Mwenyekiti
wa CCM Mkoa wa Rukwa Hiporatus Matete wapili kushoto kwa niaba ya
viongozi wa chama na Serikali Mkoa wa Rukwa akimuombea dua Makamu
Mwenyekiti wa CCM Taifa Ndugu Philip Mangula wakwanza kushoto aweze
kusafiri salama kuelekea Mkoani Mbeya katika maagano yaliyofanyika
Mpakani mwa Mkoa wa Rukwa na Mbeya tarehe 13 Novemba 2013. Wa kwanza
kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya.
Makamu
Mwenyekiti wa CCM Taifa Ndugu Philip Mangula akionyesha mchoro wa asili
wa Twiga aliopewa na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya wa
pili kushoto katika hafla ya chakula cha jioni kilichoandaliwa na Mkuu
huyo wa Mkoa tarehe 12 Novemba 2013 kama ishara ya kulinda na kuzipenda
maliasili za taifa na kuendeleza vita dhidi ya ujangili nchini. Wa
kwanza kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Rukwa Ndugu Hiporatus Matete
na wa kwanza kulia ni Katibu wa CCM Mkoa huo Bi. Rahel Ndengeleke.
Mhe.
Mangula amesema amejifunza mengi Mkoani Rukwa ikiwemo mipango
mbalimbali ya maendeleo ya Chama na Serikali, alipendezewa na maendeleo
aliyoyaona sasa Mkoani Rukwa tofauti na miaka 10 iliyopita alipofika
Mkoani hapo kwa mara ya mwisho. Alifurahishwa na Mpango wa Serikali ya
Mkoa wa Rukwa wa ONYARU; Ondoa nyasi Rukwa ambao umehamasisha wananchi
wengi kuondoa nyasi na kuezeka bati katika nyumba zao.
No comments :
Post a Comment