Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Tuesday, May 29, 2012

ST.AGUSTINE MABINGWA SAFARI POOL HIGHER LEARNING COMPETITION 2012.



Wachezaji wa St.Agustine wakiwa na furaha
 Meya wa Manispaa ya Iringa, Aman Mamwindi akimkabidhi Kombe nahodha wa timu ya St.Agustine, Jimmy Nicas baada ya kutwaa ubingwa wa mashindano ya Safari Higher Learning Pool Competition yaliyomalizika Mkoani Iringa mwishono mwa wiki.Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Pool(TAPA) Fred Mushi. 
Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo akizungumza na wachezaji kutoka vyuo mbalimbali mara baada ya kumalizika kwa mashindano ya Safari Higher Learning Pool Competition Mkoani Iringa.
 
 Meya wa Manispaa ya Iringa, Aman Mamwindi akizungumza na wachezaji kutoka vyuo mbalimbali mara baada ya kumalizika kwa mashindano ya Safari Higher Learning Pool Competition Mkoani Iringa.
Wachezaji wa Chuo cha St.Agustine wakiwa wamembeba nahodha wao mara baada ra Jimmy Nicas kabeba kumbe mara baada ya kuibuka mabingwa wa Safari Higher Learning Pool Competition Mkoani Iringa.
CHUO cha St.Augustine cha mkoa wa Mwanza juzi kilitawazwa kuwa mabingwa wapya wa mashindano ya mchezo wa pool kwa wanafunzi wa vyuo vikuu yanayojulikana kama 'Safari Higher Learning Pool Competition 2012 baada ya kuibuka na ushindi wa magoli 13-9 dhidi ya waliokuwa mabingwa watetezi chuo cha IFM kutoka mkoa wa Dar es salaam katika mchezo wa fainali wa mashindano hayo.
Fainali za mashindano hayo ambazo zilishirikisha vyuo vinane ambavyo vilikuwa mabingwa katika mikoa yao ngazi ya mikoa ya mashindano hayo na kudhaminiwa na wadhamini wakuu wa mchezo wa pool nchini,Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager,zilifanyikia kwenye ukumbi wa Iringa All Fear mkoa hapa.
St.Augustine kwa kuwa mabingwa wapya wa mashindano hayo walijinyakulia fedha taslim Sh. Mil.2.5 pamoja na kikombe kikubwa cha ubingwa huo.
IFM ambao licha ya kucheza vizuri katika fainali hizo na kujikuta wakipoteza ubingwa huo walizawadiwa fedha taslim Sh.Mil.1.5 kwa kushika nafasi ya pili, chuo cha RUCO kutoka Iringa chenyewe kiliondoka na Sh.Mil.1.3 kwa kushika nafasi ya tatu na St.John's kutoka mkoa wa Dodoma kilishika nafasi ya nne na kupewa Sh. Mil.1.
Vyuo vya MUCCOBS (Kilimanjaro), IAA (Arusha),Mzumbe (Morogoro) na TIA (Mbeya) vyenyewe vilizawadia Sh.500,000 kila chuo ikiwa ni kifuta jasho cha kushiriki fainali hizo.
Kwa upande wa mchezaji mmoja mmoja (wanaume) mchezaji wa chuo cha St. John's cha Dodoma, Obiara David alitwaa ubingwa huo baada ya kumgaragaza vibaya Jackson Raphael wa  chuo cha MUCCOBS (Kilimanjaro) magoli 4-0 katika mchezo wa fainali.
Obiara kwa kutwaa ubingwa huo alijinyakulia fedha taslim Sh.300,000 na ngao wakati ambapo Jackson kwa kushika nafasi ya pili alizawadia fedha taslim Sh.200,00, Said Mohamed (RUCO) alishika nafasi ya tatu na kupewa Sh.150,000 na Patrick Peter (IFM) aliambulia Sh.100,000 kwa kushika nafasi ya nne.
Kwa upande wa mchezaji mmoja mmoja (wanawake), Modesta David (IFM) alitwaa ubingwa huo na kuzawadiwa Sh. 200,000, Remmy Jackson (St.John's) alishika nafasi ya pili na kupewa Sh.150,000, Suchi Anatasia (KCMC) alishika nafasi ya tatu na kupewa Sh.100,000 na Violeth Silas (IAA) aliambulia Sh.50,000 kwa kushika nafasi ya nne.
Aliyekuwa mgeni rasmi katika fainali hizo ni Meya wa Manispaa ya Iringa, Amani Mwamwindi.
Wachezaji wa St.Agustine wakiwa na furaha
 Meya wa Manispaa ya Iringa, Aman Mamwindi akimkabidhi Kombe nahodha wa timu ya St.Agustine, Jimmy Nicas baada ya kutwaa ubingwa wa mashindano ya Safari Higher Learning Pool Competition yaliyomalizika Mkoani Iringa mwishono mwa wiki.Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Pool(TAPA) Fred Mushi. 
Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo akizungumza na wachezaji kutoka vyuo mbalimbali mara baada ya kumalizika kwa mashindano ya Safari Higher Learning Pool Competition Mkoani Iringa.
 
 Meya wa Manispaa ya Iringa, Aman Mamwindi akizungumza na wachezaji kutoka vyuo mbalimbali mara baada ya kumalizika kwa mashindano ya Safari Higher Learning Pool Competition Mkoani Iringa.

Monday, May 28, 2012

MISS NYAMAGANA WAENDELEA KUTESA




Shindano la Miss Nyamagana 2012, Litafanyika katika ukumbi wa Gold Crest Mwanza, tarehe 02/06/2012 ambapo wasanii Linah, Ditto na Hafsa Kazinja watalipamba jukwaa. Mc katika shindano hilo ni msanii maarufu katika tasnia ya uchekeshaji na mzungumzia Mpoki. Jumla ya warembo 20 watapanda jukwaani kumpata Miss Nyamagana 2012, kabla ya shindano la kumpata mrembo wa Mkoa wa Mwanza.
Katika mahojiano yaliyofanyika, warembo wameonekana kuwa na shauku kubwa ya ushindi, wakiaahidi kurudisha taji la Miss Tanzania Mkoani Mwanza. Shndano la Miss Nyamagana 2012 linaandaliwa na Stoppers Entainment ya jijini Mwanza.

Mustafa Sabodo Atoa Billioni 5 Kwa Ajili ya Ujenzi wa Jengo la Kuegesha Magari Jijini


 Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa akimkabidhi Mfanyabiashara maarufu nchini, Mustafa Sabodo vibali vya ujenzi wa jengo hilo, kushoto ni  Mwenyekiti wa Madhehebu  ya Khoja Shia Shiraz Walji
--
MFANYABIASHARA maarufu nchini, Mustafa Sabodo ametoa zaidi ya sh.bilioni 5 kwa madhehebu ya Khoja Shia Ithnaashri Jamat kwa ajili ya kujenga jengo la maegesho ya magari.
 
Akizungumza katika hafla ya kupokea vibali vya ujenzi wa jengo hilo Dar es Salaam leo kutoka kwa Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa alisema jengo hilo litasimamiwa na madhehebu hayo.
 
Alisema jengo hilo lililopo katika mitaa ya India na Morogoro la ghorofa 14 litakuwa na uwezo wa kuhifadhi magari 180 kwa wakati mmoja.
 
Silaa alisema fedha zitakazopatikana kwa malipo ya maegesho ya magari katika kipindi cha miaka 10 zitafanya kazi ya kuchimba visima katika maeneo mbalimbali ya nchi yetu.Meya alisema kwa muda mrefu Jiji la Dar es Salaam limekuwa likikabiliwa na maeneo ya kuegesha magari na kuwa jengo hilo la kwanza kubwa litakuwa ni mkombozi mkubwa.
 
"Kwa muda mrefu tumekuwa na matatizo ya kuegesha magari katika jiji letu hivyo msaada aliotoa ndugu yetu Sabodo kwa madhehebu hayo ya ujenzi wa maegesho hayo itasaidia sana kupunguza tatizo hilo," alisema Silaa.
 
Alisema Manispaa imepokea jambo hilo kwa mikono miwili na ndio maana imekamilisha vibali ili ujenzi huo uende pasipo kikwazo chochote.
 
Alisema jengo hilo litaitwa Sabodo Car Park jambo litakalo weka kumbukumbu ya mchango wake katika kufanikisha shughuliza za maendeleo.
 
Mwenyekiti wa Madhehebu hayo Shiraz Walji, alimshukuru Sabodo kwa msaada wake huo na kuahidi kusimamia vizuri mradi huo ambao utakuwa wa manufaa kwa Watanzania wote.

Taswira Mbalimbali za Maandamano Visiwani Zanzibar Yaliyozua Taharuki na Hali Tete



Kiongozi wa Jumuiya ya kikundi cha uamsho, Sheikh Farid Hadi Ahmed
 Mmoja wa waandamani wa Kundi la Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislam (JUMIKI) Kisiwani Unguja,Zanzibar akionyeshan kitambaa kilicho na Damu mapema leo Asubuhi wakati wakiendelea na maandamano yao ambayo yamesababisha vurugu kubwa kisiwani humo,iliyopelekea kuchomwa moto kwa moja ya makanisa pamoja baadhi ya magari yaliyokuwa yameengeshwa karibu na njia wapitazo.vurugu hizo zimeanza jana usiku baada ya kukamatwa kwa kiongozi wa Juimuiya hiyo
 Maelfu wa wazanzibari wakiongozwa na Taasisi za Kiislamu na Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI) wakifanya matembezi ya amani katika barabara za Zanzibar na kupeleka ujumbe wao kwa viongozi wa serikali za Zanzibar na ile ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Umoja wa Mataifa wakitaka Zanzibar huru ambapo baadhi ya watembeaji hao wakiongoza na Kiongozi wa Jumuiya hizo, Sheikh Farid Hadi Ahmed na viongozi wengine
 Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) liliopo mtaa wa Kariakoo mjini Unguja limechomwa moto jana usiku wa kuamkia leo na watu wasiojulikana
 Gari la Kiongozi wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) Bishop Dickoson Maganga lililochomwa moto usiku wa jana katika eneo la Kariakoo nje ya kanisa hilo ambapo uharibifu wote unaelezwa kuwa umegharimu shilingi millioni 120.
 Gari la Kiongozi wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) Bishop Dickoson Maganga
lililochomwa moto na watu wasiojulikana usiku wa leo katika eneo la Kariakoo nje ya kanisa hilo ambapo uharibifu wote unaelezwa kuwa umegharimu shilingi millioni 120.
 Kikosi cha Kuzuwia Fujo FFU kikizunguka kikiwa kimejihami katika maeneo ya Michenzani ambapo tayari jeshi la polisi limepiga marufuku mikusanyiko yoyote Mjini hapa
Katibu wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI) Sheikh Abdallah Said Ali ambaye ni miongoni mwa wanaotafutwa na jeshi la polisi akizungumza na Radio DW asubuhi mapema kabla ya taarifa ya kutafutwa kwao kutolewa kwa vyombo vya habari
---
Maelfu ya wazanzibari leo wamefanya maandamano amani kuishindikiza Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kuitisha kura ya maoni juu ya Muungano na kupeleka ujumbe kwa Umoja wa Mataifa wa kutaka Zanzibar kujitenga kama ilivyofanya Sudan ya Kusini.

Wazanzibari hao wakiongozwa na Sheikh Farid Hadi Ahmed walitembea kutoka viwanja vya Lumumba na kupitia barabara ya Kinazini, Mpigaduri, Michenzani Maskani ya CCM Kisonge, kwa Biziredi na kurudi tena viwanja vya Lumumba.

Maandamano hayo walioyaita matembezi ya amani yalifanyika na kuhudhuriwa na maelfu ya wazanzibari ambapo awali kuliandaliwa kongamano kubwa lililoandaliwa na Taasisi za Kiislamu kwa kushirikiana na Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI) kwa lengo la kuzungumzia mfumo wa elimu Zanzibar.

Akizungumza na maelfu ya wazanzibari kabla ya kuanza maandamano hayo yaliitwa ni matembezi ya amani, Sheikh Farid alisema wazanzibari wana haki kama walivyokuwa na haki wananchi wengine ulimwenguni kote kudai haki yao ndani ya nchi yao.

“Sisi wazanzibari kama wananchi wengine wowote duniani tuna haki ya kikatiba kudai nchi yetu kama walivyodai Sudan ya Kusini, mbona Sudan ya wameweza kujitenda na kupata nchi yao kwa nini sisi kama wazanzibari tusikubaliwe kudai nchi yetu sasa sisi tunampelekea salam katibu mkuu wa umoja wa mataifa kumwambia kuwa wazanzibari sasa wanataka nchi yao” alisisitiza Sheikh Farid huku akiungwa mkono kwa mamia hao kuinua mikono na kusema ndiooooo.

Awali Sheikh Farid alisema salamu hizo anataka zimfikie Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Kin moon ambaye kwamba wazanzibari wamechoshwa na kuwepo ndani ya Muungano ambao umedumu kwa miaka 48 lakini bado ukiwa na kero nyingi na malalamiko ambayo yanaonekana utatuzi wake ni mdogo na usiowezekana ambapo alisema Muungano wa Tanganyika na Zanzibar hauna manufaa yena na wazanzibari.

Katika kuonesha kwamba hawataki tume ya katiba ije kuchukua ya maoni ya katiba mpya Sheikh Farid alisema wanataka kwanza kuamuliwe suala la Muungano kabla ya jambo lolote na kuahidi kwamba wataendelea kufanya makongamano, mihadhara na maandamano kwa kadiri wawezavyo hadi hapo serikali itakaposikia kilio hicho.

“Ujumbe huu tunautoa kwa Ban Kin moon, na kwa ulimwengu mzima lakini pia tunataka rais wetu Dk Shein asikie kilio hiki na Rais Kikwete ambaye yeye ni mtetezi wa haki za binaadamu na pia ni mfuatiliaji wa nchi zinazovunja haki za binaadamu tunataka asikie kilio cha wazanzibari kuwa wanataka nchi yao” alisema. 

Alisema juzi wamefanya maombi maalumu ya kumuombea Rais wa Zanzibar lengo likiwa ni kumjaaliwa kheri na awe na maamuzi sahihi juu ya wananchi wa Zanzibar sambamba na kuwaomba Makamu wa Kwanza na makamu wa Pili wa Zanzibar kusikia kilio cha wazanzibari wasiotaka Muungano.

“Tunamuomba Rais wetu Dk Shein, Makamu wa Kwanza Maalim Seif na Makamu wa Pili Balozi Seif kwamba sisi wazanzibari tunahitaji Zanzibar huru, tunahitaji heshima ya nchi yetu na tupo tayari kwa lolote kwa hivyo tunataka salamu hizi na ujumbe huu ukufikieni” alisema Sheikh Farid huku akiungwa mkono na maelfu waliohudhuria katika kongamano hilo ambalo awali liliandaliwa kwa lengo la kuzungumzia masuala la elimu na mfumo wake.

Akiendelea kutoa salamu hizo mara Sheikh Farid alisoma kifungu cha 16 cha katiba na kuwaleza wananchi kwamba haki ya kutembea ni haki ya kila mwananchi ambayo imeainishwa katika katiba na sheria za haki za binaadamu hivyo aliwageukiwa na kuwataka wasimame na kisha kumfuata yeye.

“Haki ya kutembea ni haki ya msingi kwa mujibu wa sheria na kifungu cha 16 kinatupa haki ya kutembea sasa mimi nataka kutembea jeee mpo tayari kutembea na mimi? Alihoji Sheikh huyo huku akijibiwa na umma mkubwa kwamba ndioooo”

Aliongeza kwamba “Tunaanza kutembea na tuone mtu atukamate tunakwenda njia ya kinazini, tunapita michenzani, tunapita barabara ya kwa biziredi na kisha tunarejea hapa hapa kuendelea na kongamano letu kwa amani kabisa mmesikia….akajibiwa ndiooooo”
baada ya kusema hivyo Sheikh Farid alitoa takbir na kuanza kukamatana mikono na viongozi wenzake na huku ummati mkubwa ukiwa umekamatana mikono nyuma na kuanza safari kwa pamoja na kutembea katika barabara ambazo walizitaja awali.

Waandamani hao walikamata mabango yenye maandishi mbali mbali ikiwemo hatutaki muungano, tunataka nchi yetu, zanzibar bila ya muungano inawezekana na wengine kadhalika huku wakitembea njiani na kupiga takbir ambapo walikuwa wakisema Mwenyeenzi Mungu Mkubwa, Mwenyeenzi Mungu Mkubwa sisi hatuna uwezo isipokuwa tunakutegemea wewe Mwenyeenzi Mungu.

Waandamanaji hao walianza kutembea kwa utaratibu maalumu huku magari yakisimama na kuwapisha bila ya kuwepo jeshi la polisi ambapo viongozi wa jumuiya hiyo na wananchi wengine waliongoza utaratibu huo na kutembea katika barabara kwa utaratibu mzuri hadi kumaliza maandamano yao waliyoyaita matembezi ya amani. 

Baadae jeshi la polisi lilifika katika eneo ambalo kumefanyika maandamano hayo na kufungua mabango yao ya kuwataka watu kuondoka lakini wakati magari hayo ya polisi matatu yanafika eneo hilo la Kariakoo tayari ummati mkubwa ulikuwa umeshapita katika eneo hilo na hivyo kuingia ndani ya magari yao na kuondoka kwa salama.

Awali akitoa mada katika kongamano hilo, Maalim Abdulhafidh Malelemba alisema sekta ya elimu imekuw aikidorora Zanzibar kutokana na kukandamizwa na mambo ya Muungano ambapo kila mwaka wanafunzi wanapofanya mitihani kufelishwa kwa makusudi huku idadi ya wanafunzi wanaokwenda katika vyuo vikuu wakiwa kidogo kutokana na kufelishwa katika mitihani ambapo husainiwa na baraza la mithani Tanzania (NECTA).

Wakizungumza katika nyakati tofauti katika kongamano hilo, baadhi ya walimu walisema kukosekana kwa baraza la mitihani Zanzibar kusimamia mitihani ya elimu ya juu ndio sababu ya wazanzibari kufelishwa kwa wingi na kushindwa kuingia katika vyuo vikuu kwa kuwa wanafunzi wengi wa Zanzibar hufelishwa.


Walimu hao walitoa ushahidi wa hivi karibuni wa kufelishwa wanafunzi wa kidatu cha nne ambapo walisema lile ni tukio la makusudia lililofanywa na baraza la mitihani ikiwa ni kuwadhoofishwa wanafunzi wa Zanzibar ili wasiendelee katika masomo kwa kuwafelisha.
----

JUMUIYA YA UAMSHO NA MIHADHARA YA KIISLAMU

(JUMIKI)

للجنة الدعوة الإسلامية

THE ASSOCIATION FOR ISLAMIC MOBILISATION AND PROPAGATION

P. O. BOX: 1266 -Tel:             +255-777-419473 begin_of_the_skype_highlighting            +255-777-419473      end_of_the_skype_highlighting       / 434145- FAX +255-024-2250022 E-Mail: jumiki@hotmail.com

MKUNAZINI ZANZIBAR


Tarehe 27MAY2012 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI 

Kila sifa njema anastahiki ALLAH (S.W) na Rehma na Amani zimuendee Mtume Muhammad (S.A.W), ahli zake, Maswahaba zake na walio wema katika Uislamu.

Jumuia ya UAMSHO inatoa taarifa rasmi kwa umma wa Wazanzibari na Watanzania wote kwa ujumla kwamba haihusiki na vitendo vyote vya uvunjaji wa amani vilivyotokea usiku wa tarehe 26 Mei 2012. Kama alivyosema Mtume (S.A.W) katika Hijatul Wadaa, kwamba ni haramu kumwaga damu zenu, kuharibiana mali zenu, kuvunjiana heshma zenu ila kwa haki ya Uislamu (maana yake pale mtu anapofanya kosa na likathibitika atahukumiwa kwa hukmu ya Kiislamu). Vile vile Uislamu unaheshimu nyumba za ibada (Makanisa, Mahekalu na n.k) zisivunjwe wala zisiharibiwe.

Jumuia inatoa wito kwa Waislamu na Wazanzibari wote kuendelea kudumisha amani na utulivu wa nchi na kutoharibu mali za serikali, mali za wananchi, mali za taasisi za dini zenye imani tofauti, kwani kufanya hivyo ni kwenda kinyume na mafundisho ya dini ya Kiislamu. Jumuiya inayachukulia matukio yaliyotokea usiku wa jana, na yanayoendelea tangu alfajiri leo, kama ni njama za makusudi za wale wasioipendelea amani nchi hii, pamoja na kutaka kuipaka matope jumuiya na kutaka kuzuia lengo la Wazanzibari kudai nchi yao.

Tunatoa wito kwa Jeshi la Polisi na Vyombo vyote vya Dola wafanye kazi zao kama wanavyotakiwa kwa mujibu wa muongozo wa haki za binadamu kwa Polisi na vikosi vingine unaosema kwamba polisi na vyombo vingine vya dola wana jukumu la kutunza amani na utulivu na jukumu la kutoingilia haki za watu. Kila mtu anayo haki ya kuwekewa mazingira muafaka ya kitaifa na kimataifa yatakayomuwezesha kupata haki zake za binadamu.

Polisi na vyombo vingine vya dola wana jukumu la kutunza amani na utulivu na jukumu la kutoingilia haki za watu isipokuwa tu kwa minajil ya kulinda haki za wengine.

Polisi na vyombo vingine vya dola wana jukumu la kuheshimu, kulinda na kutetea haki za binadamu kwa watu wote.

WABILLLAH TAWFIQ .

WAPIGA PICHA ZA HABARI KATIKA MAFUNZO MAALUM LEO DAR



 Mkurugenzi wa Mfuko wa Vyombo vya Habari-Tanzania Media Fund (TMF) , Ernest Sungura, akifungua semina ya wapigapicha za habari waandamizi, leo kwenye ukumbi za Msimbazi Centre, Dar es Salaam. Kushoto ni mratibu wa semina hiyo Selemani Mpochi na watatu kutoka (kushoto) ni Ofisa Mawasiliano wa Airtel Dagio Kaniki.
Baadhi ya wapigapicha za habari wakiwa kwenye semina hiyo.
Mkufunzi kutoka Frem Tree, Mwanzo Milinga, akitoa mafunzo kuhusiana na kazi ya kupiga picha za habari, wakati wa semina hiyo

BOSCH POWER TOOLS - MARANGO LTD


This is an advertisement.
Having trouble reading this email? View it on your web browser.

Extreme Web Technologies Ltd | 3rd Floor, Osman Towers, Zanaki Street | P. O. Box 14001, Dar es Salaam, Tanzania
You are currently subscribed to our mailing list as mhamila1@gmail.com.
If you wish to unsubscribe, please unsubscribe by clicking here.
Copyright (c) 2011, Extreme Web Technologies. All Rights Reserved.
Email marketing services provided by Extreme Web Technologies
Powered by RahisishaMail.com
You might also like:

NBC MORO BRANCH SPONSORSHI​P



Meneja wa Tawi wa Benki ya NBC Morogoro, Jasson Shumbusho (kulia) akikabidhi mfano wa hundi ya shs Milioni 5.1 kwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Sanaa za Maonyesho ya Ngoma Africa Performing Arts, Davie Kitururu ikiwa ni udhamini wa NBC katika tamasha la sanaa la watoto la Paukwa. Kushoto ni Mkurugenzi mwenza wa Taasisi hiyo, Bi. Maya Davie na wengine ni baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo.

MSHINDI WA REDD'S MISS TABORA 2012 NI SARAH PAUL.



 Mshindi wa redd's miss Tabora 'Sarah Paul '
mshindi wa taji la Redds Miss Tabora 2012 Sarah Paul katikakati akiwa na washindi wengine wawili Glory Mongi kulia na Alice Amour kushoto mara baada ya kufanikiwa kutawaza washindi wa taji hilo na kufanikiwa kuingia katika kinyanganyiro cha kanda kuelekea kwenye fainali ya Redds Miss Tanzania 2012

UZINDUZI NA UTAMBULISHO WA HUDUMA YA AIRTEL SUPER 5 DODOMA



Mnenguaji mahiri wa bendi ya Mashujaa, Lilian Tungaraza ‘Internet’ akiongoza kundi la wanamuziki wa bendi hiyo kulishambulia jukwaa wakati wa uzinduzi wa huduma ya Airtel Jiunge na Supa 5 mjini Dodoma mwishoni mwa wiki.
Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando (kushoto) akikabidhi zawadi ya simu kwa, Baltazar Theobald, mshindi wa kwanza aliyeweza kueleza vizuri jinsi ya kujiunga na huduma mpya ya Airtel Jiunge na Supa 5 wakati wa hafla ya uzinduzi wa huduma hiyo Mkoani Dodoma mwishoni mwa wiki. Airtel Jiunge na Supa 5 Ilizinduliwa kwa mara ya kwanza jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
Wasanii wa muziki wa kizazi kipya wa kundi la Wanaume Family, Said Juma ‘Chege’ (kushoto) na Amani James Temba ‘Mheshimiwa Temba’wakionyesha makali yao katika onyesho la uzinduzi wa huduma ya Airtel Jiunge na Supa 5 mjini Dodoma mwishoni mwa wiki.
Mpiga tumba mahiri wa bendi ya Mashujaa Musica aliyejiunga na bendi hiyo akitokea Twanga Pepeta, Sudi Mohamed ‘MCD’ akionyesha makali yake wakati wa onyesho la uzinduzi wa huduma ya Airtel Jiunge na Supa 5 mjini Dodoma mwishoni mwa wiki.
Rais wa Bendi ya Mashujaa Musica, Charles Gabriel Cyprian ‘ Chaz Baba’ ambaye naye amehama akitokea Twanga Pepeta, akiimba wakati wa onyesho la uzinduzi wa huduma ya Airtel Jiunge na Supa 5 mjini Dodoma mwishoni mwa wiki.
Msanii wa kundi la muziki wa bongo fleva la Tip Top Connection lenye maskani yake mitaa ya Manzese jijini Dar es Salaam Hamad Ally ‘Madee’ akichengua mashabiki wake waliojitokeza katika onyesho la uzinduzi wa huduma ya Airtel Jiunge na Supa 5 mjini Dodoma mwishoni mwa wiki.

Huduma ya SUPA 5 imepokelewa kwa shangwe mkoani Dodoma huku dhamira yake ikiendelea kutimia baada ya umati mkubwa wa vijana kujitokeza ili kufahamu vyema huduma hiyo nafuu iliyozinduliwa wiki moja iliypota kwa lengo la kuwapa unafuu wateja wa Airtel ili kufurahia huduma tano nafuu

Wakati wa uzinduzi huo uliofanyika katika tamasha la wazi katika viwanja vya Barafu mjini Dodoma wasanii wa muziki wa Dansi na Bongo Flaver walitumbuiza na kufanya tamasha hilo kufana zaidi

Miongoni mwa wasanii waliotumbuiza kwenye utambilisho wa huduma hiyo mpya kabambe ni pamoja na bendi ya muziki ya mashujaa, kundi la muziki wa kizazi kipya la Tiptop Connection na kundi la Wanaume TMK.

Akitambilisha huduma hiyo mbele ya wakazi wa mji wa Dodoma na vitongoji vyake Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando amesema, wateja wa kampuni hiyo watapata unafuu mkubwa wa gharama za kupiga simu

“Huduma ya SUPA 5 inamuwezesha mteja wa Airtel kutumia mtandao wa facebook bure masaa 24, kuongea nusu shilingi na watu watatu, kupiga simu kwa robo shilingi kuanzia saa 4 usiku hadi saa 12 asubuhi na kutumia huduma ya internet bure usiku kucha” alieleza Bw, Mmbando

Huduma ya SUPA 5 itaendelewa kutambulishwa katika mikoa mbali mbali kwa kuwa huduma hiyo nafuu ni ya kudumu, mikoa inayotarajiwa kutembelewa kwa kufanyiwa utambulisho rasmi wa huduma hiyo ya Airtel Supa 5 ni pamoja na Morogoro, Iringa, Arusha, Mwanza na DSM.

BIA YA CASTLE LITE SASA IPO YA KOPO



Kopo jipya la Castle Lite linavyoonekana sasa
Bia maarufu ya Castle Lite, inayozalishwa na kusambazwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) leo imezindua rasmi muonekano wa kopo lililojazwa kinywaji hicho ikiwa ni muendelezo wa kuwarahisishia walaji upatikanaji wa Bia hiyo iliyotokea kupendwa na watumiaji wa vileo na kuifanya iwe bia inayokua kwa kasi hapa nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi huo, Meneja wa Bia ya Castle Lite Bi. Pamela Kikuli alisema; Leo tunazindua ujazo mpya wa bia ya Castle lite, bia yenu muipendayo kwa sasa inapatikana katika kopo lenye ujazo wa mililita 330. Uamuzi huu unatokana na mahitaji makubwa toka kwa watumiaji na wapenzi wa bia hii ambayo imekuwa ikipatikana katika chupa yenye ujazo wa mililita 375.

 Wateja wetu walihitaji kuipata bia yao popote pale walipo au kuwa nayo popote waendapo, hivyo kupatikana kwa bia hii katika chupa peke yake kulipunguza uhuru wa kuwa na bia yao popote waendapo kwani walihitaji kurudisha chupa kila waitumiapo.

Uzinduzi wa Castle lite ya kopo utasaidia zaidi kuongeza upatikanaji wa kinywaji hiki katika maduka ya reja reja (super markets) n.k kote nchini na kuwapa nafasi wapenzi wa castle lite kununua bia yao waipendayo na kwenda nayo nyumbani. Bei ya reja reja kwa kopo ni shilingi 1700/- na bei ya reja reja kwa chupa itaendelea kubaki ile ile 1700/-.

Kwa upande wake Meneja mawasiliano na mahusiano ya jamii wa Tbl Edith Mushi aliwashukuru wapenzi na watumiaji wa bia ya Castle Lite kwa kuweza kuipa mafanikio makubwa katika soko la bia hapa nchini, “ninawahakikishia kuwa mnafanya uamuzi ulio sahihi kwa kuchagua kutumia Castle Lite” nasi tutaendelea kuwapatia bia iliyo bora siku zote. Alisema Edith.
You might also like:

Sunday, May 27, 2012

MCHUMIA TUMBO AMGALAGAZA Bahati Mwamfiale



Baadhi ya mashabiki wakiwa wamebeba viti kwa ajili ya kujifunika wakati mvua ilipokua iki nyesha kwenye mpambano huo Dar es salaam jana.PICHA NAwwwsuperdboxingcoach.blogspot.com
Kocha wa Mchezo wa Masumbwi Rajabu Mhamila 'Super D' akiwa amepozi wakati wa mpambano huoPICHA NAwwwsuperdboxingcoach.blogspot.com
SUPER D BOXING COACH AKIONESHA DVD ZAKE ALIZOKUWA AKIZA KATIKA MPAMBANO HUO DVD HIZO ZENYE MBINU NA SHERIA ZA MCHEZO WA MASUMBWI AMBAZO ZIMEEDITIWA KITAALAM KWA AJIRI YA KUFUNDISHA MBINU ZA MCHEZO HUO KUJUA SHERIA NA KANUNI ZAKE NDANI KUKIWA NA MABONDIA WA KIMATAIFA KAMA MANNY PAQUAIO,FLOYD MAYWEARTHER,AMIRI KHANY, MOHAMEDI ALI LENOX LEWIS NA WENGINE WENGIPICHA NAwwwsuperdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Alphoce Mchumiatumbo  kushoto akimshambulia kwa makonde bondia Bahati Mwamfiale wakati wa mpambano wao uliofanyika Dar es salaam jana Mchumia tumbo alishinda kwa K,O raundi ya tatuPICHA NAwwwsuperdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Alphoce Mchumiatumbo kulia akipambana na Bahati Mwamfiale wakati wa mpambano wao uliofanyika Dar es salaam janaPICHA NAwwwsuperdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Alphoce Mchumiatumbo  kushoto akimwangalia bondia Bahati Mwamfiale  baada ya kumfulumusha makonde na kukaa chini wakati wa mpambano wao uliofanyika Dar es salaam jana Mchumia tumbo alishinda kwa K,O raundi ya tatu PICHA NAwwwsuperdboxingcoach.blogspot.com

IDDY MNYEKE AJINOA KUMKABILI FADHIRI AWADHI JUNE 9


 Bondia Iddy Mnyeke kushoto akioneshana ufundi wa kutupiana makonde na Vitor Njait wakati wa mazoezi yanayoendelea katika kambi ya ngumi ya Ilala Mnyeke  anajitahalisha na mpambano wake dhidi ya Fadhiri Awadhi utakaofanyika June 9 katika ukumbi wa Frensi kona Manzese Dar es salaam .Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.comwww.superdboxingcoach.blogspot.com
 Bondia Iddy Mnyeke kushoto akioneshana ufundi wa kutupiana makonde na Vitor Njait wakati wa mazoezi yanayoendelea katika kambi ya ngumi ya Ilala Mnyeke  anajitahalisha na mpambano wake dhidi ya Fadhiri Awadhi utakaofanyika June 9 katika ukumbi wa Frensi kona Manzese Dar es salaam .Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.comwww.superdboxingcoach.blogspot.com

RATIBA YA MSAFARA WA SIMBA KUELEKEA DAR LIVE



MAADHIMISHO YA SIKU YA AFRIKA YAFANA, LONDON-UINGEREZA



 Dada Jestina George na dada Rahma Lupatu, wakijivunia Utanzania wao katika sherehe hizo za siku ya Afrika, zilizofanyika jana, Jijini London Uingereza.
 Mheshimiwa Balozi wa Uganda, Mama Joan Rwabyomere, akifungua Maadhimisho ya siku ya Afrika nchini Uingereza, katika sherehe ambazozilifanyika katika Ukumbi wa Hotel ya Lagham Palace, London.
 Mheshimiwa Balozi wa Botswana, Bwana Roy Blackbeard, akihutubia katika sherehe za kuadhimisha siku ya Afrika.
 Kutoka kulia, Dada Rahma Lupatu, Caroline Chipeta, Bwana David Nginila, Bwana Kiondo (maafisa wa Ubalozi wa Tanzania, London) na Dada Jestina George, maarufu kama Queen wa Blog  Uingereza.
 Mabalozi ,Maafisa wa Ubalozi na wawakilishi kutoka nchi mbalimbali za Afrika na wageni waalikwa katika sherehe hizo.
Kikundi cha ngoma kutoka Ghana, wakitoa burudani katika sherehe za kuadhimisha siku ya Afrika hapa London.
***********************************
Siku ya Afrika iliadhimisha rasmi jana hapa nchini Uingereza kwa kujuisha nchi zote za Afrika zenye Balozi au Wawakilishi wao hapa nchini Uingereza. Katika sherehe hiyo rasmi ya kuadhimishwa kwa Siku ya Afrika, kulitolewa hotuba na Balozi wa Botswana na mbaye ni Mkuu wa Mabalozi wa nchi za Afrika hapa Uingereza, Mheshimiwa Roy Warren Blackbeard. 

Aidha Mheshimiwa Balozi Roy Blackbeard, alitoa salamu maalum kutoka kwa mwenyekiti wa sasa wa Umoja wa nchi za Afrika, Mheshimiwa Yayi Boni, ambaye pia ni Raisi wa Benin. 

Balozi Roy, alielezea changamoto nyingi zinazo tokea Barani Afrika na kwingineko na juhudi maalum zinazofanywa na Jumuiya ya Umoja wa nchi za Afrika kutatua migogoro na matatizo ya mara kwa mara yanayolikumba Bara letu la Afrika.

Kabla ya kutolewa hotuba hiyo, Balozi wa Uganda Mheshimiwa Mama Joan Rwabyomere, alifungua kwa kuwakaribisha Mabalozi, Wawakilishi, Marafiki wa Afrika na Wageni mbalimbali waalikwa na kuwashukuru kwa kufika kwao na kujumuika pamoja na waafrika wote duniani kuadhimisha siku hiyo hapa nchini Uingereza. 

Amani, Upendo, Ushirikiano na Mshikamano miongoni mwa nchi za Afrika vilihimizwa katika maadhimisho hayo.