Michuano
ya Kombe la Uhai inayoshirikisha wachezaji wenye umri chini ya miaka 20
wa klabu za Ligi Kuu inaanza kutimua vumbi Novemba 17 mwaka huu katika
viwanja vya Karume na Azam Complex, Dar es Salaam.
Droo
ya michuano hiyo inayodhaminiwa na Maji Uhai imefanyika leo (Novemba 8
mwaka huu) mbele ya waandishi wa habari katika ofisi za Shirikisho la
Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ambapo timu zimepangwa katika makundi
matatu.
Kundi
A linaundwa na timu za Azam, Coastal Union, JKT Ruvu Stars, Mbeya City
na Yanga, wakati kundi B ni Ashanti United, Mgambo Shooting, Oljoro JKT
na Ruvu Shooting. Kagera Sugar, Mtibwa Sugar, Rhino Rangers na Tanzania
Prisons ndizo zinazounda kundi C.
Mechi
za ufunguzi kundi A Novemba 17 mwaka huu ni kati ya Azam na Coastal
Union (saa 2 asubuhi- Karume), Yanga na Mbeya City (saa 8 mchana-
Karume). Kundi B ni Ruvu Shooting na Ashanti United (saa 4 asubuhi-
Karume), Oljoro JKT na Simba (saa 10 jioni- Karume).
Kagera
Sugar na Mtibwa Sugar (saa 2 asubuhi- Azam) na Rhino Rangers na
Tanzania Prisons (saa 10 jioni- Azam) ndizo zitakazocheza mechi za
ufunguzi Novemba 17 mwaka huu katika kundi C.
Robo
fainali ya michuano hiyo itachezwa Novemba 24 na 25 mwaka huu wakati
nusu fainali itapigwa Novemba 26 na 27 mwaka huu. Mechi ya kutafuta
mshindi wa tatu na ile ya fainali zitachezwa Novemba 30 mwaka.
No comments :
Post a Comment