Tangazo

Sikiliza kipindi cha michezo kutoka CAPITAL RADIO kilasiku 21:00


Viwanjani%20%28Maximo%29
Quantcast

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI
VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD ZA MAFUNZO SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D' Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com mhamila1@gmail.com www.superdboxingcoach.blogspot.com Mob;+255787 406938 +255774406938, +255713406938 Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania

Tuesday, October 29, 2013

MKE WA RAIS, MAMA SALMA KIKWETE AFUNGUA RASMI MAONESHO YA WANAWAKE WAJASILIAMALI NCHINI




 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akivishwa bangili na mama Esther Moreto na Nelgwe Kikoti wajasiriamali wa kabila la wamasai kutoka katika kijiji cha Kwamakweza huko Chalinze, wilayani Bagamoyo. Akina mama hao mno miongoni mwa wajasiriamali wanaoonyesha bidhaa zao Mnazi mmoja.
 Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Mama Salma Kikwete akitembelea mabanda mbalimbali ya wajasiriamali kutoka sehemu mbalimbali za Tanzania wanaoonyesha bidhaa zao kwenye maonesho yanayofanyika Mnazi Mmoja.
 Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Mama Salma Kikwete akitembelea mabanda mbalimbali ya wajasiriamali kutoka sehemu mbalimbali za Tanzania wanaoonyesha bidhaa zao kwenye maonesho yanayofanyika Mnazi Mmoja.
 Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Mama Salma Kikwete akitembelea mabanda mbalimbali ya wajasiriamali kutoka sehemu mbalimbali za Tanzania wanaoonyesha bidhaa zao kwenye maonesho yanayofanyika Mnazi Mmoja.
 Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Mama Salma Kikwete akitembelea mabanda mbalimbali ya wajasiriamali kutoka sehemu mbalimbali za Tanzania wanaoonyesha bidhaa zao kwenye maonesho yanayofanyika Mnazi Mmoja.
 Akinamama wajasiriamali wakisikiliza hotuba mbalimbali za viongozi wakati wa ufunguzi rasmi wa maonesho hayo kwenye uwanja wa Mnazi Mmoja.
 Akinamama wajasiriamali wakisherehekea ufunguzi rasmi wa maonesho yao uliofanywa na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete.

TIMU YA TAIFA YA MCHEZO WA POOL YAFANYA MAKUBWA NCHINI MALAWI




Wachezaji wa timu ya Taifa ya Safari Pool ya Tanzania wakiwa na medali zao za Fedha mara baada ya kutunukiwa kwa kupata nafasi ya tatu katika mashindano ya Pool Afrika yaliyofanyika jijini Blantyre Malawi mwishoni mwa wiki.
Wachezaji na mashabiki wa timu ya Safari Pool kutoka Tanzania wakishandilia na mchezaji Patrick Nyangusi mara baada ya kutwaa ubingwa wa mchezaji mmoja mmoja (Singles) Afrika uliofanyika Blantyre Malawi mwishoni mwa wiki.
Wachezaji na mashabiki wa timu ya Taifa ya Safari Pool ya nchini Tanzania wakiwa wamembeba mchezaji,Patrick Nyangusi mara baada ya kutwaa ubingwa wa Afrika wa mchezaji mmoja mmoja (Singles) kwa kumfunga Vishen Jagdev wa Afrika Kusini 6-4,katika mchezo uliofanyika Blantyre Malawi mwishoni mwa wiki.
Bingwa wa Afrika wa mchezo wa Pool kutoka Tanzania, Patrick Nyangusi akicheza dhidi ya mpinzani wake, Vishen Jagdev kutoka Afrika Kusini (hayupo pichani) wakati wa mchezo wa fainali uliofanyika Blantyre Malawi mwishoni mwa wiki.

TANZANIA NEXT HANDSOME MAN KUFANYIKA NOV 1 @ CLUB BILLICANAS



Usikose hili ni bonge moja la show hapa town.

Monday, October 28, 2013

AMOSI MWAMAKULA AMGALAGAZA SAFARI MBEYU


Bondia Amos Mwamakula akinyooshwa mkono juu baada ya kumchapa Safari Mbeyu kwa pointi wakati wa mpambano wao picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Amosi Mwamakula kulia akimshambulia Safari Mbeyu wakati wa mpambano wao mwamakula alibuka na ushindi wa point wakati wa mpambano wao picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

KOCHA WA KIMATAIFA WA MCHEZO WA MASUMBWI RAJABU MHAMILA 'SUPER D' ALIJIKUTA AMEMECHISHA KOFIA NA MWAMAKULA YENYE NEMBO YA TMT AMBAYO ANATUMIA BONDIA FLOYD MAYWETHER WA MAREKANI
AMOSI MWAMAKULA
BONDIA AMOSI MWAMAKULA AKIJITAARISHA
Bondia Amosi Mwamakula kulia akimshambulia Safari Mbeyu wakati wa mpambano wao mwamakula alibuka na ushindi wa point wakati wa mpambano wao picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
AMOSI MWAMAKULA

KOCHA WA KIMATAIFA WA MCHEZO WA MASUMBWI NCHINI RAJABU MHAMILA 'SUPER D'

SIMBA YAPOKEA KICHAPO CHA BAO 2-1




Azam waliendelea kulisakama lango la Simba na kufanikiwa kupata bao la kusawazisha kupitia kwa Kipre Tchetche dakika ya 45 akimalizia krosi safi ya Erasto Nyoni na kufanya timu zote kwenye mapumziko zikiwa zimetoshana nguvu kwa bao 1-1.  

 Mpaka mwisho wa mchezo Simba imepokea kichapo cha kwanza tokea ligi kuu ya Vodacom baada ya kulala kwa Timu ya Azam Fc baada ya kufungwa bao 2-1 katika mchezo uliochezwa leo uwanja wa Taifa jijini Dar.

RAIS KIKWETE NA MAMA SALMA KIKWETE WATOA POLE KWA MJANE NA FAMILIA YA BALOZI ISAAC SEPETU LEO



 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpa pole mjane wa Balozi Isaac Sepetu, Mama Miriam Sepetu, alipokwenda na Mama Salma nyumbani kwa marehemu Sinza Mori, Dar es salaam, kutoa pole kwa mjane huyo na familia ya Marehemu Sepetu aliyefariki jana jijini Dar es salaam.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitoa pole kwa wanafamilia wa Balozi Isaac Sepetu alipokwenda na Mama Salma nyumbani kwa marehemu Sinza Mori, Dar es salaam, kutoa pole kufuatia msiba Marehemu Sepetu aliyefariki jana  jijini Dar es salaam.
 Mke wa Rais Jakaya Mrisho Kikwete  akimfariji mjane wa Balozi Isaac Sepetu alipokwenda  nyumbani kwa marehemu Sinza Mori, Dar es salaam, kutoa pole kufuatia msiba Marehemu Sepetu aliyefariki jana katika jijini Dar es salaam.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete  akiweka saini katika kitabu cha maombolezo ya msiba wa Balozi Isaac Sepetu  alipokwenda  nyumbani kwa marehemu Sinza Mori, Dar es salaam, kutoa pole. Marehemu Sepetu aliyefariki jana katika jijini Dar es salaam.
 Mama Salma Kikwete  akiweka saini katika kitabu cha maombolezo ya msiba wa Balozi Isaac Sepetu  nyumbani kwa marehemu Sinza Mori, Dar es salaam. . Marehemu Sepetu aliyefariki jana katika jijini Dar es salaam.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimfariji  mjane wa Balozi Isaac Sepetu, Mama Miriam Sepetu, alipokwenda na Mama Salma nyumbani kwa marehemu Sinza Mori, Dar es salaam, kutoa pole kwa mjane huyo na familia ya Marehemu Sepetu aliyefariki jana jijini Dar es salaam.

RAIS KIKWETE AITAKA JAMII KUJENGA TABIA YA KUSAIDIA WATOTO YATIMA NA WALIO KATIKA MAZINGIRA HATARISHI



Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete  na mkewe Mama Salma Kikwete wakimpongeza mwenyekiti wa makampuni ya IPP Dkt.Reginald Mengi kwa ahadi ya kuichangia shule ya Sekondari ya WAMA Nakayama Jumla ya Shilingi milioni mia mbili kila mwaka kwa miaka mitano,wakati mahafali ya kwanza ya shule hiyo iliyofanyika katika kijiji cha Nyamisati,wilaya ya Rufiji Mkoa wa Pwani Mishoni mwa Wiki.
Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya WAMA NakayMA ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Dkt.Ramadhani Dau akimkabidhi tuzo Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete kwa mchango wake wa kuimarisha elimu nchini wakati wa mhafali ya kwanza ya Shule ya Sekondari ya WAMA Nakayama iliyofanyika huko.Nyamisati, Wilaya ya Rufiji Mkoa wa Pwani Mwishoni mwa wiki.Kuliua ni Mwenyekiti wa WAMA Mama Salma Kikwete. Picha naFredy Maro
************************************************************
 NA MAGRETH KINABO – MAELEZO
RAIS  Jakaya Kikwete ameitaka   jamii  kuwa na tabia  ya  kuwafadhili  watoto yatima na wanaoishi katika  mazingira magumu   katika kuwapatia elimu, chakula na malazi ili waweze kuendesha maisha yao kwa kujiajiri au kujariwa kwani kwa kufanya hivyo nguvu kazi  ya taifa  haitaweza kupotea.

Kauli hiyo ilitolewa jana (juzi) na Rais Kikwete  wakati wa mahafali  ya  kwanza ya kidato cha nne ya Shule ya Sekondari  ya  Wama Nakayama iliyoko  Nyamisati , wilayani Rufiji , mkoani Pwani yaliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali.

Shule hiyo  inayoendeshwa  na Taasisi ya Wanawake  na  Maendeleo(WAMA)  ,ambapo Mwenyekiti wa taasisi hiyo ni Mke wa Rais Mama Salma Kikwete. 

Rais Kikwete aliwashukuru watu mbalimbali walichangia shule hiyo kwa moyo wao wa upendo na huruma  ili watoto wa kike yatima na wanaoishi katika mazingira magumu  waweze kupata elimu, huku akisema  kama wasi wafadhili  hao isingekuwa rahisi watoto hao kuwezeshwa kusoma shuleni hapo.

“ Mtapata fadhila  kwa Mwenyezi Mungu  kwa kila mtoto atakayesoma hapa…Mkopesheni Mwenyezi Mungu atawapa fadhila zake,”alisema Rais Kikwete.
 Kauli hiyo pia iliungwa na  mkono na Mama Salma Kikwete ambaye alisema bila juhudi za pamoja kati ya  Serikali, jamii na sekta  binafsi  watoto  wengi wa kundi hilo  watakosa elimu.

Mama Kikwete alisema nchi ina Watanzania milioni 44.9 kama wapo wenye uwezo wapatao milioni tano kila mmoja akimchukua mtoto mmoja. 

“ Tanzania   isiyokuwa  na watoto wasio matumaini inawezekana,”alisema Mama Kikwete  huku akisema kwa kufanya hivyo kuwasaidia kujikwamua katika hali ya umasikini.
    
 Rais   Kikwete   aliwataka wanafunzi  hao  kuwa na malengo ya kupata elimu  ya juu ili waweze kukabiliana na changamoto mbalimbali na kulisaidia taifa, huku akisisitiza  wawe jasiri kusoma fani  ambazo wanawake wengi wanaogopa kuzisoma   ambazo zitawawezesha kuwa mabingwa mafano udaktari, wahandisi na wanasheria.

 “ Hamna budi kushukuru na kujipongeza ombi langu ni kuweni watoto wema heshima na mabalozi wa shule hii.  Shule hii itakapokamilika huduma zitakuwa bora.Shule hii ina kila sababu ya kuwa shule bora,” alisema Rais Kikwete.

Aidha  Rais Kikwete  alizitaka  halmashauri nchini  kuendelea kushishirikiana  na Maendeleo(WAMA) kuwatambua watoto yatima na wanaoishi katika  mazingira  magumu  ili  waweze kupata elimu kwa malengo ya  taasisi hiyo.

Katika mahafali hayo Mwenyekiti wa  kammpuni  za IPP, Reginald Mengi  aliahidi kuchangia shule hiyo Sh. milioni 200 kwa kila mwaka kwa kipindi cha miaka mitano na Umoja wa Wanawake Tanzania  wa Chama  cha Mapinduzi (UWT)uliahidi kutoa Sh. milioni 10  yakiwemo mashirika mbalimbali yaliyoahidi kutoa michango  kadhaa.

Rais  Kikwete katika mahafali hayo aliwatunuku vyeti wanafunzi 67 na kutoa zawadi za vyeti na fedha tasilimu kwa wanafunzi na walimu waliofanya vizuri, ambapo mwanafunzi  aliibuka mshindi baada ya kufanya vema  kwenye masomo ya biashara, historia na Kiingereza.Mwanafunzi aliyefanya vizuri kila somo alipata Sh. 100,000 na mwalimu Sh. 500,000.

MTEMVU,KIMATH WAPIGA MARUFUKU MALORI KUMWAGA MAJI TAKA MABWAWA YA KURASINI,DAR



 Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu  akimuuliza swali Mfanyakazi wa  Mamlaka ya Maji Safi na Taka Dar es Salaam (DAWASA),Omar Mlanzi, walipokwenda kupiga marufuku malori kwenda kumwaga maji taka katika mabwawa ya Kurasini, Dar es Salaam, baada ya baadhi ya wakazi wa eneo hilo kulazwa hospitali kwa kuhara na kutapika kulikosababishwa na Dawasa kutoweka dawa ya kuua bakteria kwenye mabwawa hayo.Sababu nyingine ni kwamba mabwawa hayo yamezidiwa baada ya mabwawa mengine jijini kufungwa hivyo malori yote ya taka kwenda kumwaga hapo. Wa pili ni Diwani wa Kata hiyo, Wilfred Kimath na Augustino ambaye ni mtumishi wa kampuni binafsi iliyopewa jukumu la kusimamia malori yanayokmwaga mati taka katika mabwawa hayo.PICHA ZOTE NA KAMANDA RICHARD MWAIKENDA WA KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Mtemvu akijadiliana jambo na Diwani, Kimath
 Baadhi ya malori yaliyokutwa yakimwaga maji taka kwenye mabwawa hayo.
 Moja ya malori lililokutwa likimwaga maji taka kabla ya kupigwa marufuku

 Mtemvu akiwasiliana na uongozi wa Dawasco na Dawass
 Moja ya mabwawa likiwa limefurika maji taka kupita kiasi
 Mfanyakaziwa lori akifunga baada ya kuamriwa kufanya hivyo
 Mmoja wa madereva  Hemed Abdalah akielezea adha wanayipata baada ya mabwawa ya maji taka kufungwa jijini
 Mtemvu kulia akiangalia baadhi ya malori ya maji taka
Mtemvu na Kimath wakiondoka baada ya kufunga matumizi ya mabwawa hayo

FILAMU YA "FIGO" KUTOKA PROIN PROMOTIONS KUINGIA SOKONI MUDA WOWOTE KUANZIA SASA


 
Kampuni ya utengenezaji,uuzaji na usambazaji wa filamu za kitanzania ya Proin Promotions Limited inatarajia kuingiza movie yake nyingine sokoni mapema wiki hii. Filamu ya "FIGO" ni filamu ya kitanzania ambayo imechezwa na waigizaji wakongwe katika tasnia ya filamu nchini na Ni filamu ambayo inasimimua,kufundisha na kuelemisha, Filamu ya Figo ni moja kati ya filamu ya Kitanzania ambayo imechezwa kwa ustadi wa hali ya juu na kutengenezwa kwa hali ya juu na kampuni Mahiri ya Utengenezaji na Uuzaji wa Filamu Tanzania ya Proin Promotions Limited 

Proin Promotions ni moja ya kampuni kubwa ya utengenezaji,uuzaji na usambazaji wa filamu Tanzania ambayo tayari ishaingiza Sokoni Filamu Mbili ambazo zinafanya Vizuri kama vile Foolish Age, Long Time na sasa inakuletea Filamu ya FIGO ambayo imechezwa na Jennifer Kyaka ambaye anafahamika kama Odama, Irene Uwoya, Rachel Haule, Stanley Msungu na wengineo wengi.

Filamu ya "FIGO" inatarajia kuingia sokoni muda wowote kuanzia sasa ambapo itapatikana katika maduka yote ya Uuzaji wa filamu na Kwa mawakala Wao Nchini Nzima, Vilevile Unaweza kununua filamu hiyo ya figo kupitia Ukurasa wa facebook wa Proin Promotions Limited Kupitia https://www.facebook.com/proinpromotions na kupitia pia tovuti yao ya http://www.proinpromotions.com

Pata Nakala yako Sasa

Sunday, October 27, 2013

MOHAMED BAWAZIR AONGOZA KIK AO CHA KUANGALIA MUSTAKABALI WA KATA YA JANGWANI



Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Kata ya Jangwani, Mohamed Bawazir kulia akizungumza na viongozi wa CCM pamoja na wadau wa chama hicho wa kata hiyo juu ya mustakabali mzima wa kata hiyo baada ya kuongoza ndani ya kipindi cha miezi sita kushoto Katibu Wake Majala Balawa
Baadhi ya wanachama na viongozi wa CCMwakifatilia mkutano huo
Mmoja ya wanachama wa CCM wa kata ya jangwani Maaarufu  kwa jina la mlipula na Nuguze akijitambulisha kwa wanachama wenzie
wanachama wakimsikiliza mwenyekiti
Mwenyekiti wa CCM Kata ya Jangwani Mohamed Bawazir kulia akiteta jambo na Katibu Wake Majala Balawa wakati wa mkutano wa mustakabali mzima wa kata hiyo baaa ya kuongoza kwa miezi sita

WAANDISHI WA HABARI WAPIGWA 'STOP' KURIPOTI UCHAGUZI WA TFF




Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) Juma Pinto (katikati) akizungumza na Waandishi wa Habari nje ya Ukumbi wa Mikutano NSSF  'Water Front', mahala unapofanyika Uchaguzi mkuu wa Rais na viongozi wa Soka wa Shirikisho la mpira wa miguu nchini (TFF).

KATIKA hali isiyo ya kawaida, Waandishi wa Habari  wamezuiwa kuripoti habari za uchaguzi mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), uliofanyika katika Ukumbi wa mikutano wa NSSF Water Front.
Baada ya waandishi kuzuiwa, askari waliokuwa wakilinda usalama katika uchaguzi huo waliwataka waandishi kuondoka na kukaa mbali na ukumbi huo huku  Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo (TASWA), Juma Pinto, akiwataka waandishi kususia kuandika na kuripoti matokeo ya uchaguzi huo ikiwa ni pamoja na kutoandika taarifa za TFF.
Pinto alisema kitendo cha TFF kupitia kwa Mwenyekiti wa Kamati ya uchaguzi, Hamidu Mbwezeleni, kuwazuia waandishi kuripoti habari hizo ni cha udhalilishaji kwa kuwa waandishi ndio waliokuwa mstari wa mbele kuandika taarifa za uchaguzi huo tangu mchakato wake ulipoanza Februari mwaka huu.
Alisema mbali na kutoruhusiwa kuripoti uchaguzi huo, Mbwezeleni ametoa kauli ambazo si za kiungwana na kusahau kuwa waandishi ndio waliokuwa mstari wa mbele kuwajuza Watanzania kuhusu uchaguzi huo kwa faida ya maendeleo ya soka la Tanzania.

 Kufuatia hali hiyo, iliwalazimu waandishi kukaa nje ya ukumbi huku wakiuliza kwa wajumbe kitu gani kinachoendelea ndani ya ukumbi.

BREAKING NEEEWZ!!! BABA MZAZI WA WEMA SEPETU, BALOZI ISAAC SEPETU AFARIKI DUNIA




HABARI zilizotufikia hivi punde mtandao huu, zinasema kuwa, Baba Mzazi wa msanii wa Filam nchini na Miss Tanzania wa mwaka 2006, Wema Sepetu, Balozi Issac Abraham  Sepetu, amefariki Dunia asubuhi ya leo katika Hospitali ya TMJ Mikocheni jijini Dar es Salaam, alikokuwa amelazwa.
Aidha imeelezwa kuwa, Balozi Sepetu alikuwa amelazwa katika hospital ya TMJ akitibiwa ugonjwa wa Kisukari na kiharusi uliokuwa ukimsumbua.
Hadi umauti unamkuta,Balozi Isaac Sepetu alikuwa ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Uwekezaji wa Vitega Uchumi Zanzibar.
Mtandao huu unaungana na waombolezaji wote wa Msiba huu na Mwenyezi Mungu, Aiweke Roho ya Marehemu Balozi Isaac Abraham Sepetu, Mahala Pema Peponi .
-Amen-