani milioni 219
kujenga gati 4 katika bandari ya Mtwara
ambapo tayari taarifa ya upembuzi yakinifu imekamilika.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaam na Mkurugenzi
Msaidizi wa idara ya Maendeleo ya Sekta Binafsi Uwekezaji na Uwezeshaji toka Ofisi ya Waziri Mkuu John Mboya wakati wa
mkutano na waandishi wa habari.
Akieleza zaidi
John amesema mradi huo ni matokeo ya utekelezaji wa kanuni za Ubia baina
ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP) ya mwaka 2011 ambapo sektabinafsi inahusikanakukarabati,kujenga,kuendesha,kutunza
au kusimamia mradi mzima.
Akifafanua zaidi
John amesema Ofisi ya Waziri Mkuu kupitia idara yake imeendaa mafunzo kwa
maofisa 60 walioteuliwa kusimamia utekelezaji wa miradi ya DPP.
Akitolea mfano
alisema Serikali inaweza kuwa na mkataba na muwekezaji katika mradi wa ujenzi
wa barabara yenye urefu wa km 100 wenye
viwango Fulani ambapo muwekezaji atatakiwa kusanifu, kujenga na kuendesha kwa
gharama zake na hatimaye baada ya kurudisha mtaji wake na faida,anakabidhi
mradi huo serikalini.
Alitaja miradi
mingine kuwa ni ujenzi wa barabara ya Dar es salaam-chalinze (km 100)kuwa
barabara ya haraka (Expressway)ambapo wakala wa barabara umekamilisha hatua za
awali za upembuzi yakinifu wa awali.
Mradi mwingine
ni ujenzi wa bandari mpya ya bagamoyo na eneo huru la biashara ambapo Serikali
inashirikiana na mwekezaji kutoka China, ambapo majadiliano na mwekezaji
yanaendelea ili mradi huu ulete tija kwa Taifa.
No comments :
Post a Comment