Mjumbe
wa Halmashauri Kuu ya Chama cha NCCR-Mageuzi, Dk. Sengodo Mvungi
akitolewa katika chumba cha huduma za dharura MOI na kupelekwa katika
hospitali ya Aga Khan jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kufanyiwa
vipimo.
Wauguzi wakimsaidia kuelekea katika gari la wagonjwa.
Wauguzi wakimsaidia kuelekea katika gari la wagonjwa.
Dk. Sengodo Mvungi akipata matibabu ndani ya gari la kubeba wagonjwa wakati akipelekwa hospitali ya Aga Khan.
Dk. Sengodo Mvungi akiwa na majeraha kichwani na sehemu za paji la uso.
Na Hapiness Katabazi
MJUMBE wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba nchini
na mhadhiri mwandamzi wa Sheria wa Chuo Kikuu cha Bagamayo (UB), Dk. Sengondo
Adrian Mvungi, saa saba usiku wa kuamkia leo amevamiwa na watu wasiyojulikana nyumbani kwake Kibamba nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam na
kumcharanga mapanga maeneo ya mwilini mwake ikiwemo sehemu za kichwani kwa
madai kuwa watu hao wanaosadikiwa kuwa ni majambazi walikuwa wakimshinikiza
awapatie fedha na Dk. Mvungi alipowaambia hana fedha ndipo walipoanza kumcharanga
mapanga.
Mtoto
mkubwa wa Dk. Mvungi, Dk. Natujwa Mvungi ambaye ni Mkuu wa Shule ya Sheria ya
Chuo Kikuu cha Bagamoyo Dar es Salaam, saa nane usiku alimdhibitishia mwandishi
wa habari hizi kuwa ni kweli baba yake ambaye aliwahi kuwa mgombea urais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2005 kwa tiketi
ya Chama cha NCCR-Mageuzi, lakini kura kwa upande wake hazikutosha na hatimaye
aliyekuwa mgombea mwenzie kwa tiketi ya CCM, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, ndiye
aliyeshinda na kutangazwa kuwa ndiye Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
hadi sasa alivamiwa na kujeruhiwa na mapanga na watu wasiyojulikana.
Dk. Natujwa
anasema baada ya watu hao kumjeruhi baba yake na kufanikiwa kuondoka,
walimchukua na kumkimbiza katika Hospitali ya Tumbi mkoani Pwani, na kupatiwa
matibabu ya huduma ya kwanza na kisha kumkimbiza katika Hospitali ya Taifa ya
Muhimbili ambapo alisema kwanza alipokelewa katika eneo la Emergence na kisha
saa kumi na moja asubuhi aliingizwa kwenye wodi ya Taasisi ya Mifupa Moi
kwa ajili ya kuanza kupewa matibabu.
HABARI MSETO
No comments :
Post a Comment